CHADEMA yavuna 960 kutoka CCM Arusha

weka majina na picha zao hapa wote 960 kama ni kweli? umeongeza hesabu kunogesha mjadala
 
Kwa jambo hili sioni haja ya kulibeza maana kama shida ya maji hapa mchini kila mtu anaijua,sasa kwa kuwa jambo hili limefanywa na Chadema basi najua itakuwa nongwa ila tuelewe kuwa wananchi wa hicho kijiji shida yao si vyama bali maendeleo na mojawapo ya walichokuwa wanakitaka ni maji na wameyapata,shida ya nini kuhama?
Hongera Chadema na wananchi kwa kuchangia maendeleo ya nchi yenu na jamii kwa ujumla.
 
ha ha ha....Mkuu NGONGO hao watoto wanashangaa bomba la maji tuu. ni kitu kipya kijijini kwani hawajawahi kuona toka wazaliwe.
CDM Arusha imeanza kubaini siasa si maandamano wala si Lema pekee yake.I hope hawa watoto si miongoni mwa wanachama wapya 960 ha ha ha ha ha ha ha.
attachment.php
 
Si bure Ritz unamatatizo! Kisima kimoja ni kuanzia milioni tatu leo wewe milion 40 unasema hauwezi kuchimba hata kisima kimoja! Huko ni kujidhalilisha Ritz!

Ritz kazoea mahesabu ya kwenye makaratasi
kwamba wanachimba kisima kwa 100mil. kumbe wanachimba kwa mil5 na kuweka mfukoni 95mil.
 
Na anaetoa kauli hiyo ni tmu mzima na mwenye wadhifa wake tu kichama,mara cdm wanachochea migoo vyuoni,soon uasikia cdm wako nyuma y madaktari...yaani ni full kutapatapa,cdm inawapa tabu sana,wanajua inawaua kimya kimya
 
Hongera sana CDM na Wananchi wa Arumerukwa kutatua tatizo la maji, nchi yetu ina mataizo mengi ya maji na sio vijijini tu bala hata maeneo mengi ya mijini, ushauri wangu kwa CDM kama mmeweza kupata wanachama wengi kwa njia hii basi tembeleeni maendeo mengine ya vijijini mtambue matatizo yao na kuyatatua na kisha mnawaelimisha wananchi hakika mtapata wengi.
 
Hongera saaaaaaana CHADEMA naona wasio na hoja wanadandia ,hakuna katika historia ya Tanzania chama kingine kikajenga huduma za jamii bila hiyo sehemu kuwa na mbunge
 
Duh huo ndio UMATI wa watu!!! Kha! Kweli ukipenda, hata chongo utasema ni kengeza!
Umati ili uwe umati ni kuanzia watu wangapiii? ila kama 960 ndo waliorudisha kadi ukijumlisha wasiorudisha at any measurement ni umati, any way cha msingi ni mradi huo ulozinduliwa
 
Mradi wa Sh40 Milioni? Hiyo pesa hata kisima kimoja huwezi kuchimba..

Chadema bana kila siku mnasema Arusha hakuna CCM ni Chadema tu sasa hao watu 960 wametoka wapi?
Kwa CCM hata kama ingekuwa mil400 haitoshi maana hapo ukiweka na genji ya viongozi magamba hautaona maji wala nini, lakini kwa chadema mil40 ni nyingi!! maana hakuna kupeana ulaji, kama una akili vizuri utanielewa!! lakini kuhusu ccm members 960 kurudisha kadi, si kitu cha kushangaza kwa sasa, ni nani asiyejua kuwa ugumu wa maisha tulionao unasababishwa na serikali ya magamba? kuhusu madai kuwa tunasema hakuana wanachama wa ccm na hao wametoka wapi, si jambo la ajabu kuona katika watu elfu 20000 ukakuta magamba 960 ambayo nayo yananyofuka kutoka kwa mama yao(ccm)!!. mi nafikiri uwe muungwana ushukuru hata hao wananchi wamepata hayo maji kwani ingekuwa ni nyinyi, mil 40 zingeishia kuweka alama za mabomba yatakapopita hakuna cha zaidi.
 
CDM Arusha imeanza kubaini siasa si maandamano wala si Lema pekee yake.I hope hawa watoto si miongoni mwa wanachama wapya 960 ha ha ha ha ha ha ha.
attachment.php

Huyo mama aliyefunika uso ni Malaria Sugu angalia kwaumakini mkubwa sana!
 
Mabaraza yetu CHADEMA kama vile BAVICHA, BAWACHA na lile Balaza la Wazee, ongezeni moto mkubwa zaidi hasa kwa kufungua mashina kibao vijijini kote nchini Taanzania mpaka CCM kije kishangae na roho yake.

Vijana wenzetu kote nchini tujiwekee malengo ya kuelimisha walau watu kumi kila siku kuhusu mabadiliko ya kweli ambayo CHADEMA PEKEE ndicho cham cha uhakika nchini kinachoweza kuyaleta kw faida ya wote na kutokomeza UFISADI huku maendeleo yakimiminika kwa kila Mtanzania kuanzia 2015 na kuendelea.

Nasema moto mkubwa Mhe Mnyika, Mr II, Naibu Katibu Mkuu Mtarajiwa Halima Mdee, Kamanda Lema, Zitto Kabwe ... wakati ni sasa na kazi iendelee mpaka kwenye kijiji cha ndani mwisho hapa nchini.
 
Siku zote CHADEMA hamko tayari kukosolewa wala kupokea ushauri, Suala la chama kuwa cha kikanda litawagharimu na wala hamtafikia malengo mnayoyakusudia ya kumweka Padri wenu Ikulu sana sana ataishia kwenda kunywa chai, juisi na kahawa tu.
Chadema kanda ya ziwa ni zaidi ya wabunge sita wakati kanda ya kazikazini hawazidi 5 sasa ukanda unatoka wapi kama ni hivyo kwanini msisema ni cha kanda ya ziwa... Tutapokea ushauri lakini sikila ushauri hata kama ni wakijinga no....
 
Duh huo ndio UMATI wa watu!!! Kha! Kweli ukipenda, hata chongo utasema ni kengeza!

Hata kama wangekuwa wawili tu,kadi 960 si mchezo kabisa..nadhani tujadili hili na sio kuangalia idadi ya watu waliofika.
 
Back
Top Bottom