Mkuu umeua! Isipokuwa majambazi wakichaguana nani aingie ndani kupora na nani abaki nje kulinda "usalama" huo tuwaachie CCM.
Upepo wa mabadiliko wenye harufu ya kisiasa umevigubika vyuo vikuu karibu vyote Tanzania.
Kila inapotokea fursa ya uchaguzi wagombea wa nafasi mbalimbali hasa wanao bainika kuwa ni wanachama wa ccm huwa wanakuwa na wakati mgumu kujiuza kuliko wale wa chadema.
Chaguzi nyingi zinazoendelea kwenye vyuo vikuu sasa hazitakuwa na tofauti naza mwaka wa jana. Wanachama, wapenzi na mashabiki wa chadema mara zote husimama kidete kuhakikisha m-ccm ana garagazwa. Hata kwa chaguzi zilizo kwisha fanyika na zinazo tarajiwa kufanyika tayari wagombea ambao ni wafuasi wa chadema wanang'ara na watashinda.
Mfano mwaka jana rais wa udom alikuwa mchadema, rais wa mwenge, raisi wa smucco, rais wa Tengeru na sasa hivi tayari raisi wa Saut ni mchadema. Tusubirie vyuo vingine, ni M4C kwa kwenda mbele.