Chadema yaunguruma Dodoma; Operesheni Sangara yapaa!

usiichukulie negative... point yangu ni kwamba habari hiyo ipo gazeti moja tu!!! ni ishara tosha kwamba uenezi kwa chadema unaanza kuchoka sio kama sangara ilivyoanza!!!
there are many ways to kill a man... i was delivering the message to CHADEMA kwamba uenezi wao umeishia zero grazing... na good analysists hawawezi weka mkazo kewnye gazeti la mbowe linaposifia mbowe

Time for change is passing by!!!
ULITAKA aandike kwenye magazeti ya ccm iliyo kufa bado kuzikwa mchana kweupe? au aende akatangazie ikulu ili magazeti na makamera ya muandike? MBOWE ni kamanda mpambanaji hahitaji kujinadi kwenye midia anawafikishia ujumbe wananchi moja kwa moja wananchi hawana imani na chama cha chukua chako mapema (ccm) habari ndiyo hiyoooooooooo, CHADEMA MKOMBOZI WA MTANZANIA WA HALI YA CHINI
 
Kama ungenielewa, usingesema haya uliyoandika... anyway, ndio maisha yenyewe hayo tumeumbiwa vipawa tofauti!!

Sina la ziada kwani nilikuwa kwenye strategies wewe ukaja kwenye activities... basi!!
 
safi sana luteni... hapa tuko pamoja... na mimi nachukua hii habari ya NIPASHE aisee, nimependa kwamba ipo kwingine

Hapa mezani nina CITIZEN, GUARDIAN na DAILY NEWS... sioni kitu ya namna hiyo... meaning, kazi bado sana!! coverage ni muhimu mno kipindi hiki

Na huwezi kuamni hawa jamaa nao walikuwepo.Tulikuwa na Citizen pamoja na Daily News lakini nashangaa kuona hawajaripoti chohote.
 
Ulitaka aandikeje kama kweli Simba ni bingwa au ulitaka usikie Yanga bingwa kwa vile wewe ni mpenzi wa Yanga tha is the reality
moto waendelea kuwaka wakazi wajitokeza zaidi kuchukua kadi na wa ccm wazirudisha kama mvua, kweli chadema ni chama cha maendeleo kama kinaondokewa na wanachama watatu au watano na kinaingiza wanachama wapya zaidi ya 434 ni bonge la maendeleo kisiasa na kujiimarisha kwenye jamii, CHADEMAendelezeni mapambano mpaka kieleweke big up kwa timu iliyopo sangara, kama MBOWE, HALIMA MDEE, REGIA MTEMA, na wengine wengi tupo pamoja kwenye jahazi la ukombozi
 
Big up CDM, huu mwaka wetu, Geita mwaka huu tutasimika mbunge kijana na mwenye tabasamu la ukombozi wa maisha ya wanageita, ccm mwaka huu mlie tu, Geita hamtapata kitu, tunakuja vijana na sera nzuri za maendeleo ya wanageita, wanageita kaani mkao wa kula, maendeleo yapo njiani, maji safi na salama, barabara za lami wilayani zinakuja, wakombozi wenu wanakuja, shule zenye waalimu wenye ubora wanakuja, vijana tunawaomba wanageita watupe ushirikiano ili tupige maendeleo na wanajamii ya Geita wafaidi matunda ya dhahabu yao iliyopo milangoni mwao

CDM JUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Zitto na Slaa (dr) wapo?
 
Mashabiki wa Chadema wamzuia Mbowe mara mbili Dodoma
broken-heart.jpg
Na Geofrey Nyang'oro

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) taifa, Freeman Mbowe juzi alizuiwa kushuka katika jukwaa alikokuwa akihutubia mjini Dodoma.

Mbowe alipata adha hiyo mara mbili juzi wakati alipokuwa amemaliza kutoa hotuba yake ya ufunguzi wa Operesheni Sangara uliofanyika kwenye uwanja wa barafu mkoani Dodoma.

Alizuiwa wakati alipokuwa amemaliza kutoa hotuba yake majira ya saa 12 jioni alipowaambia kwa wakati huo amefikia tamati na kwamba muda ulikuwa umemalizika, lakini mashabiki wa chama hicho walimjibu kuwa aendelee.

Mbowe baada ya kusikia sauti hizo aliendelea kuzungumza kwa dakika takribani 10 hivi, lakini alipojaribu tena kushuka waliokuwa wamefika kusikiliza mkutano huo wakataka kumzuia, lakini safari hiyo akafanikiwa na akashuka jukwaani.

Awali, Mbowe alisema kuwa chama hicho kimejiandaa vizuri na kitawapatia Watanzania kiongozi bora mwenye uwezo wa kutetea rasilimali za taifa akiwa na nia yake kusimamia rasilimali za taifa.

Alisema Chama chake kitasimamisha mgombea wa Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema mwaka huu ni mwaka wa kusuka au kunyoa kwa Chadema urais siyo mali ya Mbowe anaweza kuwa Tundu Lisu au mwingine mimi na Chadema kimetangaza nia ya kusimamisha mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Alisema kwa sasa chama hicho kipo kwenye mchakato wa kumtafuta nani wa kugombea nafasi hiyo na akawataka wananchi wa Dodoma kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuwaletea mabadiliko na kuufuta umaskini.

Mbowe alitaja sababu za umaskini kuwa unatokana na Watanzania kuendelea kukibeba Chama Cha Mapinduzi na kwamba kama hawatabadilika umaskini katika nchi hii hautatoweka. Katika hatua nyingine Mbowe aliponda utaratibu wa kuteua wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kwa madai kuwa huo si utawala wa kidemokrasia na katika mkutano huo alipinga vyeo vya kugawiana kirafiki kama nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya kwa madai kuwa huo si utawala wa kidemokrasia.

MY comment: I like the red bolded words. they show political maturity
 
Big up CDM, huu mwaka wetu, Geita mwaka huu tutasimika mbunge kijana na mwenye tabasamu la ukombozi wa maisha ya wanageita, ccm mwaka huu mlie tu, Geita hamtapata kitu, tunakuja vijana na sera nzuri za maendeleo ya wanageita, wanageita kaani mkao wa kula, maendeleo yapo njiani, maji safi na salama, barabara za lami wilayani zinakuja, wakombozi wenu wanakuja, shule zenye waalimu wenye ubora wanakuja, vijana tunawaomba wanageita watupe ushirikiano ili tupige maendeleo na wanajamii ya Geita wafaidi matunda ya dhahabu yao iliyopo milangoni mwao

CDM JUUUUUUUUUUUUUUUUUU
It is more than too much
 
mbowe anaonyesha kukomaa kisiasa na ni mtu anayehitaji kuugwa mkono
pamoja na makombora yote na kashikashi alizozipata mwaka jana sasa hivi bado anaendelea na operesheni sangara bila wenzake.
ukiangalia viongozi wengine wa vyama vya upinzani unakata tamaa kabisa
well done mbowe kaza buti kamba zisilegee zitakuangusha
 
Operesheni Sangara yamtikisa Malecela

na Joseph Senga na Janeth Josiah, Dodoma

amka2.gif
MIKUTANO ya Operesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Dodoma, jana ilitikisa nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Samuel Malecela, katika kijiji cha Mvumi Misheni baada ya wapambe wake kuingiwa kiwewe kwa kutaka kuzuia mkutano huo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wapambe wa mbunge huyo, walilazimika kuita timu za mpira wa miguu kucheza kwenye uwanja huo kwa lengo la kuzuia mkutano huku wakijiandaa kufanya fujo ambazo hazikufanikiwa.
Katika hali ya kuonyesha kuchanganyikiwa, wafuasi hao waliamua kucheza soka kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 11 jioni kabla ya kukatizwa na helikopta inayotumiwa na Mbowe kutua uwanjani hapo na wao kulazimika kukimbia.
Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alieleza kusikitishwa kwake na siasa za chuki zinazopandikizwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Ndugu zangu wananchi wa Mvumi Misheni hakuna sababu ya kugombana kwa sababu ya vyama vya siasa, tugombane kwa mustakabali wa maisha ya watoto wetu, msikubali watu kupandikiza chuki… nimefika hapa na kuelezwa kwamba kuna watu walitaka kuzuia mkutano usifanyike …hizi ni chuki ambazo hazitakiwi wala kukubalika.
Alisema muda wa Malecela kung'atuka ama kuachia ngazi umefika kutokana na kukalia kiti cha ubunge miaka mingi bila kulisaidia jimbo ambalo wakazi wake ni maskini wa kutupwa.
"Huyu amekuwa mkuu wa mkoa, waziri, waziri mkuu na makamu wa pili wa rais, makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, tangu nikiwa mdogo namsikia mpaka sasa… jamani ana jipya gani la kuwaeleza wakati hata barabara hakuna hapa Mvumi Misheni?" alisema Mbowe.
Mwenyekiiti huyo pia aliwatahadharisha wananchi wa jimbo la Mtera kutoendelea kuikumbatia CCM wakati imeshindwa kuwaletea maendeleo husasan kwa kuendelea kumchagua Malecela kwa kipindi kirefu namna hiyo; jambo ambalo limekuwa likidumaza maendeleo yao kila kukicha.
Alisema kwamba mkoa wa Dodoma ni mkoa wa pili kwa umaskini Tanzania ukiondoa Shinyanga; hali liyosababishwa na wananchi wa Dodoma kuichagua CCM.
"Tunahitaji kumpumzisha Malecela maana hata mwenyezi Mungu alifanya kazi kwa siku sita ya saba akampumzika kwa nini Malecela asipumzike?"aliuliza Mbowe.
Pia aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuondoa woga hasa kutokana na kutishwa na viongozi wa serikali ya CCM na kwamba CHADEMA ndiyo chama mbadala ambacho kitaweza kuwakomboa wananchi wa mkoa huo katika lindi la umaskini.
"Kuendelea na CCM ni sawasawa na kuendeleza utawala wa kisultani kwa maana sultan anatawala mpaka kufa kwake na kisha kumrithisha mtu anayemtaka yeye jambo ambalo kamwe haliwezi kuleta maendeleo kwa wananchi," alisema Mbowe.
Wakionyesha mwitikio, wananchi wa Mvumi Misheni walimuomba Mbowe aendelee kuhutubia hata kama ni usiku wa manane kutokana na sera alizokuwa akizinadi kwao.
Aidha, wananchi hao walitoa kilio kuhusu kero zao mbalimbali kwa mwenyekiti huyo; ikiwemo kuuziwa chakula kilichotolewa kama msaada na viongozi wa serikali ya kijiji kwa sh 1,250 na kwamba malalamiko hayo yamefikishwa kwa mbunge wao mpaka sasa hakuna ufumbuzi uliopatikana.
Operesheni Sangara imeingia mkoani hapa kwa siku kumi na tatu ikizunguka majimbo na kata zote za mkoa huo kwa lengo la kuwahasisha wananchi kuchagua viongozi na vyama mbadala. Ikiwa siku ya tatu, jana operesheni hiyo iliingia katika jimbo la Mtera na kufanya mikutano zaidi ya 12. Leo operesheni hiyo itaendelea katika jimbo la Kondoa Kusini ambapo viongozi wandaamizi wa chama hicho, akiwemo Makamu Mwenyekiti, Said Arfi, na Katibu Mkuu, Wilbrod Slaa, wanatarajia kuongeza nguvu.

h.sep3.gif
 
Kwani hiyo Oaresheni Sangara, ikitoka Dodoma inaelekea wapi?

Nahisi Tabora au Shinyanga. Wakuu wote tunaosapoti hii move tuwaunge mkono kwa hali na mali. Tupime matokeo October. I am sure CHADEMA will count on this.

I love it!
 
Nahisi Tabora au Shinyanga. Wakuu wote tunaosapoti hii move tuwaunge mkono kwa hali na mali. Tupime matokeo October. I am sure CHADEMA will count on this.

I love it!

Kabla ya Dodoma ilikuwa tuende Shinyanga ambapo maandalizi ya awali yalishafanyika yaani yale ya kupima GPS ili helkopta iweze kutua but unfortunately Shinyanga kulikuwa na mvua kubwa hivyo tulishindwa kwenda huko.Kama mvua itakuwa imeisha tutaelekea huko.

Nimesikitishwa sana na jimbo la Mtera.Pamoja na kwamba Malecera amewahi kushika ntadhifa mbalimbali Serikalini ambako naamini ana network kubwa ya ndani na nje ya nchi lakini chakushangaza jimbo lake bado liko nyuma sana kimaendeleo.Jana nilikuwa katika kata moja inaitwa Fufu i was suprised kukuta mapka leo bado watu wanishi kwenye nyumba za tembe.Katika Kata hiyo ina vijiji vitano kikiwemo cha Fufu ambako ndio Makao Makuu ya kata ndipo tulipofanyia mkutano.Wakazi wote kasoro Diwani na Tajiri mmoja wa mifugo ndio wanaishi kwenye nyumba za bati wengine wote kwenye tembe.Shule ya Msingi ina walimu wa 5 tu na ya sekondari ina walimu 4 tu.Mwaka jana katika shule hiyo ya sekondari walimaliza wanafunzi 19 hakuna hata mmoja aliyefanya vizuri kwani kulikuwa na div 4 na 0 tu...Inasikitisha.Kina mama wajawazito wanajifungulia kwenye chumba cha Sindano cha Zahanati.

Nasikitika sio mtaalamu wa kupiga picha vizuri picha zangu hazijatoka vizuri hivyo siwezi kuzituma humu...Nimemuomba Joseph Senga anifundishe kupiga vizuri hope kuanzia kesho nitakuwa nawatumia picha za hali halisi za vijijini sio hizi za mikutano.
 
Hali inasikitisha mkuu, we acha tu. CCM hakuna zaidi ya Chukua Chako Mapema aka UBINAFSI.

Kuhusu Shy na mvua hapo ndo mnaponichanganya. Ina maana hio helkopta haitui kukiwa na unyevunyevu? maana mvua maeneo haya mwaka huu sio kubwa na kwasababu tumezoea kulima mpunga inakula kwetu. Mbona Kahama hapa mvua hakuna kama mnavyosingizia? Hebu niambieni ukweli.
 
I LOVE THIS THREAD!!! Mkuu Malechela naona inabidi achutame tu sasa!!! tuleteeni picha aisee....
 
Back
Top Bottom