CHADEMA yapiga kambi jimbo la Nyang'hwale kuisambaratisha CCM

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,503
1,722
Wakuu,

Kamanda Rogers Luhega,aliyekuwa mugombea ubunge jimbo la Geita 2010 kwa tiketi ya CDM,katibu wa BAVICHA wilaya ya Geita bwana Vicent Paulo maarufu kwa jina la Dear Mama,diwani wa kata ya Kasamwa kupitia CDM bwana Mahenge na makamanda wengine wameamua kupiga kambi ya mwezi mmoja kutoa elimu ya uraia katika vijiji vyote vya jimbo la Nyang'hwale ambapo leo walikuwa katika kijiji cha Bukwimba wamefungua tawi na watu 105 walirudisha kadi za CCM na kujiunga na CDM,kesho watakuwa kijijini Karumwa.Nitaendelea kuwajuza zaidi kuhusu operation hiyo bila kusahau picha.Hakuna kulala mpaka kieleweke.

UPDATES.

Muda huu makamanda wanapita kila kitongoji hapo kijijini Bukwimba kusikiliza kero mbalimbali toka kwa wananchi ili ziweze kuwasilishwa panapohusika kwa utatuzi,baada ya hapo safari kuelekea kijijini Karumwa itaanza.
 
hao ni wale walioipigia kura ccm, na sasa wamechoshwa na usanii wa ba mwanaasha, poleni kwa kungeja maisha bora.
 
harakati kama hizo ndio antivirus za wanaosubiria maisha bora,na watazidi kukimbia tu.kazeni buti makamanda wetu.tupo pamoja
 
CHADEMA mmepasahau sana sana sana Bukoba vijijini!!! Siwasikii mkiunguruma huko, wananchi wanahitaji mabadiliko!! Tafadharini tembeleeni huko, toeni elimu ya uraia, waamsheni waliolala!!
Tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kuwafikishia ujumbe ila tunaomba mtuongezee nguvu!!
Poleni sana na hongeleni kwa kazi nzuri inayoendelea nchini, hakika UKOMBOZI u-karibu!!!
PEOPLEEEE'S................!!!
 
Kweli Chadema imekuwa ...ukiona initiative za operesheni za kisiasa zinaanzia ngazi ya jimbo ...na kupata mapokezi makubwa toka kwa wananchi basi ni dalili za kuimarika kwa chama. ......zamani operesheni ya siasa hata kwenye ngazi ya kijiji ilikuwa unasubiri kiongozi atoke makao Makuu ya chama ......Leo ....hata viongozi wa Chadema ngazi ya jimbo .....wanapata mapokezi ...

Ccm pamoja na ukongwee na mtandao wake siku hizi wakitaka kufanya operesheni za kisisasa lazima Waite angalau Wajumbe wa NEC.....na tena sio wote
..
 
Ahsante kwa taarifa hiyo, nitaifanyia tathmini ya kina baadaye kwa sasa napita tu
 
Endeleeni hivyo hivyo,mie pia huku jimbo la Bariadi Mashariki naendelea kutoa elimu ya uraia vijiji vya Lugulu,Zanzui,Kabale na Kinamweli,hakuna kulala mpaka kieleweke.
 
Wakuu,

Kamanda Rogers Luhega,aliyekuwa mugombea ubunge jimbo la Geita 2010 kwa tiketi ya CDM,katibu wa BAVICHA wilaya ya Geita bwana Vicent Paulo maarufu kwa jina la Dear Mama,diwani wa kata ya Kasamwa kupitia CDM bwana Mahenge na makamanda wengine wameamua kupiga kambi ya mwezi mmoja kutoa elimu ya uraia katika vijiji vyote vya jimbo la Nyang'hwale ambapo leo walikuwa katika kijiji cha Bukwimba wamefungua tawi na watu 105 walirudisha kadi za CCM na kujiunga na CDM,kesho watakuwa kijijini Karumwa.Nitaendelea kuwajuza zaidi kuhusu operation hiyo bila kusahau picha.Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Wambie wasisahau kijijini kwetu Busolwa
 
jamani nauliza mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa KILIMANJARO ni nani? Moshi vjjn, vunjo na same pamelala huu ni mkoa wa wasomi na wapenda mabadiliko tafadhali kamanda amka tuanze kazi, Ephata Nanyaro keshaikamata Arusha na amekua ni alama ya mkoa ww upo wp?
Cyril Chami, Anna Kilango, Maghembe, Mathayo David
Ni wa kuwashulikia mapema.
 
Big up kamanda ! Mfikishie Rogerz ujumbe huu, mavuno ni mengi mno Nkome but hakuna wavunaji, njooni huku tufungue ofsi, mabalozi wa ccm hawapo tena. Mola awa tangulie ktk harakat za ukomboz wa pili wa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom