Elections 2010 Chaguo Letu Bumbuli: January Makamba

Mzee Mwanakijiji jifunze kusema hivi "Let it go";

Wewe na mimi na wa2 wa Bumbuli yanatuhusu nini? wewe ni mpiga kura wa jimbo hilo? hapana, wewe ni mwanachama wa CCM au chama chochote kilichosimamisha mgombea kwenye hilo jimbo? no... please mzee.
Mkuu Kasheshe, sometimes unatetea mno vitu ambavyo ni dhahiri vina fall out of principles. Leo hii unatetea hili, kesho na keshokutwa the same thing will play against you au watu uwapendao.

Kupita bila kupingwa si kuchaguliwa na wananchi. Kumbuka hata wakati wa Mchonga na Mwinyi bado watu tulikuwa tunapiga kura. Huu upindishaji wa sheria kuwafaa washikaji sasa hivi, ndiko huko kunaumiza Taifa letu na kutuletea utata mkubwa mbeleni.
 
Hebu nielimisheni mimi. Huku kupita bila kupingwa ina maana hakutakuwa na printed ballots za hao wagombea au vipi?
 
Hebu nielimisheni mimi. Huku kupita bila kupingwa ina maana hakutakuwa na printed ballots za hao wagombea au vipi?

..."kutakuwa na printed ballots za hao wagombea, maana order ilishawekwa... ila the likelihood for names of registered voters from that constituency to be used elsewhere is high"... just a theory!
 
Is just YES or NO

Kwa sheria gani? Mbona sheria inasema mgombea aliyepita bila kupingwa "ataonekana kuwa amechaguliwa" ?

PART III FINAL NOMINATION OF CANDIDATES FOR PARLIAMENTARY ELECTIONS


44. Unopposed Candidates Act No. 6 of 1992 s 19 Act No. 8 of 1995 s 6.

Where only one candidate is nominated for an election in a constituency such candidate shall be deemed to be elected and the commission shall, by notice in the Gazette declare him to have been elected.

Au sheria hii ina marekebisho mengine tusiyoyajua ambayo hatujayajadili ?
 
Kwa sheria gani? Mbona sheria inasema mgombea aliyepita bila kupingwa "ataonekana kuwa amechaguliwa" ?
In fact ni utashi tu ulionituma kuandika hivyo. Iwapo upo sahihi hapana haja ya kuendelea kujadili hoja hii. Cha msingi ni kuona kwa jinsi gani Wanabumbuli watakavyoweza kujiendeleza kupitia kwa January na CCM kwa ujumla.
 
In fact ni utashi tu ulionituma kuandika hivyo. Iwapo upo sahihi hapana haja ya kuendelea kujadili hoja hii. Cha msingi ni kuona kwa jinsi gani Wanabumbuli watakavyoweza kujiendeleza kupitia kwa January na CCM kwa ujumla.

...Hakuna Jipya. Mbunge aliyetoka hapo ni kutoka CCM na kwa miaka kumi na Tano 'aliyotawala' hakuwa na Jipya. January hatakuwa na jipya kwa kuwa anatumia ilani ile ile ya Chama chao. If anything, ni kuwaonea huruma tu Wana Bumbuli ambao wameshindwa angalau hata kusimamisha mtu wa chama kingine angalau kumtikisa tu...! Poor We.
 
...Hakuna Jipya. Mbunge aliyetoka hapo ni kutoka CCM na kwa miaka kumi na Tano 'aliyotawala' hakuwa na Jipya. January hatakuwa na jipya kwa kuwa anatumia ilani ile ile ya Chama chao. If anything, ni kuwaonea huruma tu Wana Bumbuli ambao wameshindwa angalau hata kusimamisha mtu wa chama kingine angalau kumtikisa tu...! Poor We.
Tatizo lako na wengi wa Watanzania mmezoea kulishwa! Hata kama angepata mshindani asingeweza kubadili tabia hii ya kilofa ya kulishwa lishwa tu.

Maendeleo ya mtu yanaanzia nyumbani kwake.
 
Source ya Picha: Michuzi​


BUMBULI-1.jpg


Need We Say More?​
Out of place. Wafungulie watu wa Bumbuli forum yao
 
Mchukia Fisadi,

..January Makamba hana mpinzani ktk nafasi ya ubunge jimbo la Bumbuli. kwa sasa hivi, anasubiri kuapishwa tu.

..Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, naye hakupata mpinzani kwa hiyo na yeye anasubiri Nov aapishwe.
JK, nalifahamu hilo na nimeliandika makusudi nikijua maumivu makubwa yanawasubiri wana Bumbuli kwa miaka 5. Tuombe uzima utajua nasema nini!
 
Swali tu..... hivi wananchi wakishapiga kura au mbunge akishapita, huwa wanarudi nyuma " kumfuatilia" kuona kawafanyia nini?
Najiuliza hili kwa maana uchaguzi ukishapita shamrashamra nazo huisha, watu wanarudi kwenye maisha yao. Utawasikia tena baada ya miaka mitano.Wapo wachache wanaowafuata wabunge wao kwa msaada kutatua matatizo yao binafsi ( ada za watoto, matibabu, nk).Hivyo basi January akipita bila kupingwa, akichaguliwa, wanachi wake wasitegemee miujiza.
 
WOS
Katiba imevunjwa hapo
hakuna mahala ambapo katiba inamtaja mbunge wa kupita bila kupingwa.
majambazi ndo wameshika usukani tegemea maumivu zaidi
 
WOS
Katiba imevunjwa hapo
hakuna mahala ambapo katiba inamtaja mbunge wa kupita bila kupingwa.
majambazi ndo wameshika usukani tegemea maumivu zaidi

Msanii,

You are right in this. Katiba inasema wabunge watachaguliwa. Wengine wataingia kwa kuteuliwa na rais. Lakini hakuna kitu kama "kupita bila kupingwa" na kuwa decreed au kuwa deemed to be a member of the parliament katika katiba yetu. Kitu hiki ndicho kilimsukuma Mwanakijiji rightly kuandika ile thread ya "Barua ya Wazi kwa Tume Ya Taifa ya Uchaguzi" in my opinion one of the best threads inayoonyesha umuhimu wa kuwa na forum hii.

Inaweza kufunguliwa kesi dhidi ya sheria kama hizi zilizo unconstitutional. No wonder wanataka kumfunga Mtikila kipindi hiki cha uchaguzi.

Nukuu kutoka katika katiba hii hapa chini

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977

(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977,
limezingatia na kuweka pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa katika Katiba
ya Muungano tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.

SEHEMU YA PILI.

WABUNGE, WILAYA YA UCHAGUZI NA UCHAGUZI WA WABUNGE

77.-(1) Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi watachaguliwa na wananchi kwa kufuata masharti ya Katiba hii na vile vile masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu Katiba hii inayoweka masharti kuhusu uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.

(2) Isipokuwa pale ambapo Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii au Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili hiyo, itaagiza vinginevyo, kutachaguliwa Mbunge mmoja tu katika jimbo la uchaguzi.

(3) Wagombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi watatakiwa watimize masharti yafuatayo-

(a) wawe wamependekezwa mmoja mmoja, na chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi katika jimbo hilo;
(b) wamewasilisha majina yao kwa Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Bunge au uliofafanuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

Bottom line kwa mujibu wa katiba, huwezi kuwa mbunge wa kuwakilisha jimbo bila kuchaguliwa na wananchi.
 
wewe inaonekana wazi kuwa upo usingizini. January amekuwa chaguo la Bumbuli kutokana na msimamo wake juu ya maendeleo ya Wanabumbuli na Watanzania kwa ujumla.

Katika karne hii, tunahitaji watu wa aina yake, ambao wanaweza kubadilisha maisha ya wengi katika kuelekea katika maendeleo binafsi na ya taifa kwa ujumla. Zaidi wananchi wa Bumbuli wameona kitu ambao wewe hujakiona!

yeah wananchi wa bumbuli smart sana
 
Back
Top Bottom