Chama cha walimu (cwt) liwe shirikisho la vyama vya walimu.

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Kimsingi, chama chochote cha wafanyakazi kinapaswa kusimamia, kwa ukamilifu na kwa ufanisi mkubwa, maslahi ya wanachama wake. Hakipaswi kufungamana na serikali na kufumbwa mdomo na hivyo basi kuwa kama mbwa mkubwa abwekaye sana lakini asiye na meno.


Chama cha Walimu Tanzania kinakosa sifa nyingi za kuwa mwakilishi wa wanachama wake katika sehemu zao za kazi. Badala yake chama hiki kimekuwa na muda mwingi wa kusajili wanachama wapya lakini hakithubutu, kwa juhudi kubwa, kuwaelimisha wanachama wake juu ya wajibu na haki zao kazini kupitia mikutano na semina. Kimekuwa ni mkusanyaji tu wa ada zao na kujihusisha na mambo ya starehe na kujenga majumba kinyume cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004 kifungu cha
72 (3) (e). Kwa kifupi chama hiki kimemezwa na serikali na kulala usingizi wa pono.


Chama cha Walimu Tanzania kina mapungufu yafuatayo ya kiutendaji:


1. Wanachama wamenyimwa fursa na demokrasia ya kutoa mawazo na kutatua matatizo yao kwa njia ya mikutano katika vituo vyao vya kazi kwa sababu katiba ya CWT, toleo la tarehe 18 Desemba 2009 kifungu cha 11 ( a) – (c), haiwapi madaraka wawakilishi kuitisha mikutano katika sehemu zao za kazi;


2. Chama hakina sifa za kutosha za kujishughulisha kwa umakini na ufanisi mkubwa kutatua matatizo ya wanachama wake kwa sababu kina eneo pana mno la utendaji wake wa kazi. Chama kinahudumia wanachama wengi wa aina tofauti na wenye mahitaji yanayotofautiana kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, chama kinashughulika na walimu wa shule za chekechea, msingi, sekondari na vyuo. Inafaa chama hiki kubadilishwa na kuwa “Shirikisho la Vyama vya Walimu Tanzania”. Kwa mantiki hii sauti za vilio vya walimu wa shule za chekechea, sekondari na vyuo ni hafifu kuliko ya zile za shule za msingi zenye idadi kubwa ya wanachama katika CWT;


3. Mara nyingine chama kimekuwa kinaweka wawakilishi wenye sura ya maslahi ya mwajiri. Kwa mfano, siyo sahihi kwa msimamizi wa kituo cha kazi, yaani Mkuu wa Shule, Mwalimu Mkuu au Mkuu wa Chuo kuwa mwakilishi wa chama cha wafanyakazi kwakuwa hana sifa za kuwatetea na kuwawakilisha wanachama wa chama hicho;


4. Chama hakina uwazi katika matumizi ya pesa za wanachama na wasio wananachama wake. Kwa mfano, makato ya ada ya uwakala (agency fee) ya wasio wanachama yanapaswa kuwekwa katika akaunti tofauti na ile ya wanachama wake kutokana na kifungu cha 72 (3) (e) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/ 2004; na


5. Mwisho chama hiki kimeshindwa kufanikiwa katika migomo yake kwa vile kimefungamana mno na serikali.

wanasheri CWT ni kina Mabere Marando and Mr. Gabriel Mnyele; nani asiyejua ukigeugeu wa marando ata CHADEMA WANAMJUA,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom