Changamoto: Ungekuwa wewe ungefanya nini?

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wanajamvi
Naomba tujipe changamoto ya kuchagua any Decsion Making Post/Position nje ya urais. Baada ya kuchagua tutaje vission/mission zetu katika kutekeleza kazi kazi hiyo post. Jaribu kuchambua na kubainisha katika hiyo post( e.g Wizara/idara au shirika) utaoa Priority kwenye vitu/mambo gani na tatizo gani katika miaka mitano au Kumi. ya leadership yako.Utueleze wanachi tutaona/kupata faida gani baada ya hicho kipindi.

NB:
ni wazi wote hatuwezi kukubalina kwa kila kitu buts l"ets try to walk a mile on their shoes"

Nawasilisha.
 
Nachagua kuwa decision maker katika wizara ya elimu. Nitapenda kuona mfumo na mitaala ya elimu hasa primary na secondary inabadilika kumfanya wahitimu wawe chachu ya mabadiliko endelevu na maendeleo katika jamii zao.

Hivi sasa tunawaona vijana ambao hawajaweza kuchaguliwa kuendelea darasa la 7 au form 4 kama wameshindwa/failures. Mtazamo huu ni wa kinyanyapaa na naona badala ya kuwaita vijana hawa failures serikali ndio inawajibika kwa kushindwa kwao. Kwa Vission yangu itakuwa kutoa elimu ambayo itawasaidi hata wale ambao hawajafanya vizuri

Mtaala wa elimu nitakaopendekeza ni kumuwezesha mwanafunzi anayemaliza kuwa basic elimu kwa nadharia na vitendo ya kumudu mazingira yake.

Binafsi sioni sahihi kwa mwanafunzi wa shule ya monduli kumaliza darasa la saba au form4 bila kuwa na somo la ufugaji japo kwa mwaka 1ja.Sioni sababu kwa sahihi kwa mwanafunzi wa wilaya ya ukerewe asifundishwe somo la uvuvi. Sioni sababu kwa nn mwanafunzi wa lushoto amalize shule bila na elimu ya nadharia na vitendo ya kilimo cha matunda na mboga mboga.

Nina hakika kila wilaya inaweza kuwa na somo moja ambalo linaendana na mazingira ya sehemu husika. Wanafunzi watafundishwa somo hili darasa la sita na la saba vile vile kwa form 3 na form 4.

Njia za kupata walimu wa masomo husika kwa kuanzia zinaweza kutumika njia kama za upe . watu wa maeneeo husika wenye ujuzi asili wa taaluma husika watapigwa msasa na watatumiwa kuwafundisha wanfunzi. Itakuwa ni jukumu la serikali kuandaa mitaala ya masomo haya.

Nahakika kwa mabadiliko haya jamii na serikali kwa ujumla itapata faida zadi ya sasa ambapo tumekazania kwenye elimu ya kawafanya wnafunzi wafanye white collar jobs.
 
Elimu inayofaa ni sehemu tu ili watu waweze kujiafiri lakini big picture lazima kua na serikali inayofanya kazi. Serikali ndio itaunganisha huduma na mambo yote public na private ili kutoa ufanisi mkubwa wa nchi nzima. Kama serikali itakua ni ya kula starehe tu kama ya CCM hata ukabadirisha mitaala ya elimu nk hapatakua na mafanikio kwa nchi. Hata kila mmoja wetu angesoma sana kilimo, uvuvu, useremala, nk lakini bila kua na serikali inayoweza kuwawezesha watu na kuunganisha nguvu ya kila mmoja wetu kua kitu kimoja basi hamna chochote. Wizara ama waziri mmoja hata angekua na maamuzi mazuri sana lakini kama bado yupo chini ya serikali fisadi basi hamna kitu maana boss wake (serikali) ndio ana uamuzi wa mwisho. Tatizo la TZ si wizara, bali ni serikali inayoundwa na RAISI mwenye nguvu nyingi zisizopingwa na yeyote ambazo ndizo zinazomsababishia kutowajibika na kulewa madaraka.
Halafu CCM imefanikiwa sana kutupumbaza hata tumekua hatuoni wala hatusikii fukifikiri CCM ndio jibu tu tukidhani wizara ndio zinaturudisha nyuma, ati JK anaangushwa na mawaziri wake wenye maamuzi mabaya - si kweli. Halafu wengine wanadai haowaoni hata mwingine awezaye tawala zaidi ya CCM, baada ya miaka 50 ya uhuru wanaona kwa namna moja ama nyingine chini ya CCM lazima mambo yatakua murua tu.
 
Mfumo wettu umekuwa ni wa kutudumaza zaidi. Ukiangalia hata zile shule zilizokuwa zikifanya masomo kwa vitendo leo hii hakuna kabisa. Shule zile zilijengwa zikiwa na miundombinu ya machinery, bustani za kilimo, mifugo, zote zimefutwa kama si kubadilishwa. SASA NI NADHARIA FULL TIME, sisi tunaandaliwa si kuwa wabunifu, ila kuwa waajiriwa "VIMBAYUWAYU"
 
Jamani leo tupo katika "UKOLONI MAMBO LEO" wa wazi kabisa, waliobaki kufundishwa na kuwa viongozi ni ujanja ujanja tu! Lakini kwa hii elimu ya kikanda au kiwilaya mimi siungi mkono maana tutakuwa tunawafix watanzania katika kitu kimoja. Isipokuwa mitaala iwe moderated kama enzi za mwalimu, kuwa mtu nasoma mwanza, kigoma, songea na kazi nafanya popote pale. kwa kuapply ujuzi na miujanja kutoka kwa walimu wenye moyo na ari na kazi siyo waliokata tamaa kama ilivyo sasa.
 
Mie ningependa kuwa desicion maker kwa upade ushirika na masoko! Hii ni nyanja inayoomuunganisha mkulima wa Tanzania na soko la bidhaa zake za kilimo; kumekuwa uzembe mkubwa wa usimamiajai wa eneo hili na kwa mara nyingi udanganyifu umetumika pia kumwibia mkulima masikini pato alke ogo aliloambulia kupata na wakati sehemu nyingine baadhi ya mazao yameharibika kwa kushindwa kufika sokoni kabisa. Kwanza itakuwa ni kuimarisha kitengo kizima kinachoratibu taarifa ili zipatikane kwa wakati na kufikishwa kwa wakulima; kuandaa minada huru kama ule mnada wa chai kule kenya na mazao mengine amabapo wakulima ama wao binafsua ama vyama vyao huru vitawasaidia kupata be nzuri ya mazao na wakati huohuo kuweka na kusimamia sheria zinazowalinda wakulima wadogo pia kushinikiza idara ama wiza husika ya mawasiliano kuhudumia kwa dhati na makusudia njia kuu za mazao hapa nchini kwa kiwango cha kuridhisha ili kuhakikisha usafirishaji unakuwa wauhakika lakini hii itategemea vile vile serikali iliyoko madarakani inao wajibu gani kwa waanchi wake!
 
Tom, Mtwa
ok nimewaelewa lakini mnaonaje mkichagua y decision making of position of your choice. Mnaweza kutueleza strategically mtafanya nini.Lengo langu haikuwa thread ilkuwa tufanye assumption sisi wanajamvi tuna cheo fulani sasa tuseme tutafanya nini. tutakosoana baadae.
 
Back
Top Bottom