Elections 2010 CHADEMA's Free Education Promise not a Hoax, a long awaited Response

Hata kama ni 1%, hii ina maana 1% wakilipia, system itakuwa na uwezo wa ku absorb 1% more ya wale wasioweza kujilipia, au (kwa mfano kama tukitimiza ndoto ya kusomesha wote, asiwepo asiyejiweza ambaye atakosa nafasi) hata kupeleka hizo funds katika kusomesha wasiojiweza vyuo vikuu, au hata kutumia hizo funds katika social services nyingine. Tusitake kujifanya kama tushamaliza matatizo yetu yote na hii elimu mpaka form six ndilo tatizo letu la mwisho, si kweli, tunahitaji kila senti tutakayoweza kuipata, serikali yetu haina fedha kwa hivyo. Na hata tukiweza kuongeza mapato ya kodi kuna mambo lukuki yanaisubiri kodi hiyo hiyo. Barabara, umeme, maji, afya you name it. Sasa kwa nini tusiwalipishe watu wenye uwezo wa kulipa?

Ni rahisi sana ku dismiss kwamba wenye uwezo ni wachache, lakini je ushawahi kujiuliza ungejisikiaje kama wewe ndiye ungekuwa huna uwezo halafu mwenye uwezo kachukua nafasi yako ?

Leo tukisema tuue Mtanzania hata mmoja utasema mtu mmoja ni idadi ndogo sana ukilinganisha na watanzania ? Vipi kama tukiamua kwamba mtu mmoja huyu awe wewe?

Kitu cha kujadili hapa, ni kwamba mwenye uwezo kujilipia kutolipishwa ni sawa au si sawa, one only has to look at our private schools and the type of lifestyles some kids live, hivi tunataka kujitwika mizigo ya kusomesha wote hawa bila sababu ya msingi ?
Uwezo wa kulipia for me is a relative term, Mengi anaweza kukuambia hawezi kulipia hiyo elimu cos anadaiwa loads of money na mabenki aliyokopa pesa. Mie naweza kuwa na milioni 50 lakini kutokana na mahitaji yangu nikashindwa kuafford kununua gari, it all depends pesa zangu zinamipangilio gani. Thats why free education for all will deal with all these complications.
 
Najua tofauti iliyopo kati ya funding na providing.

Ninachomaanisha katika hili ni ku-provide free education. Who funds is non of anyone's business.

Education has to be a main agenda in country's development. Hakuna society itakayokuwa bila good education to its people. Hata kama tuna matanio makubwa au madogo kiasi gani.

Siku hizi wanasema "kula na kulipa ndio mtindo wa kisasa" ukitaka kula bila kulipa na kusema " Who funds is non of anyone's business." kuna jina jipya siku hizi watakuita "mwanamme suruali".

Jokes aside, kama uko seroius huwezi kusema "nataka serikali isomeshe watu wote bure, sijali itapata wapi hela". Utataka serikali yako ijiingize katika biashara ya madawa ya kulevya, au kuifanya nchi iwe nuclear waste dump just because that will give it the funds to send all children of age to school, in the process killing them all by either narco-bullets or nuclear waste radiation ? Si umesema hujali hela zitatoka wapi, kwenye kuuza mdude na kukubali takataka za nuclear kuna hela nzuri tu nako.

Acheni utani wa kulazimisha vitu tu just because mnataka easy ride.
 
Uwezo wa kulipia for me is a relative term, Mengi anaweza kukuambia hawezi kulipia hiyo elimu cos anadaiwa loads of money na mabenki aliyokopa pesa. Mie naweza kuwa na milioni 50 lakini kutokana na mahitaji yangu nikashindwa kuafford kununua gari, it all depends pesa zangu zinamipangilio gani. Thats why free education for all will deal with all these complications.

Always looking for the easy way out, even if it is not economic. Hapa kuna hesabu za kufanywa, na tunategemea Mengi afanye elimu ya watoto wake priority kuliko madeni yake. Kama anaweza kulipa mishahara mamia ya wafanyakazi ataweza kuwalipia watoto wachache. Kama unataka kuleta excuses mbona kila mtu atakwambia anataka ile Benzi mpya ya mwakani S 700 na kwa hiyo hawezi kumlipia mtoto shule, bajeti ya shule ita affect lifestyle yake.
 
