CHADEMA, Zitto na hadithi ya 'baniani mbaya'...

Kim unampenda Zitto naona

Sio hivyo boss,unajua mimi nisichopenda ni unafiki wa watu wa chadema,ndio maana unaona nawananga kujaribu kuwarudisha kwenye mstari kwa kuwakumbusha wanayojisahaulisha,kipindi zitto anatishia kumng'oa pinda jamaa wa chadema waliibeba ile hoja ya zitto ambayo kimsingi haikua ya chama bali ilikua ya mbunge binafsi kwa wafuatiliaji wa siasa za humu watakumbuka nilipoona mashabiki wa chadema wameibebea bango ile hoja na kutaka kuifanya ni ya chadema nikaanzisha thread maalum kuwakumbusha nikisema Hoja ya Zitto sio ya CHADEMA,basi naam nikawa nimeuwasha moto,kila mtu alinizomea na kujaribu kuonyesha jinsi gani zitto ni mzalendo mali ya chadema,sasa kuona leo watu wale wale waliokua wakijitapa na zitto wakijaribu kumchafua na kumkejeli kisa anataka kumtest mgombea wao kwenye uchaguzi wa kumpata mgombea urais wa cdm ama kwenye nafasi ya uenyekiti wa chadema kumtest mzee,ndio ninapowaona hawa jamaa ni wanafiki sana na wanamtumia zitto kama condom,pale wanapomhitaji tu,wakimaliza matumizi wanamtupa na kudai eti anatumiwa!

Mambo ya Kim Kardashian!Wapi Kanye West lol!
kim_kardashian5.jpg

Hayo mambo ungewaachia watoto wa face book kule,that kind of childish kufanywa na senior expert member wa jf ni kuidhalilisha jf na wana jf.

Halafu unaelewa kuna adhabu ya name calling lakini?tena mbaya zaidi mtu uliyecall name yake sio kim kardashian achilia mbali kwamba sio member wa jf bali sidhani hata kama anaifahamu jf,acha mambo kibororonyi hapa.
 
mleta uzi acha majungu hakuna mahali na wakati wowote viongozi na wanachama wa CDM wametoa tamko au maazimio ya kumzua zito asigombee uraisi

ni kwamba mchakato bado ukifika kuna utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya chama,

kama kuna tuhuma anazushiwa ni kwa sababu ya mienendo yake isiyoeleweka vizuri mara yuko kwa Jack zoka wa TISS, mara anaonekana kwa Rostam Aziziz anopokea bahasha mara yuko na JK wapiga Umbea,watu makini tunashindwa kumwelewa

Sasa wewe nawe unajua nini?ushasema wewe mliberali(mkameruni)
We unajua sera zenu za mambo yenu yale mliyomwomba obama awasaidie kutambulika.
Mbona huzungumzii urafiki wa karibu kati ya lowassa mbowe na slaa?
ulishawahi kumsikia mbowe akimsema vibaya lowassa hadharani?
Na vipi zile hela slaa alizoenda kuchukua kwa mengi na sobodo kwa ajili ya harusi yake?au unajifanya hujui?
Mbinu zenu zakumchafua zitto hazitofanikiwa kamwe.
 
Hayo mambo ungewaachia watoto wa face book kule,that kind of childish kufanywa na senior expert member wa jf ni kuidhalilisha jf na wana jf.

Halafu unaelewa kuna adhabu ya name calling lakini?tena mbaya zaidi mtu uliyecall name yake sio kim kardashian achilia mbali kwamba sio member wa jf bali sidhani hata kama anaifahamu jf,acha mambo kibororonyi hapa.

Huyo j mushi ni mjinga asiejua chochote,tunamjua fika,ndo maana tunasema chadema ni chama cha kichaga,si unaona wenye cha chao hao wanavyopaliwa na zitto
 
Zitto ndio mtu pekee atakayeweza kuwaunganisha watanzania wote ndan ya chadema.
 
Kazi nzito ni kwa CDM kuwafikia wananchi huku vijijini na kukubalika kama taasisi. Baada ya hapo, atakaye peperusha bendera ya chama 2015 atapatikana. Ni kupoteza mwelekeo kushabikia nani awakilishe CDM 2015 wakati vijijini hawana habari chama kinasimamia nini na kitafanya nini pindi kikipewa ridhaa ya kuongoza dola.
 
We hujui wanacho mpingia hawa chadema ni dini aliyokuwa nayo zitto na wala sio utendaji wa zitto
 
Wangeanza magamba kwanza kama kweli wanaijua demokrasia, Wanamtumia cha matusi Lusinde kisha wanamwaga ujumbe wa NEC, Filikunjombe nae kwa kuwa alitumia haki yake kikatiba kutia saini ya kumng'oa waziri mkuu nae kaonekana mwiba mchungu kwa magamba kachinjiwa baharini, Mkono mmmmh sisemi..........!

kwa andiko hili maana yake unakiri kuwa ndani ya CDM hakuna demokrasia kwa kiasi fulani......ila unadhani kule kwa "Magamba" ndiyo hakuna demokrasia kwa kiasi kikubwa.....
 
nyie endeleeni kupiga mayowe mkiwa mmekaa tu na laptop zenu mkifuatilia mambo jf mkajiona nyie ndio chadema sana,wenye chadema yao wako vijinijini huko jana walikua karatu leo sijui wapi all in all wanajenga chama nyie mnawabomoa kwenye laptop zeu
 
zitto na lowassa are the disaster kwa chadema na ccm na inavyoonekana hakuna namna ya kuwazuia wasitimize malengo yao,nyie watu wa vyama mna kazi kubwa sana huko kwenye vyama vyenu na hao waungwana,sisi tunawasubiri kwenye sanduku la kura baada ya kupima nani ana sera nzuri na zinazotelezeka za kutuondoa hapa tulipo kutupeleka mbele,that's it,hatutampima wala kumchagua mtu kwa sura yake ama chama chake bali sera zake ambazo tutajiridhisha zinatekelezeka
 
Ni kweli Zito Zuberi Kabwe ameweza kujenga hoja changamshi ndani ya Bunge. Hali hii ilifanya watanzania waone manufaa ya kuwepo kwa upinzani ndani ya Bunge. Serikali inahofia kufanya mambo fulani kiholela kwa kuchelea kuumbuliwa Bungeni na wapinzani akiwemo Zito. Lakini sio Zito peke yake mwenye hoja nzito. Kuna wengine pia waliibua hoja nzito ingawa kwa uzito tofauti kimizania. Wapo pia waliounga mkono hoja za Zito. Nao sio wa kuwabeza maana kama hoja haikungwa mkono haiwezi kuwa na mshiko. Tazama hoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya nishati na madini aliyenunua mafuta bila kufuata sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inayotaka kupata kazi kwa ushindani lakini yeye akaipa kazi Kampuni ya BP bila ushindani kwa misingi kuwa aliokoa pesa za serikali. Hoja hii haikuungwa mkono badala yake ikamgeukia Zito kama miungoni mwa wala rushwa. Hivyo waungamkono hoja ni muhimu pengine kuliko mtoa hoja mwenyewe.
Tatizo ninaloliona kwa ZZK ni kuwa anarahisisha mno kiti cha Uraisi. Nasema hivi kwa sababu naona ZZK baada ya kutoa hoja mbili tatu zilizoungwa mkono Bungeni anaona moja kwa moja anafaa kuwa Raisi wa Tanzania. Ni kama mtu anayeridhika haraka na kujikweza juu haraka mno. Anaona katika chama chake anajiona yeye tu haoni mtu mwingine mwenye uwezo kuzidi yeye. Zito anakuwa mchezaji na mtazamaji yeye mwenyewe wakati huo huo. Nijuavyo mimi jicho hutumika kuona vitu vingine na kamwe haliwezi kujiona lenyewe. Likiingiwa na mdudu, jicho huomba jicho la jirani lisaidie kutoa mdudu. Kabwe hujipa sifa yeye mwenyewe.
Ni kawaida yetu watu kungoja kusifiwa na sio kujisifu binafsi tena kabla ya mtu yeyote kukuuliza sifa zako. Kawaida ni kama sheria. Zito Zuberi Kabwe anaposhindwa kufuata kawida hii ndgo kabisa, jamii inaanza kuhoji umakini wake. Kama anakosa umakini kwa jambo moja tu la kuwa na SUBIRA, je; atawezaje kuwa na subira kwa mambo mengi ya nafasi ya uraisi? Umri wake pia kwa mujibu wa katiba ilyopo unamtaka awe na subira. Hili nalo hataki. Anajiondolea sifa hii muhimu.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaonya watanzania, akasema ''Ukiona mtu anakimbilia Ikulu, mwogope kama ukoma.'' Kwa Zito kuwa na hamu sana kwenda Ikulu, tena hata kabla ya kuanza mchakato wa kumtafuta Raisi, anajiweke katika mazingira ya kuogopwa kama ukoma. Anawezekana akawa na baadhi ya sifa za kuwa Raisi lakini hili la kuwa na haraka peke yake linatoa nafasi ya kuhoji sababu za kutaka kwenda ikulu. Maswali mengine anaweza akawa na majibu yake, lakini sio wote watapata nafasi ya kumuuliza akawajibu kwa ufasaha. Wengine watajiuliza nakujibu wenyewe. Washindani wake hawataulizwa swali hili kwa sababu watakuwa wakijinadi wakati mwafaka hivyo wataonekana kutokimbilia Ikulu bali wanagombea kwa sababu wakati utakuwa umefika.
Hapa ndipo naona ZZK anaweza kuwa dereva mzuri asiyejua barabara anamoendeshea gari lake. Ili ufike salama U salimini unahitaji kuwa dereva mzuri unayeijua vema barabara yako.
Unaposema Chama kinataka kumtumia kisiasa ni kweli kazi ya siasa kila nayeomba ansema anataka kuwatumikia wananchi. Hasemi anataka kujinufaisha yeye binafsi. Kama anataka uraisi kwa manufaa binafsi na sio ya chama, hakika hatufai. Tunataka kiongozi atakayekiletea ushindi chama chetu kwa manufa ya chama na sio mafanikio binafsi. Tunataka tukae pamoja kama chama, tuseme nani atakayetuletea ushindi chama chetu, kwa pamoja tuse ''Zito Zuberi Kabwe''.
Vinginevyo kila mtu atajiona anafaa na tutaparaganyika, hatutashinda. Tutaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe itakuwa kama vita ya panzi na kutegenza shibe kwa KUNGURU a.k.a. Binafsi Zuberi hutashinda na CHADEMA hakitashinda tutatoa ushindi kwa CCM
 
bwana shilole huwa unasoma magazeti?soma hii kutoka kwenye gazeti la mbowe:

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.

Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.

Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C

Source: Gazeti la freeman mbowe-Tanzania Daima
...Lakini si ilishapatwa kusemwa na makamanda wetu siku zilizopita (muda mfupi kidogo baada ya uchaguzi wa 2010) kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi na kampeni za uchaguzi unaofatia?..let's keep that spirit dearly, and within that spirit let's have no fear with "waroho wa madaraka ya juu "( kama kweli wapo)....tukumbushane...chadema stands for...chama CHA DEMOKRASIA.....na MAENDELEO.....
 
Ni kweli Zito Zuberi Kabwe ameweza kujenga hoja changamshi ndani ya Bunge. Hali hii ilifanya watanzania waone manufaa ya kuwepo kwa upinzani ndani ya Bunge. Serikali inahofia kufanya mambo fulani kiholela kwa kuchelea kuumbuliwa Bungeni na wapinzani akiwemo Zito. Lakini sio Zito peke yake mwenye hoja nzito. Kuna wengine pia waliibua hoja nzito ingawa kwa uzito tofauti kimizania. Wapo pia waliounga mkono hoja za Zito. Nao sio wa kuwabeza maana kama hoja haikungwa mkono haiwezi kuwa na mshiko. Tazama hoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya nishati na madini aliyenunua mafuta bila kufuata sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inayotaka kupata kazi kwa ushindani lakini yeye akaipa kazi Kampuni ya BP bila ushindani kwa misingi kuwa aliokoa pesa za serikali. Hoja hii haikuungwa mkono badala yake ikamgeukia Zito kama miungoni mwa wala rushwa. Hivyo waungamkono hoja ni muhimu pengine kuliko mtoa hoja mwenyewe.
Tatizo ninaloliona kwa ZZK ni kuwa anarahisisha mno kiti cha Uraisi. Nasema hivi kwa sababu naona ZZK baada ya kutoa hoja mbili tatu zilizoungwa mkono Bungeni anaona moja kwa moja anafaa kuwa Raisi wa Tanzania. Ni kama mtu anayeridhika haraka na kujikweza juu haraka mno. Anaona katika chama chake anajiona yeye tu haoni mtu mwingine mwenye uwezo kuzidi yeye. Zito anakuwa mchezaji na mtazamaji yeye mwenyewe wakati huo huo. Nijuavyo mimi jicho hutumika kuona vitu vingine na kamwe haliwezi kujiona lenyewe. Likiingiwa na mdudu, jicho huomba jicho la jirani lisaidie kutoa mdudu. Kabwe hujipa sifa yeye mwenyewe.
Ni kawaida yetu watu kungoja kusifiwa na sio kujisifu binafsi tena kabla ya mtu yeyote kukuuliza sifa zako. Kawaida ni kama sheria. Zito Zuberi Kabwe anaposhindwa kufuata kawida hii ndgo kabisa, jamii inaanza kuhoji umakini wake. Kama anakosa umakini kwa jambo moja tu la kuwa na SUBIRA, je; atawezaje kuwa na subira kwa mambo mengi ya nafasi ya uraisi? Umri wake pia kwa mujibu wa katiba ilyopo unamtaka awe na subira. Hili nalo hataki. Anajiondolea sifa hii muhimu.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwaonya watanzania, akasema ''Ukiona mtu anakimbilia Ikulu, mwogope kama ukoma.'' Kwa Zito kuwa na hamu sana kwenda Ikulu, tena hata kabla ya kuanza mchakato wa kumtafuta Raisi, anajiweke katika mazingira ya kuogopwa kama ukoma. Anawezekana akawa na baadhi ya sifa za kuwa Raisi lakini hili la kuwa na haraka peke yake linatoa nafasi ya kuhoji sababu za kutaka kwenda ikulu. Maswali mengine anaweza akawa na majibu yake, lakini sio wote watapata nafasi ya kumuuliza akawajibu kwa ufasaha. Wengine watajiuliza nakujibu wenyewe. Washindani wake hawataulizwa swali hili kwa sababu watakuwa wakijinadi wakati mwafaka hivyo wataonekana kutokimbilia Ikulu bali wanagombea kwa sababu wakati utakuwa umefika.
Hapa ndipo naona ZZK anaweza kuwa dereva mzuri asiyejua barabara anamoendeshea gari lake. Ili ufike salama U salimini unahitaji kuwa dereva mzuri unayeijua vema barabara yako.
Unaposema Chama kinataka kumtumia kisiasa ni kweli kazi ya siasa kila nayeomba ansema anataka kuwatumikia wananchi. Hasemi anataka kujinufaisha yeye binafsi. Kama anataka uraisi kwa manufaa binafsi na sio ya chama, hakika hatufai. Tunataka kiongozi atakayekiletea ushindi chama chetu kwa manufa ya chama na sio mafanikio binafsi. Tunataka tukae pamoja kama chama, tuseme nani atakayetuletea ushindi chama chetu, kwa pamoja tuse ''Zito Zuberi Kabwe''.
Vinginevyo kila mtu atajiona anafaa na tutaparaganyika, hatutashinda. Tutaanza kugombana wenyewe kwa wenyewe itakuwa kama vita ya panzi na kutegenza shibe kwa KUNGURU a.k.a. Binafsi Zuberi hutashinda na CHADEMA hakitashinda tutatoa ushindi kwa CCM
Nani unapenda au unadhani atashinda?mtajeni mbona mnamficha mnahofia nini na yeye anahofia nini kutamka(sio kufanya kampeni)hadharani ili tumchunguze?
 
KIM naona uko nje kabisa ya mantiki ya hizi mada zote zinazomuhusu huyu dogo ZK. Ila unajitahidi kuonyesha mahaba ya wazi kwake.

Kimsingi, hakuna mtu anayekataa mtu fulani asigombee nafasi fulani katika chama fulani katika utaratibu fulani.

Na kwavile chama si cha mtu mmoja tunategemea togetherness kwa kila jambo kubwa ambalo mwanachama fulani kutoka chama fulani atataka kulifanya.

Huyo dogo ambaye wewe una mahaba naye anakosea mambo mengi sana ambapo sisi watanzania wenye akili tunagundua mapema anachotaka kufanya.

Kwa taarifa yako zito anajua kuwa hawezi kuwa raisi wa nchi hii hata miaka mia ipite. Na huenda hata interest hana, Ila dili lake ni kubwa kuliko hata huo uraisi.

Watanzania tutamgawana, we muache aendelee na hiyo mission yake.
 
Mzee wa ngono tuna tatizo moja...watanzania nyerere ametuharibu sana hivi kwanini tunapenda kudhani vyeo au cheo fulani ni kwa ajili ya watu fulani tu wengine hapana?

Tunahitaji mapinduzi ya kifikra kama anavyosema mbunge wa zamani wa arusha mjini yule Lema,tujifunze kutoka kwa walioendelea kidemokrasia kama marekani,kuna mtu kwenye kutafuta nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya Republican alikua anaitwa Ron Paul mwenyewe akijiita the champion of liberty sijui kama umepata kumsikia.

Ni mtu mmoja mzee yani babu watu wote walijua hawezi kupitishwa kuwa rais lakini haikua sababu ya kumzuia kutumia haki yake ya kikatiba,aliachwa na matokeo yake alifika mbali sana lakini baadae alitolewa,y not zitto,kwanini asiachwe kwa maslahi ya kuilinda demokrasi then aje kukataliwa na wapiga kura ndani ya chama?

kwanini mnataka kumziba mdomo?mnaogopa nini na weakness zake mnazijua ambapo najiridhisha hawezi kupitishwa na vikao halali,kwanini msimuache akachinjiwe huko?acheni uoga muacheni kijana atumie haki yake ya kuchagua na pia kuchaguliwa.
 
Macho yanauma kusoma ujuha wa habari kama hii.

Lini umesikia CHADEMA ikimponda Zitto? Kama sio kuchanganywa tu ID fake za humu JF.

Hey boy Be a guy.

Ina maana hujui kinachoendelea au unafanya makusudi tu?
 
Back
Top Bottom