Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
Sikubaliani na uamuzi wa kutokwenda mahakamani. Katika mabandiko yangu ya nyuma nilieleza suala hili kwa urefu sana na kuonyesha kuwa Mahakama ya Rufaa ilikwisha tamka kuwa kitendo chochote kile cha Tume ambacho kimefanywa kinyume cha sheria kinapingwa. Nilijitahidi kuwasilisha maoni yangu kwa mwanasheria wao lakini inaelekea wamekataa. Inasikitisha.
Bado ninasisitiza kuwa Mahakama Kuu inabanwa na uamuzi ule wa Mahakama ya Rufaa na hapo ndio ungekuwa uwanja mzuri wa Chadema kuanika ushahidi hadharani. Lakini Wanasheria hutofautiana mbinu za kupambana.
Wanashindwa kwenda mahakamani kwa kuwa hawana ushahidi wakutosha zaidi ya maneno ya uchakachuaji tu... Nimechukizwa sana na mwenendo huu wa viongozi wetu.. Eti leo walikuwa na tafrija ya kurekea ushindi! Ushindi upi huo? Au ni huu wa viti 24 vya wa bunge?