Changamoto za madereva na abiria wa Uber na Bolt. Tupia yako

moneymakerman

Member
Jan 20, 2014
93
230
Habari za leo wanajamvii, natumai wote mko salama. Kuna vituko na visa vingi tunapitia kama abiria na madereva wa taxi mtandao yaani huduma za uber, bolt na nyinginezo. Hebu tutoeni ushuhuda wa matukio mbali mbali yaliyowahi kutupata na kutufurahisha ama kutukasorisha.

Hii ilitokea kama dereva, abiria wa bolt jinga saana, Kani reaquest Tank Bovu nafika pale ananiambia ingiza Gari ndani, naingia wanaleta bonge la sufufia limejaa mtori, eti kaka fungua buti wapakie, hata kwa IST halikai kaka laza siti. Anatoka mwingine, anamwambia ni pale kawe imesoma 2000.

Daah, hebu tuchangie uzi maana wengi wetu yanatugusa.
 
Niliwahi kuitisha Uber maeneo ya Mbagala inipeleke maeneo ya Tandika sokoni. Wakati naita range ya nauli ilikuwa kati ya Tsh 9000 hadi Tsh 11,000; wakati wa safari niliona kwenye ramani kama route imecheza na kuonesha tuko pande za Kipawa - Gongo La Mboto tunaitafuta Temeke. Kufika Tandika nauli inasoma Tsh 23,000.

Nikakumbuka siku chache zilizopita nilisoma malalamiko hapa JamiiForums kwamba kuna madereva wa Uber wameanza wizi wa kucheza na ramani/route na kufanya bei ya nauli isome kubwa, nikajua na huyu amenichezea picha la kihindi. Nikagoma kumlipa hiyo Tsh 23,000 nikakomaa hadi nikamlipa Tsh 11,000 yake na kusepa.

F@l@ sana yule dereva
 
Back
Top Bottom