Chama cha wanasheria tanzania semeni msikike.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Nchini mwetu pamoja na viongozi wakuu kula kiapo cha kuilinda katiba kabla ya kuingia madarakani, mara nyingi wamekuwa wakitenda kinyume na katiba hiyo. Mfano mzuri ni wa rais wa awamu ya tatu B.W.Mkapa; wakati akijua wazi kwamba ibara ya 9(c) inasema "kwamba shughuli za serikali zitekelezwe kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla." Aidha ibara ya 9(j) inasema; "kwamba shughuli za uchumi zisiendeshwe kwa njia zanazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache." Rais Mkapa alivunja vifungu hivyo vya katiba na vingine vingi chini ya ibara hiyo. Ilitegemewa ya kwamba, suala la serikali kuendesha mambo yake bila ya kuzingatia matakwa ya sheria mama, lingelikikuna chama cha wanasheria nchini, kiasi cha kukifanya chama hicho kujitokeza wazi na kuweka msimamo wake bayana juu ya suala hilo na mengine mengi yanayofanana na hayo. Lakini mpaka sasa chama hicho akijaweza kuonyesha mwelekeo wowote wa kutaka kujihusisha na masuala yanayo husiana na utawala wa sheria hapa nchini. Tufanye nini ili tupate ushiriki wa chama hiki katika suala hili?
 




Chama cha wanasheria Tanzania kipo kipo tu, sheria za nchi zinavyurugwa lakini hawasemi chochote.
 
Back
Top Bottom