CHADEMA wana claim watakuja na a more efficient revenue collection system, ukiwa na an efficient revenue collection system utajua wananchi wako wana vipato gani, kulingana na vipato vyao unaweza kusema mtu yeyote mwenye kipato cha zaidi ya shilingi kadhaa kwa mwaka hatasomeshewa wanawe bure na serikali. Hii itahakikisha kina Rostam Aziz, Mengi na wengine wenye uwezo hawatasomeshewa watoto wao bure.

Kama una system nzuri ya revenue collection hili la kujua nani anaqualify na nani ha qualify si tatizo. Marekani watu mamia ya mamilioni lakini serikali inajua vipato halali vya watu, na hata ukidanganya kwenye tax returns kuhusu interest uliyomake kutoka kwenye bank account fulani, benki nayo inapeleka taarifa zako IRS wanafanya comparison.

Sisi hatujaweza hata kukusanya kodi vizuri tushaanza kuistretch matumizi yake.
Unachosema hapo juu ni sahihi kama kweli serikali inaweza kuestablish an efficient revenue collection system. However, it takes time to establish vipato vya kila mwananchi kwa usahihi. Hii inasababishwa na aina za shughuli zinazofanywa na wananchi na pia utambulisho uliopo kwa wananchi wote.

Nchi ambayo hadi sasa hakuna mwananchi hata mmoja mwenye utambulisho wa kudumu, sio rahisi sana kufikia lengo la kutambua nani anafanya nini na anapata kipato cha kiwango gani. Kama ikiwezekana, itasaidia sana kuboresha ukusanyaji wa revenue na kuhakikisha wananchi wenye uwezo mdogo wanawekewa mikakati ya kuwakwamua pale wanapohitaji msaada, si wa seriklai pekee bali hata kutoka kwa wananchi wenzao, na mashirika yanayojitolea kufanya hivyo.
 
Siku hizi wanasema "kula na kulipa ndio mtindo wa kisasa" ukitaka kula bila kulipa na kusema " Who funds is non of anyone's business." kuna jina jipya siku hizi watakuita "mwanamme suruali".
Kiranga, kuna majukumu ya msingi ya serikali. Serikali haiwezi kujitoa katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata haki sawa katika huduma zinazotolewa na serikali yake.

Haya mambo ya kula na kulipa ni sawa kwa taasisi za kibiashara (profit making organisations). Serikali pia inatakiwa kutegemea wananchi katika kukuza uchumi wake (nakubali hilo). Ila nayo ina wajibu wa kuhakikisha kuwa inatoa huduma kwa ukamilifu, usahihi na kwa malengo yanayoweza kuiongezea mapato zaidi (kupitia kodi) na kuhakikisha kuwa hali za wananchi wake zinakuwa bora zaidi. Kama serikali haiwezi kutekeleza majukumu yake hayo, ni vyema kuachia wengine wenye uwezo na nia ya kuyatekeleza. Hatutegemei serikali ijitoe katika kila kitu hadi kutoa huduma kwa wananchi, na kubaki kukusanya kodi za kuisaidia kupata vitafunio maofisini, kulipia warsha na matumizi mengine yasiyo ya msingi.


Jokes aside, kama uko seroius huwezi kusema "nataka serikali isomeshe watu wote bure, sijali itapata wapi hela". Utataka serikali yako ijiingize katika biashara ya madawa ya kulevya, au kuifanya nchi iwe nuclear waste dump just because that will give it the funds to send all children of age to school, in the process killing them all by either narco-bullets or nuclear waste radiation ? Si umesema hujali hela zitatoka wapi, kwenye kuuza mdude na kukubali takataka za nuclear kuna hela nzuri tu nako.

