CHADEMA yawa gumzo Marekani, vua gamba vaa gwanda!!

Hizo picha wamepiga wapo kwenye sebule halafu imekuwa gumzo Marekani? Mie naipenda ile picha huyu Mwanamke anacheza kiduku mbona umeitoa.
Marekani hakuna mikutano ya chini ya miembe, mambo yote yanafanyikia ndani ya majengo, naona roho inakuuma lakini ndio utafanyaje tena maji yameshamwagika, Halafu ungejuwa jinsi huyo Dada Linda alivyotoka jimbo la mbali anakoishi na kwenda MD Kwa ajili tu ya kujiunga na Chadema nadhani ungejinyonga kabisa.
 
Tawi la CHADEMA Washington DC lazidi kumwaga kadi za uwanachama DMV...!!!


_DSC9521.JPG

Mwenyeketi wa Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Kalley Pandukizi akiwa na katibu wachama hicho,Ndugu Libe Mwang'ombe alipotoa kadi rasmi kwa Beautician maarufu na designer wa kiTanzan Linda Bezuidenhout (LB)

Katika miaka ya nyumba Linda aliwahi kusponsor matukio mbali mbali kwenye miaka ya 1990 wengi wao wakimjua kwa Linda Express Nchini Tanzania ambae ambaye hivisasa anajishughulisha na biashara ya nguo za kiume milanovita.com pamoja na zakike ambazo anadesign mwenyewe kwa brand name ya Linda kutoka Atlanta, Georgia Nchini Marekani.


_DSC9526.JPG

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia CHADEMA Washington DC Mhe. Kalley Pandukizi, pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe akimkabidhi rasmi mwanacham mkareketwa ambae ni mwana mitindo Linda Bezuidenhout (LB) kati ya uwanachama wa chama cha Demokrasia Chadema katika ofisi ya tawi la Tawi la Chama Washington DC.


_DSC9531.JPG

Mwenyeketi wa tawi la Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Washington DC Mhe. Kalley pamoja na katibu wake Mhe. Libe Mwang'ombe wakipata picha ya pamoja na Linda Bezuidenhout Atlanta, Georgia na wanachama wa tawi la chadema Washington DC


_DSC9545.JPG

Viongozi wa tawi la chadema Washington DC wakipata Champagne

_DSC9542.JPG

Linda Bezuidenhout (LB) furaha baada ya kuvua kamba kuvaa gwanda na kuchukua kadi kuwa mwanachama kamili wa
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).


Msikilize kwa makini mwana mitindo mbunifu wa
Linda Bezuidenhout (LB) Aakilonga na Swahilivilla



Haya magwanda tunamuomba dada ayateneze kwa ajili ya wapiganaji huku bongo pia yana mvuto sana yametulia hasa hili la kike limetulia sana wajameni
 
Huyo Linda ni dada yake na Richard yule aliyewahi kushinda BBA, hilo Gwanda amedesign yeye mwenyewe kwa kutumia lebo yake ya LB.
Nataka kuwasiliana naye kama anaweza kuimport hizi Gwanda kwa ajili ya kina Dada kwa bei nafuu.

Mkuu Molemo,nitakuwa wa kwanza kununua ni nzuri na zinavutia hasa.
 
Marekani hakuna mikutano ya chini ya miembe, mambo yote yanafanyikia ndani ya majengo, naona roho inakuuma lakini ndio utafanyaje tena maji yameshamwagika, Halafu ungejuwa jinsi huyo Dada Linda alivyotoka jimbo la mbali anakoishi na kwenda MD Kwa ajili tu ya kujiunga na Chadema nadhani ungejinyonga kabisa.

Sasa kama wamefanyia ndani huo mkutano utasemaje Chadema yawa gumzo Marekani?

Halafu punguza porojo Matola mbona kina Obama, Bush tulikuwa tunaonafanya mikutano ya viwajani chini ya miti..eti Marekani mikutano wanafanyia ndani.
 
Sijaona Bado... Wauza sura tu!! Kwani nani asiyewajua watz kwa kuutafuta umaarufu kwa bei yeyote??? Sasa kwa sababu Chadema is currently trending ndio kila mtu anatafuta pa kutokea... Haya Dada kaongeza pato kwa kutengeneza overall hizo... All the best. I hope u guys won't be surprised in 2015.. I just hope so..
 
Hatua nzuri mmefika cdm big up mafanikio yanakuja kwa kujituma!
 
Angalieni hata nyuso zao zinaonyesha matumaini lakini za wenzetu CCM utafikiri wanakunywa kloriti(Hii ni dawa ya kimasai ni chungu kuliko nyongo)[/QUOTE]tupia hapa picha yao tuone walivyotepepeta kama matope.lete mambo,
kuna raha yake ukijtambua.
 
gwanda 1.JPG gwanda 2.JPG
mwenyekiti wa chadema tawi la Washington DC na katibu wake wakimkabidhi kadi ya uanachama mwana mitindo Linda Benzuidenhout (LD) katika ofisi za chama

Gwanda la ukweli kabisa kwa akinadada kweli nimemkubali huyu ni mwanamitindo ningejua ninaweza kupata wapi gwanda kama hilo ningemnunulia shemeji yenu , chadema should used such creative member to design their uniform .

source: michuzi
 
Magamba wanafuatilia hii thread roho inawauma kwasababu ile minguo yao na Rangi zao zinafanana na DDT (hii ni sumu kali sana ambayo imepigwa marufuku duniani)

Ha haa you make my day Loh mnapata wapi haya maneno, duh nimecheka sana kila mtu amenishangaa.
 
Sidhani kama Chadema inahubiri ufukara, sioni tatizo lolote kwa kila mtu kujikuna anapojiweza, matabaka hayawezi kuisha labda raia wote tuanze kuvaa Uniform na show room zote ziwe zinauza Bajaj.
Matola najua tanzania tuna kila sababu ya kujivunia rasimali zetu lakini kutokana na uroho wa wachache huwezi amini kuna watu vijijini hata sh.500 kwa wiki ni pesa ya anasa au unadhani chadema itagawa bure uniform hizo?
 
Last edited by a moderator:
maji hayafundishwi njia ya karibu kufika mtoni, magamba wakichekelewa kuisoma namba watakuja kuulizana 2015.
 
Back
Top Bottom