Elections 2010 CHADEMA yatoa masharti mgogoro wa mameya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
CHADEMA yatoa masharti mgogoro wa mameya


Na Reuben Kagaruki

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa masharti ya kumaliza mgogoro ya uchaguzi wa mameya katika maeneo yote yenye utata vinginevyo kitaitisha maandamano ya amani nchi nzima ifikapo Januari 5, mwaka huu.Katika
masharti hayo, kimependekeza uitishwe mkutano wa majadiliano baina yake na viongozi wa juu wa serikali, ikiwezekana ahusike Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, viongozi wa TAMISEMI na kusitishwa kwa chaguzi za wenyeviti na mameya katika maeneo yenye utata.

Maeneo yenye utata yametajwa kuwa ni pamoja na Mwanza, Arusha, Hai, Kigoma Ujiji, ambako chama ghicho kimedai uchaguizi umevurugwa katika mazingira yanayoashiria kuwapo maelekezo kutoka ngazi za juu.

Barua ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa ya Desemba 22, mwaka huu ilieleza kwamba, iwapo madai hayo hayatatekelezwa hadi Januari 4, 20211 chama kitaitisha maandamano siku inayofuata bila kujali yana kibali cha polisi au la.

Masharti ya chama hicho ni pamoja na kutaka usifanyike uchaguzi wowote wa mameya au wenyeviti wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Manispaa ya Arusha na Hai.

"Kama unavyojua, uchaguzi wa wenyeviti na mameya hao umevurugika kwa sababu ambazo zina utata na kwa vyovyote vile kuonesha dalili ya kuwa na maelekezo kutoka ngazi za juu, jambo ambalo limeleta utata mkubwa ikiwa ni pamoja na uvunjifu wa amani," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza;

"CHADEMA tumejitaidi kutuliza wapenzi wetu hata baada ya wananchi kupigwa mabomu na polisi bila sababu," alisema Dkt. Slaa

Chama hicho kimesema polisi ni watuhumiwa katika matukio ya Arusha, hivyo kama hakutakuwa na maridhiano serikali itakuwa imewalazimisha kuchukua hatua ya kuandamana.

Pia kimetaka masharti yote yaliyotolewa Arusha yaendelee, yaani Mkurugenzi wa Manispaa ajiuzulu kwa ukiukwaji wa kanuni za halmashauri na kusimamia uchaguzi kinyume na taratibu, uongozi wa TAMISEMI uliingilia uchaguzi hasa Kigoma/Ujiji, hivyo wahusika wote wachukuliwe hatua.

Chama hicho kimeitaka serikali kumchukulia hatua OCD wa Arusha kwa kuingia na kumkamata mbunge ndani ya kikao halali kinyume na kanuni za uendeshaji wa halmashauri. Kwa mujibu wa barua hiyo, chama hicho kinamtaka OCD huyo ajiuzulu au aondolewe.

"CHADEMA sasa tumefikia mahali tumechoka na unyanyasaji, serikali ijue hivyo. Ni imani yetu kama serikali inataka haki itendeke, hatua stahiki ziwe zimechukuliwa kwa wahusika kabla ya terehe 4 januari, 2011," ilieleza barua hiyo.

Katika barua yake Dkt. Slaa alieleza kuwa chama chake kinaheshimu mazungumzo yake na Bw. Tendwa na yale ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Bw. Said Mwema.

"Kama tulivyokubaliana kati ya Dkt. Slaa na Bw. Tendwa, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa itaratibu mkutano huo na kuwajulisha wahusika juu ya malalamiko ya CHADEMA," ilieleza barua hiyo.

Alisema chama hicho kitaitisha mkutano wa waandishi wa habari kuomba wananchi wa Arusha watulie hadi watakapojulishwa hatua zaidi, iwapo serikali haitakuwa imechukua hatua.

 
Tatizo ni akina Makamba na wenzie ambao walilelewa kwenye mfumo wa Chama kimoja tu................................................................................hawana uzoefu wa mfumo wa vyama vingi.......................na ndiyo maana hawaambiliki kabisa...................
 
Soma maoni ya wengineo waliojitokeza kwenye gazeti la Majira................................

5 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Chadema wananchi watanzania tupo nyuma yenu kwa ajili ya mapambano na utawala wa mafisadi wa CCM. Wao hawakuzaliwa wawe watawala na wengine watawaliwa! Nchi hii ni yetu sote siyo yao pekee yao. Mapambano lazima yaendelee mpaka ushindi upatikane. Tanzania itakuwa Ivory Cost kwa ajili ya uroho wa madaraka wa watu wa CCM. Ni nani asiyejua Chadema ina madiwani wengi Arusha? Hivi inawezekanaje CCM washinde ikiwa kura zitapigwa kwa uhalali? Wabunge wa CCM wapo wengi ndani ya bunge dunia ingeshangaa kama Anne Makinda asingepita hivyo hivyo lazima dunia ishangae kwanini mgombea wa CCM apite mahali ambapo kuna madiwani wengi wa Chadema. Jamani hii CCM inatupeleka pabaya Tanzania na huo ni mwanzo wa CCM kusambalatika kama wananza kutumia nguvu kuchukua madaraka ya halmashauri ndio maana tunaamini hata Kikwete alichakachua matokeo. Watanzania wameichoka CCM. Hata kama itanyaje. Dawa ni wao kuachana na ufisadi unaofanya maisha ya wengi yaendelee kuwa ya ufakala wa kutpwa. Na wao na watoto wao wakineepa. Tanzania ni yetu sote siyo ya kikundi cha wana CCM.
December 23, 2010 11:54 PM
blank.gif

Anonymous said... Ebwana umenena mtu mzima wasitufanye Watanzania ni mataahira hiyo amani wanayoisema haitakiwi tu mdomon ila ni kwa vitendo wasifikiri amani ya Tanzania inajengwa kwa mazoea bali kwa haki na matakwa ya wananchui yanaheshimiwa hivi wao wanapanda bangi wantegemea kuvuna mihogo waache upumbavu la sivyo mahakama za uhalifu za kimataifa zinawasubiri.
December 24, 2010 12:30 AM
blank.gif

Anonymous said... Ningependa kuona amani ikiendelea katika nchi yetu Tanzania, na si kutoweka kwa manufaa ya wachache,CCM lazima wakubali kila lenye mwanzo halikosi mwisho na hasa kwa sasa.Kwamtazamo wa kina wananchi wa Tanzania wamechoshwa na ukiritimba wa muda mrefu unaofanya na viongozi wa chama CCM.Waswahili wanasema wengi wape,sawa kusoma hatujui basi hata picha.Wingi wa madiwani wa chama cha CHADEMA mkoani Arusha, unatoa picha kamili ya nafasi ya umeya katika mkoa uwo.Chonde AMANI ndio rasimali kubwa tunayojivunia na kuna dalili zote zinazoashiria utokomeaji wake .TUSIPO ZIBA NYUFA TUTAJENGA UKUTA...........CCM someni alama za nyakati watu wameamka sasa kila sehemu mnataka kuchachua hata nafasi zisizo chakachuliwa .............
December 24, 2010 1:16 AM
blank.gif

JOJAS BRAND said... Mh.Dr.slaa,ukumbuke kuwa polisi niwa serikali ya CCM.Itakuwa ni vigumu sana serikali kuchukua hatua za kinidhamu kwa wahusika uliowataja hapo juu.Chamsingi mwambie mungu aingilie kati suala hilo.Suala la maandamano lisahau hutopewa kibali cha maandamano kwa sababu ya ubabe wa CCM na serikali yake.
December 24, 2010 1:19 AM
blank.gif

Anonymous said... Kwa nyakati hii iliyopo sasa hivi ni kuingia barabarani tu watapiga wangapi, wataua wangapi, na hapo ndipo dunia itajua mahali CCM ilipotufikisha. Tumechoka na kiburi cha CCM, Kama FFU NA POLICE watafanya watakavyoagizwa basi na wafanye lakini tunaomba maandamano ya amani tueleza dunia kilio chetu kama hawataki kutusaidia sisi masikini.

Wanasema tufanye kazi, kazi gani? Wao wanafikiri wamachinga kukimbaa kimbia na maduka mkononi ni wao wamependa, na ninani amewafikisha hapo. Mtu unamkuta amesoma vizuri anaelimu nzuri aituie wapi kila kona ni wazee hawataki kustaafishwa na ndio maana TANESCO INASUMBUA HII NI KASUMBA YA HAO WAZEE. WAACHE VIJANA WENYE TECHNOLOGY YA KISASA WAFANYEKAZI. HAO WAZEE WALISHAZOEA MGAO. Na kama sio hivyo basi kutakuwa kuna mtu anataka kuuza genereta zake hilo la umeme ni biashara.

Serikali lazima mjiulize haki ya mtanzania ipo wapi? Akiwa na lengo lolote mnamzuia ni kwa nini? Yaani maandamano ya amani hata sikumoja hayazuiliwi kwa sababu lazima yatakuwa na ujumbe fulani, na ule ujumbe lazima utafutiwe ufumbuzi kama inawezekana. Mbona nchi zilizoendelea maandamano kwao ni kama kawaida na wanapewa ulinzi mkali mbele na nyuma.
December 24, 2010 9:10 AM
 
Today, the values of Democracy, open society, respect for human rights, and equality are becoming recognized all over the world as universal values. To my mind there is an intimate connection between Democratic values, such as Transparency, The rule of law and Freedom of information, and The fundamental values of human goodness good without any expectations – based on realizing that "the other person is also just like me and you". Mendous difference - approaching others with the thought of compassion in our mind is the best waymendous difference - approaching others with the thought of compassion in our mind is the best way. Let us Support CHADEMA. "Together we Can"
 
Big up DR. Slaa ccm haitakubali amani bali shari. Tutakufa na watazaliwa wengine kuendelea kuisaidia nchi hii kwa damu ya mashahidi waliotangulia.
 
Back
Top Bottom