Chama cha wananchi cuf chatoa mfano nachingwea je mfano gani?

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
Chama cha wananchi cuf kimenifurahisha suala moja kilipo fika nachingwea kimefanya jambo ambalo ni mfano kwa vyama vingine vya siasa.

Jambo ni kuwachangisha kiasi fulani cha pesa ambachokitasaidia masuala fulani ya jamii mfano ELIMU,MIUNDOMBINU,nk.laitikama viongozi wengine wngekua na moyo kama hu mi nadhani tungekua mbali mfano wanapo kuja chama cha chadema wakachangisha pesa. Pesa iliyo patikana ikasaidia kufanya mambo mengine.

Kwahiyo ombi langu kwa wana siasa wengine ni WAGOMBEA WASHINDANE KWA MAENDELEO NA SI MANENO KAMA UME SHINDA USIENDE IKULU AU BUNGENI MOJA KWA MOJA UKAWASAHAU WANANCHI MOJA KWA MOJA wabillahi tawfiq
 
Mkuu ni Nachingwea ninayoifahamu mimi au nyingine? Ni ile Nachingwea iliyotopea kwenye umaskini wa kutisha kama yalivyo maeneo mengi ya nchi yetu miaka 50 baada ya uhuru au ni Nachingwea ya USA? Ni Nachingwea ambayo wananchi wake hata mlo mmoja kwa siku ni tabu ndio ya kujenga mabarabara chini ya CUF? Hebu tuache mizaha.

Hivi kazi ya msingi ya chama cha siasa na hasa cha upinzani ni nini? Ni kuchangisha wananchi ili kujenga mabarabara? Hata chama tawala sio majukumu yake hayo! Naona baadhi ya vyama vimeanza kupoteza kabisa mwelekeo na kusahau wajibu na majukumu yao. Hicho ilichokifanya CUF huko Nachingwea ni miongoni mwa majukumu yaliyopo ndani ya Katiba yao? Au Msajili analifahamu hilo jukumu waliloamua kujitwika?

Hebu waache kutafuta umaarufu wa kijinga wajikite kwenye majukumu yao ya msingi. Ukombozi wa fikra, pale ambapo haupo, una thamani kubwa kuliko kujenga maelfu ya kilometa za barabara au kupeleka "mahindi" ya msaada. Tafakari.
 
Chama cha wananchi cuf kimenifurahisha suala moja kilipo fika nachingwea kimefanya jambo ambalo ni mfano kwa vyama vingine vya siasa.

Jambo ni kuwachangisha kiasi fulani cha pesa ambachokitasaidia masuala fulani ya jamii mfano ELIMU,MIUNDOMBINU,nk.laitikama viongozi wengine wngekua na moyo kama hu mi nadhani tungekua mbali mfano wanapo kuja chama cha chadema wakachangisha pesa. Pesa iliyo patikana ikasaidia kufanya mambo mengine.

Kwahiyo ombi langu kwa wana siasa wengine ni WAGOMBEA WASHINDANE KWA MAENDELEO NA SI MANENO KAMA UME SHINDA USIENDE IKULU AU BUNGENI MOJA KWA MOJA UKAWASAHAU WANANCHI MOJA KWA MOJA wabillahi tawfiq
Unazungumzia Yule wife wa ccm?
 
1km=1b sasa hizo fedha walizochangisha wamepata kiasi gani na watatengeneza barabara ipi na kiasi gani cha madawa watanunua?
 
Back
Top Bottom