CHAMI: Ekelege na Joyce wameniponza

Huyu jamaa ni buege wa kutupa..Watafuata wapi? Kwa kauli ya jana JK amesema 'kwa misingi ya sasa', thats means from now on (from yesterday- 4 May 2012) ndio watafuata, manake kwamba dhambi ya kabla ya hapo zimesamehewa!

Wacha upunguwani, ktia maana zisizokuwepo na kujijaza ujinga.
 
duh Chami hilo ni kielelezo tosha, kwamba ukubwa wa miaka sio usmart! mbona Nyalandu amekiruka kigunzi kwa kutoa ushauri wa kimaandishi kwa mujibu wa taratibu wa kazi yake.Ulipotoka kubali tu!
 
alifeli kwenye familia(ndoa kuvunjika)

umefeli siasa(uwaziri ikifuatiwa na ubunge 2015)
 
kama kuna kitu alichosema Rais juzi cha maana ni kua watakaowajibishwa sio mawaziri tu bali na wakurugenzi na watendaji wengine wa wizarani na mashirika ya umma safi sana.

Mheshimiwa Rais naomba uanze na bodi ya dawasco, ipigwe yote chini ianze upya... bosi wa tbs aondoke na achunguzwe mali zake pamoja na huyo katibu wa hiyo wizara ya viwanda...kila mtu aliyetajwa kwenye ile report ya cag apigwe chini hakuna msamaha.
 
Tired and hence retired. If you are an entrepreneur you will understand how user unfriendly this ministry is!
 
Rais Ekelege karuhusu condom zisizo na viwango na watu wanakufa hovyo sasa,tafadhali ashughulikiwe
 
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.

Hakika,kwa hili,Chami ameonewa!
 
Wakubwa mimi mtazamo wangu naona kama Maawaziri wengi ni wahanga wa mfumo mbaya wa utawala ambao tunao Tanzania.Mamlaka karibu yote ya utawala yako kwa raisi wa nchi ambae amehodhi nguvu zote.Waziri na hata waziri mkuu hawana mamlaka yoyote ya kuwawajibisha Wakurugenzi wa mashirika,wizara,au makatibu wakuu,ambao ndio hasa madudu yanapofanyika.Kinachofanyika ni kwamba waziri/waziri mkuu anatoa ushauri tu kwamba fulani hafai utendaji wake.Mimi nafikiri lawama zote za wizi huu apelekewe mkuu mwenyewe maana yeye ndio aliowachagua hao wahuni wezi wa mali zetu na ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuwawajibisha.

Mimi siamini kama Ekelege na timu yake wamefanya madudu yote hayo kwa muda mrefu bila usalama wa magamba kumfikishia taarifa mkuu,isipokuwa tu aliona uzito kuwatoa maswahibu wake.

Tusiridhike na kubadilishiwa sura za mawaziri bali kinachotakiwa ni kupambana katika marekebisho ya katiba mpya kujenga mfumo mzuri wa uwajibikaji ambao nguvu ya utawala itatawanyika badala ya kubaki kwa mtu mmoja tu.
Tujenge mfumo ambao Waziri mkuu kama mtu anaesulubiwa kwa utendaji wa serikali bungeni apewe uwezo wa kuhire and fire watu wa timu yake.Hii itampa nguvu ya kweli ya usimamizi wa shughuli za serikali.
Na mawaziri nao wajengewe uwezo wa kuondoka na shingo za watendaji walio kwenye wizara zao.Isiwe mtu mwingine achague watu waajabu na wala hamuwezi kumuhoji kawateua kwa kigezo kipi halafu madudu yao wakifanya wanaowajibishwa mawaziri ambao pengine toka siku ya kwanza hawajaridhika na utendaji wao.

Uthman,

..mfumo wetu hauna matatizo.

..mbona CM Msuya alipokuwa waziri mkuu alipendekeza Mrema afukuzwe kazi baada ya Mrema kuishambulia serikali bungeni??

..Augustino Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani naye alipendekeza Silvano Adel[katibu mkuu mambo ya ndani] na Tryphon Maji[rpc dar] wafukuzwe kazi na Mzee Mwinyi akakubali ushauri wa Waziri.

..viongozi tuliowachagua wameshindwa kazi sasa wanakimbilia kusingizia wanakwazwa na mfumo uliopo.
 
Mkuu lazima tukubaliane kwamba kuna wakati mawaziri ambao ni wanasiasa huwa wanawajibika kisiasa na si kwamba wameshiriki moja kwa moja kwenye uwivi ama ubadhirifu.

Katika wizara mtu ambaye ni Afsa Uhasibu (Accounting Officer) ni Katibu Mkuu akisaidiwa na wakurugenzi. Kwa hiyo kwa mambo yote ya kitaalamu kuanzia fedha hadi utendaji KM ndiye mwajibikaji.

Jana JK amesema vyema. Kama kwa mfano Bodi za Mashirika yaliyo huru zikichukuliwa hatua tutaanza kuona uwajibikaji kwa kuwa hakuna wajumbe wa boadi watakao kubali kuwa rubber stamps kama ilivyo sasa.

what is this thing Kuwajibika kisiasa?....kutokana na maelezo yako it sounds like si sahihi kwa Waziri kuwajibika kwa kwa matatizo ya kiutendaji yatakayotokea katika wizara yake kwa sababu si accounting officer!! i thought waziri ana jukumu la ku-lead ministry husika...pls naomba kufahamu role ya waziri katika wizara ni nini hasa?
 
Unajua baada ya watu wengi ku'ipindisha' hiyo kauli ya mkuu, nikaanza kuquestion uelewa wangu. Coz nilielewa kuwa next time, wengi watahusika; na kwa mtazamo wangu that was very weak of him. Why next time why not now, wakati sheria inaruhusu.

Na kingine ni swala la kutuhumu kuwa watu wengine wanapika majungu/fitina; yaani pale ndipo aliponichefua zaidi. Yaani kinachomuuma mkuu ni hao maswahiba wake kupikiwa majungu na wala si pesa za walipa kodi watanzania ambao kubahatisha milo miwili kwa siku ni heavens kwao zinavyotafunwa. Honestly huyu baba ananichefua!!!!!!!!

Very well said! Nashangaa wanao-refer maneno ya raisi kama ni busara. Afterall anachosema raisi sicho anachokitenda. Personally na-prefer anyamazage kimya kuliko ku-comment chochote.
 
Anyamaze wakati anaonewa?
Very well said! Nashangaa wanao-refer maneno ya raisi kama ni busara. Afterall anachosema raisi sicho anachokitenda. Personally na-prefer anyamazage kimya kuliko ku-comment chochote.
 
Mkuu lazima tukubaliane kwamba kuna wakati mawaziri ambao ni wanasiasa huwa wanawajibika kisiasa na si kwamba wameshiriki moja kwa moja kwenye uwivi ama ubadhirifu.

Katika Wizara mtu ambaye ni Afsa Uhasibu (Accounting Officer) ni Katibu Mkuu akisaidiwa na wakurugenzi. Kwa hiyo kwa mambo yote ya kitaalamu kuanzia fedha hadi utendaji KM ndiye mwajibikaji.

Jana JK amesema vyema. Kama kwa mfano Bodi za Mashirika yaliyo huru zikichukuliwa hatua tutaanza kuona uwajibikaji kwa kuwa hakuna wajumbe wa boadi watakao kubali kuwa rubber stamps kama ilivyo sasa.

Aanze na bodi ya PPF maana ni takataka, DG ndiye mwenye maamuzi, bodi hukaa kama mazuzu tu
 
Wana JF baada ya badiliko la mawaziri lililopelekea aliyekuwa waziri wa viwanda na Biashara ndg Cyril Chami kutemwa,imedhihirika ripoti zote za CAG hazimtaji moja kwa moja ila ni Ekelege(mkurugenzi mkuu TBS na katibu mkuu wake bi Joyce Mapunjo ambao wamekuwa wakila dili
"Kilichoniponza ni kutoipitia taarifa ya CAG na kutoa mapendekezo kama waziri,pia nilimuamini sana katibu mkuu ambaye yeye na wenzake walinigeuka na kuanza kuwa makuwadi wa kampuni feki za ukaguzi ambazo ni zao wenyewe tena hewa..
Nimegundua kosa langu la kumtetea Mkurugenzi wa TBS na kampuni zao.
Najua kama alivyosema rais na wao wataniafuata"
Mwisho wa kunukuu.
Hizi habari toka kwa Mtumishi wa ofisi yake ambae walikuwa nae jana usiku wakisikitika.

Kumbuka nilikuandikia email nyingi sana chami , lakini ukanipuuza,
Je unamkumbuka mjumbe mwenye hasira kali sana wa kule kwa mjengwa? Ndio mimi, nilikutumia email kukutaarifu kuhusu huu ushenzi wa TBS ukaniona mpumbavu. sasa unasikitika nini?
hizi dili za kijinga za akina Ekelege nina uhakika hakuna hata senti umepatiwa kwa sababu ni vidili mbuzi sana lakini ukawakingia kifua na kusema tunamuonea. sasa umepoteza kitumbua chako kwa sababu ya kutetea ujinga
 
Kumbe ulimuonya? Ngoja ile kwake

hivi raisi hua anaangalia vigezo gani kumteua waziri?sasa kama huyu si vioja!?badala ya kushughulikia mambo mwenyewe anawaamini walio chini yake yeye kazi yake ni kupokea mshahara tu!what a shame?afu bado anabwabwaja its better akae kimya..
 
Back
Top Bottom