Mtanzania umesema kweli na ninaamini kuna mambo machache ambayo mwandishi asiyachukulie at face value au kuyakubali tu. Kwa mfano Rais aliposema "watu hawali mapanki" au pale aliposema "BAE ni kampuni ya Serikali ya Uingereza" waandishi hawana budi kuangalia kauli hizo na kuhakikisha ukweli wake. Mtu anaposema fulani ni mwanachama wa chama fulani ni bora uhakikishe anachosema ni sahihi. Nakubaliana na wewe 100% kwamba ni jukumu la wale wanaoandika habari au maoni to be as accurate as humanly possible especially ambapo ni rahisi kuverify certain information.
Nina tatizo hata hivyo na mahitimisho yako kadhaa.
Kudai kuwa habari nzima ni uongo mtupu nafikiri ni exaggeration of the first order. Nadhani umeweza kuonesha ni yapi ambayo factually are just simply wrong. Hayo yanayohusiana na facts ni rahisi kuyaweka sawa. Kama hili:
Nadhani hapa itakuwa ni maneno yako against maneno yao; kwanini tuamini kuwa vita hivyo havipo? aidha kwa sababu havipo au kwa vile umesema havipo?
Hapa inabidi watu waamini "sources" zako ambazo ni unnamed na hatujui zina maslahi gani katika pande zinazohusika. How balanced are you sources? Maana hilo gazeti na wenyewe wanasema wana "sources" zao hapo hapo Mbeya. Kwanini sources zako ziaminike zaidi ya sources zao?
Hili nadhani ni kweli kabisa; lakini it is the nature of the beast. Siasa ni moves, counter moves na moves na anti-moves! Jinsi gani waandishi wanashikiri katika michezo hii ya kisiasa? Nadhani ni sehemu yenyewe ya siasa. Kuna uhusiano wa ajabu sana kati ya vyombo vya habari na wanasiasa siyo Tanzania tu bali dunia nzima.
Wenzako wanasema kipo, wewe unasema hakipo. Mmoja wenu hayuko sahihi. Ni nani? time only will tell. Umesema Prof. hana mpango wa kugombea you might be very right, lakini ukweli wa kauli hiyo utaonekana 2010, kabla ya hapo ni jambo la probability tu. Sasa akigombea 2010 unaweza ukasema in 2008 hakuwa na mpango huo..
Of course, siasa ndivyo ilivyo. Labda kuna mambo hayapaswi kuwa hivyo (in a perfect world where personal interests are not at play) lakini katika ulimwengu ambao maslahi, matamanio, chuki, hasira, kinyongo, ushabiki, mapenzi nk vipo, utakutana na watu wa namna hiyo.
Don't be too harsh.
Kwa yeyote anayeijua Mbeya vizuri anajua hilo.
Nakubaliana na wewe; nilichoshtuka ni wewe kusema kuwa habari nzima ni "uwongo mtupu" wakati ndani yake kuna mambo ambayo (using your own words) "Ukweli ulioko kwenye hiyo makala ni ule ambao tayari tunaujua.."
Kama kuna chembe ya ukweli katika makala hiyo then makala nzima haiwezi kuwa uongo "mtupu" isipokuwa ni uongo kwa maana ya factually wrong si kwa maana ya kulaghai.
Otherwise, nadhani kuna mitazamo miwili tofauti na sidhani kama "pseudo-obviousness" ya mambo ya Mbeya yana exclude madai yaliyotolewa kwenye makala hiyo.
Hivyo:
Nadhani wengine wanaoijua Mbeya vizuri wanaweza kuwa wanajua tofauti na hilo, nadhani ni mitazamo based on their own biases, experiences, prejudices etc.
Kwa hiyo mimi niko skeptical katika pande zote mbili, kwamba katika ulimwengu wa siasa, lolote lawezekana, only time will tell siwezi kupuuzia unayoyasema na yale waliyoyasema moja kwa moja.
Mwanakijiji,
Hayo magazeti hivi kweli hata editors wanafanya kazi wanazotakiwa kufanya?
Maana kwa gazeti lililokuja na nguvu na lenye waandishi wengi wa maan kama Raiamwema, sikutegemea kosa la msingi kama hilo la kwamba Dr. Mwakyembe ni mjumbe wa NEC liweze kupita.
Makala ya habari kuitwa ni ya uongo sio lazima kila kitu kiwe uongo. Kama ni mahakamani, kwa kukosea mambo madogo kama hayo, tayari kila kitu kinatupwa.
Hata yale magazeti ya udaku, yanakuwa na ukweli angalau 10%, utaamini vipi habari ya mwandishi ambaye anashindwa kuchek info muhimu kama hiyo? Angeweza kuingia kwenye mtandao na kujua Mwakyembe sio mjumbe wa NEC.
Mimi sioni sababu ya kui-discount moja kwa moja habari hiyo na kusema kuwa ni uongo kwa nguvu tu ya hoja za Mtanzania ambaye na yeye anategemea habari za kuambiwa, tena kwa kutokea mbali.
hata kama ni ndugu ndio vyanzo vya kuwa na uhakika wa habari kiasi hicho, bado kuna sababu za kusita kuamini kuwa ukweli wote unasemwa hapa.
- Mtanzania, ni kweli Mwakyembe alitakiwa na mwenyekiti wa mkoa asishiriki mapokezi ya kumpongeza?
- Ni kweli Mwakyembe alienda kwenye mapokezi hayo kinyume na mapendekezo au ushauri wa Mwenyekiti wake wa Mkoa?
- Ni kweli alisema kwenye mkutano kuwa alishauriwa asitokee na hivyo kufanya ushauri wa siri kuwa hadharani?
Lakini nani amfunge paka kengere wakati safu ya uongozi imejaa watu wenye uchafu?
I will side with Mtanzania on one thing, Raiamwema ingawa ni very credible, wana uzembe fulani wa wahariri kupitia habario kabla ya habari kuchapwa.
...........What is Kengere? I have never heard of such a word in Kiswahili!...........
Kurudia swala aliloleta Kuhani hapo nyuma.
Je wanasahihisha?
Maana hata NYT, IHT na WSJ kila siku wanafanya makosa, jamaa wanasahihisha hata kama wakikosea middle initial ya mtu!
Sawa sawa nimekupata Mtanzania.
- Ni kweli kuwa viongozi wa dini waliingilia kati jaribio la kwanza la kuwatuhumu kina Mwandosya na Mwakyembe kwa madai hawakupewa nafasi ya kujitetea kwenye kikao cha Februari?
- Ni kweli kwamba baadhi ya watu wakimuona Dr. Mwandosya mitaani wanamuita "Rais"?
- Ni kweli kwamba Dr. Mwakyembe anajua uwepo wa tuhuma hizo dhidi yake?
Hii habari hapa chini toka Raiamwema ni uwongo mtupu. Mwandishi ameshindwa hata kutambua jambo rahisi la kujua kwamba Dr. Mwakyembe sio mjumbe wa NEC ya CCM.
Acheni kuutumia mkoa wa Mbeya kuendeleza vita ambavyo havipo.
Sources zangu zote za huko Mbeya zinaonyesha hakuna kitu kama hicho. Baadhi ya waandishi wa habari wana sababu zao za kutaka kuona ugomvi huu unaendelea kwa cost ya wananchi wa Mbeya.
Hakuna kikao cha kuwajadili Mwandosya na Mwakyembe na wala Prof. hana mpango wa kugombea urais mwaka 2010.
Inaelekea kuna watu wanakuza hayo maneno kwa faida zao binafsi.