Acheni utani wa kulazimisha vitu tu just because mnataka easy ride.
Mimi sina haja ya kujua serikali ina/itajiwekea mikakati gani ya kupata mapato yake. So long as mapato hayo yanapatikana kwa njia halali na zinazokubalika kitaifa na kimataifa. Ikitafuta mapato hayo kwa kuangamiza ustawi wa jamii, tutaihukumu kwenye sanduku la kura muda utakapofika. Tunataka serikali iwajibike kwa wananchi wake kwa ukamilifu, na wananchi pia wawajibike kwa Taifa lao kwa ukamilifu.

Kuuliza kama serikali iingie kwenye biashara za madawa ya kulevya au kuifanya nchi iwe nuclear waste dump ni kujaribu kupotosha mjadala kwa makusudi. Kwa ufupi, nachukulia kauli zako hizo kuwa ni sarcastic na zinzojaribu kufupisha mjadala kwa hitimisho lisilo sahihi.

Unajua wazi kuwa njia hizo mbili ulizozitaja hapo juu si halali na haziendani na sheria, wala busara ya kawaida ya kulinda ustawi wa jamii na mazingira yao. Si njia nilizotegemea kuwa wewe Kiranga ungeweza kudhani ndizo zinazofaa kwa kuongeza pato la Taifa.

Mwanakijiji ameelezea kwa uchache tu sehemu ambazo serikali inafanya matumizi yasiyo na maana na ambazo zingeweza kuwezesha vijana wa nchi hii kupata elimu ya kutosha bure, walau hadi Form 6. Sina haja ya kuzirudia kwakuwa naamini umezisoma na kuzielewa. Naamini mjadala huu haukusudii kujaridu kutafuta visingizio vya mapato. Bali unajaribu kubainisha mapungufu ya vipaumbele vyetu katika matumizi ya mapato yaliyopo.

Nilielewa vyema sana challenges ambazo Mr. Tayari alizibainisha. Nazo ni kuweza kushawishi au kuepuka matakwa ya IMF na WB. Ameelezea pia umuhimu wa kutoa huduma hiyo kwa wasiojiweza tu. Hoja ambayo pia wewe umeielezea kwa kirefu. Na mimi pia sizipingi. Challenge hizo ni real.

Ila, ni challenge ambazo zinahitaji serikali iliyo pro-active ili kuweza kutetea mipango yake na inayoweza kubainisha kwa usahihi vipato vya watu wake.

Tusidanganyane kwa misingi ya kutetea hata yaliyo bayana kabisa.

Kesho serikali ikisema inaweza, nina uhakika utarudi hapa na kusema ni kweli inawezekana. Ni mpaka nani aseme kuwa inawezekana ndipo tuone kweli uwezekano upo? Narudia tena, ili tuendelee tunahitaji kujenga jamii iliyo na upeo bora zaidi, yenye kuweza kusimamia na kushirikiana na vyombo mbalimbali katika kutekeleza maazimio na mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Jamii mbumbumbu ni hatari na ni ya gharama kubwa kwa Taifa. Kama Elimu ni ghali, jaribu ujinga.
 
Ningependa wataalamu wanijibu yafuatayo.

1. Hizi arguments naona zime-base sana sana kwenye ada na wanafunzi waliopo sasa na affordability apart from that, je tunazo enough school to implement the policy iwapo kila mwenye umri huo akiitaka nafasi yake iwepo maana hio ndio maana ya free education for all. Na ni watanzania wangapi roughly account for those students. Au, ndio kuendeleza hulka yetu ya kelele tu.

2. Ningependa kufahamishwa idadi ya vijiji vilivyopo maana argument ime base sana kwenye rural ignorance na sidhani kama kuna shule ambazo zipo in existence aready katika vijiji vingi, hivyo new ones have to bebuilt. Realistically atuwezi jenga shule ya msingi na wala ya secondary katika kila kijiji hivyo wataalamu lazima wachague eneo moja ambalo lina almost equal distance hili shule ijengwe. kwa kuwa ni vijijini linakuja swala la transportation na nauli za kila siku maana atawakisema wawekewe usafiri(though i doubt if there will be enough buses to cover all the villages) je wazazi wanaweza lipa ada za usafiri kila siku au wapewe charity na hiyo pia.

