Chama cha mapinduzi Tunashukuru kwa haya

Josephine

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
786
812
Chama cha mapinduzi,kimetufanyia haya,ambayo kwa hakika yameonekana mazuri machoni mwa wengi ndiyo maana leo wanapambana kukutetea.

1. umetuuwa fikira zetu ,kwa kutupa Elimu tegemezi ambayo kila kukicha watoto wetu wanasoma ili wapate kazi na kuajiliwa na makampuni flani makubwa nchini.Hakuna mtoto anayesoma akiwaza kubuni au kutumia elimu yake kufanya kitu kipya nchini. ASANTE SANA CCM

2.mmekiua kilimo chetu na tumekuwa tegemezi hata kwa chakula,mmetufanya watu wa njaa wakati wote.

3.Mmetufanya tuamini bila misaada hatuwezi kusonga mbele,mkasahau kutegemea kodi kupanga mipango yenu kodi zetu mnatumia kufanya starehe zenu sababu kuna misaada.

matokeo yake huduma zote muhimu ambazo tuliwachagua ili mziendeshe na kutupa ama kutuhuzia kwa bei nafuu,zote mmebinafshisha,ndiyo maana leo rasilimali zetu zote zinachukuliwa kwani hatuna cha kuwalipa hao mnaowakumbatia.

Usalama- wafadhili wanalisaidia
Elimu- wafadhili wanatusaidia
Afya- wafadhili
Miundombinu- wafadhili

Huduma zote hizi zinaudumiwa na wageni,ni kwanamna gani mtatuthamini watanzania?mkaacha kuwathamini wafadhili wanaowapa fedha? Watanzania hatuna faida kwenu,Donors are number one to you.
Ndiyo maana mmeanza kutupiga risasi kama watu tusiokuwa na haki,na hakuna mtu anayeona ametenda kosa.
Ohhhhhhhhhhhhhh my Tanzania.
 
Ila wewe First Lady una tatizo fulani. Kwa nini wewe ni mzungumzaji sana kiasi kwamba mtu anaweza kudhani wewe ndio msemaji wa CHADEMA?!. Kwa nini usifuate mfano wa mke wa Mbowe ambaye si mropokaji wala msemaji sana?!. Jaribu kuji-behave wewe ni First Lady mtarajiwa. Huu ni ushauri tu ila kumbuka ushauri si deni.
 
"Walioanzisha ukabila ndio hao hao wameanzisha tena Udini"...JK.

Wazo: si uwataje na kuwashughulikia?
 
Mkuu Mpungati hii ni forum unataka awe bubu? Mbona hata mke wa Obama anakuwa kwenye forums tofauti tofauti mwishoni utasema kwanini asiwe kama mke wako
 
Last edited by a moderator:
"Walioanzisha ukabila ndio hao hao wameanzisha tena Udini"...JK.

Wazo: si uwataje na kuwashughulikia?

kiuongozi hii nchi ni kama kuku aliyekatwa kichwa! Hatuna kiongozi anayeweza kushughulika na mambo ya msingi! Afterall, kama walianzisha wao, watajishughulikiaje!?
 
Mfumo dume ulioganda ubongoni mwako hausemeki. Mbona hillary rodham clinton ameingia kwenye siasa na wakati mumewe yuko rais? Mbona salma kikwete anaongelea elimu ambayo mumewe anaididimiza?
Kwa sababu mke wa Mbowe hana interest na siasa haimaanishi wake wa viongozi wengone wamuige. Na hapa anaongea kama Josephine na sio kama chadema.

Watu wa aina yako huwa wananishangaza sana. Nafasi ya mwanamke aio jikoni tu.
Ila wewe First Lady una tatizo fulani. Kwa nini wewe ni mzungumzaji sana kiasi kwamba mtu anaweza kudhani wewe ndio msemaji wa CHADEMA?!. Kwa nini usifuate mfano wa mke wa Mbowe ambaye si mropokaji wala msemaji sana?!. Jaribu kuji-behave wewe ni First Lady mtarajiwa. Huu ni ushauri tu ila kumbuka ushauri si deni.
 
Na wewe tuna kushauri uwe unanyamaza kama huna cha kuchangia! Baada ya kuchangia mada wewe unaanza kupambana na mtu!

Jiulize kwa nini na wewe unaongea utafikiri umetumwa kupambana na mtoa mada!

Hii inaonesha hata kwenye familia yako jinsi wengine unavyo waziba mdomo!

Acha ukweli usemwe hata kama una uma!

Ila wewe First Lady una tatizo fulani. Kwa nini wewe ni mzungumzaji sana kiasi kwamba mtu anaweza kudhani wewe ndio msemaji wa CHADEMA?!. Kwa nini usifuate mfano wa mke wa Mbowe ambaye si mropokaji wala msemaji sana?!. Jaribu kuji-behave wewe ni First Lady mtarajiwa. Huu ni ushauri tu ila kumbuka ushauri si deni.
 
Ila wewe First Lady una tatizo fulani. Kwa nini wewe ni mzungumzaji sana kiasi kwamba mtu anaweza kudhani wewe ndio msemaji wa CHADEMA?!. Kwa nini usifuate mfano wa mke wa Mbowe ambaye si mropokaji wala msemaji sana?!. Jaribu kuji-behave wewe ni First Lady mtarajiwa. Huu ni ushauri tu ila kumbuka ushauri si deni.
ww nawe? hapo kazungumzia Chadema au katoa mawazo yake, mbona haumsemi aliyepita bila kupingwa.
 
"Walioanzisha ukabila ndio hao hao wameanzisha tena Udini"...JK.

Wazo: si uwataje na kuwashughulikia?

unataka ajitaje hiyo haitatokea kama ambavyo haitatoke kwenye swala la richmond kikwete ni fisadi mnafiki anajidai msafi kumbe anamtumia mwanae na marafiki zake kutafuna mali za watanganyika..
 
Dada Josephine, mimi ni mfanyakazi na ninafanya vibiashara vyangu, siku zote nilikuwa nasikia tu watu wakidai kwamba uchumi wetu unaanguka, kwasasa nimegundua baada ya mimi kuguswa directly na utendaji mbovu wa Serikali, huwezi amini leo hii nafanya shughuli zangu mtaani ili nipate faida ya laki moja inabidi nipambane kweli kweli na mbaya zaidi kwasasa ukitoa laki moja kwa familia inatosha kununua vikorokoro vichache tu vya jikoni tena kwa siku mbili tatu, ilihali mishahara ya Serikali ni mibovu na biashara haziendi vizuri maana purchasing power ya walaji wa huduma na bidhaa inashuka kila kukicha. Kweli CCM imetutenda vya kutosha
 
"Walioanzisha ukabila ndio hao hao wameanzisha tena Udini"...JK.

Wazo: si uwataje na kuwashughulikia?
Mtoto aliyekojolea kuran alifanya kosa pamoja na utoto wake, LAKINI yule aliyeweka kuran ikojolewe hana cha kusemewa.
Kutatua tatizo kwa kukata matawi badala ya mizizi, hii ndio style ya uongozi tanzania.
 
ila wewe first lady una tatizo fulani. Kwa nini wewe ni mzungumzaji sana kiasi kwamba mtu anaweza kudhani wewe ndio msemaji wa chadema?!. Kwa nini usifuate mfano wa mke wa mbowe ambaye si mropokaji wala msemaji sana?!. Jaribu kuji-behave wewe ni first lady mtarajiwa. Huu ni ushauri tu ila kumbuka ushauri si deni.

napita tuu maana mm nikichangia kuhusu aliyeleta hii thread nitapigwa ban huyu ana kinga hapa jf ukimgusa unakula ban
 
ccm ilipoiwekea tanzania gea ya rivasi tulifikiri wanataka kuikwamua nchi kwenye matope kisha tuendelee na safari kumbe wamesinzia kwenye stearing na gari inaongeza kasi kurudi nyuma na mguu wameusahau kwenye mafuta.
kila dereva anavyoota ndoto ndipo mwendo unaongezeka na majuha wanashangilia.
 
Back
Top Bottom