CHADEMA yapinga tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Chadema mbona amueleweki huyo Tundu Lissu anasema Tanzania hakuna majaji, sasa hiyo tume ya nini, halafu mbona Chadema hawapingi sensa.

Tundu Lissu wa Chadema amesema baadhi ya majaji na amewataja kwa majina.
Sasa huyo wewe unayemrefer bila shaka ni Tundu Lisu wa magamba ambaye hajui chochote kuhusu sheria za nchi yetu, labda anajua sheria za ccm.
 
Jibu swali, kwa hiyo kauli ya mwanachama/kiongozi wa cdm ndio kauli ya chama? Rejea kauli za Nassary

We UAMSHO huku Tanganyika unatafuta nini? haya mambo ya bara hayakuhusu na huyaelewi.
Tundun Lissu ni mkurugenzi wa Sheria na Katiba, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 
Mh.Lisu yuko sahihi kabisa, wizara ya mambo ya ndani ni watuhumiwa pia katika mauaji ya mwandishi Daud Mwangosi. Waziri Nchimbi anaendeleza itikadi zile zile za ulevi wa madaraka. HATA TUME INGEUNDWA NA RAIS MNGESEMA SERIKALI NDIYO WATUHUMIWA HAWAWEZI KUUNDA KAMATI YA UCHUNGUZI. NAONA CHADEMA MNGEUNDA TUME YENU MCHUNGUZE MNASHINDWA NINI?
[/QUOTE]
 
Chadema anzisheni uchunguzi wenu halafu toaeni majibu.

Unadhani Chadema ni mbumbumbu wa sheria na katiba kama mlivyo ninyi magamba? Chezea Tundu Lissu weye? anawakimbiza mchakamchaka magamba bila kupenda kila kukicha.
 
Sishangaii kwa analolisema Mh Lissu kwani hii serikali yetu inayojiita sikivu na makini wanapenda sana kukurupuka katika mambo ambayo yanavuma na wananchi yanawakera......
 
mawaziri wa jeikei kama kawaida yao kukurupuka au si ndo alitumwa inawezekana
 
Hamjielewi sasa ikiwa wengi wao hao majaji ni voda fasta; kinachotafutwa ni ukweli je iwapo majibu ya tume yatofautiana na hisia zenu mtakubaliana nayo wakati tayari Lissu kauli zake za awali zinamsuta mwenyewe? Kwa nini Chadema msijiundie tume yenu mtayo iamini si mnao wanasheria wengi tu ila tu hiyo tume yenu ianze na uchunguzi na kauli ya Dr. Slaa LIWALO NA LIWE

Chama
Gongo la mboto DSM safarini Brussels
chama siku hizi umekuwa low minded sana, hadi umebaki kutukana tukana tu kila post unayoweka hapa JF.

Hao majaji wa vodafasta wasiojua hata kuandika hukumu ndio tusiotaka kuwasikia wakitumika kuunda kamati ya uchunguzi. Na kwa bahati nzuri Tundu Lissu alishawataja kwa majina, na huyu Ihema ndiye alishindwa kuandika hukumu kwa zaidi ya miaka minne lakini jaji mwenzake alipopewa kesi hiyo ilimchukua wiki mbili kuandika hukumu. Mtu kama huyo ukimkabidhi tume ya uchunguzi una uhakika wa kupata ripoti ya uongo asilimia 100 from day one.

Sasa katika wale majaji wenye kuheshimika na ambao wanafahamika kwa utendaji kazi wao, na ambao ni weledi wa shughuli za kisheria na wamethibitika kutokuwa na matatizo ya kuandika hukumu zao ndio wapewe kazi hiyo ili wafanye kazi nzuri na ukweli wa mambo ubainike.

Kwa mujibu wa sheria Chadema hawawezi kuunda tume hiyo ya uchunguzi, na kwakuwa Chadema si mbumbumbu wa sheria kama mlivyo huko magambani ndio maana unaona unavyokurupuka na kumbwelambwela. Alichofanya Tundu Lissu ni kuwakumbusha jeshi la mauaji na waziri wa mauaji kwamba tume iliyoundwa ni batili kwa kujibu wa sheria.
 
Boomerang has re bounced. Ni kama wae waliosema kifua mbele kuwa nchi iko tayari kupigana na malawi wakati wakijua anayetakiwa kutoa kauli hiyo ni amiri jeshi mkuu. They are supposed to be punished for insubordination.
 
samahani labda nitakuwa sijuhi. hivi kisheria waziri mwenye dhamna ya wizara, mipaka yake ya kuunda tume ndani ya wizara yake inaishia wapi, sitaki kuingilia sana kuhusu Tindu lissu ila nataka nijuwe kila tume lazima iundwe na rais au kwa tukio lolote la mauaji kwa sababu linausisha uhai wabinadamu ni Rais pekee mwenye mamlaka ya kuunda tume?
 
inawezekana mzee kaomba msaada je? kwamba awe anapunguziwa kazi zingine! zaidi waziri labda ka-overlook, hakufikiri habari ya mipaka ya kazi yake. kama mmesema ni vyeo vya kupeana, ni saa ngapi mtu atakuwa makini kujua mipaka na sheria zaidi ya kupigania ukada!
 
Miaka fulani nikiwa katika Sekondari nilisoma kitabu kimoja cha Riwaya kiitwacho KULI kilichoandikwa na Adam Shafi. Muhusika mkuu katika Kitabu hicho anaitwa Rashidi. Alipambana sana na udhalimu wa wakoloni akiwa anafanya kazi bandarini, kwani Ujira- yaani mshahara ulikuwa mdogo. Alifkisha taarifa za mapinduzi ya kimaslahi kwa kutumia karatasi zilizotumika kufungia maandazi. Akihamasisha ukombozi wa mweusi katika ulimwengu wa ajira na unyonyaji. Leo sisi tunawasiliana kwa mitandao. Na tunaona kwa picha video na picha mnato za mtandao.

Wakoloni waliondoka. Na sasa kuna wakoloni wenzetu yaani mafisadi, wanatunyonya mpaka damu, wanawaua waandishi wanaotupasha habari ili waendelee kujinufaisha. Hivi viapo vya polisi ni kuua watu wanaotetea haki zao? Hivi Polisi wanaochukua bunduki na kuua ni waumini wa dini gani? Au wao ni wachina hawana dini? Mbona wenzetu wanatunyanyasa kuliko hata mkoloni?

Nini maana ya Uhuru? Yawezekana mie sijui neno kujitawala. Sisi tunakuwa wajinga kuliko aina nyingine za wanyama. Wanyama wa aina moja huwa hawauani hata wakigombana. sisi tukifanya mkutano unaishia kuua mwenzako. Nani mwenye akili kati yetu na wanyama wa aina nyingine. Wanyama wengine wakipigana bado wanapeana nafasi ya kuendelea kuishi? Sisi inakuwaje?

Polisi na viapo vyenu, hebu fikiri juu ya maamuzi mnayoyafanya. Sadam Hussein hakuwahi kufikiri kwamba siku moja angelijificha chini ya ardhi kama panya buku kwa sababu ya udhalimu wa matendo yake. Aliwaua wakurdi na roho zao zikamfuata. Hitler alipotea katika uso wa dunia hata mwili wake haukuonekana. Tumeyaona ya Misri na Libya. Tusidhani kwamba kule watu walipenda kupigana kuondoa uongozi madarakani. Watu walichoka. Amini nawaambia watanzania watakapochoka polisi na mkaendelea kutumia bomu, mjue kuwa mnaandaliwa mazingira ya kutulizwa kinyama.

Nchi hii ni ya wote, tumezaliwa tumeikuta na wote tutaiacha. kuiacha ni kwa zamu, iweje wewe bora kuliko wengine. sipati picha.

"Haya yote yana Mwisho"
 
Kumbe "Bwanyenye" alikuwa anatwanga maji kwenye kinu pamoja na mbwembwe zote ni mbumbumbu wa Sheria! Duh, hawa ndio mawaziri wetu. Hawajui hata wajibu na mipaka yao wanaingilia mpaka kazi za dhaifu! Kweli kule juu kuna guo guo!


Hivi huyu jamaa Emmanuel Mchimvi ana shahada ya Udaktari gani vile??

Niliwahi kusikia ndiyo kwanza alikuwa anasoma aidha Mzumbe au OUT ili kupata hiyo PhD yake na bado hajamaliza lakini tayari anajiita Daktari wa nini sijui!. Hii inadhihirisha ukihiyo alionao huyu jamaa Mchimvi. Hii mijitu ambayo imelelewa kwenye mikono ya jumuia za chama Twawala hakuna lolote. Hii yote ni inatokana kubebwabebwa tu tokea enzi za UVCCM, jitu halina sifa za uongozi linapachikwa tu sehemu ili kupata ulaji!! Jamaa kaongea kwa mbwembwe na majigambo mengi kuonyesha tu kuwa kichwani hamna kitu!

Nilimsikia jamaa akibwabwaja ati, oh,mimi nikijiuzulu hamtapata Waziri wa Mambo ya Ndani mzuri kama mimi!
Nonsense!
 
Waziri kivuli wa sheria na katiba wa chama pendwa CHADEMA mh.TUNDU LISU amesema tume iliyoundwa na mh. EMANUEL NCHIMBI ni batili kutokana na katiba ya jamhur ya muungano wa Tanzania kwan mwenye uwezo huo n Mh. Rais na ndie anayetoa hadidu za rejea za tume husika pia mh waziri mhusika hvyo hapasw kuunda tume ya uchunguz kwn wizara yake ni watuhumiwa pia

CDM, chama changu nakipigia saluti kuwa na viongozi wenye muono na ambao vichwa vyao wanavitumia vizur na sio kufuga nywele kama werema. ina maana mchimbi hana mwanasheria wa wizara?
 
Kukurupuka kwa Nchimbi ni wasifu wake. Na hata hivyo unaweza kugundua kuwa kuwa wasifu huo pia uko kwa viongozi wengine ambao wanajiona Mungu mtu. Mfana yule anayetishia kufuta chama cha siasa; kisa eti ana mamlaka kisheria. Kwa ufupi huu ni baadhi ya wasifu wa viongozi wa serikali ya CCM inayoongozwa na JK

1. Kujipendekeza kwa Kiongozi aliye juu yako yaani Rais
2. Kukurupuka katika kufanya maamuzi bila kufuata taratibu za Utawala Bora
3. Kudanganya katika gharama za bei halisi kwa kuongeza bei za vitu katika Budget
4. Kupenda kupata utajiri wa harakaharaka
5. Kujilimbikizia mali
6. Kuwaona wananchi wengine kama takataka
7. Kulaumu vyama vingine kwamba vinachochea uvunjifu wa amani.
8. Kupata misamaha ya Rais hata kama makosa wanayofanya ni jinai.
9. Kufikiri kwamba wao wapo juu ya Sheria
10.Kuendelea kuanika udhaifu wa rais kwa kumpatia taarifa za uongo zisizo chambuliwa vyema
11. Kutoa ahadi nyingi hewa kwa wananchi wake. nk ongeza zingine
12.
13.
14.
 
mawaziri wa jeikei kama kawaida yao kukurupuka au si ndo alitumwa inawezekana
Nadhani issue ya Dr. Mwakyembe pale bandarini kuunda tume utekelezaji hautakuwepo lakini kizuri katika ile process ni kuwa aliwazuia waliosimamishwa wasije hata bandarini kwa maana wanaweza kuharibu ushahidi au ku-influence tume ya uchunguzi, unajua hawa watu wa pesa we!
Lakini hili la tume ya Iringa linachekesha kwa maana ushahidi hauitaji maelezo hata kwa mtoto wa darasa la pili. Hapo hapo unaunda tume wakati wauaji, RPC aliyekuwepo na wote waliowatuma wako ofisini na kibaya zaidi ndio hao hao waliounda tume.
Kupotezeana muda tu na kuharibu pesa za Watanzania
 
mimi sio mwanasheria, Tundu Lisu kanifumbua macho sikujua kama waziri hana mamlaka kisheria kuunda tume za uchunguzi

mkuu tundu lisu ameongea ukweli. unakumbuka ile kesi ya zombe? tume ya yale mauaji iliundwa na jk na sio waziri wa mambo ya ndani. issue ni ile ile sasa why jk haundi tume yeye? thanks Allah kwa kutuletea tundu antipas mughwai lisu.
 
kauli ya lissu imekuwa ya chadema? kweli mweshimiwa 6 hakukosea!

Hivi u mbishi tu au nakuelewa huelewi pia?

Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Mwanasheria wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu kimesema, tume ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi ni batili.
 
Back
Top Bottom