Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
Niko mjini Wete kwa shughuli za kikazi kwa siku tatu sasa. Nimepata nafasi ya kukutana na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti kuzungumzia upepo wa kisiasa. Wakiwemo vijana, wazee, na wafanyabiashara. Suala la kuzama kwa meli linaonekana kugusa hisia zao kisiasa.
Wapemba wengi wanausikitikia mwafaka na wanasema umewamaliza kwa vile sasa hakuna upinzani. Mfano wanaoutolea ni suala la kuzama kwa meli ya spice. Wanasema, suala kama hilo ambalo limeondosha watu takribani 4000 katika kisiwa cha watu takribani 400,000 ni sawa na 1% ya wakazi lilipaswa kuwa moto sana lakini sasa sawa na kama waliokufa ni sisimizi tu. Wengi wamesema - "Tunasubiri chama mbadala".
Nilipomhoji aliyekuwa mmojawapo wa wagombea ubunge wa CUF aliyebwagwa kimizengwe kwenye kura za maoni, alisema yeye yuko tayari kuingia chama chochote mbadala. "Niko tayari kwenda chama chochote mbadala. Napima upepo tu". Nilipomhoji juu ya mtazamo wake kuhusu CHADEMA kama chama mbadala, alisema: "Tumekuwa tukilijadili hilo na wenzangu hata wengine waliokuwa wakigombea uwakilishi na tunatambua uimara wa CHADEMA hasa katika kusimamia mambo ya kitaifa. Kina viongozi madhubuti na wenye upeo mkubwa kama Dr. Slaa na wengine. Kama kitakuja kujitambulisha vema huku, tutatafakari mwelekeo wakati huko. Sisi hatukuzaliwa na CUF".
PENDEKEZO: Naomba viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wapange namna gani ya kutumia vaccum hii iliyotengenezwa na CUF, ili kuwa chama mbadala katika visiwa hivi viwili.