CHADEMA yateka kusini - Soma hotuba yao

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
267598563.jpg

DHANA ya kuwa mikoa ya kusini ni ngome ya Chama cha Mapinduzi jana ilifutika vichwani mwa wakazi wa mikoa hiyo, baada ya umati mkubwa kujitokeza, kuulaki msafara wa viongozi na hatimaye kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Mtwara. Msafara huo wa kitaifa ukiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ulipata mapokezi ya vijana wakiwa katika msafara wa pikipiki magari na baiskeli karibu na daraja la Mikindani na kuelekea katika uwanja wa Mashujaa ambapo umati mkubwa wa watu ulifurika kupita kiasi.

Mbowe tayari kufa kwa ajili ya Watanzania

Akihutubia katika mkutano huo Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe alisema ameshajiandaa kisaikolojia kufa kwa ajili ya kutetea haki na kwamba wananchi wasiogope kupigania haki zao. Alisema ikitokea akafa akiwa katikati ya mapambano waliobaki wasihuzunike bali wahakikishe huo ndiyo unakuwa mwanzo wa ukombozi. "Nikifa katika mapambano haya uinueni mwili wangu uwekeni pembeni na kisha endeleeni na mapambano kwa kuwa haya si ya Mbowe peke yake bali ni ya Watanzania wote," alisema Mbowe.
Aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa hawakwenda pale kutafuta jimbo au kata bali kuleta ukombozi wa kweli kwa kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha nchi inakombolewa.
Akizungumzia kuhusu udini, Mbowe alisema viongozi wa serikali wanaotumia udini, ukabila na ukanda kuwagawa watu wamekata tamaa ya kuwatumikia.Alisema kuwa kwa hali ilivyo itakuwa ni hatari zaidi kwa ustawi wa Tanzania kama hata tone moja la mafuta yatapatikana huku nchi ikiwa inaongozwa na serikali ya CCM kwa kile alichodai tayari wamemwaga damu kwa tamaa ya mali katika rasilimali zilizokwishaanza kupatikana.

Dr. Slaa awaonya Polisi na Vurugu Zanzibar

Naye Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, aliwataka polisi kuacha kuwanyanyasa raia na kueleza hata yanayotokea Zanzibar kwa sasa ni udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka kuzuia watu wasitoe maoni. Alisema hatua ya kuwataka watu wasijadili suala la Muungano wakati unawagusa haiwezi kukubalika na kwamba polisi wawe na akili ya kuambiwa na kisha kuchanganya na zao kwa ajili ya maslahi ya Tanzania. "Kikwete amesababisha hali hii ya Zanzibar, maana hakukuwa na haja ya kumkamata mtu aliyekuwa anatoa maoni juu ya mustakabali wa nchi yake," alisema Dk. Slaa.

Kuhusu bajeti ya 2012/2013 Dk. Slaa alitaka isimamishwe na mishahara ya wafanyakazi iboreshwe. Kuhusu korosho, Dk. Slaa alisema wakazi wa Mtwara wanafanywa maskini huku korosho zao zikienda kutoa ajira kwa wananchi wa India na wajanja wachache wa hapa nchini. "Tanzania haitakombolewa bila mikoa ya kusini kuwa huru, tunataka mtuunge mkono katika kila hatua ili tuchukue nchi 2015," alisema Dk. Slaa.

Mnyika adai Bunge ni Kanyaboya
Mbunge wa Ubungo John Mnyika akihutubia umati huo alisema Bunge la Tanzania halina nguvu ya kuiwajibisha serikali na kama litafanya hivyo Rais anaweza kuwatimua wabunge wote. Alisema hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na Katiba liyopo ambayo alisema ni lazima Watanzania wajitokeze na kuingiza mambo ya msingi wakati wa kutoa maoni. Aliongeza wakazi wa Mtwara wanashindwa kufaidika na gesi iliyoko mkoani humo pamoja na kukosa uwezo wa kumiliki ardhi kwa amendeleo yao.

Mawazo abeba silaha
Aliyekuwa diwani wa CCM kata ya Arusha Alphonce Mawazo aliwaambia wakazi wa Mtwara kuwa mabadiliko ya kweli huanza kwenye akili na mtu akishafungua akili kila kitu chake kitaenda kwa ufasaha na kuwa huru. Huku akishangiliwa na umati wa watu uwanjani hapo Mawazo alisema wameenda Mtwara wakiwa na silaha za nguvu ya umma, na kuwataka wasitengane katika kutafuta mabadiliko ya kweli, na kuachana na waliowasaliti kwa kuwaingiza katika maisha magumu. Aliwaeleza wakazi wa Mtwara kuwa wamefungwa na minyororo ya umaskini na kwamba minyororo hiyo ni mibaya kwa mustakabali wa maisha yao kuliko hata minyororo ya chuma waliyokuwa wakifungwa watumwa enzi za ukoloni

Millya: CCM imeshaanza kuaga
Kwa Upande wake aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha James Millya alisema harakati zilizoanzishwa na CCM hivi karibuni kutaka nafasi ya mgombea urais ihojiwe mahakamani ni baada ya kugundua mwaka 2015 hawatakuwa na nafasi ya kushinda hivyo kimbilio lao ni mahakamani. "CCM wanatuaga na mkitaka kuamini hilo sasa wameanza kutaka nafasi ya urais ihojiwe mahakamni kwa kuwa huko ndiko kimbilio lao lililobaki kwa sasa," alisema Millya. Alisema CCM inaichukia CHADEMA kwa kuwa inataka uhakika wa maisha hata kwa mtoto wa maskini ambaye hajui hatma yake ya maisha kwa siku zijazo. Aliongeza kuwa ni wakati muafaka sasa kwa Watanzania kuachana na watu waliowasaliti kwa kushindwa kusimamia wajibu waliokabidhiwa.
 
Gud work guyz, Endeleezemi mapambano sisi tuko nyuma yenu kuwawezesha kifedha na kisaikolojia. (tunwaombea) natamani nikuwa mstari wenu... kibarua baba LOL
 
Hongereni sana Makamanda kiukweli mmejipanga si mchezo!!

MUNGU AWATANGULIE!!
 
hivi na hii nayo NAPE ata comment ? kwa mtu serious kabisa ndani ya CCM ataweza kuona ni kwa jinsi gani CCM inaelemewa na kasi hii...lakini watasema ni UPEPO TU UTAPITA..
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezI kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezi kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.
peeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeoooooooppppppplllllleeeeeeeeeez.
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezI kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.

chadema hakuna mtu anaitwa mboye,mpaka hapo tayari nitakuwa nimeshakuvurugia buku yako kwa nape,pole sana
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezI kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.

Mfa maji..........!!? Siaza za aina hii hazina nafasi kwa sasa. Mliweza enzi za CuF, mkafunga nao ndoa. Hilo halitatokea tena, wananchi wanajua kila kitu ikiwa ni pamoja na hila zenu. Jiandaeni vyema kuachia madaraka.
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezI kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.

Maendeleo yapi hayo mkuu?

Tiba
 
siamini kama watz wameamua kuitumbilia mbali ccm kiasi hiki.
Mpaka kieleweke.

mungu akiwa upande wa cdm nani aliye kinyume nasi? Fitina, hapana, uchawi hapana, ruiushwa hapana, hapana nasema hapana cdm inaunganisha watanzania woooote karibuni dodoma wakati wa bunge tufanye mabadiliko makubwa sana
 
mboye unadhani watz hawajui kuwa wewe wewe ni mchuuzi , kweli mmiliki wa danguro awe rais wa nchi watz wanajua na ulimwengu unajua. Dr slaa analipwa mil 7.5m kwa mwezi. Akiwa rais atataka kulipwa 100m kwa mwezI kwa vile amekaa nje ya bunge kwa muda. Tamaa ,ukanda na uroho wa madaraka ndio sifa ya viongozi wa chadema. Maendeleo yaliyopo kusini sasa ni matokeo ya kazi ambao mtu mwenye akili timamu hawezi kubisha.

Si mlisema jana kuwa vua gamba vaa gwanda limepata dhoruba huko kusini, sasa mmekuja na mpya la danguro. Tutawaona.
 
Kwa hakika Chadema inawakomboa wengi toka kwenye mzito wa mawazo mgando toka CCM,hali ikiendelea hivi basi tutarajie mabadiliko makubwa 2015
 
Back
Top Bottom