Chama Kipya (CCJ) na Hatima ya CCM - lisemwalo...

Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.
 
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.

Mbona mkuu MMKJ umeanza kuchoka hata kabla ya safari yenyewe kuanza kwani ulipochungulia katiba yao umeona nini ndani au wametoa photocopy tu katiba ya CCM nini tuambizane mapema wote ni wadau.

If CCJ is nothing then the rest will be something, It means that if CCJ is the same those mafisadis we shall then support the rest part of CCM and vice versa, what people need is the split of the giant CCM party.
 
Kwa vile CCJ kinaanzishwa kisirisiri, nitakubaliana nacho tu nikishajua tofauti baina yake na CCM
 
USHAURI KWA CHAMA CHA JAMII (CCJ)​

HODI:
Mniwie radhi, naingia pasi hodi ya hishma maana nimesikia Tabibu yule ajaye anatembelea leo maskani haya.
Nimekuwa nasumbuliwa na radhi la kujitakia linalotibika tangu 2007, natamani hata nishike tu upinde wa kanzu ya Tabibu -CCJ. Nimenyanyasika, nimehuzunika, nimeahibishwa kwa muda mrefu nikatamani kumwona atakayeniokoa kutoka katika hili gonjwa ili nirejee siha yangu.

Jamani kwa wale tunaoamini kuwa ujio wa CCJ utaleta matumaini mapya na ukombozi wa kweli basi tunaweza kutoa ushauri uliokwenda shule nini kifanyike kimkakati ili

tuone mabadiliko ya kweli ya kumkomboa mtanzania.

MATUMAINI:
Niwatoe wasiwasi watu wanaofikiri kuwa pengine msajiri hawezi kutoa usajiri kamili au sijui CCM kamwe haiwezi kuondoka madarakani au sijui watu hawawezi kumeguka mpaka wapate pension au sijui CCM ikisigana basi kutakuwa na mtafaruku nchini na kuhatarisha amani.
Kinyume cha hayo yote yanawezekana na nchi yetu itapiga hatua kubwa kimaendeleo kiuchumi na kijamii!

Nguvu na Amani ya Serikali duniani, viko mikononi mwa JAMII (WANANCHI) period!
Si msajiri, wala Kamati Kuu ya CCM, wala fedha za Pension. Hata UWT, Majeshi yote, Mahakama na Bunge ni vyombo tu vinavyotekeleza matakwa ya JAMII. Ukiona vyombo hivyo vinaungana na kundi dogo kunyanyasa JAMII ujue kuwa JAMII hawajavinyesha waziwazi msimamo wao period!

Chukua sekunde kufikiri mifano miwili ya karibu kabisa na pengine katika mazingira yanayoshabihiana zaidi kijiographia na kijamii.

Ni nani hapa kwetu tunaweza kumlinganisha ubabe wake na ulivyokuwa wa mwanasiasa mzamivu mzee jirani yetu Daniel Toroitich Arap Moi (NYAYO). Je unaweza kulinganisha ukubwa na athari za ubadhilifu wowote wa hapa na na skandali zilizomuhusisha NYAYO na maswahiba wake kama vile Goldenberg scandal ambayo imeligharimu Taifa la Kenya zaidi ya 10% ya GDP yao na madudu mengi yasiyoorodhesheka hasi jamii ya kimataifa kuwapiga stop kupata visa na kusafiri kwenda mfano Uk. Mbona hayo ya BOT ni cha mtoto?

Je ni akina nani kwetu unaweza kuwalinganisha na matajiri kufuru na wenye mitandao ya chuma kama akina Ali Nasir, Kamlesh Pattin, Nic Biwott, waliokuwa tayari kufanya lolote kuziba kelele ya chura yeyote. Mbona hizo shule za akina Mh. Mkono sijui Chief Ihunyo ni Servant Quarters za ma-Sekondari, ma-Vyuo ya ufundi (Polytechnic), ma-Hospitali, Vituo vya Afya vingi sana alivyojenga Biwott na wa namna yake?

Mbona utajiri wa Rostam ni sawa na stock tu katika mizania ya hesabu za watu kama akina Sir, Charles Njonjo? Leave alone akina Kamlesh Pattin nk.

