CHADEMA yasafisha tuhuma za Nape kupitia Channel ten - Kisha wamburuta Kwa Msajili

Mdutch

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
214
77
Mkurugenzi wa fedha na utawala wa CHADEMA Anthony Komu yuko Channel Ten akimchanachana NAPE juu ya tuhuma zake juu ya CHADEMA kupokea fedha kutoka nje na kwamba inafanya usanii katika harambee zake.

Komu anasema ni kweli CHADEMA inashirikiana na KAS shirikia la kijerumani kama wao CCM wanavyoshirikiana na FES shirika la kijerumani.

Komu anasema CCM wanapokea fedha kutoka NDI kama wao CHADEMA kupitia TCD lakini mpaka leo hii CCM hawajawahi kutoa mrejesho wa fedha hizo kama wao CHADEMA wanavyofanya.

Komu ameweka wazi kuwa CHADEMA inapokea ruzuku ya shilingi milioni 230 kwa mwezi. Ameweka wazi pia mapato ya harambee zote za Arusha, Dar es salaam na michango ya Jangwani.
Nape kakurupuka kapiga simu anaambiwa ataje majina ya hao wanaotoa fedha chafu CHADEMA akabwabwaja maneno kama kawaida kwa kushindwa kuwataja.

Mwandishi kamwambia ataje kiasi cha fedha kilichoingia CHADEMA kutoka nje akabwabwaja tena maneno kwa kushindwa kukitaja kiasi chochote.

NAPE kaulizwa aseme vyanzo vya fedha vya CCM kabwabwaja maneno kwa kushindwa kuvisema vyanzo hivyo. Kashindwa kuwataja hata washirika wao wa CHINA na aliposhindiliwa kuwa na ushirikianao na FES ndio akakubali kishingo upande.
KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa.

Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali
Wachangiaji wamemjia juu bwana mdogo NAPE kwa kumtaka kama moto wa CHADEMA umekuwa mkali kiasi hicho basi na wao wajaribu kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kama wanauwezo huo ili wakijenge chama chao kinachokufa.

Kijembe kimerushwa kwa NAPE kutoka kwa mchangiaji kuwa ni kwanini CCM waliopokea fedha chafu za EPA, KAGODA na Deep Green mpaka leo wameshindwa kuwachukulia hatua. Fedha hizi zilitumika kuiingiza CCM madarakani mwaka 2005 na 2010.

Komu kaja juu tena kwa kusema kuwa CCM wana vyanzo vingine vya mapato kwa mfano umiliki wa majengo na viwanja vya michezo ambavyo wamevipora kwa kuwa vilijengwa na umma enzi za chama kimoja lakini mpaka leo hiii hawawezi kuweka wazi mapato yao ukiacha yale ya ruzuku.
Eti NAPE amedai kuwa hajaona maswali ya wachangiaji kwa kuwa ameshatoka nyumbani kwenda ofisini.

NAPE anarudi tena hewani na kudai kuwa CHADEMA ni dhaifu na haina social base kwa hiyo haihofii CHADEMA. Anajitetea kuwa yeye ni mkweli na ndio maana yuko tayari kukisema hata chama chake.

Analalamika kuwa wanaosema anaiua CCM wanamuonea kwa kuwa anjaitahidi kukijenga chama chake. Anaambiwa ataje majina ya watu wanaotoa fedha chafu anacheka cheka anapata kigugumizi.

Anasema kuwa kama CHADEMA wasipochukua hatua za kuweka wazi vyanzo vya fedha zao watachukua hatua anaulizwa ni hatua gani watachukua anashindwa kusema.

