CHADEMA yamtikisa Maige, alazimika kukimbilia jimboni

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Ahmed Makongo, Kahama

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, ameonekana kutikiswa na maandamano yaliyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga hivi karibuni, baada ya kuamua kukimbilia jimboni kwake kuzima moto uliowashwa na chama hicho.
Juzi na jana, Waziri Maige alilazimika kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali vya Jimbo la Msalala analoliongoza.
Katika mikutano hiyo, Maige alitumia nafasi hiyo kuwabeza CHADEMA akisema maandamano na mikutano yao haina tija yoyote, bali ni kuzorotesha shughuli za maendeleo ya wananchi.
Wananchi wengi ambao sasa wanakabiliwa na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali waliambiwa na Maige kuwa huu ni wakati wa kutekeleza wajibu wao wa kujiletea maendeleo kuliko kutumia maandamamo ya chama hicho ambayo yana nia ya kuwapotosha.
Maige alikwenda mbali zaidi akiwataka wananchi waache kudai haki zao kwa kutumia maandamano hayo, kwa sababu wanatumia muda mwingi wa uzalishaji mali kwenye mambo yasiyo na tija.
"Uchaguzi ulisha kwisha, sasa maandamano ya nini….watu wanaacha shughuli za kuzalisha mali na maendeleo kwa ujumla wanakwenda kwenye maandamano ambayo hayana tija yoyote, wananchi tusikubali kudanganywa," alisema.
Aidha, Waziri Maige aliwataka wananchi kuelekeza nguvu zao katika kutekeleza majukumu yao ya kifamilia, sanjari na kutekeleza miradi ya maendeleo hususani katika sekta za elimu na afya. Sekta ambazo zote zimekuwa zikilaumiwa kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali yasiyokidhi haja za wananchi. Maige ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Msalala, hata hivyo alishindwa kutetea hoja yake ya kuwataka wananchi wasiandamane kutokana na ugumu wa maisha badala yake akijikuta akitambua bayana juu ya changamoto zinazolikabili jimbo hilo katika kujiletea maendeleo. Wakati huo huo alichangia mifuko ya saruji zaidi ya 4,000 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, ambapo kila kijiji alikipatia jumla ya mifuko 20, na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa zahanati katika vijiji vyao.
 
Juzijuzi nilikuwa jimboni kwake, ukweli CDM inakubalika huko na nafikiri kama wasingechakachua basi sasa hivi habari ingekuwa nyingine
 
Hapo poa, Maige anatetea kitumbua chake, Badala ya CCM kuishutumu chadema waishukuru kwa kuwahamusha kutoka usingizini na kuwakumbusha majukumu yao. Vile vile wajue CDM sio chama cha msimu kama walivyokuwa wanasema ktk kampeni bali ni chama cha wakati wote
 
Pesa alizotumia kununulia mifuko ya saruji ni fedha za jimbo sio zake. Asitake kuwadanganya watu kuwa ni fedha zake kutoka mfukoni.

Hata akibwabwaja kiama kinakuja. Kansa bado inawala taratibu
 
Masikini kijana, atakua aliogopa kusikia CMD wamekwenda kubomoa ngome, kweli CMD ni mawimbi makali, kila mtu anachanganyikiwa akisikia wimbi limepita, anakurupuka kwenda kupoza, wataahirisha shughuli zao nyingi wakifuatilia kila wimbi litakapopita.
 
SASA WANA JAMIII NDIYO TUJUE UMUHIMU WA MAANDAMANO,JE ANGEPATA MUDA SANGAPI KUDHURU JIMBONI KWAKE KAMA SIKIFO CHA NYANI?UNAJUA HAWA VIONGOZI NI WANAFKI SANA NA WANATUMIA UDHAIFU WA WANANCHII KUWADANGANYA KWA MAFUMBO NA KEJELI SIZIZO NA MSINGI,KWA KIFUPI CCM WAMELOWA NA HAWANA JIPYA NA SIDHANI KAMA WAZIRI WA NCHI YUKO SAHIHI KUZUNGUMZIA CHADEMA MAJUKWAANI KWANI HIYO NI KAZI YA MAKAMBA NA YEYE VYEMA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA KISERIKALI KWA MASLAI YA TAIFA NA SIKULETA KEJELI SIZIZO NA MANTIKI MAJUKWAANI KUWA CHADEMA WANAKOSEA KWANI SIKAZI YAKE KISHERIA NA ANATAKIWA KUFANYA KAZI KWA VITENDO NA SILAZIMA ATOE MSAADA KIPINDI CHA MATATIZO TUUU LENGO KUZIMA MOTO,NAAFAHAMU KUWA WATU WENGI WAMESOMA NA HATUNA KAZI KUTOKANA NA URASIMU WA VIONGOZI,KWAIYO MUDA TUNAWO WA MAANDAMANO KWANI TUNAPUNGUZA STRESS NA KUBUY TIME,ATAFUTE HOJA ZA MSINGI NA SIKUJIBARAGUZA KUFUTA MADHAMBI YAKE NA YA CHAMA CHAKE!!!PEOPLE POWER:wink2:
 
