Chadema yashinda nafasi ya mwenyekiti wa halmashauri wilaya ya Hai

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
CHADEMA imeshinda kiti cha Mwenyekiti wa Halmasahuri Wilaya ya Hai. Hatimaye CCM wamesalimu amri baada ya CHADEMA kukinyakua kiti hicho. Wilaya ya Hai ilikuwa ni mojawapo ya maeneo ambayo kulikuwa na mvutano mkubwa wa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na baada ya mshikemshike wa Arusha CCM wamesalimu amri kama ilivyokuwa Mwanza! Aluta Continua!!!
 
Ccm wanataka mpaka watuchinje ndipo watupatie haki yetu kwani nchi hii kwa sasa ccm na akina makamba na kikwete ndiyo wanaoshikiria haki za watz........mpo juu lakini mwisho wenu wa kuhadaa watz umeisha
 
No source no comments

Sasa Kurunzi unataka source iwe Mwema au Makamba!! Source ni mimi mwenyewe ebo!! Niko Hapa na Nashuhudia tukio!!

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti inarudiwa baada ya kura kufungana! Nitakurushia taarifa zaidi zoezi hilo likikamilika ndugu!
 
Mgawanyo wa idadi ya madiwani kwa vyama ukoje huko?
 
Idadi ya wajumbe ni 11 kwa 11.

Mwenyekiti amepata kura 12. Baada ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti kurudia wamefungana tena hivyo makubaliano yamefikiwa mgombea wa CCM nafasi ya Makamu mwenyekiti aanze kwa kipindi cha Mwaka Mmoja then baada ya hapo makamu mwenyekiti atatoka CDM kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa kama ilivyorekebishwa!!

Kwa hesabu za haraka utaona kwamba kuna diwani wa CCM ametupigia kura kumpata Mwenyekiti!! Subiri watakavyotafutana mchawi!! Si walitaka kura ya siri wakiamini watanunua madiwani wetu ili wawapigie, sasa imemeza kwao (sio hata imekula kwao).......
 
Thank you Msando..

Na vipi kuhusu hii kauli ya Tambwe Hizza, unasemaje mkuu?

.......Alisema anasikitishwa na CHADEMA kuhoji uhalali wa Mbunge wake wa viti maalumu, Bi. Mary Chatanda, kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati sheria ziko wazi kuhusu eneo gani mbunge wa viti maalumu atawakilisha.

"Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

"Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa, sasa wanachohoji ni nini kama si kupotosha tu wananchi kwa makusudi ili wajitafutie umaarufu bure," alisema Bw. Tambwe.

..........................
 
Big up CDM huyo mayor afanye kazi kiukweli kweli uchaguzi ujao tupite tena bila matatizo, tunapoweka misingi haitakiwi ije kuchukuliwa na ccm kamwe. Tujitofautishe nao kwa matendo na si maneno pekee, we need to talk the talk and walk the walk ktk maeneo yote tuliyochukua
 
Idadi ya wajumbe ni 11 kwa 11.

Mwenyekiti amepata kura 12. Baada ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti kurudia wamefungana tena hivyo makubaliano yamefikiwa mgombea wa CCM nafasi ya Makamu mwenyekiti aanze kwa kipindi cha Mwaka Mmoja then baada ya hapo makamu mwenyekiti atatoka CDM kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa kama ilivyorekebishwa!!

Kwa hesabu za haraka utaona kwamba kuna diwani wa CCM ametupigia kura kumpata Mwenyekiti!! Subiri watakavyotafutana mchawi!! Si walitaka kura ya siri wakiamini watanunua madiwani wetu ili wawapigie, sasa imemeza kwao (sio hata imekula kwao).......

Wewe Alberto? Unataka makamba afe siku si zake?
 
CHADEMA imeshinda kiti cha Mwenyekiti wa Halmasahuri Wilaya ya Hai. Hatimaye CCM wamesalimu amri baada ya CHADEMA kukinyakua kiti hicho. Wilaya ya Hai ilikuwa ni mojawapo ya maeneo ambayo kulikuwa na mvutano mkubwa wa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na baada ya mshikemshike wa Arusha CCM wamesalimu amri kama ilivyokuwa Mwanza! Aluta Continua!!!

Hongera sana, hiyo ndio demokrasia. Lakini sio kuingia mitaani bila idhini.
 
For sure damu ya kina Ismail (R.I.) haiwezi kwenda bure.

Hongera CDM wilaya ya Hai, fanyeni kazi na kuonyesha uongozi uliotukuka ili wana Hai waone tofauti yenu na waliokuwepo.
 
CDM mmepewa rungu chapeni kazi sasa ili uchaguzi ujao madiwani wote wawe ni wa chadema B>>>I>>>>G>>>U>>>P sana kwa cdm aluta continua!
 
Hongera cdm na nguvu ya umma kwa ushindi sasa tutumikie umma kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom