CHAN Finals: Live from Ivory Coast

Mkuu Tiba ukisha click kwenye hiyo link unaweza ukaenda moja kwa moja kwenye hiyo channel au inaweza ikaja page yenye orodha ya nchi pamoja na idadi ya channels ambazo zipo kwenye hizo nchi (hii ipo upande wa kushoto) ,so wewe itafute senegal then click itakuja hiyo channel kwani ipo hiyo tu. Ukitaka kuingia kwenye hiyo channel click kwenye jina lake(RTS1) then utaipata .Kama bado huipati nadhani kuna tatizo lingine. enjoy!!
 
Bado wantambikia na ngoma zao sijui wanasubiri nini kuanza kuonesha timu zinavopiga njaramba...
 
Aisee mbona wanatuzengua na sumo zao za mchangani hawa?!?!?
Hivi ni kweli watatuonyesha mtanange au wanataka tuone vioja vyao tu?!?
 
Asanteni wadau, nipe hapa najipatia game hiyo. Mungu Ibariki Tanzania. I hope they can prove Mzee Ruksa this time!
 
Aisee jamaa walitaka kunifurahisha, naona English na French ziliingiliana, nikajua watatangaza kikwetu du
 
Damn our players are short LOL!

Lets go TZ!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Diego alikuwa mdogo vilevile, lakini alikuwa najua nini cha kufanya.....
Eeeehh Kidedea.....!!!!
 
Forward yetu haijatulia... Stars wanaonekana kuwa imara mpaka dakika hii ya nne. Bado mapema lakini
 
Uzuri tunachezea soka nusu yao....vijana wanatakiwa watulie......wetu hawa...
 
TANZANIA Line Up
18-MOHAMED SHABAN DIHILE, 2-SWEDI SALUM, 3-SHABAN HARUNA MOSHI, 6-SHINDIKA HENRY JOSEPH, 8-NGASA MRISHO, 9-NAMWANDU GEOFREY BONNY, 10-TEGETE JERSON, 13-ALI NADIR HAROUB, 14-SHADRACK NSAJIGWA, 16-KHALFAN NIZAR, 21-JABU JUMA
 
Jamani ni mimi tu au? mbona ngoma imekatika?
Mi naipata kupitia TBC1 kwa njia ngumu lakini. Wamepitia DSTV kisha nimewanyaka kienyeji tuu...


Dakika ya 11 bado mabao ni 0 kwa Tanzania na 0 kwa Senegal.

TBC1 walichochemsha kikubwa ni kukatika kwa matangazo ya kiswahili na kuingia ya kiingereza ghafla.

Mbaya nyingine ni wao kuonesha configurations kwa clients wakti haikutakiwa kabisa.
 
Back
Top Bottom