Chama kinapowaondoa mashujaa wake: Mbowe, Slaa iweni makini

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
Mara nyingi chama au kikundi chochote cha kijamii na hata timu za mpira huwa mashuhuri kutokana na mashujaa wake.

Tunapozungumzia "mashujaa" hapa tunamaanisha watu wanaokifanya chama au kikundi kiwi maarufu.

CCM ilikuwa na watu waliotokea na kuonekana mashujaa, waheshimiwa Samuel Sita, Mwakyembe, Anne Kilango, Lucas Selelii nk. Wote hawa kimewaondoa na kubakia hakina tena shujaa.

Huko nyuma kuliwahi kuwepo na Mh. Lyatonga Mrema, Rais mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi akaona ampandishe cheo. Akawa shujaa wa CCM kwa kuwa aliyoyafanya yalionyesha kuungwa mkono na mkuu wa nchi na mwenyekiti wa chama. Hata Kama aliyoyafanya Mh. Mrema yalionekana kukiuka baadhi ya taratibu na sheria lakini machoni pa watanzania alikuwa ni shujaa wa wakati ule.

Kwa bahati mbaya mashujaa wote (namaanisha wote) wamepigwa vita wameuawa kisiasa. Sasa hata wabunge wanaoinuka na kutetea maslahi ya Taifa hata kama ni kwa umashuhuri wao, CCM imewaua. Yuko Makongoro Nyerere na wengine walioshupalia ufisadi leo wanajuta.

Timu yoyote ya mpira ni wachezaji wake. Watu wanakuwa mashabiki wa wachezaji.

CCM imewamaliza wachezaji wake na haina anayepiga tena kelele kwa kuonekana.

Hii ndiyo inayofanya CCM ikishinda uchaguzi mkubwa wowote kwa sasa itakuwa ni muujiza. Nina maana uchaguzi unaohitaji kumtuma shujaa wa kusimama jukwaani na kukitetea chama kwa mvuto wake. Mmewaua wenyewe kwa sababu za kibinafsi zisizokuwa na tija kwa chama chenu.

CHADEMA mna manufaa makubwa kwani nyie mnao mashujaa wengi machoni pa watu, hata kama mnajua madhaifu yao, lakini kwa jamii ni mashujaa. Kinacholeta umashuhuri ni mashujaa wenu.

MASHUJAA WENGI WA CHADEMA
Kabla sijamzungumzia Dr. Slaa na Mh. Mbowe hebu nianze na watu viongozi wa kawaida.

Lema huko Arusha ni shujaa aliyetengenezwa na CCM na CHADEMA kwa pamoja.

Mnyika ni shujaa aliyetengenezwa na CHADEMA na kwa kiasi kidogo mgombea wa CCM jimbo la Ubungo.

Mh. Tundu Lissu ni shujaa aliyetengenezwa kwa utetezi wake bungeni na upinzani usiokuwa na msingi wa viongozi wa Bunge.

Mh. Nassari ni shujaa aliyetengenezwa na wakubwa wa CCM akiwemo Mh. Mkapa na wakubwa wengine hususan Lusinde aliyeachwa na chama kuonyesha msimamo mpya wa nguvu ya matusi.

Mh. Halima Mdee, Mh. Msigwa, Mh. Vincent Nyerere, Mh. Sugu, Mh. Arfi, Mh. Natse, na wengine wengi.

CCM waulizeni wananchi wawatajie wabunge wanaoonekana ni mashujaa hawataweza kukumbuka wengi wa CCM.

Kinacholeta ushujaa ni hoja unazosimamia na mambo ya msingi yanayogusa watu.

Ikitokea Kampeni CHADEMA wakapeleka mashujaa wake hawa wote haijalishi ni nani atakayekwenda upande wa CCM, basi CHADEMA watashinda uchaguzi wowote popote watakapowapeleka watu hawa.

ONYO KWA CHADEMA
Msiwaogope mashujaa wenu, wasaidieni wasitafute umashuhuri wa kibinafsi bali wa chama. Mmoja huko kwenu CHADEMA amejimaliza japo hajui kwa kuwa ameufanya ushujaa wake uwe wa kibinafsi na kwa maslahi binafsi. Kila anayejitahidi kukiimarisha chama chenye mtazamo wa kuwasaidia wananchi atajikuta anajipa umaarufu. Kila anayetafuta umaarufu wa binafsi atajikuta anapoteza ushujaa wake.

Ikumbukwe shujaa sio anayethubutu mambo kwa ajili yake kibinafsi au kwa sifa yake. Shujaa ni yule aliye tayari kupoteza lolote na hata ikibidi maisha yake kwa ajili ya wengine na hasa taifa lake. Wako watu wabinafsi ambao kinyume cha mashujaa, wao wako tayari kulipoteza taifa au chama chao kwa maslahi binafsi. Dr. Slaa umeendelea kuwa shujaa kwa mambo ya msingi ya kitaifa unayotetea, kufichua na kuyasimamia.

Mh. Mbowe umekuwa jasiri na kudhibitisha wazi kuwa wewe sio fisadi. Umehimili mikiki mikiki mingi.

KABLA CCM YA WATU KUSHTUKA endeleeni kusaidia wabunge wote wawe mashujaa. Mbowe ulipompisha Dr. Slaa kugombea huo ni ushujaa. Umeonyesha kuwa chama sio mtu mmoja bali ni misingi inayosimamiwa na yeyote anayeijua kwenye chama. Hoja za msingi wazungumze na kuzitetea kwa nguvu. Kuwa na mashujaa wengi ni kukisaidia chama.

LINDENI MASHUJAA WENU, WANAOTAFUTA USHUJAA WAO BINAFSI WAACHENI WANAJIMALIZA WENYEWE.

MASHUJAA WATABAKIA KUWA NI WATU AMBAO MASUALA YA MSINGI YA TAIFA YATAKUWA NI FURAHA YAO. WATAKUWA WAKO TAYARI HATA KUTOKUWA NA CHEO endapo nafasi waliyo nayo itafanya malengo ya moyo juu ya watu na taifa lake yatimie.
 
Uchaguzi unaoendelea kwenye chama sio tu kwamba umemalizia kuwaondoa mashujaa bali umedhibitisha kuwa kuja aina mpya ya ushujaa unaotengenezwa.
 
umenena yaliyo mema na kweli tupu.nikufanye nini mtu wewe? yafaa ni kuite cheo nilicho mpa MKWAWA kuwa YOU ARE THE GREAT THINKER OF OUR TIMES.
 
Umeandika mengi ya busara mkuu!

Chadema inatakiwa kuendeleza mfumo wa kuwajenga vijana wengi wawe na chachu ya kujengea umaarufu chama na si wao kama watu binafsi. Sambamba na hilo, kuna haja ya kunoa vijana kwa ajili ya majukumu mengine ya kichama, thamani ya vijana kwenye chama isionekane wakati wa vuguvugu la mabadiliko pekee, hata kuwaandaa kusababisha mabadiliko yenyewe kwa tija na weledi.
 
Umeandika mengi ya busara mkuu!

Chadema inatakiwa kuendeleza mfumo wa kuwajenga vijana wengi wawe na chachu ya kujengea umaarufu chama na si wao kama watu binafsi. Sambamba na hilo, kuna haja ya kunoa vijana kwa ajili ya majukumu mengine ya kichama, thamani ya vijana kwenye chama isionekane wakati wa vuguvugu la mabadiliko pekee, hata kuwaandaa kusababisha mabadiliko yenyewe kwa tija na weledi.

Asante! Natumaini watazingatia!
 
Nimeipenda hii. Unanikumbusha Dr. Slaa alivyoombwa na kulazimishwa kugombea urais. Mashujaa wanajulikana kwa matendo yao na si maneno. Tena hawahesabu wamefanya nini ila watu ndio wanasema kwaajili yao. Shujaa anajulikana haitaji kujitangaza. Watu wanamjua kwa matendo yake na maneno yake. Hawaongei ovyoovyo
 
Goog analysis pal! Ila hata hao wanaopotoka wabaki kuwa mashujaa in invverted comma just for the sake ya growth chama!
 
Nimeipenda hii. Unanikumbusha Dr. Slaa alivyoombwa na kulazimishwa kugombea urais. Mashujaa wanajulikana kwa matendo yao na si maneno. Tena hawahesabu wamefanya nini ila watu ndio wanasema kwaajili yao. Shujaa anajulikana haitaji kujitangaza. Watu wanamjua kwa matendo yake na maneno yake. Hawaongei ovyoovyo

Nimependa hapo kwenye red, kwahiyo tumshauri mheshimiwa wa Kigoma naye atengeneze watu wa kumuomba, kumbembeleza na hata kumlazimisha agombee URAHISI. Ingawa kimtindo naona kama tayari kazi hiyo imeshaanza kufanywa na habib mchange na dr kitila mkumbo(rejea makala zao hivi karibuni kwenye RAIA MWEMA)
 
Nimeipenda hii. Unanikumbusha Dr. Slaa alivyoombwa na kulazimishwa kugombea urais. Mashujaa wanajulikana kwa matendo yao na si maneno. Tena hawahesabu wamefanya nini ila watu ndio wanasema kwaajili yao. Shujaa anajulikana haitaji kujitangaza. Watu wanamjua kwa matendo yake na maneno yake. Hawaongei ovyoovyo

Ni kweli shujaa hajitangazi hutangazwa, hajipendekezi hupendekezwa kwa sababu ya ushujaa WAO.
 
Back
Top Bottom