Elections 2010 Changamoto kwa wagombea ubunge Dar 2010

Mrekebishaji

Senior Member
Mar 19, 2009
168
63

Ndugu zangu, si vibaya kama wadau wa maendeleo ukaanza kujadili kero mbalimbali za jiji letu la lukuvi.

Kwa ufupi ni kwamba kwa mtu kama mimi, naitwa mrekebishaji, najua kabisa siwezi kugombea ubunge 2010 ila najindaa mwaka 2015. Hodi Mbeya mjini au Ukonga. Hili halina mjadala nina haki ya kikatiba.

Wana JF. Naomba tuibue mjadala wa kero za hapa jijini halafu wanataka ubuge tusasaidie namna ya kuzitatua na watakapofika kwenye kampeni watueleza namna mabavyo wanaweza kutatua.


USAFIRI:
Hilo ni tatizo kubwa.Kana mengi yatokanayo na hilo. Wanafunzi wanachelewa shule na kurudi majumbani. Na pia hutia mwanya wa ma-denti kupitia ‘sehemu zao’ na wakichelewa kuzingizia usafiri. Wafanyakazi wanaotaka kujiendeleza kielimu muda wa jioni hukosa muda huo, , baadhi wamechelewa usaili na hivyo kuskosa kazi(japo hii ni kukusa u-serious wa kuwahi) na matatizo mengine mimi nimetaja baadhi tu.

SULUHISHO:
Ø Kwa kuwa reli tunazo, wakazi wa kitunda, gongo la mboto, ukonga, vingunguti, segerea, majumba sita, yombo na maeneo yaliyokaribu na reli ya kati na TAZARA wanachohitaji ni mabehewa machache tu kuwaleta mjini wakati wa asbh na jioni hii itapounguza foleni barabarani. Pia reli ya tabata mpaka UFI ieendeleze kupitia manzese, iende kinondoni mpaki masaka. Hawa watakaopisha uendelezaji wa reli wapate fidia, wajenge nje ya mji mna watakubali kwani hata wao kuja mjini haitakuwa taabu tena.
Ø TAZA, UBUNGO. MWENGE, TANDIKA vinanzishwe vituo vya parking. Gari ndogo zote ziishie maeneo haya. Halafu huku mjini gari za ‘public transport’ ndiyo ziruhusiwe tu, pamoja na za ofisi.Condition. MAGARI YA PUBLIC TRANSPORT yawe masafi nay awe na wahudumu walio wasafi.Hata sasa tujue kuwe wengi hutumia gari binafsi sababu ya usumbufu wa public transport.
Ø Manispaa ziwe na makatapila ambayo kila mwezi yatakuwa yanafanya ukarabati wa njia za panya. Hili linawezekana na lengo ni kuboresha njia ndogo.

USAFI WA JIJI.
Ø Hapa kwa kweli tumekosa utashi mdogo tu. Ni wape mfano, mimi nimekuwa nikiteseka sana.Kuna nchi nilipita, ukinywa maji au ukiwa na uchafu kidogo mkononi, utakuta kuna waste bin au dust bin nyingi na unatupa uchafu wako. Lakini hapa kwetu, unaweza kutoka mwenge mpaka mbagala usikute sehemu ya kutupa taka(hizo ni barabara) ingia mitaani, mambo ni mabaya zaidi. Sasa tunalaumi vipi watu kutupa taka ovyo.
Ø Huduma za vyoo. Unakuta sehemu imeandikwa usikojoe na hakika ndio ina mazingira yote ya kuhamasisha kukojoa hata kunya. Suluhisho ni kuweka vyoo vingi, maeneo mbalimbali tena bure. Uendeshaji wa huduma hizi si gharama.Kwani hakuna ambaye atakojoa hpovyo kama pembeni tu kuna huduma ya choo. Hata hivyo, wale wachache, watahitaji elimu na adhabu kali kama watachafua maeneo mengine wakati huduma zipo bure tena maendeo hayo hayo.

Kwa leo naishia hapa. Lazima nitumie muda mwingine kwa ajili ya mwaajiri wangu. Unajua tena lazima niwe mchapakazi ili nitekutumia vizuri hata haki yangu ya kuomba ridhaa ya wananchi mwaka 2015 ktk majimbo ambayo nimeyasema.

Wana JF jimwageni kwa kero zingine na hata ku-challengi za kwangu, Wote ni jukumun letu.
 
Back
Top Bottom