3. Hata ukitatua usafiri watoto watapata muda wa kujisomea saa ngapi. There is no point kuwachosha watoto wengine kwenda shule tu itakuwa ni kama 'chore' based on travel distance. Halafu wakirudi jioni kuna kazi za nyumbani zina wasubiri (ukweli wa kimaisha kijijini). Sasa sijui watasoma saa ngapi na watakuwa watoto saa ngapi?

Tuwe realistic kwa hali ya vijijini hapo ni kujenga boarding schools if we are serious about fighting ignorance in those parts, na ukifanya hivyo zinakuja gharama nyingine ambazo hata kuzisema ni tabu. Hizi ni kama akili za 'Mwalimu JKN' kukurupuka bila ya kuifikiria the impact of the whole policy. Maana hapa atuja aanza hata kufikiria ya kuwa this is pro-poverty policy kwenye nchi ambayo hipo classified as poor already.

Hivyo there is no doubt the policy would prove to be popular. Kama mta somesha vijijini wote bure na mjini wasio na uwezo wa kuwapeleka watoto zao privatey watataka nafasi. Shule tena itabidi zijengwe kuwapatia nafasi sijui mna idadi ya dar-es-saalam tu, kuna wanafunzi wangapi hawaendi mashule kutokana na umaskini na kukosa kuchaguliwa darasa la saba. Na hata hizo shule za serikali tu zilipo so far zinafanya shift kuweza ku accomodate. Bado ujamfikiria mwalimu kwani yeye ni robot na achoki, bado mnahitaji walimu wengine ambao waweze jaza nafasi ya shule zitakazo kuja. Hivi si hawa walimu pia wanataka mishahara yao iongezwe, halafu vyote hivyo wenzetu mtafanya bure Haki-ya-Mungu na tuna ma expart wa Havard na Yale ambao wanasema it is possible. Wengine wamediriki kusema as soon as next July.
 
Always looking for the easy way out, even if it is not economic. Hapa kuna hesabu za kufanywa, na tunategemea Mengi afanye elimu ya watoto wake priority kuliko madeni yake. Kama anaweza kulipa mishahara mamia ya wafanyakazi ataweza kuwalipia watoto wachache. Kama unataka kuleta excuses mbona kila mtu atakwambia anataka ile Benzi mpya ya mwakani S 700 na kwa hiyo hawezi kumlipia mtoto shule, bajeti ya shule ita affect lifestyle yake.

Bado you are hitting around the bush Kiranga, swala langu lipo pale pale uwezo wa kulipa ni relative connotation, kwanza huwezi kumpangia wewe Mengi kuwa priority yake iwe elimu kwa watoto kuliko madeni wakati madeni ndo yanayoendesha shughuli zake na hata masomo ya watoto wake. Yeye ndiye anayechagua priorities zake na sio wewe Kiranga. So bado tunarudi palepale, anaweza kuona ni bora watoto wasome public school wakati anasave pesa ya kuwasomesha University. Ni choice ya mtu na kwa sababu anachangia kodi kubwa ya elimu hiyo ni mtu asiyefikiri vizuri anayeweza kutunga policy ya kumbagua.

Nevertheless, its more likely that people like Mengi will not send their children to public schools because of where they have positioned themselves in the society interms of social status or class if you like.

Na ndio maana Toyota Vits is a good car lakini 50 Cents would go for Mercedes S 700.
 
Wakuu zangu,
Naona maswali mengi yanalenga kutoelewa maana ya ELIMU BURE kwa wote. Mnakuja na tafsiri zenu wenyewe kwa jinsi mnavyofikiria badala ya kuelewa kwanza maana ya elimu bure kwa wote inasimamia maudhui gani. Ni sawa na kubisha Usawa wa binadamu kwa kuzungumzia kwamba mwanamke hawezi kuwa mwanamme ukashindwa ku address kinachozungumziwa ktk usawa wa gender equality.

Kwanza labda niwakumbushe tu kwamba Tanzania ni nchi iliyokubuhu kwa Ufisadi, hii habari ya elimu bure kwa watoto wetu hadi form six imekuwa pigo kubwa sana kwa CCM kiasi kwamba wanatafuta pa kutokea lakini wanajua fika kwamba INAWEZEKANA. Ni Ufisadi peke yake unaofanya kila kitu hakiwezekani nchini, sasa kama CCM wanashindwa elimu bure kwa watoto wetu ni kipi hasa wanachokiweza!.

Kama alivyosema Mwanakijiji toka mwanzo elimu ya shule ya msingi leo hii ni bure lakini hakuna mtu aliyesema Mengi alilazimika kupeleka watoto wake shule ya bure! tena mnakumbuka awamu ya kwanza ya Mkapa mlisema hivyo hivyo kwamba elimu ya bure -Haiwezekani na ndio maana ikafutwa. Serikali ikaweka ada kwa watoto wa shule za msingi matokeo yake watoto waliojiandikisha shule ilishuka hadi kufikia low record ya taifa. Na kibaya zaidi over 50% kati yao hawakuweza hata kumaliza darasa la saba, tukarudi ktk mpango huu wa kutoa elimu ya msingi bure na tumejifunza makosa.

Tulipotangaza elimu bure ya msingi haikuwa overnight achievement, ila policy ilipita awamu ya pili ya Mkapa na hadi leo tumefikia kiwango ambacho karibu asilimi 98 ya watoto wanaotakiwa kuanza shule ya msingi wanajiandikisha kila mwaka pamoja na kwamba shule zetu bado hazijafikia kiwango kinachotakiwa.

Na hakika hatukuweza fikia mafanikio mazuri kwa sababu mimi naamini kwamba fedha nyingi za msaada wa MDGs pia zimeliwa.. Ipo haja kubwa ya kupitia matumizi ya fedha zile kwa sababu haiwezekani wananchi kulazimishwa kujenga shule za kata hali kuna fedha za msaada zilizotolewa kulingana na matumizi..

Nina hakika mkakati mzima wa MDG umepigwa panga la ajabu (ufisadi) na pengine labda niseme the all idea behind MDG ni famba kwa sababu ukitazama - To eradicate extreme poverty and hunger, sijui serikali ya Mkapa au Kikwete wamefanikiwa kiasi gani zaidi ya Umaskini kuzidi kiwango hata alichoacha Mwinyi.. Gender Equality and empower women - Malengo yamekuwa kuwaingiza wanawake ktk siasa yaani uuwiano kuwepo bungeni na utawala wa nchi yaani tunalenga kusiko kabisa.. - Combat HIV na Malaria hapo ndipo usiseme kabisa yaani fedha inaliwa kama hakuna jana na magonjwa ndio kwanza yanazidi na kusambaa vibaya sana. Hakuna mafanikio yoyote ambayo tunaweza yaweka mkononi kutokana na fedha lakini pia hatuwezi kudai kwamba HAIWEZEKANI kwa sababu hatuna fedha..Na toka lini fedha ikawa ndio msingi wa kuondoa matatizo yetu pasipo nia ya watalawa kuhakikisha tunaondokana na madhara haya.

Mimi nachoweza kusema inawezekana kabisa, Kwanza kabisa ni kila mwananchi kuwa na Social Security number ambayo ndiyo itakuwa TIN numba yake ya kulipia kodi. Kama leo hii wanaolipa kodi ni millioni 2 mpango huu ukikamilika tutakuwa na watu millioni 10 wakilipa kodi. Kinachotakiwa zaidi ni kuimarisha zaidi mpango mzima wa ukusanyaji kodi kuliko kufikiria kuongeza kodi zaidi kwa walipa kodi. Zipo nyumba kibao za kupangisha tena kwa dollar hawalipi kodi, Ufanisi wa kodi ktk imports na biashara bubu ambazo zote hizi ni revenues zinapotea.

Nachoweza kusema mimi ikiwa Nyerere aliweza chini ya Ujamaa usiokuwa na vyanzo vingi vya ukusanyaji kodi, masharti na sheria za IMF na World bank zilikuwa ngumu zaidi kupata mikopo yao, leo tupo ktk Utandawazi na soko huria, masharti mepesi zaidi, misamaha mikubwa tuimepewa yet tunashindwa hata kufikiwa mafanikio alokuwa nayo Nyerere ktk sekta ya elimu!. Nyote mnaoandika hapa ni wanafunzi wa Nyerere tena ajabu mmekuwa wasomi wazuri wenye kuweza kuzungumzia maswala ya elimu bure hali wenyewe ni matunda ya elimu hiyo..
Why, kwa nini msijivunia kwanza kitu kimoja by saying - Dude...U talking to free education graduate!
 
Shukran Mkandara kwa maelezo ya kutosha uliyotoa hapo juu.

Huwa nasikitika sana unapokutana na mtu mwenye uwezo wa kusoma anakuambia, "Nilishindwa kuendelea na masomo kwa kuwa Wazazi wangu hawakuwa na uwezo. Hivyo ikanipasa kuja mjini ili kutafuta maisha." Na maisha anayoyatafuta mjini ni magumu kupindukia. Ndio maana tunakuwa na watu wengi wanaotoka vijijini kukimbilia mijini ili kubangaiza ili angalau aweze kupata chochote cha kupeleka nyumbani (kijijini) kusaidia ndugu zake wanaoendelea kujitetea kwa maisha magumu na vile vile aweze kuokoa wadogo zake wasiishie kuwa kama yeye. Wengine huishia kuwa wahalifu na kupata hukumu ya dunia.

Madhara ya kushindwa kutoa elimu sawa kwa wote ni makubwa sana kuliko faida inayoweza kupatikana kwa kuchukua hatua hiyo muhimu.

Uoga wa kuitoa bure elimu hiyo sijui unatokea wapi. Wakati huu ambapo elimu ya msingi ni bure, mbona wenye uwezo hawawapeleki watoto wao kwenye hizo shule za bure? Mwenye uwezo wa kumlipia mtoto wake ada na matumizi mengine kwenye shule bora, hataacha kufanya hivyo kwa kuwa tu serikali imeamua kutoa elimu bure.
 
If at all these schools are successful and provide quality education, the limited resources devoted to this cause would attract even children from families with financial abilities to enroll in more expensive private schools. What this will mean ultimately is that, in a world of fixed and limited resources, any one chance snatched by the well off will mean one chance less for the people who cannot afford to pay. Instead of a convergence towards equality, the reverse will happen, with the haves having easier access to better education while some of the have nots (whose options are next to none) finding their chances taken by the haves (whose options are galore)

I suppose one could argue in a very academic way that, if at all the government is successful in creating adequate chances for all of our national needs, then in theory you would eliminate this shortage which may impact the have nots more than it will the haves. This is a very big if, so big so that giving the cause all the liberty one could afford and assuming a smoother than average performance, the transition to a full capacity enabled system will take at least a decade, a decade of peasants farmers not having enough schools simply because other people who can afford to pay for their education in these government schools or elsewhere are not doing so.

The only reason the haves would not enroll in these schools is if the schools do not provide a quality education. Not a good look.
And if the schools do provide a quality education, then they will attract people who do not need the government to pay for their education. Not a good look.

A poor country like ours must exhibit the most deliberate tendencies towards a sturdy frugality. The government should not pay for the education of any person who can afford to pay his/her way.

Promoting this unnecessary welfare handout from the nanny state far from creating equality, will actually leave more room for inequity than can reasonably be allowed.
Ndugu, hivi kuna mtu huwa anasomaga haya "magazeti" yako unayoyamwagaga humu jamvini???
Kwa mfano mimi sijasoma hapo juu kwa sababu najua fika utakachokuwa umekiandika lazima utakuwa uko afraid of something (as always).
Infact I see you as being afraid of your own shadow!!
 
Recta,
Mkuu wangu shukran sana kwani hawa vijana (20 yrs to 25) wanaobangaiza mijini na wengine majambazi sasa hivi ni kati ya wengi tuliwatupa miaka ya Mkapa. Na ndipo naposhindwa na UNAFIKI wa Mtanzania. hataki hata siku moja mwingine akafaidika na swala lolote kama yeye alivyoweza faidika. Apate yeye tu lakini sii mwingine yaani huu Ubinafsi sijui umetokea wapi kiasi kwamba tunathamini sana fedha na kuwa juu ya wengine ili wasifikie hadhi sawa nao.

Hata mimi sii mambo yote ndani ya sera za Chadema nakubaliana nayo, lakini hili la elimu kwa wananchi wake kusema kweli najua fika kabisa kwamba nchi yeyote pasipo kuwahakikishia elimu, haiwezi kuweka ahadi za maisha bora kwa kila mwananchi. Na kila kitu kina mwanzo wake, tumeona jinsi elimu yetu ilivyoshuka kiwango hadi shule za Private kwa sababu demand ni kubwa kuliko uwezo wa hata hao wawekezaji...
Ningependa sana kuelewa tanzania tulikuwa wa ngapi ktk The Programme for International Student Assessment (PISA) kama nasi tumejiandikisha. Halafu, hivi Tanzania tumepeleka vijana wetu ktk mashindano ya Olimpiki ya vijana maanake sijaona hata mchezo mmoja Mtanzania kushiriki.....
 
Elimu ya bure kwa wote ni sera nzuri na muhimu lakini tukumbuke kuwa umuhimu zaidi uko katika kuboresha elimu yenyewe inayotolewa.

kuna ripoti inayosema asilimia 50 ya wanaomaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika kiingereza na asilimia nyengine ya kutisha hawajui kusoma kiswahili wala kufanya hesabu.

shule hakuna za kutosha na unakuta darasa moja lina wanafunzi zaidi ya 80 ambao wana njaa, wanaokaa kwenye sakafu baridi, bila ya vitabu na nyenzo nyengine zinazohitajika kwenye kupata elimu bora.

tunahitaji kutoa fursa ya elimu kwa wote, ikimaanisha kuwa sasa wapo watoto wengi wanaokosa elimu hiyo. Sawa. Lakini ikiwa tutataka wote waingie shule ina maana kutatakiwa majengo, walimu, mishahara, milo, madawati, na nyenzo nyengine muhimu za kutoa elimu bora au itakuwa ni yale yale ya kujazana madarasani na kumaliza form 4 ukiwa hata kukokotoa hesabu nyepesi huwezi.

kwa hali iliyopo sasa tusishangae kwa nini watu wenye uwezo hata ule mdogo tu wanalazimika kupeleka watoto wao kwenye shule za binafsi.
Lakini viwango vya elimu kwenye shule za umma vikiboreshwa, wengi mno wa waliopeleka watoto wao kwenye shule za binafsi watataka kupewa nafasi kwenye shule za umma (nchi zilizoendelea shule za binafsi zina wanafunzi kutoka watu wa kipato cha juu tu).

Kuboresha huduma iliyopo tu basi gharama yake si ndogo hasa tukizingatia kuwa mfumo wa ukusanyaji kodi na mapato kutoka vyanzo vyengine bado havijaboreshwa.

sioni ubaya kwa kuendelea kuwatoza wale wanaojiweza kile kidogo (japo kwa sasa) na mapato kukusanywa kuboresha mfumo wa elimu uliopo pamoja na kuwalipia wale wasio na uwezo kabisa.
 
Huu mjadala umetulia sana. Laiti wananchi wengi ambao ndio wapiga kura wangepata taarifa hizi wahamasike kutafuta mbadala.
 
Elimu bure ilikuwepo hadi chuo kikuu kwenye awamu ya kwanza pamoja na nchi kuwa changa enzi hizo hadi wabinafsi walipoiondoa na hao wanaosema haiwezekani wamesomeshwa bure hadi chuoi kikuu, leo miaka 50 baada ya uhuru kwa nini ishindikane? Huo ni ubinafsi. Watueleze kwa nini iliwezekana wakati huo na sio sasa. Blabla za IMF au WB zimepitwa na wakati kama mtu anataka kuwa kiongozi lazima aweze kufikiri jinsi ya kutatua matatizo ya msingi vinginevyo hatufai. Ikulu sio sehemu ya picnic.
 
wanaposema hawawezi.. si kwa sababu hakuna "uwezo" bali ni kwa sababu wao hawana uwezo wa kufanya iwe kweli.

Siyo kwamba hawana uwezo ila wanajua kuwa wakitoa elimu ya bure watalazimika kupunguza matumizi yanayolenga kuwanufaisha wao binafsi na hawako tayari kufanya hivyo. Hii inaitwa "conflict of interest".
 
Free education is a recurring cost!!! and compaign cost is one time cost!!! Wachumi uchwara acheni kudanganya watu!

Sasa kama JK anasema anaweza kumpa kila mwanafunzi laptop kwa nini basi serikali ishindwe kusomesha bure, kwanini bado watoto wanakaa chini??
 
Ziangalieni na TAASISI za UMMA zinazokusanya hela nyingi kwa mujibu wa sheria zilizoziunda zipewe maelekezo maalum jinsi ya kuchangia kwenye ELIMU na AFYA pia. Kwa sasa taasisi hizi zinafuja sana mapesa haya kwa kujenga maghorofa ya ajabu, safari za ndani na nje ya nchi za viongozi na watendaji wao zisizo na tija kwa taifa, wanakopeshana mamilioni bila riba na UBADHIRIFU ni mkubwa sana tena kwa kushirikiana na wanasiasa wetu kama Mawaziri na viongozi wa CCM. Taasisi hizo ni kama vile EWURA, TCRA, NSSF, PPF,SUMATRA, TPDC, REA, BOT.Mishahara na mafao kwenye taasisi hizi ni kufuru kwa Watanzania.
Nimeandika mara kadhaa humu kwamba hata BUNGE letu ni kubwa sana kwa uchumi wetu wa sasa. Hatuna haja ya VITI MAALUM wala vile viti 10 vya Rais. Kila Halmashauri, Manispaa, mji ingetoa Mbunge mmoja tu.
 
Sera ya elimu ya bure kwa wote ni muhimu bila kubagua mtoto wa mwenye uwezo zaidi au kidogo. Umuhimu wake ni kwamba tunachohitaji ni taifa la watu walioelimika na mchango wa watu walioelimika ni mkubwa kwa taifa kuliko kwa familia ya muhusika, yaani mzazi hanufaiki na elimu ya mwanae kama taifa linavyonufaika. Normally mwenye elimu kubwa anatarajiwa kupewa majukumu makubwa zaidi, kupata kipato kikubwa zaidi iwe ni kwenye biashara binafsi au kuajiriwa na mwishowe kulipa kodi kubwa zaidi. Hivyo ni jukumu la serikali kusomesha watu wake ili liwe na raia wanaojitegemea na inaowategemea. Wenye kipato zaidi watalipa kodi kubwa zaidi na hiyo kodi isomeshe watoto wa maskini na wa kwao pia. Kumbuka kwamba wapo matajiri ambao elimu kwa watoto wao sio kipaumbele kwenye matumizi yao kwa hiyo elimu kwa wote itasaidia hata watoto wa matajiri ambao baba zao hawajaipa elimu kipaumbele wasome.

Afterall kwa nini matajiri wachangie kodi kubwa zaidi na wasinufaike na kodi yao?? Kuna siku mtasema wenye uwezo wajitengenezee barabara zao wenyewe na hospitali zao wenyewe. Vilele ifahamike kwamba walio maskini hawakuletewa umaskini huo na matajiri ila umaskini umesababishwa na mfumo mbovu wa jamii au uzembe wa familia husika.
 
taib..taib..

Hizo shule za kata matokeo yake yaliyopita vijana zaidi ya 70% walifeli kwa maana ya kupata div 4 mpaka sufuri..hawa ccm ni wauaji kabisa..they want to enslave us all and put into chains of ignorance until the day we die.

Really hopeless & selfish bastards

source ya hizi data ni hii, nina shida nayo sana
 
Back
Top Bottom