Kauli yake hii ya kuonyesha kuihofia CHADEMA hii hapa kwamba yeye NAPE anafanya hivi kuikosoa CHADEMA kwa kuwa ni chama kinachotaka kuiongoza nchi na CHADEMA wajisafishe ili nchi yetu isije ikatawaliwa na watu dhaifu.
"CCM ni kama panya. Mtu ukiwa haupo nyumbani panya huingia mpaka sebukeni. Ila mwenye nyumba anapokuja mapnya hukimbia sebuleni na kuingia uvunguni na maeneo mengine ya nyumba. CHADEMA ndio mwenye nyumba na yuko nyumbani kwa hiyo mapanya yamekimbia sebuleniu kuelekea uvunguni.

Kwamba sebule ni majimbi yote ya mjini kama mwanza, Arusha, Mbeya , Ubungo, Kawe, Moshi Iringa na sasa inaingia mpaka uvunguni yaani majimbo ya vijijini kumsakanya panya. Operesheni sangara inayoendelea Morogoro na mikoa ya Iringa, Dodoma, na Manyanya kukijenga chama ni sawa na kumtimua panya uvunguni."

Kauli ya kumalizia ya Anthony Komu.

Kwa maelezo na maendeleo zaidi ya Sakata,

Chadema ‘wamburuta' Nnauye kwa msajili
Send to a friend
Wednesday, 15 August 2012 21:04

Boniface Meena
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimemshtaki Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, ili aweze kujieleza kuhusu madai kuwa Chadema imekuwa ikitumia harambee zao kuhalalisha mabilioni ya fedha wanazopewa na wafadhili nje ya nchi.

Pia, chama hicho kimesema kuwa kimepeleka nakala kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, kutaka jeshi lake lishughulikie shutuma hizo na pia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi katika vyama.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu, alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu madai yaliyotolewa na Nnauye, dhidi ya chama chake.Komu alisema chama chake, hakijawahi kufadhiliwa na wahisani kutoka nje na kwamba mapato yake yanatokana na ruzuku ya Sh235 milioni inayotolewa na Serikali kila mwezi.

"Tumekuwa tukipata fedha kutokana na michango ya wanachama wetu ya kila mwaka,"alisema Komu.
Hata hivyo, Nnauye kwa upande wake alisema chombo chochote kitakachohitaji ushirikiano wake kuhusu suala la Chadema atakuwa tayari kufanya hivyo.

Alisema kama Chadema wataendelea kumung'unya maneno, ataanika hadharani kinachofanywa waziwazi na chama hicho.

"Chadema wakiendelea kuumauma maneno kuhusu mikataba yao nitawaanika wazi wazi,"alisema Nnauye.
Kaimu Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Piensia Etanga, alisema hajapata taarifa kutoka Chadema kwa kuwa yupo safarini."Sijapata barua hiyo na niko nje ya ofisi, tupo Mtwara hivyo hatuwezi kujua kama imepelekwa ofisini au la,"alisema Etanga.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alisema hakuna nakala yoyote kutoka Chadema iliyoelekezwa katika jeshi hilo, ikizungumzia kuhusu suala hilo."Hakuna barua yoyote iliyoelekezwa kwetu kuhusu suala hilo,"alisema Senso.

Hivi karibuni Nnauye alisema CCM imeshangazwa kuona Chadema kikiwahadaa Watanzania kufanya harambee ili kuhalalisha fedha kutoka kwa wafadhili.

"Chama Cha Mapinduzi kimeshangazwa na kusikitishwa sana na usanii huu mkubwa unaofanywa na Chadema kwa kuwahadaa Watanzania kwa usanii wa kufanya harambee, ili kuhalalisha uwepo wa mabilioni waliyopewa na wafadhili wao wa nje ya nchi."

Aliongeza: "Mfano mzuri wa usanii huu ni kwenye Hoteli ya Serena ambako ilifanyika harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni."

NB:
Nape amepewa nafasi ya kusema ukweli na kuthibitisha kauli zake. Ikizingatiwa serikali yao ndio yenye dola tunategemea usalama wao wa Taifa, polisi, msajili, CAG, Bolozi zote za nchi ambazo anadai zinatoa fedha zitamsaidia kutoa ushahidi wake kuthibitisha kwamba CDM wanatumia wananchi ili kuingiza fedha kutoka nje kwenye mfumo.

Akishindwa au msajili akishindwa kuanisha hizo fedha na CAG pamoja BOT ambo wote wanatakiwa kudhibiti fedha chafu tutashindwa kumwelewa Nape. Haya sasa kapata sehemu ya kupeleka ushahidi.
 
Nape kakurupuka kapiga simu anaambiwa ataje majina ya hao wanaotoa fedha chafu CHADEMA akabwabwaja maneno kama kawaida kwa kushindwa kuwataja.

Mwandishi kamwambia ataje kiasi cha fedha kilichoingia CHADEMA kutoka nje akabwabwaja tena maneno kwa kushindwa kukitaja kiasi chochote.

NAPE kaulizwa aseme vyanzo vya fedha vya CCM kabwabwaja maneno kwa kushindwa kuvisema vyanzo hivyo. Kashindwa kuwataja hata washirika wao wa CHINA na aliposhindiliwa kuwa na ushirikianao na FES ndio akakubali kishingo upande.
 
Asubuh hii kwenye chanel ten, Nape amehojiwa akitakiwa kuthibitisha madai yake juu ya chadema kuchangiwa fedha namataifa ya nje. Katika maeleo yake amegoma kutaja watu wanaoichangia Chadema na kiasi cha pesa. Ila amesema kuwa alikuwa anawatahadharisha kuwa hela hela hio sio nzuri kwa maendeleo ya nchi. Amesisitiza kuwa hawezi taja hadharani sasa.

Pia ametakiwa Kusema wao wamechukua hatua gani maana ishu ya fedha hafu ni kosa kisheria, akasema alikuwa anaitahadharisha tu chadema. Swali ni kuwa, kwanini Nape anataka kucheza na akili zetu wananchi Maana hawezi kutoa madai makubwa namna hiyo hadharani tena kwenye press conference halafu aseme alikuwa anawatahadharisha tuu chadema?
 
KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa.

Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali
 
Ukiwa 'smart' uko smart tuu...mjinga hata aje vipi hakusumbui. Kwa sababu mpaka sasa wote Chadema wanaomjibu Nape (CCM) wanaonekana smart, na yeye (Nape) mjinga....and too bad, that is the fact!

Mbona wamekuwa wengi sana wanaomjibu NAPE mmoja wanahofu ya nini?
 
KOMU kamlima kishoka NAPE kamwambia kama yeye anadhani CHADEMA inapokea fedha chafu kutoka nje basi ni uzembe wa serikali yao dhaifu inayounda serikali yenye mamlaka na BOT inayosimamia benki zote za Tanzania ambamo CHADEMA ina akaunti zake kwa kuitaka itoe hizo taarifa. Pia Komu kasema TRA ni chombo cha serikali chenye mamlaka ya kufuatilia vyanzo vya mapato vya CHADEMA na kuvikagua. Kama CCM wanaona kweli kuna fedha chafu zinaingizwa CHADEMA basi Tanzania haina serikali
Hayo aliyosema KOMU ni kauli ya CDM au ya kwakwe? wasije wakaanza kutoana manundu tena. Tusubiri tuone.
 
Mbona wamekuwa wengi sana wanaomjibu NAPE mmoja wanahofu ya nini?

Nape (mmoja, unless uniambie alitumwa na CCM kama taasisi) ameshutumu Chadema...taasisi, inayoundwa na watu wengi tu! Na kila mmoja kwenye taasisi (Chadema) kwa wadhifa wake, ana jukumu la kumjibu Nape! Na majibu anayapata kweli...
 
Nape aje sasa, au awaite waandishi wa habari leo jioni'

Mbona unakuwa na haraka Mkuu? NAPE kiboko yao CDM si unaona wanavyotapa tapa , mpaka sasa waliozungumzia kauli ya NAPE wamefikia 3 na wote wanarudia jambo hilo hilo kwa nini? NAPE anasubiri wamalize wote kubwabwaja.
 
