CHADEMA yasafisha tuhuma za Nape kupitia Channel ten - Kisha wamburuta Kwa Msajili

Chadema ‘wamburuta’ Nnauye kwa msajili Send to a friend
Wednesday, 15 August 2012 21:04

Boniface Meena
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimemshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ili aweze kujieleza kuhusu madai kuwa Chadema imekuwa ikitumia harambee zao kuhalalisha mabilioni ya fedha wanazopewa na wafadhili nje ya nchi.

Pia, chama hicho kimesema kuwa kimepeleka nakala kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, kutaka jeshi lake lishughulikie shutuma hizo na pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi katika vyama.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu, alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu madai yaliyotolewa na Nnauye, dhidi ya chama chake.Komu alisema chama chake, hakijawahi kufadhiliwa na wahisani kutoka nje na kwamba mapato yake yanatokana na ruzuku ya Sh235 milioni inayotolewa na Serikali kila mwezi.

“Tumekuwa tukipata fedha kutokana na michango ya wanachama wetu ya kila mwaka,”alisema Komu.
Hata hivyo, Nnauye kwa upande wake alisema chombo chochote kitakachohitaji ushirikiano wake kuhusu suala la Chadema atakuwa tayari kufanya hivyo.

Alisema kama Chadema wataendelea kumung’unya maneno, ataanika hadharani kinachofanywa waziwazi na chama hicho.

“Chadema wakiendelea kuumauma maneno kuhusu mikataba yao nitawaanika wazi wazi,”alisema Nnauye.
Kaimu Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Piensia Etanga, alisema hajapata taarifa kutoka Chadema kwa kuwa yupo safarini.“Sijapata barua hiyo na niko nje ya ofisi, tupo Mtwara hivyo hatuwezi kujua kama imepelekwa ofisini au la,”alisema Etanga.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema hakuna nakala yoyote kutoka Chadema iliyoelekezwa katika jeshi hilo, ikizungumzia kuhusu suala hilo.“Hakuna barua yoyote iliyoelekezwa kwetu kuhusu suala hilo,”alisema Senso.

Hivi karibuni Nnauye alisema CCM imeshangazwa kuona Chadema kikiwahadaa Watanzania kufanya harambee ili kuhalalisha fedha kutoka kwa wafadhili.

“Chama Cha Mapinduzi kimeshangazwa na kusikitishwa sana na usanii huu mkubwa unaofanywa na Chadema kwa kuwahadaa Watanzania kwa usanii wa kufanya harambee, ili kuhalalisha uwepo wa mabilioni waliyopewa na wafadhili wao wa nje ya nchi.”

Aliongeza: “Mfano mzuri wa usanii huu ni kwenye Hoteli ya Serena ambako ilifanyika harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni.”

NB:
Nape amepewa nafasi ya kusema ukweli na kuthibitisha kauli zake. Ikizingatiwa serikali yao ndio yenye dola tunategemea usalama wao wa Taifa, polisi, msajili, CAG, Bolozi zote za nchi ambazo anadai zinatoa fedha zitamsaidia kutoa ushahidi wake kuthibitisha kwamba CDM wanatumia wananchi ili kuingiza fedha kutoka nje kwenye mfumo.

Akishindwa au msajili akishindwa kuanisha hizo fedha na CAG pamoja BOT ambo wote wanatakiwa kudhibiti fedha chafu tutashindwa kumwelewa Nape. Haya sasa kapata sehemu ya kupeleka ushahidi.
 
6.JPG

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye

Wednesday, 15 August 2012 21:04

Boniface Meena
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimemshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ili aweze kujieleza kuhusu madai kuwa Chadema imekuwa ikitumia harambee zao kuhalalisha mabilioni ya fedha wanazopewa na wafadhili nje ya nchi.

Pia, chama hicho kimesema kuwa kimepeleka nakala kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, kutaka jeshi lake lishughulikie shutuma hizo na pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi katika vyama.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu, alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu madai yaliyotolewa na Nnauye, dhidi ya chama chake.Komu alisema chama chake, hakijawahi kufadhiliwa na wahisani kutoka nje na kwamba mapato yake yanatokana na ruzuku ya Sh235 milioni inayotolewa na Serikali kila mwezi.

“Tumekuwa tukipata fedha kutokana na michango ya wanachama wetu ya kila mwaka,”alisema Komu.
Hata hivyo, Nnauye kwa upande wake alisema chombo chochote kitakachohitaji ushirikiano wake kuhusu suala la Chadema atakuwa tayari kufanya hivyo.

Alisema kama Chadema wataendelea kumung’unya maneno, ataanika hadharani kinachofanywa waziwazi na chama hicho.

“Chadema wakiendelea kuumauma maneno kuhusu mikataba yao nitawaanika wazi wazi,”alisema Nnauye.
Kaimu Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Piensia Etanga, alisema hajapata taarifa kutoka Chadema kwa kuwa yupo safarini.“Sijapata barua hiyo na niko nje ya ofisi, tupo Mtwara hivyo hatuwezi kujua kama imepelekwa ofisini au la,”alisema Etanga.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema hakuna nakala yoyote kutoka Chadema iliyoelekezwa katika jeshi hilo, ikizungumzia kuhusu suala hilo.“Hakuna barua yoyote iliyoelekezwa kwetu kuhusu suala hilo,”alisema Senso.

Hivi karibuni Nnauye alisema CCM imeshangazwa kuona Chadema kikiwahadaa Watanzania kufanya harambee ili kuhalalisha fedha kutoka kwa wafadhili.

“Chama Cha Mapinduzi kimeshangazwa na kusikitishwa sana na usanii huu mkubwa unaofanywa na Chadema kwa kuwahadaa Watanzania kwa usanii wa kufanya harambee, ili kuhalalisha uwepo wa mabilioni waliyopewa na wafadhili wao wa nje ya nchi.”

Aliongeza: “Mfano mzuri wa usanii huu ni kwenye Hoteli ya Serena ambako ilifanyika harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni.”

Ina maana Chadema hawana kazi ya kufanya mpaka washindane na huyu mwehu?
Kama Bosi wake Mukama kichwa chake ni kama panzi mnategemea Nape apate wapi akili? Au mmeshasahau kwamba Mukama ndiye alisema Chadema imeingiza Magaidi kutoka Afghanstan kule Igunga?

The snake is dead himself so why u should use stick? CCM tayari ni chama cha upinzani Chadema sasa ni lazima ijifunze uvumilivu maana mnaweza mkaja kutufunga wengi mkiapishwa rasmi.
 
hii inaonyesha kuwa CCM inawaeleza watanzania kuwa wameshindwa kuliongoza taifa na sasa wananchi wafanye kazi yao hata kabla ya 2015 ikibidi, maana kama chama kitaweza kuingiza pesa bila wao kujua maana yake wote ni dhaifu wala si mkuu wa kaya pekee. wamechoka.
 
Msajili wa vyama vya Siasa!!! Si ndiye yule jamaa anayeitwa John Tendwa???

John Tendwa si ndiye aliyemushauri Godbless Lema asiende Arumeru Mashariki kupiga kampeini vingenevyo wazee wa kishiiri wangemua? Am I missing something?

Kama ndiye nothing good will come from Msajili wa vyama vya siasa.
 
Huyu kijana bado mchanga sana kisiasa, mwacheni awamalize. CCM wamempa viatu vikubwa sana, atatembeaje?
 
Nape kachokoza bila kujua athari zitakazo jitokeza kwa chama chake itakapo bidi Msajili na CAG watakapolazimika kuikagua CCM
 
Back
Top Bottom