''Chagua moja, JF au mimi''

mysteryman

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
977
176
Ni kauli ya mpenzi wangu toka juzi hatuna story anasubiri jibu, nichague kuwa na yeye au jamii forums.....nakiri kuwa toka nimejiunga na JF ni mimi na simu,..simu na mimi, nikiamka jf, nikienda toilet jf, nikiwa na kazi zangu pia jf nipo nayo, nikilala jf pembeni, yaani sitaki kupitwa na kitu humu jf...sasa bibie kaseemaa wee mwishowe kachoka na kasusa kushiriki chochote na mimi mpaka nimpe jibu eti either nibaki na yeye au niendelee na jf....nifanyeje wanajamvi? Kiukweli nampenda sana lakini at this point kuiacha jamii forums ni ngumu pia...
 
Kumbe tuko wengi nilidhani ni mimi peke yangu, jana kachomoa betri ya simu kaificha halafu kasingizia mtoto! Kisa ni hicho hicho, hataki nisome na nikisoma kinachofurahisha hataki nicheke, nikicheka ananuna! Itabidi JF iwe na muda maalumu wa kui-access ili kuokoa ndoa!
 
Hahaha dah...hivi cjui wanafikiri na huku ni kama fb, nilijaribu kumwelewesha kwamba huku hakuna kutongoza wala hakuna kutag picha huku ni full nondo za kujadili taifa nk lakini waapi...
 
hata vitabu vya Mungu ivnasema " Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni Kaisari". hivyo hata wewe Bibie apewe nafasi yako ambayo ni ya muhimu na JP ipewe nafasi yake. Fanya hivyo usiwekeze zaidi JF utawezakosa yote.
 
Kiukweli jf ni ugonjwa mbaya sn,mie ilifikia mahali hata ule mda wa kusoma biblia na kusali ukachukulia na jf na hapo nilikuwa sijajiunga. Nilipojiunga siku za kwanza nikawa najikuta nalala usiku wa manane, nasahu kwenda lunch, mda mwingine nikiwa kwenye pc hata cm ikiita sisikii, yani ilimradi jf ikachukua mda wote.

Nashukuru Mungu nimeweza kujikontroo na sasa nina mda maalumu wa jf na naweza kufanya mambo yangu mengine. Nakushauri jitahidi kupanga mda maalumu wa kuwa jf na wa kuwa na mpenzi ili muende sawa!
 
Weka muda special kwa ajili ya mamaaaa na muda special kwa ajili ya JF, mfano mzuri ni mimi mwenyewe huwa nipo JF kama sina kipindi (nafundisha chuo kikuu fulani) Pia kama nipo busy huwa naiweka JF pembeni hadi nimalize lakini kabla ya kulala lazima niangalie leo kulikuwa na nini na kuchangia kidogo na kulala kwa ajili ya kesho kuwahi tena kazini. Hayo ndio maisha yangu kwa muda huu.

Okoa ndoa yako mkuu, mpe nafasi yake mkeo, msikilize kwani ana umuhimu pia katika maisha yako usiwasahau na watoto pia kama unao.
Pia mshawishi mkeo nae ajiunge huku JF ili aamini na aone ya kuwa hamna vitu vibaya unavyofanya huku JF.
 
JF !

JF wengine imetusaidia kuimarisha hu uhusiiano wenyewe!

Lazima kausaid kutokuwa addicted na mtandao kwa ujumla lakini sio kukulazimisha kuacha JF!
 
alikuepo member mmoja mwenye ID ya kike miezi fulani sijui alikua nani yule, akapost kwa nguvu saaana yaani kwa siku anaweza akawa na post zaidi ya mia moja halafu ghafla akapotea.

Sijui ilikuaje, labda na yeye kuna jambo lilimsibu, JF kweli ni nyumbani, hata wakiweka kiingilio cha bei gani, siiiachi JF, nina karibia miaka mitatu hapa jukwaani sasa lakini sijawahi kuwa bored ila maudhi sometimes ni sehemu ya raha yenyewe
 
Kumbe tuko wengi!mimi kwangu nilisuluhisha kwa kumwunganisha(join)jf!sa hivi ugomvi kwishney!yeye na pc yake mi ya kwangu!nawe fanya hivyo pia,utamu wa jf ukimkolea atanywea tu.
 
Weka muda special kwa ajili ya mamaaaa na muda special kwa ajili ya JF, mfano mzuri ni mimi mwenyewe huwa nipo JF kama sina kipindi (nafundisha chuo kikuu fulani) Pia kama nipo busy huwa naiweka JF pembeni hadi nimalize lakini kabla ya kulala lazima niangalie leo kulikuwa na nini na kuchangia kidogo na kulala kwa ajili ya kesho kuwahi tena kazini. Hayo ndio maisha yangu kwa muda huu.

Okoa ndoa yako mkuu, mpe nafasi yake mkeo, msikilize kwani ana umuhimu pia katika maisha yako usiwasahau na watoto pia kama unao.
Pia mshawishi mkeo nae ajiunge huku JF ili aamini na aone ya kuwa hamna vitu vibaya unavyofanya huku JF.

mi nna mark xamz.ila jf ipo kushoto!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom