CHADEMA yatikisa vigogo wa CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Waandishi Wetu


Arusha


230_siyoi_img_0.png



Siyoi Sumari


HALI ya wasiwasi imezidi kuenea ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na pingamizi jipya dhidi ya mgombea wao katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, Siyoi Sumari, na sasa chama hicho tawala kimekuwa kikiendelea na kampeni zake kwa kusubiri huruma ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa mujibu wa taarifa zilizobainiwa na Raia Mwema, endapo pingamizi hilo lililowekwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) litaridhiwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), CCM itaweza kutupwa nje ya kinyang'anyiro hicho cha ubunge kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Awali, gazeti hili lilipata taarifa kuwa CCM kilikuwa na mpango wa kumteua mgombea wake namba mbili katika duru la pili la kura za maoni katika chama hicho, William Sarakikya, kuwa mgombe ili kujiepusha na uwezekano wa Sumari kuwekewa pingamizi ambalo linaweza kukigharimu chama hicho kikongwe katika historia ya chaguzi ndogo nchini.


Katika kile kinachoweza kuelezwa kuwa ni jitihada za kushughulikia kadhia hiyo inayoitia hofu CCM, tayari Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu, Damian Lubuva, ameanza vikao na timu yake kuchambua rufaa ya CHADEMA, ambayo msingi wake ni kulalamikia kutupiliwa mbali kwa pingamizi lao waliloweka dhidi ya Sumari kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Tracius Kagenzi.


"Viongozi wameanza kuzungumzia na hata kutafakari namna ya kumudu changamoto inayoweza kujitokeza endapo pingamizi la CHADEMA litakubaliwa na kwa hiyo, Siyoi Sumari akaenguliwa kwenye mbio za ubunge zilizokwisha kuanza. Hata hivyo, licha ya kuanza kutafakari suala hilo, bado wanaamini tume itamwacha Sumari aendelee ingawa kwa kweli hawana uhakika na hilo. Kuna wasiwasi kati yao," anaeleza mtoa habari wetu ndani ya CCM.


Rufaa ya CHADEMA

Mgombea wa CHADEMA jimboni Arumeru, Joshua Nassari ndiye aliyekata rufaa NEC, akipinga hatua ya msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Tracius Kagenzi, kutupilia mbali pingamizi aliloweka kuhusu utata wa uraia wa mshindani wake kutoka CCM.

Nasari na chama chake wanataka ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume hiyo ya Uchaguzi, wakidai kuwa msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo kashindwa kufafanua sheria za masuala ya uhamiaji.








 
  • Thanks
Reactions: GIB
Back
Top Bottom