"chama kimetukomboa"

kingfish

JF-Expert Member
Apr 15, 2011
571
159
WALE VIJANA WA ZAMANI WATAKUMBUKA MWAKA 1983 HADI MWAKA 1984 KULIKUWA NA VITA DHIDI YA WAHUJUMU UCHUMI.NAKUMBUKA REDIO TANZANIA(SASA TBC)WALIKUWA NA KIPINDI CHA "MIKINGAMANO"AMBACHO KILIKUWA KIKITOA HABARI NA KUWAFICHUA WAHUJUMU UCHUMI.WIMBO ULIOTAMBULISHA KIPINDI HICHO ULIKUWA NA MANENO YAFUATAYO:
MWIMBISHAJIChama, chama kimetukomboa chama.
WAITIKIAJI:Chama,chama kimetukomboa chama.
MWIMBISHAJI;Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.
WAITIKIAJI:Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.

Vipi wana JF huu wimbo unaweza kuimbika sasa katika midomo ya watanzania?
 
Nani anathubutu hata kukitaja chama hicho maarufu kama 'GAMBA PARTY' kama siyo kiongoz au mke wa kiongoz na watoto wao?wengine wanaokitaja ni wanaotarajia kupewa elfu mbili za mlo wa mchana ili siku ziende. CCM imekufa na tunasubir kuizika ifikapo 2015.
 
WALE VIJANA WA ZAMANI WATAKUMBUKA MWAKA 1983 HADI MWAKA 1984 KULIKUWA NA VITA DHIDI YA WAHUJUMU UCHUMI.NAKUMBUKA REDIO TANZANIA(SASA TBC)WALIKUWA NA KIPINDI CHA "MIKINGAMANO"AMBACHO KILIKUWA KIKITOA HABARI NA KUWAFICHUA WAHUJUMU UCHUMI.WIMBO ULIOTAMBULISHA KIPINDI HICHO ULIKUWA NA MANENO YAFUATAYO:
MWIMBISHAJIChama, chama kimetukomboa chama.
WAITIKIAJI:Chama,chama kimetukomboa chama.
MWIMBISHAJI;Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.
WAITIKIAJI:Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.

Vipi wana JF huu wimbo unaweza kuimbika sasa katika midomo ya watanzania?

Ndiyo unaweza kuimbika! MWONGOZAJI:Chama chama kimetuangusha chama WAITIKIAJI:chama chama kimetuangusha chama MWONGOZAJI:WANAMAPINDUZI NI CCM imetuangusha
WAITIKIAJI:WANAMAPITUNDIZI NI CCM imetuangusha. Maswali:1.Je Gari likikuangusha na ukapona wewe unafanyaje?2.Je mwenye gari lililo anguka ana wajibu gani kwa abiria waliokuwemo kwenye hilo gari?3.Je abiria hao wakiendelea kusubiri gari hilo pale walipo ili litengenezwe,lipone na kuondoka nalo tena watakiwa na akili au matope?
 
WALE VIJANA WA ZAMANI WATAKUMBUKA MWAKA 1983 HADI MWAKA 1984 KULIKUWA NA VITA DHIDI YA WAHUJUMU UCHUMI.NAKUMBUKA REDIO TANZANIA(SASA TBC)WALIKUWA NA KIPINDI CHA "MIKINGAMANO"AMBACHO KILIKUWA KIKITOA HABARI NA KUWAFICHUA WAHUJUMU UCHUMI.WIMBO ULIOTAMBULISHA KIPINDI HICHO ULIKUWA NA MANENO YAFUATAYO:
MWIMBISHAJIChama, chama kimetukomboa chama.
WAITIKIAJI:Chama,chama kimetukomboa chama.
MWIMBISHAJI;Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.
WAITIKIAJI:Watanzania,wanamapinduzi ni C.C.M yajenga nchi.

Vipi wana JF huu wimbo unaweza kuimbika sasa katika midomo ya watanzania?
Wimbo huu ulikuwa maarufu sana.

Halafu katikati ya kipindi kulikuwa na muziki wa bendi nimeisahau jina. Ulikwenda hivi:

Bomu limeshapasuka, mabepari wanahangaika, wahujumu wanatapatapa
Milanguzi nayo iko ndani eeeeeeh!

Nilikuwa mimi silali, nikihangaishwa na mawazo, nikifikiria maisha, maisha yamepanda aaah!
Kweli yamekuwa magumu eeeeeeeh!

Kila nilichofanya, sijui kilikokwenda, kazi nilifanya, mshahara nilipata aaaaah!
Oooooh maisha magumu eeeh

Nilikuwa na wake wawili, mmoja nimeshamuacha, sababu ya matatizo , maisha yamebana aaaah!
Sababu ya hao walanguzi eeeeh!

Nikilala nikiamka ah! Sukari haionekani!
Nikilala nikiamka ah! Unga hauonekani!
Nikilala nikiamka ah! Sabuni haionekani!
Nikilala nikiamka ho ho hooooo! Mchele hauonekani
Kumbe sababu ya walanguzi eeeeeeh!

Sasa vita imetangazwaaaaa jamaaaaa.....wananchi wote tuwe imaraaa x 2
vijijini na mijini tusisite kuwafichua wahujumu na walanguzi eeee x2

Mziki ukiisha kipindi kinaendelea kwa dakika kadhaa halafu anaingia Mzee Ng'winamila na wimbo wake wa kinyamwezi "Ulanguzi magendo eee"

Ulanguzi magendo eeeeeh!
Ulanguzi magendo na rushuwa nini......
..........................................................

Sasa hali imerudi, maisha yamebana lakini tunaambiwa uchumi umekuwa, tuko uchumi wa kati.
 
ccm ina mazuri na mabaya yake, ila mabaya ni mengi mno.
Wakulima wamekuwa ktk umaskini kutokana na sera mbaya za ccm
wafanyakazi wanadhulumiwa sana kupitia mifuko ya jamii kutokana na serikali ya ccm kuchota fedha zao na kuzitumia ktk mambo ya aibu kabisa.
 
CCM wamekenua sana kusikia uchumi wa kati. Ila nimegundua neno "KATI" ndio limrwafurahisha zaidi. Maana ndicho kilichobaki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom