CHADEMA yawapa raha watanzania: Taifa Lazizima

Hongera kwa viongozi wa ukweli!....... Mligundua kuwa Baba Mwanaasha kaingizwa choo cha kike mkamshtua naye akafuata maelekezo yenu......... Walaniwe Anna Kilango na timu yake iliyotaka kuingiza Taifa kwenye machafuko kama yaliyotokea Kenya......... Hongera kwa JF members wote kwa kufuatilia mchakato kwa makini!...... Big up kwa moderators kwa kuweka kizuizi kwa serikali ya Magamba ili tusifungiwe na kusababisha kukosa utamu wa kupashana habari!

halafu huyu mama cimpendi mie.. yaani anajifanya anajua kila ki2.. anaongea kama cherehani.. halafu anajifanya ati mpambanaji.. mnafiki wa ku2pwa...
 
jana mbowe aliongea kwa ukali sana na kutahadharisha kuwa kama mkitushinda bungeni kwa kura sisi tutaenda kwa wananchi,ikafika kipindi aliinuka na kwenda kwa mwanasheria mkuu nafikiri alipeleka wazo la kuwaweka wote wawili dc na ded baada ya kuona ccm wamekomaa na dc..kuna kipindi kilango aliwalazimisha vilaza wenzie wasimame kuunga mkono hoja na kumlazimisha speaker wapige kula ni kama aliogopa kuruhusu hilo maana anajua kwenye kura ccm watashinda halafu wananchi hawatamwelewa..hata mwanasheria mkuu hakuwa tayari kwa hili mpaka wenyewe wakazikimbia kura...........viva chadema
 
Wapo pia akina Kafulila wa NCCR ambao walikuwa sambamba na Makamanda wa CDM katika hili, nakumbuka walizomewa sana walipokuwa wanatoka bungeni. Bila shaka wabunge wa ccm wamejifunza kuweka ushabiki pembeni na kutanguliza maslahi ya Taifa.
 
Nami naungana na wengine kutoa pongezizangu za dhati, lakini niseme huu ni mwanzo tu kuelekea kupata KATIBA NZURI YAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Waheshimiwa Dr. Slaa, Mbowe, Zito, Lissu n.k naomba niwapongeze kwa kuuongozavyema kambi ya upinzani na kuwezesha hili kufanikiwa. Niseme hu ni mwanzo tukuelekea kupata KATIBA NZURI itakayowezesha kuwakomboa watanzania nakuwafikisha hatua nyingine nzuri ya maendeleo. Naomba muelewe kuwa MISUKOSUKONA MAWIMBI mtaendelea kuvipata lakini hivi visiwakatishe tamaa. Safari yakuwakomboa watanzania ni sawa na safari zingine ambazo vikwazo vinavyopatikananjiani havimfanyi mtu kuacha kufika anakoelekea.

Uzuri wa CHADEMA ni kuwa mna wafuasi wengi ambao ni vijana na watoto na hawandiyo wanafanya na wataendelea kukifanya chama cha Demokrasia na Maendeleokukomaa na kuota mizizi katika nchi nzima.

Natoa pongezi zangu za pekee kwa rais wangu niliyemchagua mwaka 2005 lakini2010 nikamnyima kura yangu, umefanya jambo kubwa sana na umewafurahisha kwahakika watanzania walio wengi. Hata kama wapo wana CCM ambao wanaweza wasieleweulilolifanya lakini wenye akili nzuri zilizokaa sawa wanaelewa kitu kizuriulichofanya. Umetanguliza Maslahi ya NCHI zaidi ya CHAMA na huu ndiyo UZALENDO.Kwa hili nakupa pongezi sana na naomba kwamba huu uwe mwanzo tu wa kuelekeakupata KATIBA NZURI ILIYOPATAA RIDHAA YA WATANZANIA WALIO WENGI. Ukifanya hivikabla ya kumaliza muda wako, ninakuhakikishia watanzania watakukumbuka kwahili.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika

Nakubaliana nawe kuwa ikipatikana katiba bora ya watanzania ambayo itapelekea kupatikana tume huru ya uchaguzi, mwaka 2015 kwa mara nyingine baada ya Nyerere atapatikana rais bora kwa ajili ya watanzania.
 