Watu wanalia na vimajengo sijui huko Pwani n.k hivi nani amefika katika kijiji cha Moi huko Kabarak akashuhudia matusi. Ninyi mnalia na wanaojengewa swimming pools, watu huko walikuwa waona kawaida mtu anajengewa kiwanja cha ndege katika makao yake si ya Serikali!?

Ni wapi hapa kwetu kuna suruba za kubinywa sawasawa kwa stahili za ‘tocha’ za Nairobi Nyayo House na Nyati House? Pamoja na hayo yote mzee NYAYO aliponyanyua rungu lake tu juu katika halaiki, watu walikenua meno NYAYO! huku waki-bleed internally!

Eti mnaogopa kuanzisha Chama kwamba mtanyimwa pensheni? Enzi za Moi kunyanyua tu vidole viwili (alama ya upinzani) ilikuwa unasema kuwa unakubali kuurekebisha uumbaji wa Mola kwa kutoa sadaka vodole hivyo vikatwe bila dawa ya ganzi. Eti tunapigia kelele Kijana wake kuwa UVCCM na sijui mwingine Chipukizi mbona hizo ni chekechea za siasa? Je hamjui kuwa Watoto wa Moi walifanywa kuwa Wabunge tena wenye sauti na wafanyabiashara maarufu sana?

Swali sasa; pamoja na mtandao mkali na rungu la dora na fedha leo yuko wapi Kenya? Amebaki kuwa mzee wa chama cha upinzani siyo chama tawala! Yaani hata wakimbiaji wa Marathoni toka Kenya wanaweza kuwa nacoverage kubwa katika vyombo vya habari kuliko huyo mzee ambaye ilikuwa hakuna habari bila kuanza na 'Mtukufu..

Au mkitaka mfano zaidi basi nipeni ulinganifu wa yeyoye hapa na ngunguri ya IDD Amin Dadaa. Je umaarufu na ubabe wake uliishia wapi; mbona hata mazishi ya kijana mwehu yeyote maskini wa kutupwa yanaheshimiwa na kukumbukwa kuliko yalivyokuwa ya huyu Nduli?

Ninacho jaribu kusema si kudharau mateso tunayopata au uongozi mbovu uliopo bali nasema pamoja na kuwepo MTANDAO tunaodhani kuwa una nguvu au UTABIRI FEKI wa kutishia nyau wa mzee YAHYA, JAMII tumeamua basi inatosha hao watabaki historia tu!

USHAURI:
Popote tulipo nawaita wale wote wanaojua kuwa wanasifa za uongozi bora na wasio na mawaa isipokuwa ya kupakaziwa kisiasa, kuhama na kujiunga na CCJ bila kusita. Msiogope chochote, mtakumbukwa katika kuleta mabadiliko chanya makubwa nchini mwetu kwa vizazi na vizazi.

Bila hofu nawaita wafuatao wainuke sasa na kutangaza waziwazi kuunga mkono CCJ na kutoka waliko ili kuleta ushindi.
Hawa ni waheshimiwa, S.Sita, Prof. Mwakyembe, Prof.Mwandosya, Dr. Silaa, Prof. Beregu, Magufuri,
Wengine ni Dr.Salim H. Salim, Prof. Lipumba, Lwakatare (Ex MP),Waryoba, Mama Mpiganaji (sote tunamfahamu), Dr. Shayo (Diaspora), Sanctus-Rais TPN, Kawawa (MP), Makongoro Nyerere, Dr. Chinuno (Ex DC), present RC Morogoro na timu yao ya wanahabari ikiwa na Jerry Muro, Michuzi, Kubenea na Mwanakijiji kama PR Officer.

Mkijitokeza tu tosha tutajiunga na chama mpaka mseme basi. Jamii ya Watanzania sasa imetamka kuwa imetosha na tunasema hatutalala hata kama ni kwa kuandamana kila kukicha mpaka hiki chama kisajiriwe kwa ukamilifu maana masharti yote yametimizwa.
Ni kutoka katika hao sita wa mwanzo hapo juu, mchakato mkali utafanyika kwa wazi kubakiza watu watatu tu na kupigiwa kura ya maoni nani agombee dhidi ya mtabiriwa wa mzee Yahya.

Wengine nawakaribisha pia kuchangia maoni yenu maana haya ni yangu.

Ni rahisi sana kumpata rais mwingine Tanzania 2010, kuliko mtu kufa kwa utabiri wa yahya!

Mwanachama wa CCJ
 
Lol, wengi uliowataja wamekaa serikalini muda mrefu bila tija. Iweje leo wawe wakombozi?

Ninaamini kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM lakini si kwa mtindo wa CCJ. CCJ imechelewa kuanzishwa na watu bado wanasubiri maslahi yao ndani ya CCM ili watoke. Hawana uzalendo wa Mrema Lyatonga. Watoke sasa .........

Bado nawapa nafasi kubwa Chadema kuliko CCJ.
 
waungane na kile cha wakaulima nacho kimeanzishwa hivi karibu, by the way hivi hakuna limit ya vyama vinatakiwa kufika ngapi? maana inaweza ikifika kila watanzania 200 wakawa na chama ati?
 
- Inaelekea vigogo wengi wakubwa hawamo hiki chama, kama niliyoyasikia ni kweli basi ni bora hawa CCJ wangejiunga na Chadema, ni ushauri wa bure tu!

- Nina wasi wasi, kuna vigogo ndani ya CCM, wanataka kukitumia hiki chama kipya kama cover ya mambo yao, ni mawazo yangu tu!

Respect.

FMEs!
 
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!

Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?
 
Bila hofu nawaita wafuatao wainuke sasa na kutangaza waziwazi kuunga mkono CCJ na kutoka waliko ili kuleta ushindi.
Hawa ni waheshimiwa, S.Sita, Prof. Mwakyembe, Prof.Mwandosya, Dr. Silaa, Prof. Beregu, Magufuri,
Wengine ni Dr.Salim H. Salim, Prof. Lipumba, Lwakatare (Ex MP),Waryoba, Mama Mpiganaji (sote tunamfahamu), Dr. Shayo (Diaspora), Sanctus-Rais TPN, Kawawa (MP), Makongoro Nyerere, Dr. Chinuno (Ex DC), present RC Morogoro na timu yao ya wanahabari ikiwa na Jerry Muro, Michuzi, Kubenea na Mwanakijiji kama PR Officer.

Ndugu shatora umetoa mawazo mazuri sana lakini mbona chama chenu kimekuja kwa kujificha, humu JF kuna viongozi wa vyama mbalimbali wanajitambulisha kwa majina yao halisi unaonaje na wewe ukifanya hivyo.

Kuhusu hayo majina uliyoyasema sita ya mwanzo ndio waanzilishi wa CCJ kama ni waanzilishi ni lini watajitokeza hadharani ili watueleze hasa nia yao, vile vile vipi swala la katiba yenu tunaomba utuwekee humu tuisome kabla ya kufanya maamuzi pamoja na hayo tunapongeza ujasiri wenu.
 
Kama Katiba yao ndivyo ilivyo, I can say with absolute confidence; CCJ is nothing but a disappointment in the making.

I second you.

Kusikia maoni kwamba upinzani wa kweli lazima utoke ndani ya CCM, wakakurupuka kuanzisha chama kipya.....I see nothing other than uchu wa madaraka! Hakina tija kwa ukombozi na maendeleo kwa watanzania.

Sorry CCJ folks.
 
- Inaelekea vigogo wengi wakubwa hawamo hiki chama, kama niliyoyasikia ni kweli basi ni bora hawa CCJ wangejiunga na Chadema, ni ushauri wa bure tu!

- Nina wasi wasi, kuna vigogo ndani ya CCM, wanataka kukitumia hiki chama kipya kama cover ya mambo yao, ni mawazo yangu tu!

Respect.

FMEs!

Hivi kama ni ya vigogo wanaogopa nini wanajificha nini? naona wako huru na wananchi wanahitaji huo mpasuko huko CCM..it will be great for Tanzania political framework

Huko kujificha ficha inaonyesha ni kelele tu za watu wenye kutaka nafasi...wanachofanya ni bullying of the sytem waonekane.
 
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!

Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?

- Kigogo mmoja ameniambia kwamba agenda yao ni kupinga ufisadi, sasa ninajiuliza maswali mazito kwamba kwa nini vigogo wengi wapinga ufisadi niliowagusa leo wote walikuwa wanashituka kuhusu hiki chama kwamba hawajui lolote!

- Halafu chama chenye nia njema na wanachi wote na hasa taifa, kwa nini kinakuwa na viongozi wanaojificha? Nimejaribu kuangalia historia ya siasa sijaona chama chochote duniani kilichowahi kuanizishwa kwa njia za siri za ajabu kama hiki, halafu kikaja kuwa mkombozi wa taifa, I mean hatuna all the facts, lakini nina wasi wasi sana kwamba something is not right na hiki chama kipya! Ingawa pia I could be wrong, lakini moja jumlisha moja, sioni jawabu likiwa mbili so far! kutokana na yote niliyoyasikia!

- Sijawahi kuona siri ya siasa inayolindwa kama ya hawa vigogo wa hiki chama kipya ambacho nia na madhumuni nimeambiwa ni kuondoa ufisadi, damn! wanaogopa nini kujitokeza tuwashangilie ili kutoa tumbo joto kwa mafisadi? Maana for sure sio chama cha kina Lowassa, wala Six, sasa cha nani? Something is not right!

Respect.

FMEs!
 
Naomba kujuzwa, inawezekana kuanzisha chama kipya ukiwa bado mwanachama wa chama kingine?

Ninachomaanisha hapa ni kwamba, hawa waanzilishi wa CCJ kama kweli ni miongoni mwa wanaCCM ni watu wanaotaka kuwa wanachama wa vyama viwili kwa wakati mmoja.

Kama sivyo basi ni ma-opportunist ambao wanataka kujaribu kwanza zali, likifeli waendelee kubaki CCM. Je watabaki kuwa wanachama waaminifu?
 
CCJ wenyewe naona wanatafuta popularity tu kujifanya ni chama kutokana na vigogo wa CCM, naona hakina tofauti na kile cha wakulima...kilichoanzishwa hivi karibuni..

CCJ naona hiyo strategy yao ya kupata public attention na kweli wameipata..damn..they think they are smart..
 
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine! Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?

Mwanakijiji kuna wapenzi na wanachama wengi wa CCM kama mimi ambao tunabakia ndani ya CCM kwa sababu ya Imani, Malengo na Madhumuni ya chama yametuingia mnoo na hakuna chama cha upinzani ambacho kinasimamia malengo na imani zinazofanana na CCM. HIvyo binafsi naamini kama kuna chama kinasimamia malengo, imani na madhumuni kama CCM na wanatofautiana kwenye kupiga vita Ufisadi kwa vitendo, basi nitakuwa wa kwanza kujiunga nacho.
 
mkuu.. you might be very right.. wakati mwingine ili kujua maji ya moto kiasi gani inabidi utumbukize mkono. CCJ ilivyo na itikadi yake haijatoa sababu ya kwanini inataka kuwa chama kipya! Karibu malengo, nia, madhumuni, muundo na mfano ni carbon copy ya CCM tofauti ni herufi tu "J" na "M".. wao wameelezea yale yale yaliyoelezewa na CCM kwa maneno mengine!

Labda ningependa kujua zaidi ni ajenda yao hasa ni nini?

Mkuu,

Angalia kwa makini kuwa chama kitachotekeleza sera za CCM bila kulinda mafisadi basi kitakuwa ni chama kizuri sana. Kwa jumla sera za CCM siyo mbaya kabisa labda sehemu chache chache za haopa na pale, ubaya wote wa CCM uko kwenye viongozi wake na jinsi wanavyotumia madaraka waliyokabidhiwa na umma.
 
Na Mwandishi wetu

TAARIFA za mchakato wa kusajili chama kipya, Chama Cha Jamii (CCJ) kinachoaminika kuhusisha makada wenye majina makubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikalini, zimewashtua na kuwatikisa vigogo kadhaa wa CCM, Tanzania Daima imebaini.
Tayari vigogo hao wameanza mkakati wa kukihujumu chama hicho kisipate usajili ili kisishiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Chanzo cha habari kimoja kimeliambia Tanzania Daima kuwa CCJ imeanza kuonekana kuwa tishio zaidi kwa CCM kwa kuwa kina vigogo 27 wa CCM ambao ni wabunge wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Bunge.
Baadhi ya vigogo wanaotishika ni wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi, kwa vile chama hicho kimetamba kwamba vita ya ufisadi ndiyo ajenda yake kuu, na hakitakuwa tayari kumpokea mwanachama yeyote mwenye tuhuma za ufisadi.
Moja ya sera kuu za CCJ ni kutetea na kulinda rasilimali za taifa ili zisitumiwe na watu wachache kwa manufaa yao.
Waanzilishi wa CCJ wanasemekana kuwa ni baadhi ya vigogo waliochoshwa na CCM, hasa kwa madai kuwa chama hicho tawala kinawafumbia macho baadhi ya makada wanaotuhumiwa kwa ufisadi kiasi cha kuyumbisha nchi na chama chenyewe, huku wananchi wakiendelea kuwa masikini.
Kuna orodha ya wabunge wanaodaiwa kuwa waanzilishi wa chama hicho ambao hawajaweka wazi majina yao, na wamewatanguliza wengine kwa sababu za kiusalama na kimkakati.
Zipo taarifa pia kwamba tayari vyombo vya usalama vimeanza kuifuatilia CCJ ili kubaini majina ya vigogo waliomo.
Taarifa nyingine zinasema baadhi ya vigogo wamekuwa na hofu na mustakbali wao ndani ya CCM hasa baada ya kuelezwa uanzishwaji wa CCJ umetokana na kile kinachoonekana ni udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, anayetuhumiwa kwa kushindwa kuchukua maamuzi magumu dhidi ya makada wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.
“Ndugu yangu kuna baadhi ya vigogo sasa wana wasiwasi kuwa chama kinaweza kuwatosa ili kinusurike na aibu ya kumeguka ambako bila shaka kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuja kwa CCJ,” kilisema chanzo kimojawapo.
Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa hatua hiyo ya baadhi ya wanachama wa CCM kuanzisha chama chao ni kitisho au shinikizo kwa Rais Kikwete, ili achukue hatua kali dhidi ya wanachama wanaokitia doa chama hicho tawala.
Shinikizo hilo linapata nguvu kutokana na dhana kwamba asipochukua hatua kali “chama kinaweza kufia mikononi mwake”, jambo ambalo asingependa kuhusishwa nalo.
“CCJ inaweza kuwa shinikizo la baadhi ya makada wa CCM kumshinikiza Mwenyekiti (Kikwete) kukisafisha chama kwa kuwaondoa wale wote wanaotuhumiwa katika kashfa mbalimbali,” kilisema chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutambulishwa gazetini.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa chama hicho kipya, Richard Kiyabo amesema ana uhakika wa kutimiza masharti ya usajili wa kudumu ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa ili waweze kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kiyabo alisema hayo kama majibu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa ambaye juzi aliliambia Tanzania Daima kuwa chama hicho hakitaweza kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa mchakato wa kukifanya kipate usajili wa kudumu utachukua muda mrefu.
Mwenyekiti huyo alisema hadi sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kupata wanachama 200 kwa mikoa 10 kama walivyoagizwa na msajili wa vyama vya siasa na kusisitiza kuwa watashiriki uchaguzi ujao.
Kwa kujiamini, mwenyekiti huyo alisema hadi sasa kwa Dar es Salaam peke yake tayari wamepata wanachama 2,000 watakaohudhuria siku ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu kwenye ofisi za msajili.
“Hili jambo kwamba hatutashiri kwenye uchaguzi ujao limewashtua sana wanachama wetu…tumepokea simu za kuulizwa kila wakati, ndiyo maana nikaenda kwa mmoja wa wanasheria wa ofisi ya msajili.
“Katika kufafanua jambo hilo, nimeambiwa hata kesho kama tunaweza tupeleke majina ya wanachama wetu 200 kila mkoa kwa mikoa nane ya Tanzania Bara na miwili ya Visiwani, si lazima miezi sita,” alisisitiza na kuongeza kwamba idadi hiyo ikishatimia kinachofanyika ni kukamilisha baadhi ya taratibu ndani ya chama.
Alisema CCJ imejizatiti kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao, na baadhi ya wanachama watagombea ubunge iwapo ofisi ya msajili itafanya bidii katika kupitia taarifa za wanachama wao.
Hata hivyo Kiyabo alikanusha taarifa za chama hicho kuasisiwa na baadhi ya vigogo wa CCM.
“Chama chetu kimekuja kufanya mapinduzi kwenye siasa za upinzani. CCJ haitakubali kuwapokea majeruhi wa ufisadi kutoka vyama vingine. Nakumbuka Mwalimu Nyerere aliwahi kusema upinzani wa kweli utatoka CCM. “Tumejizatiti kujenga jamii yenye usawa kwa kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wote…tutapigana vilivyo na ufisadi,” alisema.
 
Source???!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom