Chai ya Maziwa Fresh ya Viungo

Last edited by a moderator:
Dada AshaDii,sasa hii chai unayoweka ni yoyote au?Mimi nataka nikutumie chai nyeusi(black tea) nzuri kuliko zote Tanzania,niambie niikutumie je 250gm. Leo ngoja nikawapikie wanangu hii menu ninywe nao.Kuna watu inabidi mzidi kuishi tu!Sala zetu ziwafikie!
 
Hata Chai ya rangi pia inafaa... Ila kwa chai ya rangi unapotenga tu maji yako pale pale yanapoanza kupata vugu vugu kwa mbali ndipo unapoweka viungo vyako pamoja na majani ya chai. Mara nyingi chai ya rangi viungo hukolea haraka hivyo vinakuwa ni kiwango kidogo kuliko kwa ajili ya Chai ya maziwa.

Chai itakapo anza kuchemka ndipo waweza Sukari. Sukari ya kuchemka kwenye chai ni bora zaidi kuliko ya kuungia kwenye kikombe hasa kama ni chai ya familia pale asubuhi inakua rahisi zaidi. Ndio mana ni vema kupika kwa vipimo ili kuepusha kubaki ikamwagika mwagika.

Thanks for the acknowledgement. Pamoja Saana.
 
Habari za leo!

Naombeni msaada wa namna ya kupika chai ya maziwa ikawa na ladha.

Kuna mgahawa flani wa wahindi kule mjini pembeni ya chef pride (nao ni mgahawa) wanatengeneza chai ya maziwa ambayo ni tamu sanaa. Cjui wanaweka nini mule ndani. Na ninatamani sana kujua.

Inakuwa na ladha km cjui chocolate cjui vanilla ila ni tamu sana. Nijuzeni plz kwa mnaofahamu hizo siri za upishi.
 
Chemsha maji kidogo kwanza na viungo vyote ispokua majani alafu mimina maziwa weka na majani kdg subiria ichemke kidogo huku unakoroga alafu weka sukari wacha ichemke alafu chuja mimina kwenye vikombe au chupa
 
Majani ya chai yana nicotin na ile ni drug hvo siyapendi kutumia.

Mie nachofanya kama mbadala wa majani ya chai ni haya ili kupata rangi ya kahawia kama ya majani ya chai ktk maziwa..

1. Nakaanga sukari hadi inakuwa rojo rojo na kuungua kidogo kisha naeka maziwa yangu

2. Nakaanga mbegu za ubuyu kisha nazisaga na kuchekecha ili kupata unga wake.. Kisha nautumia kama kiungo katika hot drink yangu.
ladha ni kama ya cocoa ila hapa unapata natural seasoning item na yenye faida kiafya.

Halafu hii hot seasoned milk inanoga kipindi cha baridi ama ukiwa na uchovu. Unaishushia na bites ama nuts zako taraaatibu.
 
Wakati tunaongea hapa nilikuwa sijakunywa chai yako wifi AshaDii.
I declare, in the whole wife world; hakuna chai nzuri niliyokunywa maishani ikazidi chai yako kwa ladha na ubora.

Najialika Leo, ntakuja na vitumbua vyangu mkononi. Kaka Kaizer naomba usiwepo nataka niongee umbea na wifi
 
Unaongea tu utekelezaji zero!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom