Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
na Edward Kinabo
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka serikali kuitikia wito wa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, ikiwa ni pamoja na kuufanyia marekebisho muundo wa sasa wa muungano ili kuirudisha nchi ya Tanganyika iliyopata uhuru wake mwaka 1961.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kinondoni, John Mnyika, wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana wa chama hicho, lililoandaliwa mahususi kutathmini miaka 48 ya uhuru wa Tanganyika.
Nashangaa tunaposherehekea uhuru wa nchi ambayo haipo. Kimsingi uhuru tunaousherehekea wa miaka 48 ni uhuru wa nchi iitwayo Tanganyika, kwani ndiyo iliyopata uhuru mwaka 1961.
Lakini Tanganyika kikatiba haipo, nchi zilizopo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Zanzibar ipo lakini Tanganyika iliyoungana nayo haipo, tunasisitiza tena wito wetu wa kuitaka serikali kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, ikiwa ni pamoja na kuufanyia marekebisho muundo wa muungano utakaoirejesha Tanganyika. alisema Mnyika.
Alisema wakati Tanganyika ikiadhimisha miaka 48 ya uhuru wake, bado haijafanikiwa kupambana na maadui wanne; ambao ni ujinga, umaskini, maradhi na rushwa.
Ujinga bado upo, serikali inajenga sekondari za kata zisizokuwa na walimu wala vifaa vya kutosha kuondoa ujinga. Maradhi yapo, leo hapa Wilaya ya Kinondoni tu tunakabiliwa na kipindupindu na mama wajawazito wanaendelea kupoteza maisha yao pale Hospitali ya Mwananyamala.
Umaskini upo, kwa mfano wakati wa Mwalimu, pato la Mtanzania lilikuwa dola mbili kwa siku (takriban sh 2,000 kwa siku), leo pato la Mtanzania ni chini ya dola moja kwa siku (chini ya sh 1,000 kwa siku). Rushwa ya kawaida iliyokuwapo wakati wa Mwalimu, sasa imeota mizizi na kuwa ufisadi unaotamalaki ndani ya mfumo mzima wa uongozi, alisema Mnyika.
Alisema wakati Tanganyika ikiadhimisha miaka 48 ya uhuru wake, hali halisi inaonyesha kuwa taifa hilo ambalo halipo kikatiba, linakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na tishio la kuvunjika kwa amani na umoja uliojengwa na waasisi wake.
Waasisi walijenga amani na umoja. Leo mijadala ya kidini imekithiri na inazidi kufufua hisia za ubaguzi wa kidini kati ya waumini wa dini moja na nyingine. Leo pengo la kiuchumi kati ya matajiri na maskini linazidi. Migogoro ya kirasilimali nayo inazidi.
Tumeshuhudia mapigano kati ya wakulima na wafugaji kugombania rasilimali ya ardhi. Tumeshuhudia Watanzania wakiondolewa bila taratibu katika ardhi yao kupisha wawekezaji, mfano kule Loliondo na kwenye maeneo yenye madini. Chaguzi zetu pia zimekuwa za hatari, tumeona ya Zanzibar na tumesikia na kushuhudia umwagaji damu katika chaguzi ndogo za ubunge kwenye majimbo ya Tarime, Kiteto, Busanda na Biharamulo. Haya yote ni tishio kwa amani na umoja wa taifa letu, alisema Mnyika.
Alitoa wito kwa Rais Kikwete kukubali kufanya maamuzi magumu ya kulinusuru taifa kama ilivyopendekezwa katika maazimio ya kongamano la Mwalimu Nyerere na yale yaliyotolewa katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichomalizika hivi karibuni. Katika kongamano hilo, Mnyika alizindua tuzo kwa vijana ya uhuru wa kweli ya Freeman Mbowe Freeman Mbowe Youth Real Freedom Award, itakayokuwa inatolewa kila ifikapo Desemba 9 ya kila mwaka, kwa vijana wa umri wa miaka 18 hadi 35, watakaokuwa wanashinda mashindano ya uandishi wa hotuba kuhusu uhuru wa Tanganyika, yatakayokuwa yanaandaliwa na uongozi wa CHADEMA Mkoa wa Kinondoni.