Nape (mmoja, unless uniambie alitumwa na CCM kama taasisi) ameshutumu Chadema...taasisi, inayoundwa na watu wengi tu! Na kila mmoja kwenye taasisi (Chadema) kwa wadhifa wake, ana jukumu la kumjibu Nape! Na majibu anayapata kweli...

Haya sasa, nawe unajitokeza ni nani tena ndani ya CDM unayejua nyadhifa za kila mmoja ndani ya CDM?
 
Wachangiaji wamemjia juu bwana mdogo NAPE kwa kumtaka kama moto wa CHADEMA umekuwa mkali kiasi hicho basi na wao wajaribu kuchangisha fedha kutoka kwa wananchi kama wanauwezo huo ili wakijenge chama chao kinachokufa.

Kijembe kimerushwa kwa NAPE kutoka kwa mchangiaji kuwa ni kwanini CCM waliopokea fedha chafu za EPA, KAGODA na Deep Green mpaka leo wameshindwa kuwachukulia hatua. Fedha hizi zilitumika kuiingiza CCM madarakani mwaka 2005 na 2010.

Komu kaja juu tena kwa kusema kuwa CCM wana vyanzo vingine vya mapato kwa mfano umiliki wa majengo na viwanja vya michezo ambavyo wamevipora kwa kuwa vilijengwa na umma enzi za chama kimoja lakini mpaka leo hiii hawawezi kuweka wazi mapato yao ukiacha yale ya ruzuku.
 
Nape ni kawaida yake refer magamba chenge, el, rostam alivyokuwa anajiapiza lazma waondoke mara baadae mwenyewe tena akakanusha so kukurupuka ni kawaida yake
 
Eti NAPE amedai kuwa hajaona maswali ya wachangiaji kwa kuwa ameshatoka nyumbani kwenda ofisini.

NAPE anarudi tena hewani na kudai kuwa CHADEMA ni dhaifu na haina social base kwa hiyo haihofii CHADEMA. Anajitetea kuwa yeye ni mkweli na ndio maana yuko tayari kukisema hata chama chake.

Analalamika kuwa wanaosema anaiua CCM wanamuonea kwa kuwa anjaitahidi kukijenga chama chake. Anaambiwa ataje majina ya watu wanaotoa fedha chafu anacheka cheka anapata kigugumizi.

Anasema kuwa kama CHADEMA wasipochukua hatua za kuweka wazi vyanzo vya fedha zao watachukua hatua anaulizwa ni hatua gani watachukua anashindwa kusema.

Kauli yake hii ya kuonyesha kuihofia CHADEMA hii hapa kwamba yeye NAPE anafanya hivi kuikosoa CHADEMA kwa kuwa ni chama kinachotaka kuiongoza nchi na CHADEMA wajisafishe ili nchi yetu isije ikatawaliwa na watu dhaifu.
 
Leo asubuhi nape, katibu mwenezi taifa wa chama cha mapinduzi, Simu nyingi zilizopigwa na kumuona Nape kama mpayukaji tu. Swali aliloulizwa anarukaruka tu.

Pia ameogopa kuwataja watu ambao wanaichangia CCM kwa fedha chafu ambapo mwanzo amesema yupotayari kuwataja watu hao alipokua akizungumza kwa simu leo asubuhi chanel ten.

Swali:

Je, Nape ni mpayukaji ambaye hayajui maneno anayoyazungumza?

Je, Nape anawaogopa mafisadi ndani ya chama chake?
 
Hayo aliyosema KOMU ni kauli ya CDM au ya kwakwe? wasije wakaanza kutoana manundu tena. Tusubiri tuone.
Komu ni Mkurugrnzi wa Fedha na Utawala wa CHADEMA . Kwa hiyo kauli yake juu ya hili ni kauli ya CHADEMA
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom