Mkali Tozz
JF-Expert Member
- Aug 9, 2012
- 278
- 80
Mkuu Dr. (Ph.D) Kupeng'e,
Kwenye utendaji wa mahakama kuna kitu kinaitwa "jurisdiction" ambayo ni mamlaka ya kisheria ya mahakaka kusikiliza mashauri. Hii "jurisdiction imegawanyika sehemu mbili ambazo ni " pecuniary jurisdiction" inayohusisha uwezo wa mahakama fulani kusikiliza shauri lisilo zidi kiwango fulani cha fedha, mfan mahakama ya mwanzo mwisho wa uwezo wake ni kesi za lets say chini ya laki 500,000 hivyo shauri likisha zidi hapo, mahakama hiyo inakuwa haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo hivyo linahamishiwa mahakama ya juu inayoitwa "the court of competent jurisdiction".
Jurisdiction ya pili ni "teritorial jurisdiction" yaani ni mipaka ya mamlaka ya kisheria katika eneo husika. Hii ni inamaanisha mahakama ya eneo fulani haina uwezo wa kisheria kusikiliza shauri la nje ya eneo husika. Mfano tukio likitokea Arusha kesi inafunguliwa eneo la tukio na kuendeshewa kwenye mahakama yenye mamlaka husika ya eneo hilo.
Ingawa Mahakama Kuu inaitwa ni Mahakama yenye "inherent jurisdiction" ikimaanisha haina mipaka yoyote kwa kiwango chochote na mahali popote, lakini sidhani kama inaweza kuhamisha kesi toka Kanda moja ya Mahakama Kuu hadi kanda nyingine!.
Kuna kitu kinaitwa "public interest" kama mahakama inajiridhisha kuwa kama shauri fulani likisikilizwa eneo fulani linaweza kupelekea haki isitendeke au ku hatarisha amani kufuatia public interest, then mahakama inaweza kuihamishia kesi hiyo mahakama nyingine yoyote yenye "competent jurisdiction".
Kama authorities wa Arusha wameiandikia mahakama kuthibitisha kuwa siku ya hukumu ya kesi ya Lema jiji la Arusha linakosa amani kutokana na mashabiki wa Lema, hivyo uamuzi wa mahakama unaweza ku spark public outcry hivyo kuhatarisha amani, kesi inaweza kuhamishwa!.
Kama wanaamisha kwasababu ya kuhofia uvurugikaji wa amani, ni wazi hukumu inajulikana kuwa Lema atashindwa! hata kabla ya kusikilizwa pande zote! Lema hana chake,ndomaana wanahofia kuvurugika amani!