Chaguzi ndogo 16/6 na 14/7 majumuisho na tathmini

Mkuu nakupa big up san kwa ufafanuzi mzuri sananadhani wenye kuelewa wataelewa na wenye kukataa kuelewa kivyao, kidogo hapo kwenye kuungana kidogo napatashida kidogo kuna watu ambao wanaona bora waipigie CCM kuliko kuwapa CHADEMA na wengine VIRSE VERSA.
 
Si sahihi kusema CHADEMA ina shinda kwasababu tu ccm imechokwa, CDM imejipambanua kwa wananchi kama chama chenye kuleta matumaini zaidi na ukombozi wa kweli ma tatizo sugu yanayowakabili watanzania toka Uhuru na mengine mengi ya hovyo yaliyoasisiwa na ccm kama Ufisadi, Chama kukosa viongozi wenye uwezo wa kuongoza na kazi za siasa kufanywa na polisi, chama kukabidhiwa genge la vijana wahuni wajifanyie wanachotaka na ccm kuwa kampuni badala ya chama cha umma.
Mkuu Bob G, hapo ndipo haswa ninapopataka.
Tangu tumepata uhuru, taifa letu limekuwa likikabiliwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi. CCM katika utawala wake wa miaka 50, imeweza kufanya abc na d kutatua matatizo hayo lakini imeshindwa na imeongeza maadui wengine wawili, rushwa na ufisadi!.

Chadema sasa inatakiwa ituambie yenyewe itafanya nini, how with what resources.
Mfano hili la Elimu, itatoa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kutumia resources from abcd. Vivyo hivyo itatoa huduma za afya bure, how kwa kutumia resources abc na d. Na katika kuondoa umasikini, itafanya abc na d vivyo hivyo katika ku deal na rushwa na mafisadi inaweza kuamua kutumia Beijing formular, ukikutwa, unathibitishwa na kugeuzwa history, kuwa ulikuwepo!. Ili 2015 watu tuichague Chadema for a reason besides kuichoka CCM!.
Pasco.
 
Hamy-D, kama unachungulia huu uzi utajifunza nini huu ndio uchambuzi wa Kisayansi, ambapo una-analyse na ku-evaluate badala ya kuja na propaganda zako kuwa CCM ndio wameshinda ktk chaguzi za udiwani.
 
Kuungana na Cuf au NCCR na TLP ni kujiangamiza na am sure hata hao wenyewe mamluki hawawezi kukubali kwani kazi yao ni kukwamisha demokrasia.
 
Mkuu Pasco, mimi nakubaliana na wewe kwenye mengi uliyosema, lakini mambo mawili sikubaliani nayo kimantiki na kiuhalisia.

1) Kwamba kila ukiangalia huoni kitu ilichofanya CHADEMA, lakini CCM inafanya vitu, huku ukitolea mfano wa barabara ya Morogoro na Fly-overs za Ubungo zinatengenezwa na CCM wakati CHADEMA hawajafanya kitu.
Mkuu, ulinganisho wa CCM na CHADEMA kwa mizaia hiyo ni potofu na kuendelea kuhubiri habari hiyo ni muendelezo wa siasa chafu za CCM. Serikali inajenga barabara sio chama cha siasa katika ulinganifu huu.

2) Kwamba CHADEMA wanachaguliwa kwasababu watu wameichoka CCM, This is another twisted opinion - twisted with a purpose to mislead. If that is the case, kwanini wasichague TLP au CUF? Have you ever bothered to think about that sir?
CHADEMA inapigana usiku na mchana na M4C. Inatoa eliu ya uraia na kuwaeleza wananchi nini hasa tatizo la serikali hii ya CCM kwenye nchi tajiri kama Tanzania kwenye natural resources lakini yenye watu masikini zaidi.

Kazi iliyofanywa na M4C kwa miaka miwili inaonekana sasa. Lakini wewe Pasco, sir, hutaki kuona hilo. Unafikiri CHADEMA wanavuna wasipopanda. You are wrong, again.

cc: Ngongo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzizi wa Mbuyu, solid reasons are given na sio za kuuliza kama mtu anaona au haoni!. Hili swali la solid reasons nimekuwa nikiliuliza tangu ushindi wa Chadema wa 2010 kwenye baadhi ya maeneo, nikasema Chadema imeshinda kwa sababu CCM imechokwa ns sio imeshinda kwa sababu imejipanga kwa ushindi huo kwa sababu maalum za kushinda!.

Kuelekea 2015, we need more than this!, we need solid reasons why Chadema, not why not CCM!.
Kama unazo sababu why Chadema besides why not CCM ndizo zianze kuhubiriwa sasa kuelekea 2015, Chadema ikabidhiwe Ikulu kwa sababu hizo na sio kwa sababu CCM imeshindwa kufanya abcd bali kwa sababu Chadema itafanya abcna d kwa kutumia resources kuytoka abcd, ether kwa kubana matumizi abcd, hivyo kuokoa kiasi abcd cha fedha kitakacho tumika kufan ya abc na d, au CCM imekuwa haikusanyi kodi abcd katika maeneo haya abcna d au Chadema itaanzisha vyanzo vipya vya mapato abcd, vitakavyozalisha abcd na kayatumia mapato hayo kufanya abcd etc, etc, giving out reasons za kuichagua Chadema!.

Hizi ndizo mimi ninazoziita politics of sustainability na sio just politics of politiking!.

Pasco.

Unachokitaka CHADEMA mbona wanfanya sana Pascal! Rejea kampeni za Dr Slaa 2010.....alifikia kusema hai bei ya mfuko wa smenti utauzwa shilingi ngapi..!
Bungeni kina Tundu Lissu kila wakati bungeni wamekuwa wakitmka wazi nini kinatakiwa kifanywee a serikali.....kwa mfano...walililia sana kuipa uhuru mahakama...lakini weabunge wa CCM wakatumia wingi wao wakapitisha zisimamiwe na wakuu wa wilaya.... Pasco wananchi wanaona hayo...na ndio maana wanaikubali sana CDM!

Pia umesahau kujiuliza kitu kingine cha wazi mno.....kwanini CHADEMA na si CUF wala CHAUSTA?
 
Mkuu Bob G, hapo ndipo haswa ninapopataka.
Tangu tumepata uhuru, taifa letu limekuwa likikabiliwa na maadui wakuu watatu, ujinga, umasikini na maradhi. CCM katika utawala wake wa miaka 50, imeweza kufanya abc na d kutatua matatizo hayo lakini imeshindwa na imeongeza maadui wengine wawili, rushwa na ufisadi!.

Chadema sasa inatakiwa ituambie yenyewe itafanya nini, how with what resources.
Mfano hili la Elimu, itatoa elimu bure hadi chuo kikuu, kwa kutumia resources from abcd. Vivyo hivyo itatoa huduma za afya bure, how kwa kutumia resources abc na d. Na katika kuondoa umasikini, itafanya abc na d vivyo hivyo katika ku deal na rushwa na mafisadi inaweza kuamua kutumia Beijing formular, ukikutwa, unathibitishwa na kugeuzwa history, kuwa ulikuwepo!. Ili 2015 watu tuichague Chadema for a reason besides kuichoka CCM!.
Pasco.
CCM imechokwa for a reason. People are Hoping CHADEMA will correct the mess created by CCM in the last 50 year.
Sasa lazima tuangalie sababu za msingi za kuchagua CHADEMA, CHADEMA inasema nini kwenye ukusanyaji wa kodi, priority areas kama Elimu, na Afya, wanasemaje kuhusu sera ya nishati na madini, wanasema nini kuhusu sera ya mafuta na gesi?.
 
for the first time in last 12 months tumepata mtu anayeweka analysis ambayo ni ya kisomi, yenye takwimu na isiyopendelea wala kushabikia upande wowote..THANKS MTU WA SHAMBA Kwa kutupa uwanja wa kujadili kwa kuzifikirisha bongo zetu na sasa ninadhani ni ruhsa kwa wale wanaofikiri ki-vyama kuikokotoa post kwa mitazamo ya mapenzi ya vyama vyao.
1.KWANZA NIANZE NA NAFASI YA CCM KATIKA SIASA ZA TANZANIA KATIKA MIAKA 5 ILIYOPITA.
ni mtu mjinga tu na asiyependa kukubali ukweli atakayekataa kuwa ndani ya miaka mitano iliyopita CCM imekutana na changamoto kubwa kiushindani kuliko kipindi chochote katika historia yake.
ni katika kipindi hiki ambako zile kashfa kubwa zilizofanyika katika utawala wa awamu ya tatu(under mkapa regime) zilihamia kwenye majukwaa ya siasa na muhanga mkubwa akawa ni CCM(na ilistahili) na katika kipindi hiki ndio chama cha CHADEMA kikawa na safu ya watu wenye uwezo wa kujenga hoja na kushawishi hadhira hata kama hoja waliokuwa wanaiongelea ni UZUSHI NA UONGO MTUPU.. kwa kubweteka na kudhani ukubwa na ukongwe wake ndio immunity!! CCM ikawa imapuuza na kuzibeza harakati za CDM bila kuona athari za waziwazi katika kupoteza uungwaji mkono miongoni mwa wananchi. mpaka walivyokuja kushituka CDM ikawa imekwisha pata nguvu katika maeneo mengi ya mijini hapa nchini na kujizolea wafuasi wengi.
kikubwa kinachoiweka CCM katika hadhi tofauti na vyama vingine na kukifanya kuwa chama tawala kwa miongo kadhaa ijayo ni UWEZO MKUBWA WA KUHIMILI MISUKOSUKO, KASHFA. MIFARAKANO BAINA YA VIONGOZI, DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA NA KUPIMA UPEPO WA MATUKIO NA JINSI YA KU-DEAL NAYO.
hapa ndipo CCM inapopewa credity na mchambuzi yeyote wa kisiasa, imeweza kuhimili mashambulizi mfulizo tena ya kiwango cha kutisha toka CDM, imeweza kuhimili migongano na minyukano miongoni mwa viongozi wake waandamizi na imeweza kuhimili vuguvugu la mabadiliko linaloendelea kote duniani bila kutetereka.
kwa anayejua kuzifuatilia siasa za tz, hivi sasa ataona kuwa CCM hawajihami tena dhidi ya mashambulizi toka chadema bali wao nao wameshaanza kushambulia. athari za mashambulizi ya CCM kwa CHADEMA ziko wazi, ile taswira ya CHADEMA mbele ya jamii imeshaanza kuchafuka, kuna watu wengi tuu miongoni mwa watz ambao wanaiangalia CDM kwa jicho la MASHAKA na nina hakika hata ile EXPANSION YA chadema imeshadhibitiwa na kitakachofuata ni kuondolewa taratibu katika yale maeneo waliyoyateka( ntakuja na ushahidi kuhusu hili siku nyingine).
2. UZUSHI JUU YA CHADEMA KUENEA KUTOKA VIJIJINI KUELEKEA MIJINI

Nadhani tuwe wakweli kwa kulinganisha mambo kutokana na uhalisia wake,
leo hii, ARUSHA, MBEYA, MWANZA na DODOMA ni majiji kama lilivyo DAR ES SALAAM. kuita kuenea kwa CHADEMA toka maeneo hayo eti ni kupanuka toka vijijini na kuelekea mjini ni uongo wa wazi. labda tuipate upya tafsiri ya neno MJI na KIJIJI, Lakini kwa tafsiri tunayoijua kwa ujumla, huwezi ukasema MSIGWA,SUGU,G.LEMA,NDESAMBURO,WENJE na wengineo eti wanawakilisha watu wa vijijini pale bungeni.
ukweli ni kwamba,CHADEMA kama vilivyo vyama vyote vaya kisasa duniani, vinakubalika zaidi mijini na kama kupanuka vinapanuka toka mijini kuelekea vijijini na hata uchaguzi wa 2010 unadhihirisha na kuonyesha direction of expansion ya chama kama utaangalia kwa makini.
3. KINACHOIANGUSHA CHADEMA NA KUIPA NGUVU KUBWA CCM HUKO TUENDAKO
kama nilivyatangulia kusema hapo mwanzo, kwamba CCM wako in OFFENSIVE, ni wazi mashambulizi yao wanayaelekeza kwa CHADEMA. na chadema hawatakubali kamwe kukaa tu bila kujilinda na kujitetea kutokana na mashambulizi toka CCM, hivyo basi mkakati wao wa kushambulia utakuwa paralysed kwa sababu hawana ENOUGH ORGANISED TEAM TO DEFEND AND ATTACK AT THE SAME TIME(offence/diffence). na hilo limedhihirika jinsi ambavyo KUANZIA UONGOZI WA JUU KABISA WA CHADEMA hadi makada wa chini kabisa wanavyohangaishwa na mtu mmoja tu toaka CCM anayeitwa MWINGULU NCHEMBA. huu ni udhaifu mkubwa sana kitimu na kitaasisi. leo hii kama CCM itaanza mashambulizi toka kwa watu wengi tofauti wenye mtindo wa mwingulu nchemba, ni wazi kabisa CHADEMA kita-collapse ndani ya muda mfupi sana. kigezo cha pili ni jinsi ambavyo CHADEMA bado zinawekeza nguvu nyingi kupita kiasi katika maeneo ambayo walishayatangaza kuwa ni ngome zao( hii inaonyesha bado hawajajiamini katika ulinzi wa ngome zao na kwamba muda wowote ngome zinaweza kutekwa). rejea uchaguzi wa madiwani wa arusha ulioisha jana.hii inawapunguzia sana nguvu ya kujitanua na kutengeneza ngome mpya na hivyo kuendelea kuwa grounded on the same grounds and never expand.
4. KAULI ZA VIONGOZI NA WAFUASI WA CHADEMA NI KUROPOKA NA KUASHIRIA SHARI
Kuna dhana imejengeka miongoni mwa viongozi wa chadema na wafuasi wao kuwa eti'WATU WAMECHOKA'.
WAMESAHAU KUWA HAKUMA MWANADAMU ANAYECHOKA KUISHI.Wanapopata wafuasi katika mikutano yao ya hadhara wanajenga taswira kuwa wale ni mbuzi/farai/nguruwe wasio na akili ambao wakiambiwa chochote watakifuata. na kwa kujidanganya huko, wamejenga kiburi na majivuno juu ya dhana kwamba wao wako juu ya sheria, wanaweza kusema na kutenda lolote kwa sababu eti PEOPLE'S POWER iko nyuma yao.
wamefikia hatua ya kutunga uongo na kuuamini wenyewe, kufarakana kwa makusudi na vyombo vya ulinzi na usalama, kuchochea ghasia na maasi, kuchochea watu kutokufanya kazi wala kuchangia shuhuli za maendeleo na kufurahia pale serikali inaposhindwa kutumikia ipasavyo wananchi.
hawa viongozi na wafuasi wa chadema, wameshajitenga na taifa hili la tanzania na wako sambamba na maadui wa nchi yetu eti kwa sababu tu tanzania iko chini ya utawala wa CCM!!!! kamwe hawashangilii neema yoyote inayopatikana tanzania, hawaoni lolote jema chini ya anga la tanzania,wako tayari kujiunga na jeshi la (MSEVEN/KAGAME/BANDA/KENYATA) au yeyote atakayetaka kutushambulia kwa vile tu tuko chini ya utawala wa CCM. NA hili tunaliona humu J.F na tunawasikia hata mitaani jinsi ambavyo wanaropoka kauli ambazo zinakikosesha chadema sifa za kuwa mbadala wa CCM.
Nilipata kuwa katika miji mikubwa ya ZAMBIA wakati LEVY MWANAWASA akishinda uchaguzi katika awamu ya pili na jinsi PF(PATRIOTIC FRONT) KILIVYOKUWA kinazidi kujitanua kuelekea vijijini, nilishuhudia jinsi matokeo ya kushindwa kule yalivyowapa furaha na matumaini ya ushindi baada ya miaka mingine mitano, na katika bahati isiyo ya kawaida, nikawepo tena wakati MICHAEL CHILUFYA SATA na PF yake walivyoshinda ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa miaka 3 iliyopita.
dicpline katika utendaji na kutanguliza uzalendo ndio mambo ambayo waafrica wengi wanayataka.waafrica wengi wameshachoshwa na vita na mapigano ambayo yanawafaidisha wanasiasa.
kwa kiburi cha uongozi wa chadema pamoja na wafuasi wao,leo hii wameshakinasibisha chama chao na vurugu, ghasia na vita. na hawachukui hatua yoyote ya kuzuia hali hiyo zaidi ya kujenga mazingira ya kuthibitisha kuwa wao(chadema) wamejipanga kivita zaidi kuliko kujipanga kisiasa. hali hii inawatia doa na kuondoa umaarufu wao katika hadhi ya chadema.
mmetegewa mtego nanyi mmeingia kichwa kichwa na kitanzi kimekaa tayari shingoni.
noja niwafumbue macho kidogo......
watu wenye busara zao ndani ya taifa hili walishaiona dhamira chafu ya waasisi wa chadema tangu mwanzo. ila kwa sababu walitaka kuijua kwa ushahidi, wakaamua muendelee kufanya siasa zenu bila bughudha ili ile dhamira yenu ije kuonekana wazi.
mkafika mahali mkabweteka, mkajidanganya kuwa raisi J.K ni dhaifu na hivyo mkaamua kujiachia na kujisahau na mwisho mmeonyesha hata zile dhamira zilizojificha. mmejivua nguo mbele ya jamii ambayo ilishaanza kuwategemea, mmejiweka katika hali ngumu ya kuelekea anguko ambalo litaifanya CHADEMA IWE HISTORIA.
MMECHAGUA UPANDE WA MACHAFUKO NDANI YA NCHI AMBAYO HAKUNA MACHAFUKO NA WATU WAKE NI WAPENDA AMANI???
Hilo ni kosa amabalo mtakuja kulijutia milele.
 
notradamme Mkuu umejitahidi sana kupotosha baadhi ya mambo mengi katika uchambuzi wako.Kwanza ni makosa sana kuihusisha Chadema na vurugu.Ingekuwa vizuri ukatambua kwanza nini maana ya vurugu na chanzo chake ni kipi.(VURUGU-kuvunja/kuharibu utaratibu flani/kufanya mambo kinyume).

Kwa tafsiri hiyo ndogo nnaomba tujiulize kati ya CHADEMA/police na Serikali kuu ni nani anafanya vurugu.Kwa mujibu wa katiba yetu inaturuhusu kukusanyika/kujadiliana na inatutaka tu kutoa TAARIFA kwa jeshi la police ili watupatie wananchi haki yetu ya kulindwa.Chadema wanatoa matangazo kwa raia kuhusu mkutano na wananchi wanaitikia mwito,tatizo linakuja kwa police na Serikali.Police wanatoa katazo la kutokufanya mkusanyiko wowote(kumbuka police hawana mamlaka ya kuzuia mkusanyiko wao hupewa TAARIFA tu).Wanapokuja na kulipua mabomu ya machozi na risasi za moto kisa kutawanya mkutano halali(kwa mujibu wa katiba yetu)ni nani kati ya hawa(police/Chadema/Serikali)wanafanya fujo-kuvuruga utaratibu?

Mlipuko wa bomu Arusha uliosababisha maisha ya watu kupotea tuliona fujo za police/ccm/Seikali.Lukuvi aliamka Bungeni na kuudanganya uma,Nape nae aliibuka mbele ya waandishi wa habari na kudanganya uma na alifika mbali zaidi kwa kuitaja Chadema ndio wahusika wakuu.Police kupitia kwa Chagonja aliibuka na vitisho vya hali ya juu kwa viongozi wa Chadema kwa kuwataka wajisalimishe kwake utafikiri Mbowe na Lema ndio watuhumiwa wakuu.Police/Serikali/CCM ndio vyanzo vikuu vya vurugu nchini.

Tukio la Mwangosi police walimuua live bila chenga mwandishi wa habari Daudi Mwangosi mbele ya RPC Kamhanda na bila ya woga wakaja na sinenma yao kuwa waliomwua Mwangosi ni wafuasi wa CHADEMA na alikufa kutokana na kitu kizito kilichorushwa na hao wafuasi,TUNASHUKURU MUNGU PICHA ZILIWAUMBUA WAKIMUUA MWANGOSI picha likageuka na kumfungulia masitaka askari alieua na kichekesho zaidi wakampandisha cheo Kamhanda(kwa kusimamia mauaji).

Katika matukio yoote mabaya yanayofanywa juu ya Chadema ili mkiangamize hamtaweza asilani abadani,angaliana uchambue mambo kiuhalisia na sio kihisia zaidi.Kama chama cha CHADEMA ni hatari kwa nini msajili wa vyama vya siasa hajakifuta?Tuna matatizo mengi sana ya kujadili katika nchi hii tajiri inayonyonywa na Watawala(Mafisadi)wachache,Ushauri wa bure CCM pambaneni na matatizo yanayoikabili nchi hii acheni kupambana na chama cha CHADEMA.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mtu wa Shamba,
Kwanza asante sana kwa tathmini iliyokwenda shule.

Tathmini yako inaonyesha wazi CCM is loosing big time na Chadema id gaining big gain!.

Kwa upande wangu, kushinda au kushindwa ni matokeo, nataka nijikite zaidi katika the reasons behind that loss or gain kwa vyama viwili tuu, CCM na Chadema tuu!......
.....Mzee leo umetula sana...hongera
 
Wagombea wa Chadema wote Wachaga kweli hiki chama watu hawajakijua
 
Mkuu Mzizi wa Mbuyu, solid reasons are given na sio za kuuliza kama mtu anaona au haoni!. Hili swali la solid reasons nimekuwa nikiliuliza tangu ushindi wa Chadema wa 2010 kwenye baadhi ya maeneo, nikasema Chadema imeshinda kwa sababu CCM imechokwa ns sio imeshinda kwa sababu imejipanga kwa ushindi huo kwa sababu maalum za kushinda!.

Kuelekea 2015, we need more than this!, we need solid reasons why Chadema, not why not CCM!.
Kama unazo sababu why Chadema besides why not CCM ndizo zianze kuhubiriwa sasa kuelekea 2015, Chadema ikabidhiwe Ikulu kwa sababu hizo na sio kwa sababu CCM imeshindwa kufanya abcd bali kwa sababu Chadema itafanya abcna d kwa kutumia resources kuytoka abcd, ether kwa kubana matumizi abcd, hivyo kuokoa kiasi abcd cha fedha kitakacho tumika kufan ya abc na d, au CCM imekuwa haikusanyi kodi abcd katika maeneo haya abcna d au Chadema itaanzisha vyanzo vipya vya mapato abcd, vitakavyozalisha abcd na kayatumia mapato hayo kufanya abcd etc, etc, giving out reasons za kuichagua Chadema!.

Hizi ndizo mimi ninazoziita politics of sustainability na sio just politics of politiking!.

Pasco.

Tunapoongelea kuchaguliwa au kupata sifa ya kuaminiwa na wananchi si lazima uwe umefanya kitu. Na mpaka ufanye kitu ni mpaka upewe nafasi ya kufanya hivyo. Chadema hawajapewa nafasi ya kuongozwa dola ulitegemea labda wafanye nini?? Ili uweze kuongoza watu unaaminiwa kwanza kisha unapewa nafasi na kuaminiwa kunaanza kwa hoja na mipango ya jinsi mnavyoeleza sera zenu kwa watu. Ili uweze kukitathmini chama unaanzia huko kisha unakipa nafasi. Kujaribu kufananisha chama kilichokaa miaka 50 madarakani na chadema utakuwa unatafuta huruma ya kuhalalisha ccm iendelee kutawala kisa walishatawala. Chadema kimefufu tumaini la watanzania ambalo ccm wanaonekana kuzika na ukikumbuka kuwa siasa si maneno mengi na maswali mengi yasiyo na tija siasa ni mipango na mbinu vinginevyo utabakia na swali na jibu utapata kwanye uchaguzi. Ukitaka kujua mtu amekufanyia nini ni lazima umpe nafasi ya kufanya hilo utakalo kisha uhoji.
 
Scientific analysis! full of data which is readable and easy to understand. kimsingi CDM inakubalika zaidi na kwa kasi kuliko vyama vyote.wazo lako ni zuri lakini vyama vingine vya upinzani haviko serious! uweke umoja na CUF?TLP?NCCR? hawa wote ni ccm B! muhimu ni kuongeza kasi ya mapambano na kujiimarisha hasa vijijini,huko akina mama wapewe uongozi kwa lengo maalumu na walipwe. kwa kufanya hivyo tutajenga mtandao mpana zaidi
 
Wagombea wa Chadema wote Wachaga kweli hiki chama watu hawajakijua
Hata meya wa Arusha CCM ni mchaga pia.

Ajenda hizo ndio mnapaswa kujitafakari kama zinakijenga chama au zinakiongezea kukataliwa na kuchokwa.

Wapiga kura ndio wanaamua.
 
for the first time in last 12 months tumepata mtu anayeweka analysis ambayo ni ya kisomi, yenye takwimu na isiyopendelea wala kushabikia upande wowote..THANKS MTU WA SHAMBA Kwa kutupa uwanja wa kujadili kwa kuzifikirisha bongo zetu na sasa ninadhani ni ruhsa kwa wale wanaofikiri ki-vyama kuikokotoa post kwa mitazamo ya mapenzi ya vyama vyao.
1.KWANZA NIANZE NA NAFASI YA CCM KATIKA SIASA ZA TANZANIA KATIKA MIAKA 5 ILIYOPITA.
ni mtu mjinga tu na asiyependa kukubali ukweli atakayekataa kuwa ndani ya miaka mitano iliyopita CCM imekutana na changamoto kubwa kiushindani kuliko kipindi chochote katika historia yake.
ni katika kipindi hiki ambako zile kashfa kubwa zilizofanyika katika utawala wa awamu ya tatu(under mkapa regime) zilihamia kwenye majukwaa ya siasa na muhanga mkubwa akawa ni CCM(na ilistahili) na katika kipindi hiki ndio chama cha CHADEMA kikawa na safu ya watu wenye uwezo wa kujenga hoja na kushawishi hadhira hata kama hoja waliokuwa wanaiongelea ni UZUSHI NA UONGO MTUPU.. kwa kubweteka na kudhani ukubwa na ukongwe wake ndio immunity!! CCM ikawa imapuuza na kuzibeza harakati za CDM bila kuona athari za waziwazi katika kupoteza uungwaji mkono miongoni mwa wananchi. mpaka walivyokuja kushituka CDM ikawa imekwisha pata nguvu katika maeneo mengi ya mijini hapa nchini na kujizolea wafuasi wengi.
kikubwa kinachoiweka CCM katika hadhi tofauti na vyama vingine na kukifanya kuwa chama tawala kwa miongo kadhaa ijayo ni UWEZO MKUBWA WA KUHIMILI MISUKOSUKO, KASHFA. MIFARAKANO BAINA YA VIONGOZI, DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA NA KUPIMA UPEPO WA MATUKIO NA JINSI YA KU-DEAL NAYO.
hapa ndipo CCM inapopewa credity na mchambuzi yeyote wa kisiasa, imeweza kuhimili mashambulizi mfulizo tena ya kiwango cha kutisha toka CDM, imeweza kuhimili migongano na minyukano miongoni mwa viongozi wake waandamizi na imeweza kuhimili vuguvugu la mabadiliko linaloendelea kote duniani bila kutetereka.
kwa anayejua kuzifuatilia siasa za tz, hivi sasa ataona kuwa CCM hawajihami tena dhidi ya mashambulizi toka chadema bali wao nao wameshaanza kushambulia. athari za mashambulizi ya CCM kwa CHADEMA ziko wazi, ile taswira ya CHADEMA mbele ya jamii imeshaanza kuchafuka, kuna watu wengi tuu miongoni mwa watz ambao wanaiangalia CDM kwa jicho la MASHAKA na nina hakika hata ile EXPANSION YA chadema imeshadhibitiwa na kitakachofuata ni kuondolewa taratibu katika yale maeneo waliyoyateka( ntakuja na ushahidi kuhusu hili siku nyingine).
2. UZUSHI JUU YA CHADEMA KUENEA KUTOKA VIJIJINI KUELEKEA MIJINI

Nadhani tuwe wakweli kwa kulinganisha mambo kutokana na uhalisia wake,
leo hii, ARUSHA, MBEYA, MWANZA na DODOMA ni majiji kama lilivyo DAR ES SALAAM. kuita kuenea kwa CHADEMA toka maeneo hayo eti ni kupanuka toka vijijini na kuelekea mjini ni uongo wa wazi. labda tuipate upya tafsiri ya neno MJI na KIJIJI, Lakini kwa tafsiri tunayoijua kwa ujumla, huwezi ukasema MSIGWA,SUGU,G.LEMA,NDESAMBURO,WENJE na wengineo eti wanawakilisha watu wa vijijini pale bungeni.
ukweli ni kwamba,CHADEMA kama vilivyo vyama vyote vaya kisasa duniani, vinakubalika zaidi mijini na kama kupanuka vinapanuka toka mijini kuelekea vijijini na hata uchaguzi wa 2010 unadhihirisha na kuonyesha direction of expansion ya chama kama utaangalia kwa makini.
3. KINACHOIANGUSHA CHADEMA NA KUIPA NGUVU KUBWA CCM HUKO TUENDAKO
kama nilivyatangulia kusema hapo mwanzo, kwamba CCM wako in OFFENSIVE, ni wazi mashambulizi yao wanayaelekeza kwa CHADEMA. na chadema hawatakubali kamwe kukaa tu bila kujilinda na kujitetea kutokana na mashambulizi toka CCM, hivyo basi mkakati wao wa kushambulia utakuwa paralysed kwa sababu hawana ENOUGH ORGANISED TEAM TO DEFEND AND ATTACK AT THE SAME TIME(offence/diffence). na hilo limedhihirika jinsi ambavyo KUANZIA UONGOZI WA JUU KABISA WA CHADEMA hadi makada wa chini kabisa wanavyohangaishwa na mtu mmoja tu toaka CCM anayeitwa MWINGULU NCHEMBA. huu ni udhaifu mkubwa sana kitimu na kitaasisi. leo hii kama CCM itaanza mashambulizi toka kwa watu wengi tofauti wenye mtindo wa mwingulu nchemba, ni wazi kabisa CHADEMA kita-collapse ndani ya muda mfupi sana. kigezo cha pili ni jinsi ambavyo CHADEMA bado zinawekeza nguvu nyingi kupita kiasi katika maeneo ambayo walishayatangaza kuwa ni ngome zao( hii inaonyesha bado hawajajiamini katika ulinzi wa ngome zao na kwamba muda wowote ngome zinaweza kutekwa). rejea uchaguzi wa madiwani wa arusha ulioisha jana.hii inawapunguzia sana nguvu ya kujitanua na kutengeneza ngome mpya na hivyo kuendelea kuwa grounded on the same grounds and never expand.
4. KAULI ZA VIONGOZI NA WAFUASI WA CHADEMA NI KUROPOKA NA KUASHIRIA SHARI
Kuna dhana imejengeka miongoni mwa viongozi wa chadema na wafuasi wao kuwa eti'WATU WAMECHOKA'.
WAMESAHAU KUWA HAKUMA MWANADAMU ANAYECHOKA KUISHI.Wanapopata wafuasi katika mikutano yao ya hadhara wanajenga taswira kuwa wale ni mbuzi/farai/nguruwe wasio na akili ambao wakiambiwa chochote watakifuata. na kwa kujidanganya huko, wamejenga kiburi na majivuno juu ya dhana kwamba wao wako juu ya sheria, wanaweza kusema na kutenda lolote kwa sababu eti PEOPLE'S POWER iko nyuma yao.
wamefikia hatua ya kutunga uongo na kuuamini wenyewe, kufarakana kwa makusudi na vyombo vya ulinzi na usalama, kuchochea ghasia na maasi, kuchochea watu kutokufanya kazi wala kuchangia shuhuli za maendeleo na kufurahia pale serikali inaposhindwa kutumikia ipasavyo wananchi.
hawa viongozi na wafuasi wa chadema, wameshajitenga na taifa hili la tanzania na wako sambamba na maadui wa nchi yetu eti kwa sababu tu tanzania iko chini ya utawala wa CCM!!!! kamwe hawashangilii neema yoyote inayopatikana tanzania, hawaoni lolote jema chini ya anga la tanzania,wako tayari kujiunga na jeshi la (MSEVEN/KAGAME/BANDA/KENYATA) au yeyote atakayetaka kutushambulia kwa vile tu tuko chini ya utawala wa CCM. NA hili tunaliona humu J.F na tunawasikia hata mitaani jinsi ambavyo wanaropoka kauli ambazo zinakikosesha chadema sifa za kuwa mbadala wa CCM.
Nilipata kuwa katika miji mikubwa ya ZAMBIA wakati LEVY MWANAWASA akishinda uchaguzi katika awamu ya pili na jinsi PF(PATRIOTIC FRONT) KILIVYOKUWA kinazidi kujitanua kuelekea vijijini, nilishuhudia jinsi matokeo ya kushindwa kule yalivyowapa furaha na matumaini ya ushindi baada ya miaka mingine mitano, na katika bahati isiyo ya kawaida, nikawepo tena wakati MICHAEL CHILUFYA SATA na PF yake walivyoshinda ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa miaka 3 iliyopita.
dicpline katika utendaji na kutanguliza uzalendo ndio mambo ambayo waafrica wengi wanayataka.waafrica wengi wameshachoshwa na vita na mapigano ambayo yanawafaidisha wanasiasa.
kwa kiburi cha uongozi wa chadema pamoja na wafuasi wao,leo hii wameshakinasibisha chama chao na vurugu, ghasia na vita. na hawachukui hatua yoyote ya kuzuia hali hiyo zaidi ya kujenga mazingira ya kuthibitisha kuwa wao(chadema) wamejipanga kivita zaidi kuliko kujipanga kisiasa. hali hii inawatia doa na kuondoa umaarufu wao katika hadhi ya chadema.
mmetegewa mtego nanyi mmeingia kichwa kichwa na kitanzi kimekaa tayari shingoni.
noja niwafumbue macho kidogo......
watu wenye busara zao ndani ya taifa hili walishaiona dhamira chafu ya waasisi wa chadema tangu mwanzo. ila kwa sababu walitaka kuijua kwa ushahidi, wakaamua muendelee kufanya siasa zenu bila bughudha ili ile dhamira yenu ije kuonekana wazi.
mkafika mahali mkabweteka, mkajidanganya kuwa raisi J.K ni dhaifu na hivyo mkaamua kujiachia na kujisahau na mwisho mmeonyesha hata zile dhamira zilizojificha. mmejivua nguo mbele ya jamii ambayo ilishaanza kuwategemea, mmejiweka katika hali ngumu ya kuelekea anguko ambalo litaifanya CHADEMA IWE HISTORIA.
MMECHAGUA UPANDE WA MACHAFUKO NDANI YA NCHI AMBAYO HAKUNA MACHAFUKO NA WATU WAKE NI WAPENDA AMANI???
Hilo ni kosa amabalo mtakuja kulijutia milele.
Asante mkuu kwa mchango wako.

Naomba nikujibu kwenye namba 3 na 4.
Ni kweli CCM wanaishambulia Chadema. Lakini wanaishambuliaje? Nilivyoshuhudia kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mashambulizi yameelekezwa

1.Kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Chadema ni Wahalifu. Hili linafanyika kwa kufungua kesi nyingi, ambazo kwa bahati mbaya nyingi zinaishia kufutwa kwa kukosa ushahidi, hatimaye madhara ya shambulio yanarudi kwa CCM wenyewe.
2. Kuhusisha Chadema na fujo na mauaji. Hili pia linaweza kuwa limeaminiwa na watu wa CCM na wengine ambao hawakujipa muda wa kutafakari vizuri. Kwanza Polisi haruhusiwi kutumia risasi za moto isipokuwa katika mazingira ambayo wanalazimika kujilinda maisha yao, au mhalifu hatari anapojaribu kutoroka na hapo wanapaswa kulenga miguuni. Polisi wanapoua katika mazingira kama aliyouawa Mwangosi, hilo ni doa kwa serikali na polisi wenyewe kwani askari 7 walio na silaha wamekamata mtu asiye na silaha, hakukuwa na hoja ya kujilinda. Hili nalo linaichafua serikali na chama cha mapinduzi.

Ndio maana Chadema waliomba uchunguzi ufanywe na Tume Huru ya Kimahakama kubainisha kama ni Chadema wanahusika na mauaji hayo au la? Kwa nini serikali haiundi tume hiyo?

3. Propaganda ya Udini na Ukabila: Hii pia imeigeuka CCM kwani watu wanaona watu kama akina Zito Kabwe, Prof. Safari, na vijana kama akina mohamed Mtoi ni wanachama na wana nafasi yao kama wanachama, na hata uongozi.

4. Mashambulizi binafsi hasa kwa Dr. Slaa, Mbowe na Lema. Haya naomba wewe mwenyewe ufanye tathmini yako binafsi uone kama yameijenga CCM na kuidhoofisha Chadema.

5. Hicho unachoita dhamira chafu mimi sijakiona. Mimi nina watu wengi sana wasomi na waelewa wa mambo na wengine wamo serikalini na kwenye vyombo vya dola, lakini tunapoongea hakuna anayeisema hiyo dhamira chafu. Labda uwe wazi ni dhamira ipi chafu?

6. Mengi yanayopigiwa propaganda juu ya uhalifu wa Chadema, kama yangekuwa na ukweli yangepelekwa kwenye mkondo wa shéria na si kwenye majukwaa ya siasa. Kwenye mkondo wa sheria kwa sababu sheria ya vyama vya siasa inakataza kusajili chama cha UGAIDI, UKABILA, UDINI, FUJO. Jiulize kwa nini mambo ya kisheria yafanywe ya kisiasa kama si propaganda?

Naomba niseme kuwa iwapo wewe bado kwa dhati unaamini kuwa Mwigulu Nchemba anajenga chama, na iwapo huu ndio msimamo wa wana CCM walio wengi, na kwamba mmeridhika kuwa ndio mkakati wa kuiua Chadema, nakwambia kuwa endeleeni kumtumia, na endeleeni kutumia mbinu hizo hizo. Lakini badala ya kuua Chadema mtaua CCM.

Chama cha siasa ni lazima kitengeneze mvuto kwa wananchi. Mkakati wenye mapato ya muda mrefu ni ule unaoshawishi watu wakipende chama kwa mazuri yake, na si kwa mabaya ya wapinzani wake. Chama cha siasa chenye malengo ya muda mrefu, ni lazima kiwe na ajenda za kujiuza chenyewe na mara moja moja kuonyesha udhaifu wa wapinzani wake. Alichofanya Mwigulu Arusha, kuonyesha kuwa Chadema ni wauaji, Chadema ni waongo, Chadema ni wafanya fujo, Chadema wanataka kula Halmashauri kilisikika kwa watu. Lakini Mwigulu alipoteza fursa ya kuelezea uzuri wa CCM na mipango ambayo CCM wanayo kwa wana Arusha.

CCM ikiona umuhimu wa kutathmini haya ni vema, la sivyo mtaendelea kushangaa kwenye masanduku ya kura, huku mkiendelea kulia na propaganda zilizokataliwa na watu.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nakipongeza chama cha Chadema na madiwani na wabunge wa chama hiki kwa kujali zaidi maslahi ya wananchi na haya matokeo ndio zawadi au bahashishi kutoka kwa wananchi waliowaamini na wanaozidi kuwaamini,msirudi nyuma na harakati zenu nasi tupo pamoja nanyi katika kutimiza harakati za ukombozi wa taifa letu kutoka kwa mabepari wanaoendelea kutunyonya ila tunashukuru kwa kutoboa siri zao.
Pili idea yako mtoa mada ni nzuri sana ya kuungana vyama vya upinzani ila mimi nina wasiwasi mmoja muungano utadhoofisha CDM,sababu nikiangalia hivi vyama vingine wanang'ata na kupuliza nahisi si wapinzani wa ukweli hivyo hata wakiungana wataendelea kua vibaraka wa CCM,mimi ninachoona Chadema waendelee na harakati zao za kweli na wananchi washawaelewa bado kitambo kidogo itachukua nchi na kuwaelekeza ccm jinsi ya kuongoza ili hata wakirudi one day wasiongoze kwa mtindo wanaofanya sasa.
 
Mkuu Mtu wa Shamba congrats kwa analysis nzuri na yenye kueleweka. Hope Ma-researchers wanaweza kuanzia hapa na kutengeneza Hypotheses ili kujua ni sababu gani hasa zilizofanya TLP , CUF wapoteze viti vyao, CCM ipoteze 3 na CDM iongeze 5 na hawakupoteza hata kiti kimoja.
 
84 Reactions
Reply
Back
Top Bottom