Chama cha mapinduzi njombe kubaki katika vitabu vya historia 2014/5

lutondwe

Senior Member
Dec 20, 2010
150
74
Ziara ya M4C iliyoongozwa na kamanda John Heche imedhirisha dhahiri kuwa ili CCM ishinde katika uchaguzi wowote hapa Njombe itafanya kazi ya ziada.Kuna kila dalili kwamba wilaya ya Njombe sasa iko chini ya CHADEMA kwa 100%.Kamanda Heche ni moja kati ya viongozi ambao amefanya kazi kubwa hapa Njombe na Makambako.Akiwa Njombe alimchana vilivyo bibi Kiroboto na pia akiwa Makambako alimfanya vibaya sana mbunge wa kuchongwa wa jimbo hilo Deo Sanga(jah people).Uchumi wa Njombe umezidi kushuka wakati ni moja ya wilaya ambayo ilipaswa kuwa na maendeleo makubwa tofauti na maeneo mengi ya Tanzania.Njombe na Makambako hakuna huduma ya maji,hakuna umeme katika vijiji nje ya miji hii,hakuna barabara za uhakika,hakuna usimamizi wa raslimali za umma na hivyo kusababisha hati chafu kila mwaka na madudu mengine mengi.
Wilaya ya Njombe ni moja ya wilaya ambayo wananchi wengi wameamua kuanza kuwekeza katika siasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
katika mkutano wa jana wananchi wa Njombe wamwambia John kuwa wanajisikia aibu kubwa kuwa na spika toka Njombe ambaye ni aibu ya wananjombe kutokana na kuongoza vikao vya bunge kwa ubabe usiomithilika.​
CHADEMA NI MUZIKI MNENE,TUNAANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
 
tunangoja kwa hamu 2015 tujue kama hii ni propaganda au ni ukweli wa mambo. Halahala tusije kusema kwamba tumeibiwa kura.
 
Don't be too sure about your prediction. CCM itakuwepo na itakuwa bado ni imara ifikapo 2014/15 ni vyema mkaelewa hilo mapema ili mjiandae vyema kwa kinyang'anyiro kigumu cha kuyanyakua hayo majimbo.

Mkijidanganya kuwa CCM haitakuwepo Njombe and Makambako wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 basi ujue mnajiandalia mazingira ya kushindwa kwa kishindo na kuishia kulalamika kuwa mmeibiwa kura.
 
Huwa siwezi kujitambulisha kwa watu kuwa Makinda ni mbunge wa jimbo langu nilikozaliwa,ni aibu kwa jinsi anavyoshindwa kuliongoza bunge. Namkumbuka Sitta, ndiye ambaye bunge hili lilikuwa saizi yake lakini si huyu mama anaonyesha ukereketwa, udhaifu na upendeleo uliopitiliza. Makambako ndo kabisaaaaa. Ila ndugu zangu wa Njombe na Makambako siwalaumu, najua ni swala la ELIMU la uraia, na dhana kwamba mbunge ni "mfadhili" wa jimbo. Ni swala la muda tu, siku si nyingi mambo yatabadilika.
 
Don't be too sure about your prediction. CCM itakuwepo na itakuwa bado ni imara ifikapo 2014/15 ni vyema mkaelewa hilo mapema ili mjiandae vyema kwa kinyang'anyiro kigumu cha kuyanyakua hayo majimbo.

Mkijidanganya kuwa CCM haitakuwepo Njombe and Makambako wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 basi ujue mnajiandalia mazingira ya kushindwa kwa kishindo na kuishia kulalamika kuwa mmeibiwa kura.
Haitakuwepo. imesiginwa.
 
Ziara ya M4C iliyoongozwa na kamanda John Heche imedhirisha dhahiri kuwa ili CCM ishinde katika uchaguzi wowote hapa Njombe itafanya kazi ya ziada.Kuna kila dalili kwamba wilaya ya Njombe sasa iko chini ya CHADEMA kwa 100%.Kamanda Heche ni moja kati ya viongozi ambao amefanya kazi kubwa hapa Njombe na Makambako.Akiwa Njombe alimchana vilivyo bibi Kiroboto na pia akiwa Makambako alimfanya vibaya sana mbunge wa kuchongwa wa jimbo hilo Deo Sanga(jah people).Uchumi wa Njombe umezidi kushuka wakati ni moja ya wilaya ambayo ilipaswa kuwa na maendeleo makubwa tofauti na maeneo mengi ya Tanzania.Njombe na Makambako hakuna huduma ya maji,hakuna umeme katika vijiji nje ya miji hii,hakuna barabara za uhakika,hakuna usimamizi wa raslimali za umma na hivyo kusababisha hati chafu kila mwaka na madudu mengine mengi.
Wilaya ya Njombe ni moja ya wilaya ambayo wananchi wengi wameamua kuanza kuwekeza katika siasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
katika mkutano wa jana wananchi wa Njombe wamwambia John kuwa wanajisikia aibu kubwa kuwa na spika toka Njombe ambaye ni aibu ya wananjombe kutokana na kuongoza vikao vya bunge kwa ubabe usiomithilika.​
CHADEMA NI MUZIKI MNENE,TUNAANZA NA MUNGU NA TUTAMALIZA NA MUNGU.
Unywe maboso be mdimi??????????????????????? Hatutaki chama tunaka Viongozi bora wanaojua kuwajibika,chama ni mwavuli tu wakupata dhamana ya kuongoza....Usiwadanganye WanaNJOMBE ati CHADEMA ndiyo ina Viongozi bora..Umeyasikia ya ZITO KABWE???????????????? Time Will Tell...I am the Next MP to transform our region !
 
Mambo yote ulingoni.
 
Hata wewe ni wakuchonga? Yaani nyota ya kijani?
 
Unywe maboso be mdimi??????????????????????? Hatutaki chama tunaka Viongozi bora wanaojua kuwajibika,chama ni mwavuli tu wakupata dhamana ya kuongoza....Usiwadanganye WanaNJOMBE ati CHADEMA ndiyo ina Viongozi bora..Umeyasikia ya ZITO KABWE???????????????? Time Will Tell...I am the Next MP to transform our region !

ukisikia Chadema njombe unakurupuka kuja kutetea magamba,njombe hututaki magamba....endelela ukugala amabosi ukija kushituka chadema kimechukua jimbo.
 
Haitakuwepo. imesiginwa.

Ni jambo zuri sana kujiamini unapoingia kwenye mapambano ila kujiamini kupita kiasi ni hatari kwa mtu anayejiandaa kuingia kwenye mapambano. Hii kauli yako ina harufu ya kujiamini kupita kiasi.
 
Back
Top Bottom