CHADEMA yapigwa Marufuku kufanya maandamano Morogoro......

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
SERIKALI wilayani Morogoro imetoa onyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusitisha maandamano yake iliyokusudia kuyafanya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa ukiwamo wa Morogoro.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, mbele ya wenyeviti na watendaji wote wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 50 uliofanyika katika ukumbi wa Mount Urugulu mjini hapa.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi waandamizi wa serikali ngazi ya wilaya wakiwemo wakurugenzi, Mwambungu alisema haoni haja ya kuruhusu maandamano ya chama hicho kutokana na kuonekana kutokuwa na tija.
“Kama ni kweli wanataka kuandamana kwanini walazimishe kupita katikati ya mji...wakitaka kuandamana waanzie Bwani Mindu-kuelekea Sangaganga au Mikese kwenda Chalinze au waanzie Kihonda kuelekea Dakawa,” alisema Mwambungu. Hoja hiyo ambayo awali ilitolewa na baadhi ya viongozi akiwamo Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14, Meya wa mji wa Morogoro, Amir Nondo na Mbunge wa zamani, Issa Ramadhani Kiombwe, ilitiwa nguvu na mkuu huyo wa wilaya alipodai kuwa yanalenga kuvuruga amani nchini.
 
kwanini cdm wanaomba vibali anyway? hakuna haja, twendeni mtaani na tunasababu nyingi sana za kumwondoa kikwete na wabunge wao, wanagombania posho wakati wanancho hawana hata pesa ya mlo mmoja.

cdm this time fanyeni kitu kiwe cha ukweli na lazima tuonyeshe hatutaki hii serikali kabisa.
 
Every man got to decide his own destiny
And in this judgement there is no partiality
So arm in arm with arms we'll fight this little struggle
‘Cause that's the only way we can over come our little trouble
CHADEMA you're right. You're right. You're so right.

You're right
We go fight (We go fight)

We'll have to fight (We go fight)

We're gonna fight (We go fight)
Fight for our rights (bob marley edited)
HAO WANAOPAYUKA NI KINA NANI KATIKA NCHI HII? CHADEMA TUSIKATE TAMAA MOTO NI ULEULE MBAKA KIELEWEKE. SISI NI MBELE KWA MBELE NYUMA NI MWIKO MBAKA UKOMBOZI WA KWELI WA TAIFA HILI UTAKAPOPATIKANA
 
Yeye hajui kuwa wananchi wanaweza kumuondoa kwenye hicho cheo? hawa wanaCCM wamejisahau sana
 
Weee DC acha woga, achia watu wawashe moto. Unaogopa utakuunguza? Hata ukikataa mtaungua tu
 
Huyo mzee mbumbu wa shereia za nchi, ngoja uteuzi mpya atemwe tu
 
Huyo "KADA"mkuu wa Wilaya hajui kazi yake yeye azuie Maandamano kama nani...Maandamano yatafanyika kama kawa na akitaka Amani ivurugike awatume hao Polisi kupiga watu Risasi na Mabomu.
 
amelewa ulevi wa madaraka, ana ubavu wa kuzuia maandamano ya cdm, anatafuta cheap populirity anafiikiri morogoro ni mali ya ccm.mawazo ya kipuuzi kweli
 
Sasa anashauriwa na wajinga na yeye hazichekechi unategemea asitoe pumba. Makada wa CCM tangia lini wakakubali maandamano ya Chadema.
 
kumbe wakuu wa wilaya nao wana nguvu sana nilikuwa sijalitambua hilo.
 
SERIKALI wilayani Morogoro imetoa onyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusitisha maandamano yake iliyokusudia kuyafanya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa ukiwamo wa Morogoro.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, mbele ya wenyeviti na watendaji wote wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 50 uliofanyika katika ukumbi wa Mount Urugulu mjini hapa.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi waandamizi wa serikali ngazi ya wilaya wakiwemo wakurugenzi, Mwambungu alisema haoni haja ya kuruhusu maandamano ya chama hicho kutokana na kuonekana kutokuwa na tija.
"Kama ni kweli wanataka kuandamana kwanini walazimishe kupita katikati ya mji...wakitaka kuandamana waanzie Bwani Mindu-kuelekea Sangaganga au Mikese kwenda Chalinze au waanzie Kihonda kuelekea Dakawa," alisema Mwambungu. Hoja hiyo ambayo awali ilitolewa na baadhi ya viongozi akiwamo Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14, Meya wa mji wa Morogoro, Amir Nondo na Mbunge wa zamani, Issa Ramadhani Kiombwe, ilitiwa nguvu na mkuu huyo wa wilaya alipodai kuwa yanalenga kuvuruga amani nchini.
Huyo DC atakuwa anatumia makamasi kufikiri. Sidhani kama ana hata chembe ya ubingo ulio sawa sawa. anasema maandamano hayo hayana tija ila kuandamana kwenye mapori (mfano toka Mikese kwenda Chalinze kwake hayo yana tija!!! Hawa ndiyo vibaraka wanarudisha nyuma maendeleo ya nchiyetu kwa manufaa yao binafsi? @?~@%&(***)_
 
SERIKALI wilayani Morogoro imetoa onyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusitisha maandamano yake iliyokusudia kuyafanya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa ukiwamo wa Morogoro.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, mbele ya wenyeviti na watendaji wote wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 50 uliofanyika katika ukumbi wa Mount Urugulu mjini hapa.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi waandamizi wa serikali ngazi ya wilaya wakiwemo wakurugenzi, Mwambungu alisema haoni haja ya kuruhusu maandamano ya chama hicho kutokana na kuonekana kutokuwa na tija.
“Kama ni kweli wanataka kuandamana kwanini walazimishe kupita katikati ya mji...wakitaka kuandamana waanzie Bwani Mindu-kuelekea Sangaganga au Mikese kwenda Chalinze au waanzie Kihonda kuelekea Dakawa,” alisema Mwambungu. Hoja hiyo ambayo awali ilitolewa na baadhi ya viongozi akiwamo Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14, Meya wa mji wa Morogoro, Amir Nondo na Mbunge wa zamani, Issa Ramadhani Kiombwe, ilitiwa nguvu na mkuu huyo wa wilaya alipodai kuwa yanalenga kuvuruga amani nchini.

Mmmh! kazi kweli kweli! Mkutano wa serikali unaeuka mkutano wa itikadi za kichama. Kama ana madaraka hayo si angoje CHADEMA walete hiyo taarifa ya maandamano halafu aizuie? Yeye si ndio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ambayo mmoja wa wajumbe wake ni OCD? si angoje OCD amwambie ... 'CDM wameleta aarifa ya maandamano, unasemaje afande'; kisha aseme kwa urahisi tu neno moja: "Zuia". Kwanini anatafuta public sympathy kama sio uoga?

Nionavyo mimi; hawa wakuu wa serikali wamepewa maagizo ya kuzuia maandamano ila wanahofu yasije yakatukia ya Arusha; kwa sababu wanajua CDM hawatakubali maelezo rahisi rahisi kama vile uvunjifu wa amani.

Hee!!! Said Mwambungu unalo hilo. Jiandae kwa presha kushuka na kupanda maana CHADEMA wanakuja hao. Pi pi pi ....
 
Mwambungu anabweteka na kuntamka bila kufikiri.Asubiri nguvu ya uma ukizingatia hii nchi ni yetu sote si ya wanasiasa waliolewa madaraka ka Mwambungu.Upuuzi mtupu!!!!!!!!!!!!!!!
 
pressure ipo juu hata kabla wazee wa kazi hawajatua Moro. Kinachowapa kiwewe ni ratiba tu. Homa ipo juu, kila wakikumbuka ujumbe unavyoingia akilini mwa Raia kila mmoja anaweweseka. Wakati wa wananchi kufunguka na kuelewa ndio sasa, muda wa kuwakataa wakuu wa wilaya na mikoa ndio leo. Tumechoka na kundi la viongozi wasio na tija wanaomtumikia mtu mmoja badala ya wananchi. Moro subirieni nguvu ya umma inakuja ........
 
SERIKALI wilayani Morogoro imetoa onyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kusitisha maandamano yake iliyokusudia kuyafanya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa ukiwamo wa Morogoro.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, mbele ya wenyeviti na watendaji wote wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 50 uliofanyika katika ukumbi wa Mount Urugulu mjini hapa.
Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na viongozi waandamizi wa serikali ngazi ya wilaya wakiwemo wakurugenzi, Mwambungu alisema haoni haja ya kuruhusu maandamano ya chama hicho kutokana na kuonekana kutokuwa na tija.
"Kama ni kweli wanataka kuandamana kwanini walazimishe kupita katikati ya mji...wakitaka kuandamana waanzie Bwani Mindu-kuelekea Sangaganga au Mikese kwenda Chalinze au waanzie Kihonda kuelekea Dakawa," alisema Mwambungu. Hoja hiyo ambayo awali ilitolewa na baadhi ya viongozi akiwamo Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14, Meya wa mji wa Morogoro, Amir Nondo na Mbunge wa zamani, Issa Ramadhani Kiombwe, ilitiwa nguvu na mkuu huyo wa wilaya alipodai kuwa yanalenga kuvuruga amani nchini.

yale yanayofanywa na NAPE ndo yana tija? huyo mzee alosema kiazi kweli, yaani wakishashika madaraka wanaona km wana hati miliki na ardhi ya watanzania.
 
Every man got to decide his own destiny
And in this judgement there is no partiality
So arm in arm with arms we'll fight this little struggle
‘Cause that's the only way we can over come our little trouble
CHADEMA you're right. You're right. You're so right.

You're right
We go fight (We go fight)

We'll have to fight (We go fight)

We're gonna fight (We go fight)
Fight for our rights (bob marley edited)
HAO WANAOPAYUKA NI KINA NANI KATIKA NCHI HII? CHADEMA TUSIKATE TAMAA MOTO NI ULEULE MBAKA KIELEWEKE. SISI NI MBELE KWA MBELE NYUMA NI MWIKO MBAKA UKOMBOZI WA KWELI WA TAIFA HILI UTAKAPOPATIKANA

Umesema yote mkuu sina la kuongeza !
 
Chadema kama lile dege la vita B52...hata kama hako ka mwambungu kakatae..the B.52 will rock all over the moro twn
 
Huyo Mwambungu anakiherehere cha m...k..j.. wa asubuhi! kufanya maandamano ni haki ya raia wa nchi hii. Kusema zuia maandamano ni matumizi mabaya ya madaraka, suala la tija kwake hawezi kuona coz mwisho wa siku pple watajua haki zao na hawatapenda tena kunyanyaswa ktk kazi zao,madai na maisha kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom