Chama kipi ni kizuri kwa CCM?

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
1995: NCCR Mageuzi ikiwa kileleni na kukubalika kwa wananchi....ccm walisema ni chama cha kikabila na
blah blah kibao....hadi hii leo NCCR haina mvuto tena.

2000-2005: CUF ikiwa ngangari bin jino kwa jino huku ikipendwa na wananchi...ccm wakasema ni chama
cha kidini (Uislaam) na blaah blaah kibao....mwishowe CUF wakaambiwa na ccm kuwa wafanye
siasa za kiustaarabu na CUF nao wakaingia mkenge na matokeo yake CUF inajifia taratibu.

2010- leo 2012: CHADEMA ikiwa inatikisa bungeni,mitaani,maofisini,mashuleni,mavyuoni' yaani ni full kupendwa na wananchi"....ccm wamekuja tena na this time wanasema hiki ni chama cha kikristo,ukanda na ukabila.

Sasa swali langu ni-: Hivi nyinyi CCM na wapambe wenu wote ni chama gani cha upinzani kitakuwa kizuri kwenu? Maana kila chama kinachoonyesha kukubalika kwa wananchi ni lazima mtakipaka propaganda zenye
sumu kali sana!. Nauliza tena, je ni chama gani cha upinzani ambacho kitakuwa kizuri kwenu?
 
1995: NCCR Mageuzi ikiwa kileleni na kukubalika kwa wananchi....ccm walisema ni chama cha kikabila na blah blah kibao....hadi hii leo NCCR haina mvuto tena.2000-2005: CUF ikiwa ngangari bin jino kwa jino huku ikipendwa na wananchi...ccm wakasema ni chama cha kidini (Uislaam) na blaah blaah kibao....mwishowe CUF wakaambiwa na ccm kuwa wafanye siasa za kiustaarabu na CUF nao wakaingia mkenge na matokeo yake CUF inajifia taratibu.2010- leo 2012: CHADEMA ikiwa inatikisa bungeni,mitaani,maofisini,mashuleni,mavyuoni' yaani ni full kupendwa na wananchi"....ccm wamekuja tena na this time wanasema hiki ni chama cha kikristo,ukanda na ukabila. Sasa swali langu ni-: Hivi nyinyi CCM na wapambe wenu wote ni chama gani cha upinzani kitakuwa kizuri kwenu? Maana kila chama kinachoonyesha kukubalika kwa wananchi ni lazima mtakipaka propaganda zenyesumu kali sana!. Nauliza tena, je ni chama gani cha upinzani ambacho kitakuwa kizuri kwenu?
Dawa ya kuondoa ujinga huu ni kuanika kile wasemacho kipo ktk vyama vingine lakini wao wanacho. Kwa mfano wakuu wa sensa kuwa ndugu wa mteuaji.
 
ADC nafikiri.....

Maana naona hata huyo mke wake (cuf) kawa kama toilet paper anatumiwa pale anapoitajika.
 
ADC nafikiri.....

Maana naona hata huyo mke wake (cuf) kawa kama toilet paper anatumiwa pale anapoitajika.
Mkuu, hata hiyo ADC ikijakuwa very strong utasikia nayo wanaipaka ***** wa propaganda
 
Kwani CCM ni chama ama genge la mafisadi? Hebu uliza swali lako vizuri kwanza?
 
Tangu mwaka 1961 - 2015 Tanzania imeongozwa na mawaziri wakuu 10 tangu uhuru. Mawaziri wakuu wawili tu kati ya hao 10 walikuwa waislamu - Rashid Kawawa (awamu ya 1961-1980) na Salim Ahamed Salim (awamu ya 1981-2015). Na mmoja tu katika hao alitoka Zanzibar. Sita katika hao 10 walitoka kaskazini (watatu mkoa mmoja - Arusha) - UDINI NA UKANDA BADO NDANI YA CCM HAUPO?
 
Uwiano wa kidini na kikanda uliopo ndani ya ccm uko sawa?. Angalia safu ya viongozi ktk kila wizara na taasisi za umma!.. Sasa wakristo kwa waislamu vitendeeni haki vyama vya CDM na CUF!..
 
Kwani CCM ni chama ama genge la mafisadi? Hebu uliza swali lako vizuri kwanza?
Mkuu, kitu gani ambacho ujaelewa hapo? Jamaa anauliza ni chama gani cha upinzani ambacho kitakuwa kizuri kwa ccm?
 
Kwa sasa hivi Chama kizuri kwa CCM ni CUF hii ni kutokana na kiapo chao cha ndoa waliyofunga huko Zanzibar kuwa watapendana daima milele mpaka pale kifo kitakapowatenganisha.
 
Kwa sasa hivi Chama kizuri kwa CCM ni CUF hii ni kutokana na kiapo chao cha ndoa waliyofunga huko Zanzibar kuwa watapendana daima milele mpaka pale kifo kitakapowatenganisha.
Hii nimeipenda....lakini kumbuka waliwapunguza nguvu kwa propaganda za udini kisha wakaungana.
 
Hii nimeipenda....lakini kumbuka waliwapunguza nguvu kwa propaganda za udini kisha wakaungana.
Nii kweli kabisa uyasemayo kwa wakati ule waliwafanyia propaganda hizo coz walikuwa ni threat kwao, baada ya kuwapunguza nguvu si tishio tena kwa ustawi wa CCM ndo maana waka-join nguvu Zenji na ss wamekuwa mwili mmoja kiasi kwamba bungeni wabunge wa CUF kuwapinga CCM ni ishu sana hata kama kitu chenyewe hakina maana...........................kutokana na swali lililoulizwa ndo maana nikajibu kuwa kwa ss hv chama kizuri kwa CCM ni CUF a.k.a CCM-B
 
Chama kizuri kwao siku zote ni kisichotishia uhai wa chama kama Cuf na makafu yao sasa hawafurukuti ni kiruzi kwao bila kusahau vingine kama TLP, NCCR, CCK, UDP Hawitishi kitumbua chao CHADEMA Hakiwapi usingiz kwa kukua wanatwanga kotekote ushaid ni kutishiwa kufutwa na msajili wa ssm, tbc kuwa promoti cuf na hata tlp, nccr wakiomba wataambiwa kaisemeni chadema. Sio hilo tu uzushi wa kuhonga rasilimali na kuua ni ushahidi usio kuwa na mashaka ssm hawana hamu na chama mbadala
 
Yaah! kwa hapa umegonga ikulu....lakini kwanini wanafanya hivi? hivi ni kweli ccm itatawala milele?
 
Back
Top Bottom