Chaguzi za ndani ya CCM: Lowassa awabwaga Kikwete na Sitta

Wanaweza bila shaka!! Ona nini M4C wanafanya saa hizi. Miaka 3 iliyosalia inatosha kabisa. Mbona kampeni wanafanya kwa miezi michache tuu lakini wanapita KARIBU kila kona ya nchi. Ni kuchukua tu muda uliobaki GAWA kwa maeneo yote yanayotakiwa kufikiwa!

Kwa taarifa yako huko Arumeru Mashariki ambako CHADEMA ilishinda kwa kishindo ni katika vijiji vya kutisha ambako awali walikuwa hawajui chochote zaidi ya CCM, lakini ccm walishindwa vibaya pamoja na pesa zote walizotumia (nadhani unakumbuka kiasi walichotumia), pia ukizingatia CCM kilipeleka nguvu karibu yote kule akiwapo rais mtaafu Mkapa. Na aliyekuwa anagombea alikuwa mkwe wa huyo Lowassa!

My friend watu wa vijijini sasa wameamka!

si kwamba ninakupinga ila ninajaribu kufikiri kwa upana wake maana kama M4C itashindwa kuwafikia wote basi inaweza ikawa shughuli lakini zaidi nilikuwa arumeru na ninaishi arusha mjini
 
Hakuna siku nitakayofurahi kama Lowasa akiwa mgombea Urais kupitia CCm maana kaburi la ccm litakuwa wazi kabisa.

hakuna wa kuweza kumshinda lowasa kama akiteuliwa na ccm.hongera lowasa kwa kukata kilimilimi cha mzee wa majungu jk na mavuvuzela sita na mwakyembe
 
....Ni muhimu sana Chadema ikafanyia kazi masuala matatu:

Moja, Kanuni ya Ushindi iliyopo sasa;
Mbili, Kanuni ya ushindi iliyopo sasa; na
TATU KANUNI YA USHINDI ILIYOPO SASA;
Mchambuzi,
Nakubaliana na wewe. Hii kanuni nadhani ni moja ya kanuni zinazopaswa kubadilishwa kwenye katiba mpya. Nimemsikia Mkiti wetu Mbowe akiipinga, mara kadhaa. Ila mimi, wewe pamoja na viongozi wa Chadema kutaka kuibadili ni jambo mmoja. Kufanikiwa ni jambo jingine. Let us hope for good.
 
Ni kweli el ana popularity kubwa lakini hicho si kigezo cha yeye kushinda na kuwa president kwani anayo mengi machafu na pia kwa kuwepo kambi mbalimbali pinzani ndani ya chama chake. Hivyo cdm wakijipanga kisawasawa mapema wanaweza kupeta
 
hakuna wa kuweza kumshinda lowasa kama akiteuliwa na ccm.hongera lowasa kwa kukata kilimilimi cha mzee wa majungu jk na mavuvuzela sita na mwakyembe

Akiwashinda wote ndani ya ccm halafu akakwama kwa Chadema wewe huoni kama hiyo ni hasara pia.
 
Wana muogopa sana lowasa jamaa ana tamba sana ndani ya Ccm kwakweli ana mpandisha pressure Nape!

Mkuu,
Ni kweli Lowassa ana nguvu sana ndani ya magamba, na hakuna wa kumuzuia kwa namna yoyote, kutokana na ukwasi mkubwa alionao, na magamba kuhalalisha kupata uongozi ni lazima kutoa rushwa. kwa kifupi hakuna mtu ndani ya magamba atakae mzidi kwa rushwa Edo.

Ukiachilia mbali hao wadau uliowasiliana nao, leo ni Uchaguzi wa UVIVUCCM, hao vijana wanaingia wote ni wa timu mmoja tu, ya Edo, so kwa vyovyote vile team ya Edo kwa hao vijana wa VIVUCCM, atashinda kutokana na ile kitu Mlungula.

Kwa vyovyote vile, ile katiba tayari, tume huru ya uchakuzi ama bla bla bla LAZIMA CHADEMA kushinda 2015, ni LAZIMA...Wacha wajipange kuwa chama pinzani 2015.
 
Ni nini hicho wanachokiamini wakati sisi tunatengeneza katiba mpya itakayoleta tume huru na kuzuia wizi wa kura. Au tume huru ni changa la Macho? Sijapata jibu.

Hakuna katiba mpya 2015 mkuu, hilo liko wazi na halina mjadala. Tena kama una shughuli za kufanya, usipoteze mda wako kwenda kutoa maoni kwenye katiba hii inayotengenezwa sasa.

Kuhusu watu kutumia ela CCM, sio kwa sababu wana uhakika kuwa wakiteuliwa watashinda uraisi, no... bali wanauhakika wakiteuliwa, mahasimu wao hawatakuwa maraisi (kirahisi). Kwa Lowassa, ni afadhali x100 CDM waingie madarakani, kuliko timu ya Sitta au ya Membe (and vice versa). Anachofanya Lowassa ni kuhakikisha ama anateuliwa yeye kugombea (potelea mbali hata kama atakosa), au kama hatateuliwa, basi atakuwa na timu ya kuhaikisha timu ya Sitta na ya Membe haitashika madaraka 2015... (hata yeye hapendi kukimbilia Kenya)
 
Hakuna katiba mpya 2015 mkuu, hilo liko wazi na halina mjadala. Tena kama una shughuli za kufanya, usipoteze mda wako kwenda kutoa maoni kwenye katiba hii inayotengenezwa sasa.

Kuhusu watu kutumia ela CCM, sio kwa sababu wana uhakika kuwa wakiteuliwa watashinda uraisi, no... bali wanauhakika wakiteuliwa, mahasimu wao hawatakuwa maraisi (kirahisi). Kwa Lowassa, ni afadhali x100 CDM waingie madarakani, kuliko timu ya Sitta au ya Membe (and vice versa). Anachofanya Lowassa ni kuhakikisha ama anateuliwa yeye kugombea (potelea mbali hata kama atakosa), au kama hatateuliwa, basi atakuwa na timu ya kuhaikisha timu ya Sitta na ya Membe haitashika madaraka 2015... (hata yeye hapendi kukimbilia Kenya)

Kwenye comments zote za leo, hii ya kwako inanipa jibu sahihi zaidi ya maswali niliyokuwa nayo na niliyoyauliza kwenye uzi huu.
Sasa nitalog out nikiwa najua kwa nini wana siasa wa ccm wanahangaika sana wakati wanajua wao na chama chao hawatakiwi na wananchi - jibu hawataki kuwa wakimbizi wa makundi pinzani ya ndani ya ccm, ambayo yanaweza kuwafukuza au kuwafilisi au kuwafunga jela.
 
Lowassa hana mpinzani akiwekwa kugombea Uraisi awe Slaa awe Mbowe hawataweza kupambana naye. Hii ni kweli wala sio propaganda. Acheni mchezo Lowassa ananguvu sana hapa nchini. Keep watching.
Ni kweli kabisa tena anatokea kaskazini huenda CCM nayo ni chama cha Kikanda
 
Wachache hamtaki kukubali lakini huo ndio ukweli EL anatisha. Bila kumungunya maneno wala kupepesa macho naamini kwa sasa ni EL anayeweza kututoa hapa tulipo na kutupeleka mahali fulani kwa salama na ujasiri mkubwa. EL akiongea hata kama ni kidogo anaongea hoja na si kama wanasiasa wengine ambao kusema kweli hata kama mnawapenda hakuna la maana wanaloongea, zaidi ya kurudia waliyoyasema wenzao, inakuwaje kiongozi mkubwa wa chama anashindwa kuwa nahoja yake ya msingi nansubiri kiongozi wa chama pengine hasimu aseme naye atambae kwa maneno ya huyo na hasa kwa kuponda na kutukana halafu sie wengine tuchekele kama mazuzu badala ya kumwambia bwana mkubwa watu wanataka kusikia hoja yako; ni aibu kiongozi ambaye watu wanaonyesha ushabiki kwake kushika ofisi kubwa akashindwa kutoa hoja angalau moja na watu wakamwelewa. EL amedhiirisha kuwa ni mwanasiasa kiongozi na mtawala. Amjidhiirisha kuwa amepigia chuo kama si vyuo vya uongozi na utawala wakati ule wa mzee mnayempenda sana Hayati Mwl Nyerere. Hiyo ndiyo tofauti kati ya EL na wengine kwa upande mmoja lakini pia na ukomavu wa chama cha siasa unauona, pamoja na ukomavu huo unauona jinsi wanavyoweza kuchaguana kuanzia chini hadi juu. Tumebaki na hisia hasi lakini ukweli ni chama kimoja chenye utaratibu unaoeleweka katika chaguzi zake, na nahisi tukipata chama ambacho kitakuwa na utaratibu anagalau kidogo kama huo tunaweza kusema kwamba sasa tuna la kuwaambia wananchi. Sasa hivi, hivi vyama vimekuwa vikishuka kama viwavi jeshi na kumwaga porojo na neno ufisadi likichukua 67% katika midomo yao lakini bila kujenga hoja hata moja ya msingi ambapo EL kwa kujua udhaifu huo yeye ni kujenga hoja ambazo humu ndani mtake msitake zinawagusa na matazijadiri nje au ndani ya mitandao kwa uzuri au kwa ubaya moyoni zinawagusa!!! Nani anaweza kuniambia kwamba tangu uchaguzi mkuu uishe ni kiongozi gani wa upinzani au hata ndani ya chama tawala na wapambe wao kaongea hoja amabayo imewagusa vijana, wanawake, watoto na wazee makundi yote yakamwelewa kama ambavyo makundi hayo hayo yanamwelewa EL AKIONGEA. Tuache masihala na utoto Lowasa is a serious politician and if CCM stumbles seriously, then Edo is there to take advantage of that. And When A Politician Has No Serious Solutions and just bring blah blah kwenye majukwaa ya siasa tu akirudia neno mara 7x70 bila hoja ya maana hafai hata kidogo. Kusema kweli na ukweli unauma kwa wale vilaza wanaofikiri kwa hapo walipo, ambao kwa udhaifu wa kufikiri na ubutu wa maono hawatakubali kwa mdomo na hata maandishi kwamba mwanasiasa mahiri, shupavu ,vissionary na anayeweza kujenga hoja bila kutumia mgongo wa mwingine aidha kwa kumsifia au kumchafua hili apande ni ENLOWASA. This crown needs to be mugged by reality. EL lost completely from the heart of Dodoma's blue ridge and Coming back to you from a secured redoubt on Big walker Mountain in the heart of Dom's Blue Ridge like 'wise man who plants a tree in the shade of which he knows he will come later to sit'. Last but not least (for all of you: elders, youths and children, women and girls)- Someday, Edward will walk into your life and make you realize why it never worked out sooner with and you will pray all of you stay with you and never back where he was. Give him a hand a new Tanzania is coming for sure.
 
Shida kubwa, watanzania tunasumbuliwa na njaa, akitokea mwenye pesa huwa ana weza kuwatumia apendavyo, Lakini yote inatokana na wajanja hao kujua ukweli kuwa, wananchi wetu sio njaa tu lakini na ujinga ndo mtaji wao mkubwa wa kuendelea kuishika dola mpaka leo, Kwahiyo huo pia ndo tegemeo kubwa la Edo, kuwa pagumu ni ndani ya chama na sio nje ya chama, Thanks to chadema, wameanza kuwafanya watu watambue kweli na sasa kweli imeanza kuwaweka huru, Wameenza kulilia nchi yao na machozi yao ndo yamekuwa yakiilaani kila leo CCM, Chadema wasichoke matunda hayako mbali!
 
Ukweli Husemwa:

Tatizo letu Watanzania kila mara tunapenda kuweka mwanvuli mmoja hata katika maswala yanayohusu upembuzi unaotofautiana.

Fikra finyu tu ndizo zinafanya mtu ajiaminishe kama CCM imeishashindwa uchaguzi mkuu.

Katika nchi yoyote yenye demokrasia, chaguzi ndogo na makutano ya kisiasa siyo kipimo mbadala za kujua upepo wa kisiasa katika uchaguzi mkuu kwa sababu mara nyingi chama tawala na serikali iliyoko madarakani huwa zinakuwa na ''election manifesto hangover syndrome'. na kutokana na hili, wapinzani mara nyingi hushinda hizi chaguzi ndogo. kampeni za uchaguzi mkuu ni tofauti sana na kupiga kampeni za uchaguzi mdogo.

Ni fikra finyu pale tunapojiaminisha kila kitu kikifanyika ndani ya CCM basi kimefanyika kwa sababu bakuli la ruswa lilipita. Tunajiaminisha kama kila mshindi ndani ya CCM anatoa ruswa na wapiga kura ni wajinga kiasi ambacho hawawezi wakawa kama wananchi wanaowapa kura CHADEMA kwa kauli mbiu ya KULA CCM, KURA CHADEMA.

Ni fikra finyu pale tunapojidanganya kama pesa siyo kigezo muhimu katika uchaguzi hasa uchaguzi mkuu. Na pale mgombea anapokuwa na pesa basi tunambandika jina la mtoa rushwa. Tunaaminishwa na wanasiasa fedha siyo muhimu sana na wao hawana pesa au hawatumii pesa kama mwanasiasa au chama fulani fulani na wameshinda, wakati kauli zao siyo za kweli kwa sababu pesa wanatumia sana lakini zinakuja kwa kupitia chini ya meza na matumizi yanafanyika kwa njia ya kificho pia. Angalia nchi zilizo tuuzia hii kitu inayoitwa demokrasia jinsi wanasiasa wake kabla na wakati wa kampeni wanavyotembea kupitisha bakuli wakiomba pesa ziwasaidie kwenye uchaguzi.

Ni fikra finyu tunaposhangilia kama CCM itadondoka kutokana na makundi waliyonayo ambayo ndiyo yataidondosha katika uchaguzi mkuu. Ikumbukwe kuwa, Kwa sasa CCM wako kwenye chaguzi na mpaka sasa hakuna tingishiko kubwa lililotokea pamoja na kukatwa majina au kudodoshwa kwa baadhi ya 'vigogo' ndani ya CCM.
Chama kinapokuwa na makundi yaliyowazi ndani ya chama, kwanza' ni dalili ya kuwepo kwa demokrasia ndani ya chama kwa kuwa kila mtu ana uhuru katika fikra na pili, ni njia iliyo nzuri katika chama kujua tofauti za kifra miongoni mwa wanachama na wapenzi wake ili kuweza kuzipatia jawabu mbadala kuelekea katika uchaguzi mkuu.

Chama chochote cha kisiasa lazima kipitie kipindi kizuri na kigumu katika siasa. Kwa sasa ninaamini CHADEMA iko katika kipindi kizuri cha kisiasa, lakini nina wasiwasi na jinsi kitakavyo kabiliana na kipindi kigumu cha kisiasa hasa kama kikitokea karibia na uchaguzi mkuu. kama vile, makundi ya wazi ndani ya chama, kashfa za kisiasa na kijamii

Adui mkuu wa CCM na mgombea wake ni wanaCCM wenyewe lakini Adui mkuu wa CHADEMA na mgombea wake ni CCM, serikali na makundi ndani ya CHADEMA.

Halafu tunakuwa kama tuna fikra finyu hivi tunapoanza kumjadili mtu au mwanasiasa fulani kama ndiyo ameisha jitangaza kama mgombea urais wakati sivyo hivyo.
 
Naomba kauli ya Lowasa kuhusu;
Twiga waliosafirishwa nje ya nchi kwa kutumia ndege. Je, kama ni mzuri kiasi hicho mbona hajapeleka hoja binafisi kutusaidia wapiga kura wake?
Nini kauli yake kuhusu mabilioni yaliyoko mabenki ya nje?
Ni nini kauli yake kuhusu kila ufisadi unaoibuka ktk nchi yetu?
Hoja ya ajira kwa vijana aliianzisha sumaye, yeye kaidakia. President wa 2015 kutoka ccm ni ngumu hata akija mtu mzuri kutoka ccm. Sembuse ccm waje na mtuhumiwa wa ufisadi wa Richmond?

Anyway nadhan ukaaji kimya wake kuhusu vyote ulivyotaje si kwa sababu yeye ndo muhusika, na angalikua muhusika vyombo vya dola vinamwogopa? na je kuhusu twiga rais wenu anasemaje? waziri wa maliasili je?, kuna wengi wakuongelea mambo hayo siyo kuwa mwenyekiti wa kamati ya usalama ndo kumtwika lawama zisizo zake EDO! ni mara ngapi wenyeviti wameongelea vitu vya maslahi ya taifa wakasikilizwa? Juzi Edo kasema yuko tayari kulinda Tanzania watu mkaja juu ooh amekuwa Amiri Jeshi, Edo atangaza vita.
mabilion yalioko nje Membe si aseme? kuna Sauz mkubwa alikuta Trilion 3 za jamaa wa jeshi mbona yuko kimya mpaka leo, mnamwona Edo tu ndo mbaya.
Ufisadi wa Rich mbona mkubwa alikuwa kimya Edo alipomwambia kavu kavu kule Dom? Edo ana hela za siku nyingi siyo za juzi wala jana ndugu. Tuangalia na upande mwingine sio kumbambikia mtu lawama asizo stahili.
 
Mikael P Aweda Ukizoea kula nyama ya watu huwezi acha,hiyo ndiyo pekee njia wanayoona inaweza ikawafikisha kwenye kilele cha mafanikio ya Siasa.
ni vizuri waweke mtuhumiwa mkuu wa Richmond ili kazi ya kuikomboa Tz isiwe ngumu sana,labda wanajua wakati wa uchaguzi igp bado atakuwa mwema na waziri wake Nchimbi,takukuru wale wale walioisafisha Richmond,usalama wa taifa wale wale wanaohangaika kumkanusha stephen Ulimboka,akina kamanda Kova wanaochukua machizi kuwapeleka mahakamani ili kuwafunga mdomo wabunge mahiri wasilizungumzie bungeni kwa msaada wamaspika.
Na kama unavyohisi wanaweza wakahakikisha hata katiba mpya aidha haikidhi haja au haikamiliki kwa wakati.MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Last edited by a moderator:
Sikubaliani na wewe, hiyo ni historia.
Nina uhakika kama Lowasa akishinda Samweli Sitta atahama ccm ama atamhujuma ndani kwa ndani. Vivyo hivyo, Samawel Sitta akishinda Lowasa ama atahama Chama au atamhujumu ndani kwa ndani. Na ikifika hapo, ngome inogile.
hahhahha! sasa manategemea eti sitta amuhujumu lowassa? siamini kwamba mnategemea siasa za kama michezo ya kombolela..............mmmh! hivi kumbe bado CDM haijaamka kujipanga kisera na kimbinu za kubadili fikra za watu wengi hasa wazee na akina mama juu ya uchaguzi. tena kama mnategemea nguvu ya vijana wa vijiwen ambao wengi si wapiga kura mseme mapema nihame chama manake ukweli naona nitapoteza kura yangu bure.

kiukweli ccm ina nguvu sana sana na inapendwa sana na watu hasa akina mama ambao ndio wapiga kura wengi na wazee. najua hapa wana cdm mtawaka sana ila hata humu jamvini tu tupigekura za uccm na ucdm kisha uangalie wanao vote kwa cdm ni wepi na wanaovote kwa ccm ni wepi utajua namaanisha nn.
 
KAMBI YAKE YAPETA UWT, SASA WAJIPANGA UVCCM, WAZAZI

Waandishi Wetu, Dodoma

KAMBI ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa imeendelea kuyanyanyasa makundi mengine ndani ya CCM, ambayo yamekuwa yakijipanga kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kambi ya kiongozi huyo ni kama imehamia Dodoma ili kuhakikisha watu wake wanashinda katika chaguzi za viongozi wa juu wa jumuiya za CCM baada ya kufanikisha kile inachodai kuwa ushindi mkubwa katika ngazi za wilaya na mkoa kutokana na watu wake wengi kushinda.


Wapambe wa Lowassa wakiongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), Hussein Bashe wapo Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) na wataendelea kuwapo mpaka jumuiya zote zitakapokuwa zimefanya uchaguzi huo.

"Hapa kazi ni moja tu, hakuna kulala maana tukilala tutajikuta tumewekwa pabaya. Tumefanikiwa UWT na sasa tunaelekeza majeshi yetu UVCCM... lazima tuhakikishe tunakomesha uonevu wa kuitana magamba mwaka huu," alisema mmoja wa wapambe wa Lowassa juzi usiku.


Matokeo ya uongozi wa juu wa UWT yameongeza matumaini kwa kambi hiyo ambayo imezoa zaidi ya asilimia 80 ya viongozi katika jumuiya hiyo yenye ushawishi mkubwa katika uamuzi mbalimbali wa chama hicho.


Mwenyekiti wa UWT Taifa, Sophia Simba ambaye alitetea vizuri nafasi yake na Makamu wake, Asha Bakari Makame wanatajwa kuwa katika kambi hiyo huku wajumbe saba kati ya tisa waliochaguliwa kuiwakilisha jumuiya hiyo katika Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, wakiwa waumini wa kambo hiyo.


Walioshinda nafasi za ujumbe wa NEC ambao wanatajwa kuwa wafuasi wa Lowassa ni pamoja na Mbunge wa Ukonga, Eugen Mwaiposa, Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana.


Wengine ni wabunge wa Viti Maalumu, Diana Chilolo, Zainabu Kawawa, Mary Mwanjelwa na Subira Mgalu.

Wajumbe wawili ambao ni pamoja na Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene yeye anatajwa kuwa hana kundi lolote wakati Mbunge wa Viti Maalumu, Betty Machangu ambaye anatajwa kwamba alikuwa akimuunga mkono Mbunge wa Same Mashariki, Anna Kilango Malecela.


Kilango ambaye alikuwa akiungwa mkono na makundi ya watu waliojipambanua kuwa wapambanaji na ufisadi, aliangushwa vibaya na Simba kwa zaidi ya kura 400 katika kinyang'anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa UWT.

Vigogo wengine wanaotajwa kuwa na kambi katika kinyang'anyiro hicho cha urais wa 2015 ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambao katika uchaguzi wa jumuiya za CCM nguvu zao zinaonekana kuwa si kubwa kama ilivyotarajiwa.


 
Back
Top Bottom