Changa la Macho.....

Spear_

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,603
486
Serikali ya Tanzania kupitia waziri wa mambo ya nje imewaambia Waingereza waharakishe malipo ya fidia ya Paund Milioni 29 kwani wanataka kununua navyo vitabu na madawati......

alisema hivi.....

“Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900’

Hivi ni Tanzania ninayoijua mimi au nyingine??? mbona tuna vyanzo vingi vya hela...(madini, Kilimanjaro,Ngorongoro, serengeti,mikumi, misitu na bandari) lakini watoto wanakaa chini mashuleni???

Hili sio changa la macho??

Cha ajabu ni wao haohao ndio walizitoa huko kwa kupokea 10%. Serikali ya Uingereza imezifichua na kuwaambia mwizi mmojawapo ni Chenge, badala ya kumkamata Chenge wanajitahidi kumsafisha... kama wanayosema ni kweli si waanze na vijisent vya AC?
 
kwani hizo hela zikija kuna hata mbao mmoja utanunuliwa?? achilia mbali dawati......
 
...Kanishangaza sana huyu waziri wa mambop ya kigeni huyu MEMBE, eti anagonga meza kujidai anauchungu na hizo pesa wakati wao wenyewe walikwiba, kweli bongo zaidi ya uijuavyo!
 
BAE wanaigopa serikali ya Tanzania kama ukoma, kwani ni wao waliowashawishi waingie kwenye deal hiyo na leo tena wanataka fedha hio eti watumie kwa mahitaji aliyotoa Membe nao wameshituka wanaona ni bora wawape watu wengine kuliko mtu aliyekuingiza mkenge kisha anatia msafi.
 
Serikali ya Tanzania kupitia waziri wa mambo ya nje imewaambia Waingereza waharakishe malipo ya fidia ya Paund Milioni 29 kwani wanataka kununua navyo vitabu na madawati......

alisema hivi.....

"Serikali ya Tanzania ilikusudia kutumia fedha hizo kununua jumla ya vitabu milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaala 192,000 kwa ajili ya masomo 12 katiak shule 16,000, kununua madawati 200,000 kwenye shule zilizo na upungufu wa madawati na kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini, kujenga vyoo 2,900'

Hivi ni Tanzania ninayoijua mimi au nyingine??? mbona tuna vyanzo vingi vya hela...(madini, Kilimanjaro,Ngorongoro, serengeti,mikumi, misitu na bandari) lakini watoto wanakaa chini mashuleni???

Hili sio changa la macho??

Hii pesa haitafika kokote,wanafunzi kwa maelfu bado wanakaa chini hata hapa mjini!halafu serikali hii inalazimisha wazazi wachangie madawati,hivi kodi hazilipwi?na kwanini watoto wakae chini?inatia kichefuchefu!hatuna serikali ni kichaka cha wanyang'anyi
 
Wezi ndiyo warudishiwe MZIGO TENA??? Heri wapitishie huko kwenye Taasis zisizo za kiserikali kuna kitakachofika kwa MWANANCHI MLALAHOI..Zikirudi mkononi mwa SIRIKALI zitatufunwa tena kama kawa tuuu!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom