Elections 2010 CHADEMA yashitaki Umoja wa Mataifa

Facts1

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
307
28
Chadema yawasilisha malalamiko
Mashirika ya kimataifa pia yaelezwa


Kauli iliyotolewa na vyombo vya usalama Ijumaa iliyopita na kusomwa hadharani na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, juu ya Uchaguzi Mkuu imezua mambo mapya na sasa Chama cha Demokrsia na Maendeleo kimelalamika rasmi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa kuna njama za kuvuruga uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Waraka wa Chadema wenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/SG/02/79 uliochapishwa Oktoba 4, mwaka huu na umesainiwa na Mwenyekiti wa Kampeni za urais za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu na kupelekwa kwa kiongozi wa mabalozi walioko nchini.


Pia umenakiliwa kwa ofisi zote za kibalozi zilizopo nchini, mashirika ya kimataifa yaliyo nchini, wagombea urais wote na vyombo vya habari.

Waraka huo unasema kuwa Chadema wameguswa na kauli ya Luteni Jenerali Shimbo alipowatahadharisha Watanzania kwamba majeshi na vyombo vya usalama wamejiandaa kuzikabili vurugu zozote zitakazotokea wakati wa uchaguzi huo.


"Pasipo kutoa uthibitisho, Luteni Jenerali Shimbo alieleza hisia kwamba vyombo vya usalama vimepokea taarifa za kiintelijensia zikionyesha kuwepo vyama vya siasa vinavyojiandaa kwa ajili ya vurugu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu nchini," alisema.


Profesa Baregu ameelezea katika waraka huo kuwa ni kitendawili kwa Luteni Jenerali Shimbo kuvitaka vyama vya siasa na wagombea wao kuyakubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.


"Pamoja na kutambua haja ya majeshi ya ulinzi kuhakikisha utawala wa sheria na taratibu vinafuatwa, hasa wakati huu wa uchaguzi, tunaamini kwamba tamko hilo kwa kipindi hiki cha kampeni za kisiasa, limetolewa kwa pupa na bila vielelezo vyovyote thabiti," alisema.


Alisema Chadema inaliona tamko hilo ni kuingilia dhahiri mchakato wa uchaguzi na kupanga matokeo yake.

Alisema inapaswa kueleweka kwamba tamko la JWTZ ni kinyume cha Katiba na kwa makusudi limevuka mamlaka ya kikatiba kwa kuingilia shughuli za Jeshi la Polisi.


Pia, Profesa Baregu anasema hakuna msingi wa kutoa tamko hilo zito katikati ya kampeni, wakati hakuna uthibitisho wa tukio kubwa linalohatarisha amani na utulivu nchini.

"Nchi hii inatawaliwa kisheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria nyingine zilizopitishwa na Bunge. "Kama kuna watu wanaobainika kujihusisha na vurugu na kuhatarisha amani, jambo ambalo ni kosa la jinai hapa nchini, ni lazima washitakiwe," alisema.


Alisema Chadema haioni mantiki ya vyombo vya usalama kulalamika hadharani badala ya kuchukua hatua za kisheria kudhibiti uvunjifu wa amani na utulivu.


"Kama vyombo vya usalama vina taarifa sahihi ama za kiintelijensia, kwamba zimebaini kuwepo shughuli za jinai, vinapaswa kuchukua hatua mapema kuliko kutoa tamko la kisiasa," alisema.

Profesa Baregu alisema Chadema hakiamini kwamba tamko hilo lilitokana na taarifa zilizokusanywa kutoka katika vyanzo vya kiintelijensia. Badala yake alisema lina shinikizo la kisiasa linalokusudia kuwatisha wapiga kura na kutoa ubashiri kwamba matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao hayatatokana na kura za wananchi bali kwa hila za vyombo vya dola yakiwemo majeshi.


"Tunaamini kwamba mchakato wa kisiasa lazima uachwe bila kuingiliwa na majeshi kama hakuna sababu za msingi kufanya hivyo," alisema. Profesa Baregu alisema ijulikane kwamba tamko la JWTZ lilitolewa wakati kukiwa na mfululizo wa vitendo vya uvunjaji wa Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010, uliofanywa na mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.


Alisema Rais Kikwete amekuwa akitumia rasilimali za umma katika kampeni zake na katika matukio tofauti alizidisha muda wa kampeni unaotambulika kisheria.


Kwa mujibu wa Profesa Baregu, polisi na vyombo vingine vya usalama vina taarifa kwamba CCM imekuwa ikitoa mafunzo kwa kikundi cha Green Guards ambacho kinahusika kufanya vurugu kwenye mikutano ya kampeni ya Chadema.

Profesa Baregu alitaja baadhi ya maeneo yanayosadikiwa kuwa Green Guards wa CCM walifanya vurugu dhidi ya Chadema kuwa ni katika majimbo ya Busanda, Moshi Mjini na Ubungo. "Hakuna hatua zilizochukuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi licha ya malalamiko yetu kadhaa," alisema.


Pia Profesa Baregu alisema hivi karibuni gazeti la serikali la Daily News, lilitangaza matokeo ya mshindi wa urais kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.


Alisema kutokana na hali hiyo, Chadema imetuma waraka kwa jumuiya ya kimataifa ambapo nakala zake zimesambazwa kwa balozi za nje na mashirika ya wahisani, ili wataimbue hali hiyo. Profesa Baregu alisema Chadema inaamini kuwa Nec itatimiza wajibu wake kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu unafanyika kwa huru na haki na kwamba uamuzi wa wananchi unaheshimiwa.

Ijumaa iliyopita Shimbo akiwa amefuatana viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi aliwaambia waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi hilo kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejiandaa kukabiliana na vurugu wakati wa Uchaguzi Mkuu na kuvitaka vyama vya siasa na wagombea kuyakubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).


Katika tamko hilo lililoelezwa ni la pamoja kati ya JWTZ na Polisi, limezuia mjadala kwa kada tofauti nchini, huku watu wengi wakimkosoa kwa mitazamo tofauti.
 
HILI NI JAMBO JEMA SANA.
KIKWETE ANAYATUMIA MAJESHI YETU VIBAYA.
KWANINI ANATAKA KUIBUA KWA NGUVU NGUVU YA UMMA?
I HATE THIS CHAMA :couch2:
 
Wameyataka wenyeweeee, wameyataka wenyeweeee:music:

Haya sasa! Hongera sana Prof Baregu kwa kuchukua hatua
 
Demokrasia bado sana Tanzania, Yeyote anae opt matumizi ya mabavu Ana uwalakini!!!!!!!!!
 
Uchaguzi wa mwaka huu, ndio kipimo kama kweli kuna demokrasia hapa Tanzania. Wamefanya vizuri kuya-alert mapema hayo mashirika ya kimataifa na UN.
 
Hapa ndipo jenerali alipomwaga unga na siku zake ofisini zahesabika na ajiandae na utetezi wa Meremeta na zabuni ya matrekta ya "Kilimo kwanza"


"Pasipo kutoa uthibitisho, Luteni Jenerali Shimbo alieleza hisia kwamba vyombo vya usalama vimepokea taarifa za kiintelijensia zikionyesha kuwepo vyama vya siasa vinavyojiandaa kwa ajili ya vurugu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu nchini," alisema.
 
Hapa ndipo jenerali alipomwaga unga na siku zake ofisini zahesabika na ajiandae na utetezi wa Meremeta na zabuni ya matrekta ya "Kilimo kwanza"
"Pasipo kutoa uthibitisho, Luteni Jenerali Shimbo alieleza hisia kwamba vyombo vya usalama vimepokea taarifa za kiintelijensia zikionyesha kuwepo vyama vya siasa vinavyojiandaa kwa ajili ya vurugu zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu nchini," alisema.
 
vICHWA KAMA BAREGU NDO VINATAKIWA HAPA NCHINI, HONGERA SANA PROFF.
 
CCM ni chama cha ajabu sana. Kumbe ndo maana kilikataa kushiriki midahalo huku kikijitapa kwamba ushindi ni lazima! Maana ya ushindi ni lazima inaanza kuonekana sasa, yaani kutumia hata nguvu za majeshi, majini,wizi wa kura, ghiriba kwa wananchi wenye uelewa mdogo, ahadi za uwongo wa kitoto n.k. Ndo maana nchi yetu haiendelei. Tunapitwa hata na nchi za juzi tu kama Rwanda. Wanachi waamke na kukataa udhalimu wa CCM na masalia ya uongozi wake.
 
Nadhani ile post yangu waliisoma wakaielewa.
Nawapongeza kwa kuchukua hatua na ninaamini wanafanya hivyo kwa ajili ya WATANZANI wasiojua mlango wa kutokea na hatima yao kutokana na udhalimu na propaganda za KINAZI za CCM.

Hii ndiyo inayotakiwa. yaani mtu mbabe anapofanya mambo ya aibu dawa yake ni kumzomea tu mpaka aone aibu. Mwaka huu tunakula nao sahani tofauti.
 
Mwaka huu hawa wajinga wamepatikana, tunakaba mpaka penati safari hii, hakuna kuwapa pumzi, tunahitaji ushindi wa halali,siyo kubebwa na majeshi. JK anajitafutia aibu ya bure,angekubali kuacha mchakato wa uchaguzi ufuate mkondo wake tu hata ni kushindwa akubali matokeo kwani ni kitu cha kawaida tu, hivi ni nani kamwambia kuwa Tanzania ni kampuni yake yeye na familia yake?Kwanza mtu mwenyewe afya ndiyo inazidi kudorora kila siku, anataka kutupeleka wapi? Au kwa vile anajijua ni nusu mfu ndiyo maana anatafuata watu wa kumsindikiza.
 
Mwaka huu hawa wajinga wamepatikana, tunakaba mpaka penati safari hii, hakuna kuwapa pumzi, tunahitaji ushindi wa halali,siyo kubebwa na majeshi. JK anajitafutia aibu ya bure,angekubali kuacha mchakato wa uchaguzi ufuate mkondo wake tu hata ni kushindwa akubali matokeo kwani ni kitu cha kawaida tu, hivi ni nani kamwambia kuwa Tanzania ni kampuni yake yeye na familia yake?Kwanza mtu mwenyewe afya ndiyo inazidi kudorora kila siku, anataka kutupeleka wapi? Au kwa vile anajijua ni nusu mfu ndiyo maana anatafuata watu wa kumsindikiza.

Yaani mwaka huu CCM waandae mapipa ya maji kuwamwagia makamanda wao akina kinana, makamba, kikwete mpaka tumaini lao shehe yahaya. Maana kikwete atakapoanguka akitafutwa shehe yahaya nae wataambiwa ndio kwanza ana halimbaya zaidi alizirai tokea jana yake! Hapo kinana nae chini makamba akisikia nae chini........
 
Back
Top Bottom