Wan JF,

Ni kweli waziri Maige leo yuko Kijiji cha Kakola kilicho karibu kabisa na mgodi wa Bulyanhulu. Nimemwona akiendesha kikao cha ndani kwenye ki mgahawa kidogo sana kinachoitwa "Machame Bar". Wakati huo gari la serikali idara ya maji la wilaya ya Kahama linapita mtaani likiwatangazia wananchi wahudhurie mkutano wake kwenye shule ya msingi Kakola kuhusu siku ya wanawake.

Baada ya kikao chake anaelekea shule ya msingi kakola, ambapo nimemwona anahutubia wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wananchi wasiozidi 100 chini ya mti wa shule.

Wananchi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida hamna anayejua kama kuna waziri na mbunge wao leo pamoja na gari la serikali kupita likitangazia wananchi.
 
Jamani CHADEMA inaiweka CCM kwenye mstari! Kila mtu anajua kuwa Wabunge wa CCM wakishachaguliwa tu,wote wanahamia Dar na kuanza kuongoza majimbo yao kwa remote control. Mpaka miaka 5 inapokwisha ndipo wanarudi tena kwenda kuomba KULA.

Safari hii ni tofauti kabisa. Tunashuhudia wabunge wakirudi mara mbilimbili kwenda kuweka mambo sawa mara tu Peoples Power inapotembelea kwenye majimbo yao. Hakika hii ndiyo aina ya Upinzani tunaohitaji Tanzania kwenye hii karne ya 21.

CDM is really a Watchdog ! KEEP IT UP CDM. We love you all.
 
Mwanzo wa mwisho wao,hawana thamani tena.
 
CHADEMA nendeni majimbo yote Tanzania ili na wabunge wengine wa ccm wakatoe misaada makwao kabla kiama chao hakijafika.
 
Jamani CHADEMA inaiweka CCM kwenye mstari! Kila mtu anajua kuwa Wabunge wa CCM wakishachaguliwa tu,wote wanahamia Dar na kuanza kuongoza majimbo yao kwa remote control. Mpaka miaka 5 inapokwisha ndipo wanarudi tena kwenda kuomba KULA.

Safari hii ni tofauti kabisa. Tunashuhudia wabunge wakirudi mara mbilimbili kwenda kuweka mambo sawa mara tu Peoples Power inapotembelea kwenye majimbo yao. Hakika hii ndiyo aina ya Upinzani tunaohitaji Tanzania kwenye hii karne ya 21.

CDM is really a Watchdog ! KEEP IT UP CDM. We love you all.

Naona sasa huo ndiyo mkakati wao. Kila baada ya maandamano makubwa ya CHADEMA wanarudi majimboni ili kuweka mambo sawa na kutoa rushwa kwa pesa za walipa kodi. Nadhani hizo pesa alizonunulia saruji ndizi zile pesa ambazo Wabunge wametengewa ili kusaidia kuendeleza majimbo yao katika mambo mbali mbali.
 
Kinachonivutia kwa hawa jamaa ni kimoja kwamba:
Wanapanga mikutano yao mashuleni ili kushinikiza walimu wawalazimishe wanafunzi kuhudhulia ili wasiumbuke!!
ITS REAL CUTE!!
 
Wana kazi kubwa ya kufanya majimboni, nafikiri siku zijazo maandamano yatazuiiwa tena kwa taarifa za kiintelinsia, maana yanawapa tabu watawala
 
CCm ni kama bao la mwisho wamechooka na wanalitafua bao kwa shidaaaaa halipatikani, jasho linawatoka hadi m******n:rain:
 
Back
Top Bottom