CHADEMA yasomba wana-CCM mkoani Pwani.

nape yeye anataswira ya miaka 50 iliyopita anazani kukanusha kwa weza kunusuru chama hiki ni kiama kwa ccm
 
WanaCCM waliohama kwenda upinzani wenye majina ndani ya CCM kama Diwani n.k. hesabu yao haizidi sita (6) "by Nape"

Nepi Nauye kweli anaonekana ni mpuuzi kama siyo mjinga. Yeye anavilaumu vyombo vya habari kwamba vinalikuza hili jambo pasi na sababu. Nimemsikia akiropoka kwenye runinga kky kwamba hata hao wana-CCM wanaosemwa kati ya 2000-5000 kuhamia CDM kwenye maeneo husika ukienda pale idadi ya wanachama walioko pale hawafikii hiyo hesabu!!!Sasa mimi nikajiuliza kama hayo maeneo yanayodaiwa wana-CCM kuhama hayana idadi hiyo ya wanachama,CCM walipata wapi KURA za ushindi wa Urais na Ubnge kwenye maeneo hayo???

Nepi analeta tabia ya NBUNI. Yaani unaona moto umekuzunguka na unaunguza nyika kukufuata wewe unaamua KUFICHA KICHWA KWENYE MCHANGA maana moto utapita na wala hutakuchoma!!!Akili mbovu kwelikweli. Kwa watu wanaosoma between the lines watakubaliana na kile a Klichosema Katibu Mkuu wa zamani-CCM Bwana Makamba kwamba NEPI na MUKUMA wameifanya CCM kuwa mali yao. Wao ndiyo wenye chama na wana haki ya kusesema chochote bila kujali madhara yanayoikumba CCM. Ama kweli KUFA KWA NYANI MITI YOTE HUTELEZA.

Mimi naamini kwamba Mungu kwa sasa ameamua kusikia kilio cha Watanzania na hawa viongozi wa CCM walioko madarakani kuanzia Mwenyekiti wao KIWETE,MUKUMA na NEPI wamewekwa makusudi na Mungu ILI CCM IPATE KUFA TARAATIIIBU kwa kifo cha mende!

Pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz!Powwwwwwwwwwwwwwwwweeeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrrrrr!!!
 
Sasa ccm wanacheza ngoma ya cdm. Nape endelea kuwaroga ccm ili wasione ukweli.
 
WanaCCM waliohama kwenda upinzani wenye majina ndani ya CCM kama Diwani n.k. hesabu yao haizidi sita (6) "by Nape"

Hakuna Diwani bila wapiga kura,na hakuna diwani bila ya wanachama na chama hadi wakati huu ambapo katiba hairuhusu mgombea binafsi,hivyo basi hata kama ni madiwani sita lakini wametoka CCM na wana CCM ndio haoooo to peopleeees power.
Atakuwa anajifariji na kuishi kwa matumaini
 
hao walikuwa kwenye mkakati wa kufukuzwa na chama katika mpango ulioasisiwa na rais wa chama kujivua gamba-by nepi mniue
 
Bado familia ya Kikwete maana najua yeye Kikwte ana kadi ya chadema....
...sioni mantiki ya kuifurahia statement hii, kwa mazuri yepi ya Kikwete, kiasi ushangilie Kikwete kuwa na kadi ya CDM? hatutaki kuhamishiwa wezi kutoka CCM kwenda CDM!
 
Masikini Chama Cha Mapinduzi!!!!!!!!!!!!!!!!

Wimbi limalotikisa nchini kwa sasa la wanachama wa CCM kukimbilia CHADEMA limeingia Mkoani Pwani ambapo wanachama 250 wa CCM katika kijiji cha Mkoko, kata ya Msata, wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, wamekihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA wakati wa operesheni ya kutembelea vijiji inayofanywa na viongozi wa chama hicho.
Katibu wa CHADEMA Jimbo la Chalinze Gasper Shoo alisema kuwa wanachama hao wa CCM walijiunga na upinzani Mei 12 wakati wa operesheni hiyo iliyoongozwa na viongozi wengine wa jimbo.
"Katika operesheni yetu tuliyoifanya Mei 12 mwaka huu wanachama wa CCM 250 wamekihama chama chao na kuingia CHADEMA wakiwa na lengo moja tu la kuunga mkono viongozi wa taifa wanaopambana na ufisadi na kupigania maendeleo katika maeneo mbalimbali hapa nchini," alisema Shoo.
Aidha aliongeza kusema kuwa wataendelea na ziara yao hasa maeneo ya vijijini ambayo CCM wamekuwa wakijivunia kupata kura nyingi kutokana na baadhi yake kutofikiwa kwa muda mrefu na viongozi wa CHADEMA.
Mkoa wa Pwani umekuwa ni ngome kuu ya CCM kwa muda mrefu lakini sasa ngome zake zinaanza kusambaratishwa vibaya na CHADEMA hali inayohatarisha uhai wa chama hicho kwa siku za usoni.

Source:Tanzania Daima Ijumaa
 
Back
Top Bottom