CHADEMA yavuruga ngome ya Lowassa Monduli

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika hali ambayo haikutarajiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kimeingia kwa kishindo jimboni Monduli katika operesheni ya M4C Vua Gamba Vaa Gwanda.

Katika mikutano iliyofanyika juzi CDM imezoa viongozi wa vijiji,wajumbe wa serikali za mitaa na mabalozi wa nyumba kumi wapatao 25 huku wakitoa kadi kwa wanachama wapya 700.Operesheni hiyo iliongozwa na Mkiti wa mkoa Samson Mwigamba na Mkiti wa Bavicha Kamanda Ephata Nanyaro pamoja na makamanda wengjne kadhaa.

Tofauti na ilivyodhaniwa awali kwamba jimbo hilo ni la wafuasi sugu wa Lowassa lakini hali imekuwa tofauti kabisa kwani kila kata wanayofika makamanda wa CDM wanalakiwa kwa shangwe na kufungua mashina kadhaa ya chama,huku mwanachama mmoja akijitolea kulipia pango ofisi ya chama jimbo shilingi laki 6.

Source:Tanzania Daima
 
kila raheri makamanda tunahitaji sana mabadiliko hasa kwa kipindi hiki.......
 
sawa kabisa,peopleeeeeeeeeeeeeees!!!!!
Kila la heri makamanda tupo nyuma yenu kwa lolote,liwalo na liwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sawa kabisa,peopleeeeeeeeeeeeeees!!!!!
Kila la heri makamanda tupo nyuma yenu kwa lolote,liwalo na liwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu nimecheka sana.Neno Liwalo na liwe limewatokea watu puani.
 
sawa kabisa,peopleeeeeeeeeeeeeees!!!!!
Kila la heri makamanda tupo nyuma yenu kwa lolote,liwalo na liwe!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Namshauri Nape Vuvuzela aende ku-reverse speed kwa Edo Monduli. Labda inaweza ikawa mkakati wa maridhiano...Nikune nami nikukune mgongoni
 
aisee jamaa akisoma hii anaweza kurudi fasta toka majuu -

Mwenzenu kule ujeremani aliambiwa asipewe habari za mshtuko jf jamani hizi habari za kuandika tunachotaka siyo mafisi wafe bali wabadilike jaman jaman ana mke na watoto na wajukuu na wakwe kama siyoi
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom