CHADEMA yamkaanga Mkurugenzi kwa Waziri

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
***************************

SOURCE: Gazeti la Mwanza liitwalo MZAWA
Toleo la : 588
Date: Desemba 25, 2010,
Page: Front Page
Headline: Sakata la Umeya wa Jiji la Mwanza, CHADEMA yamkaanga Mkurugenzi kwa Waziri

***************************

CHADEMA Mkoa wa Mwanza kimeandika barua kwa kwa waziri wa tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kikituhumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wilson Kabwe kuwa ndiye aliyekwamisha uchaguzi wa meya na naibu meya uliokuwa ufanyike Desemba 17.

Katika barua hiyo katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza bw. Wilson Mushumbusi amedai kuwa mkurugenzi huyo wa jiji ndiye aliyekwamisha uchaguzi huo baada ya kushindwa kusimamia vema sheria za TAMISEMI pamoja na kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhusu namna ya kuwachagua viongozi hao wa Halmashauri.

Barua hiyo imedai kuwa CHADEMA inaamini kuwa mkurugenzi huyo ametoa taarifa za uongo kwa waziri kwamba madiwani ndiyo walikuwa wameshindwa kumchagua meya na naibu meya wa jiji hilo.

CHADEMA katika barua hiyo iliyoandikwa jana Ijumaa kwenda kwa waziri inasisitiza taarifa kuwa uchaguzi huo ulishindikana kufanyika ni za udanganyifu na kwamba chama hicho kiko tayari kwa uchaguzi huo ili mradi sheria na kanuni husika zizingatiwe.

"CHADEMA kimeona ni vema kkutaarifu wewe binafsi (waziri) kuwa, madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza hawajawahi kushindwa kumchagua meya na naibu wake, bali mkurugenzi ndiye aliyeshindwa kutimiza wajibu wake. Ni vema tukumbushane kuwa, mkurugenzi kama katibu wa mkutano wa madiwani (Kanuni namba 26 ya Halmashauri) kushindwa kwake (Mkurguenzi) kufuata kanuni za kudumu kamwe hakuwezi kutoa baraka kwa hatua ambazo anawazo ofisi yako ichukue.

CHADEMA kinaamini kwamba sheria, kanuni na hata busara ya kawaida itatumika na CHADEMA hakihitaji jambo hili linaleta mvutao wa kisheria", imesema sehemu ya barua hiyo.

CHADEMA imeorodhesha baadhi ya masuala ambayo inadai kuwa ni ukiukwaji wa sheria na kanuni uliofanywa na mkurugenzi wa Jiji katika uchaguzi huo.

Hoja zilizoma katika barua hiyo zinasema ifuatavyo: "Mkurugenzi wa Jiji ni katibu wa mkutano kwa mujibu wa tafsiri ya kanuni (namba 2) ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza ya mwaka 2003, pia kifungu cha 24(7) cha sheria ya serikali za mitaa na mamlaka ya miji na sheria namba 8 ya mwaka 1982, nayo inasema hivyohivyo.

Kazi ya katibu pia inajulikana chini ya kanuni ya 14 ya kanuni za kudumu, inashangaza kuona katika mkutano huo, mkurugenzi alikuwa mwenyekiti wa mkutano, katibu na msimamizi wa uchaguzi, CHADEMA kinaona kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni.

Mkurugenzi mkuu wa jiji ni dhahiri anaelewa kuwa huo ulikuwa mkutano wa kawaida kwa mujibu wa kanuni namba 3(1) na (2) kifungu kinachosema kuwa, mkutano wa kumchagua Meya au naibu Meya ni mkutano wa kawaida.

Kanuni namba 10(91) na 13(91) zinaeleza bayana kuwa utaratibu wa shughuli za mikutano ya kawaida. Kanuni 10(91) na 13(91) zinaeleza bayana kuwa utaratibu wa shughuli za mikutano ya kawaida utakuwa ni kumchagua mtu kuongoza kikao iwapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawapo ili madiwani waweze kujadili jambo linalotakiwa kwa mujibu wa sheria, kabla ya shughuli nyingie yoyote, pia kanuni namba 13(f) inasisitiza kuwa kujibu maswali kwa kufuata kanuni ya 21 ya kanuni za kudumu pia nayo inatoa mwongozo ni namna gani hoja zijadiliwe na maamuzi yafikiwe kwa njia yakupiga kura.

CHADEMA kimesikitishwa na Mkurugenzi wa Jiji hili baada ya kuitisha mkutano aliendelea kuwa mwenyekiti, katibu, na msimamizi wa uchaguzi. CHADEMA hakijui muhtasari wa kikao ambao ameleta kwako aliuandaa saa ngapi!

Kwa kulingana na sababu yangu ya pili hapo mkutano ilibidi umchague mwenyekiti wa muda ili kuongoza mkutano wa kwanza wa uchaguzi na si yeye kuongoza, kuratibu na kusimamia."

"kwa busara ya kawaida mkurugenzi hawezi kushindwa kusimamia uchaguzi halafu akatangaza mgogoro eti halmashauri ivunjwe ilhali haijawahi kuundwa. Waziri anaweza kuuvunja halmashauri iliyokwishaundwa na ikashindwa kutimiza majukumu yake."

"Mkurugenzi huyohuyo aliuambia mkutano wa madiwani kuwa ana barua mbili na zote zinatoka kwa katibu wa CCM (M) kuhusu utambulisho wa wagombea wa umeya na naibu meya, ya kwanza ilikuwa inatambulisha wagombea wa umeya na naibu meya na ya pili ambayo haikuonekana inamtambulisha mgombea wa umeya tu, hapa pana utata."

Barua hiyo ya CHADEMA kwa waziri inazidi kuhoji "inakuaje mkurugenzi anajihusisha na udanganyifupamoja na ubabaishaji kama huu" huku chama hicho kikikumbusha tuhuma za mkurugenzi huyo yaani tarehe 20/08/2010 alipopokea kielelezo cha tarehe 21/08/2010 na kumtangaza mgombea ubunge wa Jimbo la Nyamagana kuwa siyo raia, tarehe 20/10/2010 mkurugenzi huyo alipodaiwa kuzuia kiwanja cha Furahisha kisitumike kwa mkutano wa mgombea uraisi wa CHADEMA ilhali alikuwa na ratiba ya kampeni ya wagombea urais wote pamoja na kuchelewesha matokeo ya uchaguzi tarehe 01/11/2010 mpaka kusababisha hasara kwa baadhi ya wananchi wa Mwanza kufuata ghasia ambazo zingeweza kuepukika.

"Mgombea unaibu meya kupitia CUF naye alijiandikia barua na kuipeleka kwa mkurugenzi akijitambulisha kuwa yeye ni mgombea wa nafasi hiyo kinyume na sheria ya uchaguzi inayotaka mgombea apitishwe na chama chake" imeongeza kudai barua hiyo.

Bwana Mushumbusi katika barua hiyo amedai kuwa, kwa mazingira hayo si tu mkurugenzi amevunja kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji, bali pia amevunja katiba ya nchi ambayo haimtambui mgombea binafsi.

CHADEMA inasisitiza kuwa taarifa ya mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kuwa uchaguzi ulishindikana si sahihi na kudai imejaa udanganyifu, hukuchama hicho kikisisitiza kwamba kiko tayari kwa uchaguzi wa meya na naibu wake, ili mradi uchaguzi huo uzingatie sheria n kanuni husika pamoja na kutokuwepo aina yoyote ya ghiriba, ubabaishaji, unyanyasaji, na vitisho kwa madiwani na raia wanaotaka kujua hamashauri yao inafanya nini na kwa wakati gani.
 
ohoooo,....ntarudi kusoma baadae ndefuu ila ni habari njema sana
 
Barua hii ni nzuri sana na inaweza ikawa na athari zifuatazo; kwanza inaweza ikasababisha Mkugenzi huyo kuhenguliwa.Hatua hiyo inaweza kuchukuliwa dhidi yake hasa kutokana na barua yake aliyo wahandikia wasimamizi wa uchaguzi wa vituo, akiwaelezea uamuzi uliokuwa umefikiwa na uongozi wa juu wa kuvuruga taratibu za uchaguzi. Pili makosa hayo ya uvunjaji wa kanuni za uchaguzi yamefanyika katika sehemu mbali mbali hapa nchini, na hivyo barua hiyo inaweza ikaibua mivutano katika halmashauri hizo.
 
Nazani wakati Mwingine tunapochagua Mbunge wa CDM tuhakikishe na madiwani tunampa wote ili kusiwe na kisingizio...TAZAMA MUSOMA CDM ilishinda mbunge na madiwani kwa Kishindo hivyo ikamyima mkurugenzi nafasi ya haya kuzungumza kuhusu swala la udiwani...Ndio maana CDM walichaguana nani awe MEYA nani awe Naibu MEYA kabla hata hawajaenda kupiga kura wakiwa mchanganyiko na CCM!
 
GreAtThinkers,

Kumbukeni Wilson Kabwe ndiye aliyemuengua Mh. WENJE kugombea ubunge, kwa hivo huyo si mtu makini.Alikusudiwa kulazimisha wananchi wa Nyamagana watawaliwe na Mtu asiyekubalika.

Wilson Kabwe ni kweli amevuruga uchaguzi kwa kutaka kuvunja utaratibu, Thanks to CDM COUNCILORS wako makini sana.

Wilson Kabwe aliwahi kuwa Mkurugenzi ambaye ilikuwa afukuzwe tuu kazi ila kwa sababu Mtoto wa Mkulima ni class mate, Kaamua kupeleka REJECT ya mbeya Mwanza.
 
Hata mimi nimeiona barua ya CDM kwakweli wanahoja za msingi na kama waziri atakuwa fair anastahili kumshauri rais amfute kazi Bw. Kabwe. Hakika mkurugezi huyo ni kikwazo kwa demokrasia katika jiji la Mwanza yuko tayari kusababisha maafa kwa manufaa binafsi.
***************************

SOURCE: Gazeti la Mwanza liitwalo MZAWA
Toleo la : 588
Date: Desemba 25, 2010,
Page: Front Page
Headline: Sakata la Umeya wa Jiji la Mwanza, CHADEMA yamkaanga Mkurugenzi kwa Waziri

***************************

CHADEMA Mkoa wa Mwanza kimeandika barua kwa kwa waziri wa tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kikituhumu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wilson Kabwe kuwa ndiye aliyekwamisha uchaguzi wa meya na naibu meya uliokuwa ufanyike Desemba 17.

Katika barua hiyo katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza bw. Wilson Mushumbusi amedai kuwa mkurugenzi huyo wa jiji ndiye aliyekwamisha uchaguzi huo baada ya kushindwa kusimamia vema sheria za TAMISEMI pamoja na kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhusu namna ya kuwachagua viongozi hao wa Halmashauri.

Barua hiyo imedai kuwa CHADEMA inaamini kuwa mkurugenzi huyo ametoa taarifa za uongo kwa waziri kwamba madiwani ndiyo walikuwa wameshindwa kumchagua meya na naibu meya wa jiji hilo.

CHADEMA katika barua hiyo iliyoandikwa jana Ijumaa kwenda kwa waziri inasisitiza taarifa kuwa uchaguzi huo ulishindikana kufanyika ni za udanganyifu na kwamba chama hicho kiko tayari kwa uchaguzi huo ili mradi sheria na kanuni husika zizingatiwe.

"CHADEMA kimeona ni vema kkutaarifu wewe binafsi (waziri) kuwa, madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza hawajawahi kushindwa kumchagua meya na naibu wake, bali mkurugenzi ndiye aliyeshindwa kutimiza wajibu wake. Ni vema tukumbushane kuwa, mkurugenzi kama katibu wa mkutano wa madiwani (Kanuni namba 26 ya Halmashauri) kushindwa kwake (Mkurguenzi) kufuata kanuni za kudumu kamwe hakuwezi kutoa baraka kwa hatua ambazo anawazo ofisi yako ichukue.

CHADEMA kinaamini kwamba sheria, kanuni na hata busara ya kawaida itatumika na CHADEMA hakihitaji jambo hili linaleta mvutao wa kisheria", imesema sehemu ya barua hiyo.

CHADEMA imeorodhesha baadhi ya masuala ambayo inadai kuwa ni ukiukwaji wa sheria na kanuni uliofanywa na mkurugenzi wa Jiji katika uchaguzi huo.

Hoja zilizoma katika barua hiyo zinasema ifuatavyo: "Mkurugenzi wa Jiji ni katibu wa mkutano kwa mujibu wa tafsiri ya kanuni (namba 2) ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza ya mwaka 2003, pia kifungu cha 24(7) cha sheria ya serikali za mitaa na mamlaka ya miji na sheria namba 8 ya mwaka 1982, nayo inasema hivyohivyo.

Kazi ya katibu pia inajulikana chini ya kanuni ya 14 ya kanuni za kudumu, inashangaza kuona katika mkutano huo, mkurugenzi alikuwa mwenyekiti wa mkutano, katibu na msimamizi wa uchaguzi, CHADEMA kinaona kuwa huu ni ukiukwaji mkubwa wa sheria na kanuni.

Mkurugenzi mkuu wa jiji ni dhahiri anaelewa kuwa huo ulikuwa mkutano wa kawaida kwa mujibu wa kanuni namba 3(1) na (2) kifungu kinachosema kuwa, mkutano wa kumchagua Meya au naibu Meya ni mkutano wa kawaida.

Kanuni namba 10(91) na 13(91) zinaeleza bayana kuwa utaratibu wa shughuli za mikutano ya kawaida. Kanuni 10(91) na 13(91) zinaeleza bayana kuwa utaratibu wa shughuli za mikutano ya kawaida utakuwa ni kumchagua mtu kuongoza kikao iwapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawapo ili madiwani waweze kujadili jambo linalotakiwa kwa mujibu wa sheria, kabla ya shughuli nyingie yoyote, pia kanuni namba 13(f) inasisitiza kuwa kujibu maswali kwa kufuata kanuni ya 21 ya kanuni za kudumu pia nayo inatoa mwongozo ni namna gani hoja zijadiliwe na maamuzi yafikiwe kwa njia yakupiga kura.

CHADEMA kimesikitishwa na Mkurugenzi wa Jiji hili baada ya kuitisha mkutano aliendelea kuwa mwenyekiti, katibu, na msimamizi wa uchaguzi. CHADEMA hakijui muhtasari wa kikao ambao ameleta kwako aliuandaa saa ngapi!

Kwa kulingana na sababu yangu ya pili hapo mkutano ilibidi umchague mwenyekiti wa muda ili kuongoza mkutano wa kwanza wa uchaguzi na si yeye kuongoza, kuratibu na kusimamia."

"kwa busara ya kawaida mkurugenzi hawezi kushindwa kusimamia uchaguzi halafu akatangaza mgogoro eti halmashauri ivunjwe ilhali haijawahi kuundwa. Waziri anaweza kuuvunja halmashauri iliyokwishaundwa na ikashindwa kutimiza majukumu yake."

"Mkurugenzi huyohuyo aliuambia mkutano wa madiwani kuwa ana barua mbili na zote zinatoka kwa katibu wa CCM (M) kuhusu utambulisho wa wagombea wa umeya na naibu meya, ya kwanza ilikuwa inatambulisha wagombea wa umeya na naibu meya na ya pili ambayo haikuonekana inamtambulisha mgombea wa umeya tu, hapa pana utata."

Barua hiyo ya CHADEMA kwa waziri inazidi kuhoji "inakuaje mkurugenzi anajihusisha na udanganyifupamoja na ubabaishaji kama huu" huku chama hicho kikikumbusha tuhuma za mkurugenzi huyo yaani tarehe 20/08/2010 alipopokea kielelezo cha tarehe 21/08/2010 na kumtangaza mgombea ubunge wa Jimbo la Nyamagana kuwa siyo raia, tarehe 20/10/2010 mkurugenzi huyo alipodaiwa kuzuia kiwanja cha Furahisha kisitumike kwa mkutano wa mgombea uraisi wa CHADEMA ilhali alikuwa na ratiba ya kampeni ya wagombea urais wote pamoja na kuchelewesha matokeo ya uchaguzi tarehe 01/11/2010 mpaka kusababisha hasara kwa baadhi ya wananchi wa Mwanza kufuata ghasia ambazo zingeweza kuepukika.

"Mgombea unaibu meya kupitia CUF naye alijiandikia barua na kuipeleka kwa mkurugenzi akijitambulisha kuwa yeye ni mgombea wa nafasi hiyo kinyume na sheria ya uchaguzi inayotaka mgombea apitishwe na chama chake" imeongeza kudai barua hiyo.

Bwana Mushumbusi katika barua hiyo amedai kuwa, kwa mazingira hayo si tu mkurugenzi amevunja kanuni za kudumu za Halmashauri ya Jiji, bali pia amevunja katiba ya nchi ambayo haimtambui mgombea binafsi.

CHADEMA inasisitiza kuwa taarifa ya mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kuwa uchaguzi ulishindikana si sahihi na kudai imejaa udanganyifu, hukuchama hicho kikisisitiza kwamba kiko tayari kwa uchaguzi wa meya na naibu wake, ili mradi uchaguzi huo uzingatie sheria n kanuni husika pamoja na kutokuwepo aina yoyote ya ghiriba, ubabaishaji, unyanyasaji, na vitisho kwa madiwani na raia wanaotaka kujua hamashauri yao inafanya nini na kwa wakati gani.
 
Wilson Kabwe ni TATIZO kubwa sana kwa MWANZA.

Je mnaifahamu BIG FOUR inayolisumbua jiji la Mwanza kuhusiana na mabo ya Viwanja na Hata uhamisho wa Wafanyakazi Serikalini.

Huyu Jamaa hafai, ni 100% REJECT
 
Back
Top Bottom