Elections 2010 Chama gani kitatikisa uchaguzi mkuu mwaka 2015

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha
 
Naona cuf hawaandamwi, nccr hawaandamwi, lakini cdm mh!!!!
 
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha

miaka mitano mingi sana ndugu yangu kubashiri saizi ni ngumu sana coz chochote cha weza tokea kwenye vyamaa migongano ya kuwania nafasi za kuongoza chama
 
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha

Hueleweki unapodai kuna mikosi kwa cdm, eti mara Zito Kabwe mara Mbowe mara dr Slaa, kutaja majina ndio mikosi yenyewe?
 
Ni vigumu kubashiri sasa hivi, kwani katiba iliyoko mchakatoni inaweza kuruhusu vyama kuungana kama ilivyo Kenya. katiba ya sasa hairuhusu vyama kuungana.
 
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha

Ni mapema mno kutabiri hili maana kati ya sasa na 2015 kuna mengi mno (ambayo hatuyajui) yanayoweza kutokea na kubadilisha kabisa mwelekeo wa uchaguzi huo wa 2015.

Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha

Mkuu,
Hii kazi ya unajimu, utabiri imemshinda hata shk. yahya.

Bora tusubiri tu, tuone mwenendo wa katiba na sheria ya vyama vingi itakuwa na sura gani. baada ya hapo tutaweza kufanya utabiri kama Mzee wetu.

Migogoro au kutofautiana mawazo,hoja ni ya kawaida katika vyama.
 
Labda ungejitahidi kusoma kwenye kamusi ya kiswahili ili kuweza kujua maana halisi ya neno mkosi, maana nahisi pengine haikuwa dhamira yako. Kuwa na mawazo tofauti au kutokukubaliana jambo fulani siyo mkosi. Na kwa ujumla hakuna mahali popote, wala chama chochote katika nchi yeyote ambapo wakati wote watu wote huwa na mawazo sawa na kukubaliana katika kila jambo. Tofauti huwa ni mifumo na taratibu za kufikia uamuzi wa aina moja baada ya kuwa na mawazo tofauti. Hiyo husababisha vyama vingine kuonekana kuiwa na tofauti nyingi na vyama vingine kuonekana kama vile hakuna tofauti ya mawazo wakati wote.

Kwa sasa CDM ndiyo chenye nafasi ya kutoa upinzani mkubwa kwa CCM. Kama hali hiyo itabadilika mwaka 2015 au la, hiyo itategemea zaidi ni nini kila chama katika hivi ulivyoviataja vitafanya ili kujiimarisha zaidi. Lakini mpaka sasa naamini kuwa CDM bado ndiyo chama kinachoongoza kwa kupendwa na kukubalika kwa watanzania wengi kuliko chama chochote cha upinzani.
 
This discussion is quite pre-mature. We should stop electioneering too early in the year.
 
Wakati ndio utasema si vizuri kubashiri...maaana inawezekana hata kati ya vyama ulivyovitaja kisiwepo hata kimoja kama katiba itakuwa na mfumo tofauti na mikakati ya vyama hivyo. japo kati yavyo chochote chaweza kuwa kikuu japo sizani kama ni issue kufikiria ni kipi kitakuwa kikuu maana wewe kama ni CUF shikilia kama ni CDM shikilia Kama ni NCCR shikilia....
 
tusisubiri chama,tusubiri mtu na sera zake backed up by the histry ndugu yangu.......kwa namna hiyo tutajenga nchi..:yield:
 
Ni vigumu kubashiri sasa hivi, kwani katiba iliyoko mchakatoni inaweza kuruhusu vyama kuungana kama ilivyo Kenya. katiba ya sasa hairuhusu vyama kuungana.

Sidhani kama suala la muda mrefu au mabadiliko ya katiba yanaweza kutufanya tusibashiri ni chama gani kina nafasi ya kuchukua nchi, sasa hivi tunaweza, na kwa maoni yangu, kwa mchakato wa kuchukua nchi miaka mitano ni michache sana! Mabadiliko ya katiba ni moja ya hoja zetu za kuweka mazingira ya usawa kwenye shughuli mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi huru na wa haki; na miaka mitano ni ya maandalizi tosha ya kujua wapi palienda vibaya mpaka nchi ikaangukia kwenye mikono mibaya wakati tayari wananchi walikuwa wameamka kutoka usingizini kudai mabadiliko.

Naamini CDM ina nafasi kubwa bila kujali ni nani atasimama kugombea urais wa nchi. Chama hiki kimeanza kuungwa mkono na watu wengi makini, wenye upeo na uchungu na Taifa hili changa linaloliwa na mbwa mwitu wakali wasio na huruma. Sina wasiwasi kwa sababu najua miaka mitano ni michache kufika lengo hilo, lakini ni mingi kutoa nafasi ya kutosha kukamilisha mchakato mzima wa kuwarudishia watanzania nchi yao!
 
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha
nadhani ni mapema mno kulisemea sasa, ingawa alama za nyakati zinaonyesha dhahiri mwelekeo wa wananchi ktk kuamini nguvu ya umma, miaka mi5 ni muda, mengi yanaweza kuendelea hapa katikati mfano kusajiliwa chama kingine au vingine vikafutwa kabisa, nguvu ya umma inaweza ikafanya makubwa zaidi ikishasambaziwa elimu ya uraia kwa tz yote bara na visiwani. kumbuka katiba mpya ndo itaviweka vyama vyote sawa kwa kuanza, then jitihada binafsi hasa zenye dhamiri ya dhati ya kuondoa kero za wa tz zitavitofautisha vyama hivi kwa hoja ya nguvu ya umma. amini usiamini umma si mchezo!!
 
Mi si mtabiri ila historia na mazingira halis yanaweza kutupa picha kamili chama gani kitaongoza.
Kwanza:mara zote wapinzan wanagombea nafas ya pili ktk matokeo ya uchaguz na si kushika dola.
Pili:Inategemea CCM watamsimamisha nani?kama itamsimamisha Mkatoliki maaskofu watamuunga mkono na kuwataka wakristo kwa ujumla wao wamchague ili wasitende dhambi na hapo CHADEMA haina chake,sasa kama CDM haina chake chama gan kitawaongoza wapinzan (jibu unalo mwenyewe).Na kama CCM itamsimamisha Muislam CUF haina chake na chama kitakachowaongoza wapinzan wenzake unakijua msomaji maana maaskofu hawatafanya makosa tena kumtangaza hadharan kuwa ni CHAGUO LA MUNGU.Kwa hiyo inategemea na Mgombea wa CCM.
 
Hivyo vingine vyote ni vyama mfu au vyama vya ovyo ovyo kama mwanafalsa mmoja hapa nchini alivyowahi tamka, siyo tu kuleta upinzani CDM kinachukua dola sijui hata mmfufue Nyerere CCM kwisha habari yake
Hata sheikh yahaya analijua hilo, yetu macho
 
Mkuu,
Hii kazi ya unajimu, utabiri imemshinda hata shk. yahya.

Bora tusubiri tu, tuone mwenendo wa katiba na sheria ya vyama vingi itakuwa na sura gani. baada ya hapo tutaweza kufanya utabiri kama Mzee wetu.

Migogoro au kutofautiana mawazo,hoja ni ya kawaida katika vyama.

Nani amesema kama utabiri umenishinda?!!!
 
Jamani wanajf naomba kuuliza chama gani kati ya chadema, cuf na nccr kitakuwa mpinzani mkuu wa ccm mwaka 2015 maana chadema kinaanza kuandamwa na mikosi mara zito kabwe mara mbowe mara dk slaa

nawasilisha
This can correctly be answered by the Magomeni based .... Yahya.
 
Back
Top Bottom