CHADEMA yatoa dira ya Uchaguzi Mkuu 2015

Walinitoa jasho kikao chao kilipoamua kwa pamoja kumwangukia Slaa agombee, jambo ambalo ni nadra kwani vyama vingine huwa na ushindani wa kugombania nafasi hiyo nyeti.

Mkuu Candid Scope umenikumbusha kitu muhimu sana Wakati vyama vingine watu wanalilia mpaka kuuana kwaajili ya Urais CDM ni chama cha kipekee duniani kina muangikia mtu agombee na ana kubali kwa shingo upande kwa maana nyingine ni chama chenye watu na wanachama ambao hawana uroho wa Madaraka tofauti na vyama vingine kwi! kwi! kwi! CDM inanifurahisha mkuu
 
mimi naamini mwaka 2015 tanzania itaongozwa na chadema kwani nimebahatika kuzunguka nchi hii hakika iko tayari kuongozwa na chadema..cha msingi mashambulizi yaendelezwe na tuongeze umakini maana hawa mafisadi wanatafuta pakujishika...
Mkuu Crashwise kwa hiyo habari hapo juu nakubaliana na wewe 100% wala sikubishii. Nisije nikawa kama wabunge wa CCM wanaunga Hoja 100% halafu wanaanza kuipinga tena huko katikati
 
Hiii habari itamfanya mwigulunchemba amwage radhi bungeni.
 
MIKAKATI YA CHADEMA
Mbowe ametangaza kuwa katika uchaguzi mkuu wa 2015 Chadema haitapokea 'maskrepa' yaliyokosa nafasi katika vyama vingine, biashara ya kupokea watu waliokosa nafasi katika vyama vingine ilikuwa 2010.
Alisema tabia ya kukimbilia meli dakika za mwisho ilikuwa zamani na kwamba uchaguzi ujao hawatakubali waliokosa fursa kwa vyama vyao kukimbilia Chadema.

Mipango yao ni kupata wabunge na viongozi bora watakaopimwa kwa dhamira, uwezo na uwajibikaji kwa chama.
"Wafanyakazi wanatishiwa kufukuzwa kazi na wafanyabiashara wanafilisiwa na kubambikiwa kodi kisa wameonekana kushabikia Chadema," alisema.

Baada ya kuhutubia, wanachama wa Chadema vyuoni mkoani Dodoma wameutaka uongozi wa chuo kuondoa bango la CCM lililoko UDOM kwa maelezo kuwa ni kinyume cha Ibara ya 7 ya Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005.

Hapo kwenye red nimeipenda. Viongozi huwa wanaandaliwa, sio kukurupuka na kufuata popularity.

Viongozi wazuri ni wale watakaopikwa ndani ya chama na si kutoka kwingineko.

Nape ana hoja yake anayoitoa mara kwa mara tena kwa kicheko kwamba kuruhusiwa kwa mgombea binafsi kwenye ngazi za uongozi ni kitanzi cha wapinzani kwani hawatapata watu walioachwa na ccm na kukimbilia upinzani, ambao watakuwa wanagombea wenyewe binafsi.

Hapo Nape aanze kupata somo, na viongozi watakaokuwa bora ni wale watakaokuwa kwenye msingi wa chama!
 
Hiii habari itamfanya mwigulunchemba amwage radhi bungeni.
 
ccm wamechekelea kuruhusu mgombea binafsi akili yao ikiwatuma kwamba wapinzani wanategemea makapi yanayotemwa na ccm, sasa wajue kwamba CDM iko full kwa kila nyanja, ccm itabaki na magamba yao, halafu kutakuwa na tawi lingine la magamba binafsi.
 
ccm wamechekelea kuruhusu mgombea binafsi akili yao ikiwatuma kwamba wapinzani wanategemea makapi yanayotemwa na ccm, sasa wajue kwamba CDM iko full kwa kila nyanja, ccm itabaki na magamba yao, halafu kutakuwa na tawi lingine la magamba binafsi.

hii nimeikubali.
 
Ni mkakati mzuri sana. Wagombea shuti wapikwe waive na waende wakachukue majimbo. Nimeupenda sana mkakati huu.
 
Binafsi nadhani it is a good long term tactical strategy ambayo itawatoa nje ya uzio wadandia wa 'MELI" dakika za mwisho na hivyo kukihakikishia CDM cream ya viongozi tayari kwa mapambano ya kuteka dola 2015. Ni kweli walianza na MUNGU na wajitahidi wamalize na MUNGU.
 
duh kwa mkakati huu ccm haina chake 2015..na hili la kutopokea maskrepa ni la msingi sana hasa ukizingatia kuwa nchi haiwezi kujengwa na wazima moto..
 
Back
Top Bottom