WanaJF,
Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung’unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.

Kwanini?

· CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi
· Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi
· Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.

Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:

Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia

· Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.
· Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.
· Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.
· Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.
· Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.

  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.

Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.

WanaJF,Nawasilisha kwenu!

Nina pata wasiwasi na uwezo na upeo wako wa kufikiri. Ungeliangalia bunge leo wakati wanapitisha muswada huu , wazi kuwa CDM walikuwa wanaomba huruma ya CCM , kwa Lissu mishipa ilikuwa inamtoka mpaka Jaji Werema alikuwa anamwonea huruma. Na kama umesoma waraka wa Kafulila juu ya suala hili ni wazi kuwa CDM wamelamba garasa badala ya dume. Kwa taarifa yako ni mapendekezo yasiyozidi 5% ndio yamefanyiwa kazi, sasa hapo mtu amepata 5% unampa pongezi ya nn badala yakumsikitikia?

Mkuu nakuaminia,umepanga ukaeleweka.Viva makamanda wetu.Ni wakati sasa wa kujipanga kwa ajili
ya jimbo la Arumeru mashariki.Mikakati ianze mapema.
 
Nami najumuika na wenzangu kuipongeza chadema maana kama si kusimama kidete basi tungeburuzwa sana na hali halisi ni kwamba hata hayo madudu tunayoona yote yamechokonelewa na chadema naomba muendelee hivyo hivyo nasi tunaunga mkono kila hatua mnayopiga
 
Wakati tukiwapongeza mashujaa waliofanikisha kufika hapa, tusisahau kuwalaani na wale waliojaribu kusambaratisha hii safari takatifu. Wapo wengi lakini tuwataje wachache wawakilishe wenzao;

1. Mh. Celina Kombani
2. Mh. Anne Kilango Malecela
3. Mh. Anna Makinda
4. Mt. Seif Sharif Hamad
5. Mh. Jussa
6. Yule Mbunge mnafiki wa CUF aliyesema hao siyo Wapinzani

Eeh, Mungu uwasamehe hawa kwani hawajui watendalo. Washindwe na walegee.
 
Pamoja na cdm,mimi pongezi zangu ziende pia kwa wanaharakati mbali mbali,walioongoza jukwaa la katiba chini ya kina kibamba,shivji,ulimwengu na wengineo.nadhani kwa kiasi kikubwa wamechangia kwa kiasi kikubwa mswada kufanyiwa marekebisho!.big up..
 
WanaJF,
Tutakuwa hatutendi haki kama hatutasimama kama Watanzania kutoa pongezi za dhati kabisa kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kwa kusimamia kidete suala la Katiba mpya mpaka sasa marekebisho ya sheria ya Katiba mpya yakapitishwa na bunge leo.Ni wazi watu mbalimbali akiwemo Rais Kikwete wamechangia hili lakini bila kumung’unya maneno niseme kama si CHADEMA kusingekuwa na hoja hii ya Katiba mpya leo.

Kwanini?

· CHADEMA iliweka suala la Katiba mpya kwenye ilani yake ya Uchaguzi mwaka 2010
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge siku Rais alipolifungua bunge pamoja na mambo mengine kudai katiba mpya itakayotoa fursa ya kuwa na tume huru ya uchaguzi
· Mwaka mzima wa 2011 CHADEMA iliongoza maandamano nchi nzima kutoa elimu ya uraia na kutaka kuungwa mkono na UMMA juu ya kupata katiba mpya
· Wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya bunge mwezi Novemba 2011 kupinga mswada wa Katiba mpya uliokuwa na Mapungufu mengi na ya kimsingi
· Kamati kuu ya CHADEMA ilinyoosha Mkono wa mapatano na serikali kwa kukutana na Rais Kikwete kupinga mswada uliokuwa mbovu uliopitishwa kiushabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Rais aliridhia mapendeklezo yote ya CHADEMA na kuamuru mabadiliko ya sheria iliyokuwa imepitishwa kishabiki na wabubge wa CCM na CUF
· Hatimaye marekebisho ya sheria yakapitishwa na bunge na kufungua rasmi mlango wa kutengeneza katiba mpya ya Tanzania.

Ni wazi kwa yote yaliyotajwa hapo juu yanatufanya tuamini CHADEMA imesimama imara katika kupigania Katiba ya nchi.Watanzania wengi walikata tamaa na kudhani baada ya mswada mbovu kupitishwa mwaka jana CHADEMA ingesusia moja kwa moja zoezi zima.Lakini CHADEMA imejenga taswira tofauti kwa Watanzania kwa kupigana kwa hali yoyote kuhakikisha Katiba mpya inapatikana.

Wafuatao wanastahili heshima ya pekee:

Pamoja na CHADEMA kama taasisi kuonekana kukomaa na kusimamia agenda zake,ni lazima tuwatambue baadhi ya watu walioongoza mpambano huu kwa Amani na utulivu na siku moja wataingia katika vitabu vya historia

· Dr Wilbroad P. Slaa-Ni kiongozi makini,madhubuti na anayeweza kuyasimamia maneno yake kwa kuinadi ilani ya CHADEMA nchi nzima wakati wa kugombea urais mwaka 2010 na watu wakaamini na kuona umuhimu wa Katiba mpya.Lakini Pia ni Katibu mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa chama anayeongoza sekretariati ya chama inayopanga agenda za chama na kusimamia mikakati yote ya chama,suala la Katiba mpya likiwa mojawapo ya mkakati.
· Freeman A.Mbowe-Huyu ni kiongozi wa upinzani bungeni na muda wote ameiongoza vema kambi ya upinzani bungeni kusimamia agenda hii ya katiba mpya.Hakutetereka na amekuwa akisimamia uwajibikaji wa pamoja wa kambi yake bungeni.Kwa jinsi leo alivyohitimisha mswada huu wa katiba mpya hawezi kusahaulika kirahisi.Amewafanya watanzania sasa kutambua ni nini maana ya kambi ya upinzani bungeni.
· Zitto Z.Kabwe-Huyu ni Naibu kiongozi wa upinzani bungeni na siku zote amekuwa msaidizi muhimu na wa kuaminiwa wa kiongozi wa upinzani bungeni.Ni wazi amesaidia sana kuifanya kambi ya upinzani kuwa kama jinsi ilivyo na anastahili kufurahia matunda ya kupigania katiba mpya ndani ya bunge.
· Tundu A.Lissu-Ni mnadhimu mkuu wa upinzani bungeni.Huyu ukitaja jina lake kwa sasa hata mtoto mdogo anamjua.Hili ni jembe kweli kweli.Alipinga kwa nguvu zote mswada mbovu wa mwaka jana.Kutokana na upinzani wake kwa mswada wabunge wa CCM na CUF walimshambulia kwa kila neno baya ili kumchafua mbele ya jamii.Lakini alisimama kidete kupambana ndani na nje ya bunge mpaka leo hii walau watanzania wanafurahia mabadiliko ya sheria ile.
· Wabunge wote wa CHADEMA-Hawa kwa ujumla wao wamesimama kidete kwa umoja ndani na nje ya bunge kuhakikisha katiba mpya inapatikana.Kila walichokifanya kuhusu katiba ni msimamo wa chama chao.Wote walinena lugha moja.Hakika huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingie pale kunapokuwa na jambo la msingi la kuwatetea watanzania.Iliwashangaza wengi pale hata mbunge wa Maswa John Shibuda alipoungana na wenzake mwaka jana kutoka nje ya bunge kususia mswada mbovu uliowasilishwa.

  • Rais Jakaya Kikwete-Kwa heshima ya Pekee anastahili pongezi za dhati kabisa kwa uamuzi wake wa kukubali mwito wa kukaa na CHADEMA.Ni wazi Rais alikubali kuweka pembeni itikadi ya chama chake na kuamua kuwasikiliza CHADEMA na hatimaye kuyakubali madai yao yote.Ilihitaji moyo mkuu kufanya hivi.Aliipuuza kelele za wana CCM wenzake waliokuwa hawataki akubaliane na CHADEMA.Aliwapuuza na kuwadharau wabunge wa chama chake waliotishia kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Rais kisa eti amekubali mapendekezo ya CHADEMA ili kupata katiba bora kwa Taifa letu.Wana CCM wengine wakadiriki kusema Rais anafanya haya kwa vile anamaliza muda wake wa urais kwa hiyo anajiandalia mwisho mwema,lakini hata hawa pia Rais aliwapuuza kwa maslahi ya Katiba bora.Kwa hili hakika Jakaya Kikwete amejiandikia historia ambayo haitafutika kirahisi.
Kwa ufupi kabisa niseme waliyoyafanya CHADEMA yameingia kwenye historia mpya.Yatasimuliwa vizazi na vizazivijavyo na ni mfano kwa wanasiasa na vyama vingine vyote.Hakika wameonyesha ukomavu wa hali ya juu.Na labda niseme lakini msiniite mtabiri! Kwamba ikipatikana Katiba mpya ya watu,ambayo itatoa tume huru kabisa ya uchaguzi itakayotenda haki kwa vyama vyote mwaka 2015,basi watanzania msishangae kumuona Michael Satta wa Tanzania akimrithi Jakaya Kikwete.Na tusubiri tuone.

Mungu awatangulie watanzania katika kupata katiba bora mpya ya Tanzania.Alilolipanga Mungu mwanadamu kamwe hawezi kulipangua.

WanaJF,Nawasilisha kwenu!

Wenye akili za kuona karibu wanaweza kukubaliana na mawazo finyu kama ya kwako yenye ushabiki tu na siyo analysis.
Watanzania wanajua sana kwamba, analysis kama hizo ni za kivuvuzela tu na lengo lake ni ili baadaye wapite mitaani kwamba wao ndiyo chimbuko la kisiasa. Nashukuru kwamba umetambua mawazo ya watu walichangia kupita kwa muswada wa katiba kuwa ni Pamoja na ROJEPH WARYOBA, SALIM AHAMED SALIMU ila ukaharibu kwa kuchomekea mavuvuzela eti kisa walitoka nje ya ukumbi wa bunge, kuzunguka nchini kuwashawishi wananchi wasijihusishe na shughuli za maendeleo huku ukidanganya kwa walikuwa wanatoa elimu ya uraia. Ndugu hukumbuki kilichotokea katika jimbo la Engineer STELAA MANYANYA? huko kulikuwa ni kutoa elimu ya uraia kuhusu katiba mpya?

Wasomi wote na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao hawatawasahau akina Prof. ISSA SHIVJI, MWAITAMA, JENERALI ULIMWENGU na wengine wengi. Nakumbuka siku moja katika kongamano la katiba mpya pale UDSM, Tindu Lissu aliumbuliwa na Prof. Shivji kwa jinsi alivyokuwa akichangia kisiasa siasa tu leo nae unamtaka kwenye list yako ya mavuvuzela. Nakumbuka ambavyo wasomi walisimama kidete kuhakikisha Wanasiasa wasiteke mjadala wa Katiba mpya, leo unanitajia mzee wa Bilkana kama mwasisi na Baba Josephine Mshumbuzi. Kweli watanzania tumelala. Umeshindwa angalau kumtaka Mabere Marando? Pole.
 
Back
Top Bottom