CHADEMA yashtuka kampeni chafu

mmmh, SMH, got no clue on what to believe...whatever the case down with CCM and up with the opposition
 
Sielewi kuwa origino komedi nao ni wachambuzi wa mambo. Kila siku huwa ninamini kuwa wao wanachukua jambo lolote na kulifanya liwe komedi.
 
They should stick to comedy otherwise they may be seen to be another mouth piece of CCM as has been the case with Komba the musician/parliamentarian.
 
CUF ilikuwa bora zaidi Tarime, Mwera king’ang’anizi-Prof. Lipumba

Jana hapa Mbeya Mwenyekiti wa CUF Lipumba, amesewa kwamba chama chake na mgombea wake walikuwa bora zaidi huko Tarime baada ya kifo cha Chacha Wangwe lakini CHADEMA kwa uroho wa madaraka wakang’ang’ania kugombea. Lipumba anasema Wazee wa Mila wa Tarime walitaka zaidi mgombea wa chama hicho kuliko Charles Mwera wa CHADEMA, lakini CHADEMA wakakimbilia kuchukua fomu na kugombea. Bwana Lipumba akasema kuwa pamoja na hujuma hiyo, bado akampigia simu mgombea wa chama chake kumwambia ajitoe ili kumuunga mkono mgombea wa CHADEMA na mgombea wake kwa kulinda upinzani akafanya hivyo. Akasema kuwa hata Mbowe akipigiwa simu atathibitisha kwamba CUF na mgombea wake walikuwa bora zaidi Tarime kuliko CHADEMA baada ya kifo cha Chacha Wangwe. Profesa Lipumba amesema kwamba CHADEMA wameendeleza tabia hii Mbeya Vijijini ambapo Sambwee Shitambala alichukua fomu pamoja na kuwa mgombea wa CUF Bwana Mponzi alikuwa anakubalika zaidi na Machifu wa Mbeya vijijini na hivyo CUF kuiandika barua CHADEMA ya kutaka waaachiwe. Prof Lipumba amehimiza wananchi wa Mbeya Vijijini kuchagua mgombea wa CUF na kutaka wanachama wa CHADEMA wamuunge mkono mgombea huyo kama CUF ilivyounga mkono CHADEMA Tarime. Profesa Lipumba aliyasema hayo katika mahojiano ya moja kwa moja(Live) na Kituo cha Radio cha Bomba FM yaliyofanyika usiku. Kwa mujibu wa matangazo ya radio hiyo, mahojiano hayo maalumu yataendelea tena leo jioni kabla ya muda rasmi wa kampeni kumalizika. Kutokana na maelezo hayo ya Lipumba, wasikilizaji waliopiga simu waliishambulia zaidi CHADEMA na kuisifu CUF kwa kuunga mkono vyama vingine katika chaguzi. Hata hivyo, wapiga simu wengine walieleza dhamira yao ya kuchagua CCM katika uchaguzi huo na kumuunga mkono mgombea wake Mchungaji Mwanjali. Kampeni za uchaguzi huo zinamalizika leo na kura zinapigwa kesho Januari 25.

…..ndiyohiyo
 
Inaelekea kampeni za CUF zimedorora ndio maana sasa wanataka kumtafuta mchawi huku wakijua wazi kuwa wachawi ni wao wenyewe.
1.Inakuaje wanashambulia CHADEMA ambacho hakipo kwenye uchaguzi na wala hakina mgombea?
2.Inakuwaje wanakitukana CHADEMA na wakati huohuo wakiomba wanachama haohao wanaowatukana kuwaunga mkono?

3.Kusema kuwa mgombea wao Tarime alikuwa anaungwa mkono zaidi ni uongo na ni upotoshwaji wa wazi kabisa kwani kama CUF wangelikuwa na nguvu kiasi hicho mbona mgombea wao wa udiwani TARIME MJINI aliambulia kura 300? wakati wa CHADEMA alipata kura 6000 na ushee?
4.Kusema kuwa mgombea wa CUF alikuwa anaungwa mkono ni uongo kwani CUF haikuwa na mgombea mpaka bwana Mponzi aliposhindwa kwenye kura za maoni CCM na kuamua kujiunga na CUF ili akawe mgombea wao ,sasa huyo aliyekuwa anaungwa mkono ni nani wakati walikuwa hawana mgombea wakati huo wa mchakato wa awali?

5.Upotoshwaji mwingine unaofanywa na CUF ni kusema kuwa mgombea wa CUF mwaka 2005 alikuwa wa pili, japo ni kweli alikuwa wa pili ila kwa kura chache sana kwani wa CCM wakati huo alipata kura 65000 na mamia kadhaa , huku wa CUF alipata kura 6000 na mamia , na wa TLP naye alipata kura 6000 na mamia kadhaa .

Nawashauri CUF wapambane wenyewe kwani hata CHADEMA TARIME walipambana wenyewe , kwani wakati huo LIPUMBA alihojiwa na gazeti la THE AFRICAN na kusema kuwa wao CUF kuhusu nani wanamuunga mkono alisema kuwa wao wapo Neutral maana yake ni kuwa yeyote akishinda kwao ni sawa tuu., Leo wanalialia huku wakijua kuwa CHADEMA ilishaweka hadharani msimamo wao kuwa hawatakiunga mkono chama chochote cha siasa kwenye uchaguzi huo na wala hawakusema kuwa wapo NEUTRAL kama CUF na TARIME.

Mwisho kuna jambo ambalo watu wengi hawalijui, kuwa mgombea udiwani wa CUF kata ya ULENJE iliyopo Mbeya Vijijini alimwekea pingamizi mgombea udiwani wa CHADEMA na alipoondolewa wa CHADEMA mgombea wa CUF alijitoa na kujiunga na CCM , na hivyo kumfanya wa CCM kushinda bila kupingwa ,sasa wanataka CHADEMA iende ikawaunge mkono kwa lipi jema?

Haya kisha tunasema kuwa hawa ndio viongozi tunaowachagua kutuongoza..
Profesa mzima mawazo yake kama muuza kahawa mtaani...
Kwanza bila aibu kiongozi mzima unasimama kuwahutubia wananchgi yaliytotokea Tarime na kudai ati - chama chake na mgombea wake walikuwa bora zaidi huko Tarime baada ya kifo cha Chacha Wangwe lakini CHADEMA kwa uroho wa madaraka wakang'ang'ania kugombea.
Mheshimiwa, Chadema walikuwa na kila haki ya kusimamisha mgombea Tarime kwa sanbabu kwanza Marehemu alitoka chama - Chadema. Na kikubwa zaidi ni kwamba yule anayekubalika ndiye siku zote huwa mshindi..sasa hizi habari za CUF kukubalika zaidi zinatoka wapi?.. au mgombea wa Chadema hayupo ktk muungano huo.

Ni upumbavu mkubwa kutoa malalamiko kisha unajirudi na kusema CUF iliwaunga mkono Chadema wakati ni wanachama wa CUF wilayani hapo walioamua kufanya hivyo kinyume cha matakwa yenu..
Kama nilivyosema chama sio Lipumba wala Seif Hamad, kumbukeni ni wananchi wanaopiga kura na hata kama Chadema wamechukua fomu Mbeya vijijini kimakosa bado ni wananchi wa Mbeya vijijini watakao piga kura..Na makosa haya hayakuanza Mbeya wala Tarime bali yameanza toka muungano huu ulipovihusisha vyama vingine nje ya CUF..
Sisi wananchi tumeyaona toka Tunduru na machafu haya yamesababisha kupoteza majimbo kwa sababu nyie viongozi wetu hamkuweza kupanga mkakati madhubuti unaojenga msingi wa vyama hivi na kuviwekea nguzo zitakazo simama ktk kila jimbo, badala yake nyote mnatarajia kujenga paa la nyumba ambayo hata matofali hayajafyatuliwa..Ni ujinga mtupu na hizo elimu zenu za kuendesha baiskeli.

Hakuna kiongozi hata mmoja wa Chadema aliyeomba wananchi wa Mbeya wasimchague mgombea wa CUF. Hizi fikra za kulipa visasi ni fikra mbovu ambazo binafsi natanguliza lawama zangu kwenu na kuwaomba wananchama wa vyama vyote vya Upinzani kutafuta viongozi wengine waondokane na viongozi wachovu wa kufikiri wanaoendekeza kujenga majungu na uchawi...
NJHAA tu ndio inawasumbua, mamluki wakubwa!
 
Naona nitoe hongera ikiwa tumefikia hatua ya kutumia redia katika harakati za Uchaguzi natumai Uchaguzi Mkuu ujao ,umahiri huu wa kuwaita wagombea wetu wa Uraisi katika vituo vya television utakubalika kwa vyama vyote ili kujenga utamaduni wa Mwananchi kuweza kuchagua kiongozi muelewa ambae atakuwa live katika dibeti za maswala ya papo kwa papo.
 
Na Maregesi Paul

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeendelea kukishambulia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema chama hicho hakina nia ya dhati ya kuwakomboa wananchi kwa vile viongozi wake hawana historia nzuri ya kutetea wananchi.

Akihutubia mkutano wa hadhara Manzese jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa, alisema ingawa viongozi wa Chadema wanawaambia Watanzania, kwamba chama chao ndicho kinachowajali zaidi, kauli hizo siyo sahihi kwa vile viongozi hao hawana historia ya kitaifa.

“Chadema walikuwa hapa jana, Mbowe alisema mengi sana katika mkutano wake huo, lakini ukweli ni kwamba, chama hicho hakina jipya kwa sababu viongozi wake hawana cha maana ukilinganisha na viongozi wa CUF,” alisema Jusa.

Alisema wakati CUF kinaanzishwa mwaka 1992, viongozi wa chama hicho walidhani wangeweza kushirkiana na vyama vingine vya upinzani kuiondoa CCM madarakani, lakini kutokana na sababu ambazo haziko wazi, chama hicho cha upinzani kimegeuka na kukidharau CUF ingawa CUF kina wanachama wengi katika maeneo yote ya nchi.

Kutokana na hali hiyo, alisema njama za kuihujumu CUF zinazofanywa na viongozi wa Chadema hazitafanikiwa kwa vile chama hicho kinaheshimika kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wa chama hicho.

“Chadema wanataka kutumaliza bila sababu za msingi kwa sababu siku hizi kila wanapopanda majukwaani, ajenda yao kubwa ni kutusema vibaya kadiri wanavyoweza. Lakini, ukweli ni kwamba, hawatatuweza na kama wanataka kujua nguvu tuliyonayo, basi wakawaulize CCM kwani ndiyo wanaotujua vizuri kuliko chama kingine chochote hapa nchini,” alisema.

Akizungumzia majigambo ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kwamba viongozi wa Chadema ndiyo vinara wa kupambana na ufisadi, Jusa aliwabeza viongozi hao na kutaka waeleze historia zao katika kipindi chote walichokaa bungeni kwa nyakati tofauti.

“Mbowe anajidai yeye ni bingwa wa kupambana na mafisadi, sasa atuambie katika kipindi chote alichokuwa Mbunge alifanya nini na pia Dk. Slaa aseme alikuwa wapi kusema anayosema sasa kabla hajashinda tena kiti cha ubunge wa Karatu mwaka 2005,” alihoji Jusa .

Awali, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, Abdul Kambaya, alisema baada ya Chadema kuonyesha kuwa hawataki siasa za kweli, hivi sasa chama chake kinawahesabu kuwa ndiyo maadui zao namba moja pamoja na CCM.
 
Back
Top Bottom