CHADEMA yasambaratisha CCM Kilombero

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni humo.

Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang’ula, Msolwa na Mkamba.

“Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama 214 kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14,” alisema Kisenime.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi.

“Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge,” alisema Katanduki.

Source:Mwananchi
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimepokea wanachama wapya 256 kutoka vyama vya CCM, Cuf, na TLP kutoka katika Kata nne za Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro. Hayo yalibainishwa na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Kilombero , Moses Kisenime katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.

Kisenime alisema wanachama hao walipokelewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Taifa (Bavicha), John Heche wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara jimboni humo.

Alisema Mwenyekiti huyo wa Bavicha taifa aliwapokea wanachama hao katika mikutano minne aliyofanya katika Kata ya Ifakara, Mang'ula, Msolwa na Mkamba.

"Kutokana na mikutano yetu tunayoifanya mkoani Morogoro tumeweza kupokea wanachama 214 kutoka CCM, Cuf 28 na TLP wanachama 14," alisema Kisenime.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake aliyekuwa balozi wa nyumba kumi katika Kata ya Mkamba, Mussa Katanduki alisema ameamua kuhama kutoka chama cha CCM kwa madai kuwa chama hicho kimekosa mueleko na maadili ya uongozi.

"Sijalazimishwa na mtu kuhamia Chadema lakini kutokana na mambo yalivyo ndani ya CCM kwa ihari yangu nimeamua kuungana na chama hiki ili kuweza kuendeleza mapambano ya kutetea haki za wanyonge," alisema Katanduki.

Source:Mwananchi

The most "unruly horse" is the public policy, you will never know where it will take you!!!! Hawa watu wa vijijini usiwaamini, kesho akija mwingine watageuka, bendera hufuata upepo! Naipenda CDM lakini they should not bank on these unprincipled people! Nawaheshimu sana ndugu zangu wa vijijini, lakini nachelea misimamo yao, Kweli wameingia CDM kwa dhamira ya kuona superiority ya CDM policies over the other parties au ni bendera..........
 
Kahabari kenyewe kadogo lakini mnakakuuuza....wanachama 256??????????? duh!
 
Kahabari kenyewe kadogo lakini mnakakuuuza....wanachama 256??????????? duh!

Karibu Sana naona siku hizi unachungulia kwa mbali au wamekutoa kwenye payral nini?:wacko: Udogo unaousema ni upi wale 60 mliwapata kigoma na hao 265 ni ipi ndogo?
Mytake: Kama heche anaweza kurejesha wanachama 256 wakati Delegation ya Nape,Mwigulu na mawaziri wapatao 6 wamerudisha wanachama 60 ni Picha gani unapata hapo?
 
Kahabari kenyewe kadogo lakini mnakakuuuza....wanachama 256??????????? duh!
Kaka chama ni watu,chama bila watu ni sawa debe tupu! usiwe kama
Muhammad Saeed al-Sahhaf aliyekuwa waziri wa habari wa serikali ya Sadam Hussein,siku zote alitoa taarifa za kutia moyo kwa wairaki ilihali alijua fika hali si shwari hata kidogo.
 
Kahabari kenyewe kadogo lakini mnakakuuuza....wanachama 256??????????? duh!

Lazima kakuzwe maana tangia ccm wakose mwelekeo sijawahi sikia wamepokea wanachama toka upinzani zaidi ya kuwapoteza na bado wanazidi kuwapoteza
 
Acha urongo kilombero haipo kaskazini na kamwe hatakuwa kaskazini mbaka mwisho wa dunia!

umekurupuka kumjibu, tulia tafakari ndipo umjibu mtu,.. maana yake ilikuwa kina rejao wanadaigi cdm ni cha kaskazini sasa ilikuwa tu ni kama swali kwa rejao je moro pia ni kaskazini hivi ndivyo nilivyoelewa mimi......kutoka kwa molemo...tafadhali molemo njoo unisahihishe
 
huo ndio mwanzo wa harakati za ukombozi tanzania ,chama tawala kinameguka na wafuas wake kujiunga na CHADEMA,peopless
 
La muhimu hapa sasa ni kutoa elimu ya uraia kwa mantiki kuwa hawa wanachama wajue umuhimu wa kupiga kura. Kuwa na mwanachama asiyepiga kura haina maana.
Nawajua vizuri sana vijana wa Kilombero ni washabiki wazuri sana.
 
Back
Top Bottom